Maisha yangu na baada ya miaka 50 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maisha yangu na baada ya miaka 50

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BabaDesi, May 20, 2009.

 1. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #1
  May 20, 2009
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,793
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Nafurahi kuwajulisha wana JF kuwa tarehe 8 Juni mwaka huu 2009 nitakuwa natimiza miaka 50 toka nilipozaliwa. Miongoni mwa mambo ninayotaka kufanya ni kufahamu walipo watu ambao kwa namna moja ama nyingine nilikutana nao katika hiyo miaka 50 ya maisha yangu. Tafadhali kama unamjua mmoja wapo ama una taarifa zake nijulishe na kama wewe ni mojawapo basi tafadhali ni-PM. Natanguliza Shukurani.

  Leo naomba nianze na orodha wa watu niliosoma nao Chang'ombe shule ya Msingi kati ya mwaka 1970 nilipohamia hapo nikitokea St Anthony Tanga (siku hizi ni Changa Primary School) hadi mwaka 1973 nilipohama kwenda Mfaranyaki Songea.

  Walimu:

  1. Mr Kirwanda
  2. Mr Nkani
  3. Mr Matemu
  4. Mr Sindamwaka - Mwalimu Mkuu
  5. Mama Baruti
  6. Mama Kunambi

  Wanafunzi Wenzangu:

  1. Norman Sabuni - alikuwa na kaka yake anaitwa Noel Sabuni na mdogo wake anaitwa Nina Sabuni. Kaka yao mkubwa alikuwa Raphael Sabuni wakati huo akiimbia STC Jazz na akina Marijani Rajab.

  2. Hassan Zawayai
  3. Zuberi Zayumba
  4. Abraham Mwasongwe
  5. Helena Sebastian
  6. Gosbert Roderick na dada yake Esther Roderick
  7. Georgina Rugimbana na dada yake Rosemary Rugimbana - walikuwa dada wa Jordan Rugimbana ambaye alikuwa nyuma yetu darasa moja na sasa ni mkuu wa Wilaya Kinondoni.

  8. Mariam Himid
  9. Lucy Mkande
  10. Edith Masanja
  11. Sarah Kilua
  12. John Tesha
  13. Rosemary Tesha
  14. Mbiliyawaka Hango
  15. Mohamed Adam
  16. Patrick Rugemalira
  17. Richard Kilandeka
  18. Suna Said
  19. Neema - jina la pili nimesahau lakini mama yake alikuwa
  mwalimu hapo hapo Chang'ombe S/Msingi
  20. Penina Mhando
  21. Shabaani Mohamed na mdogo wake Faraji Mohamed
  22. Selina Mkaja
  23. Rizwan - Alikuwa muasia akiishi mitaa ya Chang'ombe
  Jamatini.
   
  Last edited: May 26, 2009
 2. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #2
  May 20, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  BABADESI BAADHI YAO NI KAMA IFUATAVYO:-

  Nina Sabuni kaolewa yuko Botwsana na mumewe na watoto
  Mariam Himid anaishi Canada -
  John Tesha - huyu alihamia Marekani
  Rosemary Tesha - yuko Dar ameolewa ni mke wa Leodgar Tenga
   
 3. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #3
  May 20, 2009
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,793
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  WoS! Nakushukuru mno kwa taarifa hii hasa hii ya Rosemary Tesha!! Woman, ulipita Chang'ombe shule ya msingi ama uliwafahamu tu through mihangaiko ya maisha?
   
 4. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #4
  May 20, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  No Mkuu sijapita huko ila si unajua kukulia DSM watu wanafahamiana.
   
 5. Mwawado

  Mwawado JF-Expert Member

  #5
  May 20, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 998
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 35
  Patrick Rugemalira - Huyu jamaa yupo Minneapolis, Minnesota.

  Penina Mhando - Prof. Penina alihamia Nairobi na bado yupo na masuala yake ya
  ualimu na uandishi wa vitabu nafikiri amerudia jina lake la Mhando
  kama sio Mlama.

  Norman Sabuni - Alisoma huko Eastern Europe nafikiri bado yupo Lugalo Hospital
  ni Daktari hapo.

  Zuberi Zayumba - Huyu Jamaa nami nafahamiana nae vizuri tulipoteana muda mrefu,
  tulionana mwaka jana Arusha katika Msiba wa James Mgani,Zuberi
  yupo Sigara na anaishi Tabata.

  Rosemary Tesha - Ni mke wa Leodgar ,huyu mama yupo Hazina

  Naona hii List ni watu wa Chang'ombe miaka ya 70 enzi za safari Tripers na Timu ya Soccer Avengers!!
   
 6. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #6
  May 20, 2009
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,793
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145

  ...kama ulikuwepo mkuu! Safari Trippers walikuwa wakifanya mazoezi yao kwenye nyumba moja pale mitaa ya Chang'ombe Maduka mawili enzi hizo Tukipaita Uhindini!
  Wimbo wa Georgina tumeanza kuusikia hapo hata kabla haujaingia Redioni! Hapo pia unazungumzia mambo ya akina Comets, Rifters na Sunburst!

  Naomba nifafanue Mkuu. Huyu Penina Mhando ninayemzungumzia siye yule mama wa Chuo Kikuu ambaye enzi hizo tulikuwa tunamfahamu kutokana na kitabu chake cha 'Hatia' ambacho ni miongoni mwa vitabu tulivyokuwa tukipenda kuvisoma.
  Penina Mhando aliyekuwa classmate wangu alikuwa anakaa magorofa ya NHC karibu na karibu na lile ghorofa la wachina!
   
 7. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #7
  May 20, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0

  Baba Desi heri ya maadhimisho ya siku ya kuzaliwa
  .

