Ndugu zangu tuchukue tahadhari tukitembelea Dodoma hususani wageni wa mji wa Dodoma (unamkuta yupo pale pa kisubiria wageni kama vile anasubiria Mgeni, kwa shepu na muonekano lazima ujichanganye. Miwani Kwenye gari anadai twende ukalale kwangu.,.).
Nimetapeliwa na demu pale SGR station Dodoma kwa njia ya ajabu Sana kwa ahadi ya mapenzi.
Demu anaonekana anajiweza sana, muonekano na gari analotumia. Ghafla akadai anafanya biashara ya pikipiki anataka tufanye wote. Tukiwa room anaomba nimtumie 3m kutoka benki yangu kwenda akaunti yake ili kumlipa supplier wake wa Dar.
Mpaka muda huu najiuliza nilitoaje Ile pesa huenda anatumia dawa aisee