Tunashukuru kwa kukusanua. Watu wengi wanakuponda, lakini ukweli ni kwamba umeokoa watu wengi ambao wangeenda kuibiwa kama wewe.
Ingawa hujaeleza vizuri lakini kama nimeelewa mchezo uko hivi.
1. Unakutana na dada mkali ambaye anajidai ni taxi driver.
2. Mkiwa njiani kuelekea sehemu ambayo unaenda anaanza kuku seduce na kukuambia yuko single unaweza kwenda kulala kwake. Unajiona una bahati sana umeokita dodo kwenye mwarobaini.
3. Mkifika kwake ana ku intertain na kukueleza story nyingi kukuamnisha kwamba yeye ni mfanya biashara mkubwa wala hana shida ya pesa. Anakununulia vinywahi, chakula yaani full intertaiment.
4. Anakupa mzigo unakula kiroho safi hadi unaridhika.
5. Baada ya game anapata dharura ambayo inahitaji kutuma pesa lakini bahati mbaya account yake ina matatizo. Ni muhimu atume hiyo hela kwa wakati huo ili biashara zake zisiharibike. Anajaribu kuwapigie wenzake lakini wote wanatoa sababu za hapa na pale. Anakugeukia wewe umsaidie atakurejeshea kesho asubuhi.
6. Kwa kuwa umekula mzigo na umesha aminishwa ni mtu wako.. unamsaidia.
7. Asubuhi anaku drop kazini na kuahidi baada ya muda bank zingefunguliwa atakamilisha mwamala. Na pia anakuambia ukimaliza mkutano mpigie aje akuchukue. Anakuuliza jioni ungependa kula nini.
8. Ukisha achana naye simu haipatikani tena. Unajaribu kuchukua tax uende pale mlipo lala jana, wanakwambia ile ni airbnb wala hawamjui. Ameondoka mchana. baada ya hapo ndo unagundua umetapeliwa.
Iko hivi matapeli hutumia mbinu mbalimbali kukamilisha adhima yao. Ila kugundua ni rahisi.
1. Principle ya kwanza. No sweet without sweat. Ukiona unapata/unapewa/unaahidiwa kitu adimu au cha ghali kirahisi rahisi bila gharama shituka. Unatapeliwa. Matapeli hapa wanatumia tamaa za binadamu kunasa wahanga. Usiwe na tamaa.
2. Principle ya pili. Urgency ya mtu mwingine is non of your business. Ukiona mtu anakuja kwako na kukuomba kitu halafu anakwambia yaani inatakiwa akamilishe haraka sasa hivi, mwambie kama ingekuwa kesho kutwa ningeweza kukusaidia. Uharaka wake si wako, wewe una mipango yako. Hapa matapeli wanatumia udhaifu unaitwa huruma. Usiwe na huruma kwa mtu usiye mjua.
3. Principle ya tatu. Acha uoga. Ukiona mtu anakutisha usipofanya hivi sasa hivi kitatokea kitu kibaya kwako. Shtuka. Hapa matapeli wanatumia udhaifu unao itwa uoga. Anakutisha na jambo halafu anakuambia ili uokoke fanya 1,2,3.... Anakutisha uingie mkenge.
Mwisho nakutakia pole sana.