  Nahakika kama wapo humu wataku pm, assuming wanataka ku re-establish contacts with any piece of you!

  Lakini sidhani kama hili jamvi lina watu wengi wa demographics yako. Nimegundua wengi aidha si watu wazima au hawa act their age. Ningefurahi sana kama mpo kina Baba Desi wengi mtuletee mitazamo ya angle yenu. Mnahitajika sana, and that's one thing I miss in this baraza. Watu mnaokumbuka foleni za kununua sukari na kadi za mgao wa petroli.

  I gotta tell you one thing though. Inahitaji uvumilivu kuwepo hapa watu wa rika lako, na nashukuru uwepo wenu mtu ka wewe na wengine wanao sound matured and responsible, the Rev. Kishoka's of the forum, the Kichuguu's, JokaKuu's, Mwawado's, Jasusi's, QM, Mama's, Mzee Mwanakijiji's, Augustine Mosha's, SteveD, WomenofSubtanc, Blueray, Painkiller, the BubuAK's, Halisi, the Fundi Mchundo's of the jamvi and a handful others, I don't care how old you are, but I read you guys as sooo matured and full of gravitas. And of course, the illustrious FMES types, when he acts his age.

  Maana kwa kweli kuna aina ya mandhari fulani humu yanaweza kufukuza watu wazima, and I put the blame squarely on Jakaya Kikwete himself, Invisible that is, maana ana very high tolerance na watu wa mizaha mizaha na mambo ya kitoto humu.

  Again, hongera na heri ya siku ya kuzaliwa Baba Desi.
   
 8. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #8
  May 20, 2009
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,793
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145

  ...Such NICE Words! You Have Said It All. Thank You So Much, Dilunga. As For the JK a.k.a Invisible thing, that is a new one to me, creative and total outrageous! THANK YOU.
   
  Last edited: May 20, 2009
 9. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #9
  May 20, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Mkuu unaweza kumsaidia babadesi kwa kile alichokianzishia thread?
   
 10. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #10
  May 20, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  I thought JF was a big tent?
   
 11. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #11
  May 20, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Hili lijamaa kazi yake kulalama lalama tuu kama limeporwa hela askirimu. Sijui halijui kuwa kuna jukwaa maalum la kulalama
   
 12. Kaniki1974

  Kaniki1974 JF-Expert Member

  #12
  May 20, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 352
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mungu akujalie ufike salama hiyo June 8. Couldn't guess we have guys of 50s here. Shikamoo.
   
 13. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #13
  May 20, 2009
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,793
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ...Marahaba! :D :D
   
 14. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #14
  May 20, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Na unajuaje sijamsaidia pembeni? Maana hata Baba Desi mwenyeye anaweza asijue Dilunga ndio fulani, na si wote tutatundika hapa mimi Yo Yo ndio Amina, nimeolewa na Albert, na rafiki yetu Maimuna pia kazaa, yuko Cambodia, aliachika na Jumanne, mimba ya pili wakatoa ....oh no, no, please, give them a break, will you?

  Lead post ina ishu ya kutimiza miaka 50, na hiyo ndio angle niliyopenda kuongelea. Au, kama ni strictly ishu ya kutafuta watu, pointi ya miaka 50 ya nini? Ilisemwa ya nini? Angeweza kusema mimi Baba Desi natafuta watu, period. Maana kutafuta watu si lazima ufike miaka 50 ndio uwakumbuke. The point is, Yo Yo, mwenzetu Baba Desi anasherehekea miaka 50 pia. Vingenevyo, pointi ya miaka 50 ingesemwa ya nini? Ha ahahahaaaaa! Yo Yo!
   
 15. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #15
  May 20, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Okay, kama pointi ndo hiyo basi stick to it. Malalamiko peleka kwenye jukwaa husika, will you?
   
 16. M

  Mtu wa Kawaida JF-Expert Member

  #16
  May 21, 2009
  Joined: May 2, 2008
  Messages: 217
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Hongera sana kwa kukatiza nusu ya karne.
  Noel Sabuni(a.k.a Nobi) huyu mheshiwa yupo Dar na Kampuni moja inayotoa huduma ya bima ya afya inayoitwa Prosperity Health. Yeye atakueleza kwa wakati huu mdogo wake alipo Norman kama bado yupo Lugalo au la.
   
 17. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #17
  May 21, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  BabaDeci
  Nakupa hongera kwa kuikaribia nusu karne siku chache zijazo. Mungu akujalie afya njema ili uweze kuiona karne nzima.
  Mzee Punda
   
 18. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #18
  May 21, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Hongera Babadesi kwa kufikisha umri huo......God should continue to bless you, upate miaka mingine 50!

  Cheers
   
 19. Kiteitei

  Kiteitei JF-Expert Member

  #19
  May 21, 2009
  Joined: Jan 14, 2009
  Messages: 1,253
  Likes Received: 147
  Trophy Points: 160
  baba desi hongera sana, nina imani waliowengi humu wako nusu au karibu na robo tatu ya umri wako! ni jambo la kujivunia ukizingatia na maisha halisi ya sasa..be blessed na maisha mema, lakini you sound like mchezaji mwenzangu kwenye team ya maveteran maeneo ya beach kulee, if yes salute! lazima mnyama amwage damu, tena ngómbe na sio mbuzi
   
 20. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #20
  May 21, 2009
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,793
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ...Asante Mkuu! mmm, huko sio sana! mara moja moja huwa naibuka pale kwa maveteran wa Basketball pale Viwanja vya Gymkhana karibu na bahari lakini zaidi ni jogging za kwenye mchanga na pia mitaa ya jangwani na Upanga!!
   
Loading...