Maisha na Muziki (Story ya maisha yangu)

Selemani Sele

Senior Member
Feb 25, 2023
148
410
Ladies and gentleman its your boy selemani sele mzee wa mastory,kinachokuja mbele yenu ni story ya maisha na mziki ni story fupi natumai watu watajifunza.

MAISHA NA MZIKI
Episode 1.
(KUZALIWA)
Miaka 30 iliyopita nilizaliwa katika jiji lenye kila aina ya uchafu madanguro, vibaka, majambazi, matapeli na wezi, jiji hilo kuitwa Mzizima au bandari salama al maarufu Dar es Salaam nikiwa mtoto wa 3 kati ya kumi mitaa ya Tandale utumbo kwenye Hood ya vijana watafutaji wenye ari ya kupata au kukosa ilimradi tusilale njaa.

Baba yetu alikuwa fundi selemala na mama mpika vitumbua hatukua na maisha magumu ila mlo mmoja wa usiku na vitumbua vya mama vilituwezesha kuwa wakubwa na mama alituasa twende shule kwakua mtaji wa maskini mikono yake mwenyewe.

Tukiwa watoto wakiume wanne na wakike sita tulihakikishiwa kwenda shule zetu za kayumba na kutosahau maswala ya dini maana Mama aliamini kuwa hatuwezi endelea bila Nguvu za Allah na hilo limenisaidia katika imani.

Hata nikikosa sijioni mdhaifu bali kunipa nguvu kuendelea kusimama na kutafuta na kufikia hapa nimekwepa mapanga, ngumi na pia madawa ya kulevya kama cocaine na bangi kufika hapa hii ndo story ya kuzaliwa kwangu.

Hatuzaliwi kwa bahati mbaya bali kwasababu.

Next episode tunaanza jinsi nilivyojua Napenda mziki.
 
Unaandika fupi hivi huwezi pata wachangiaji , shusha epsod 5 ziwe ndefu uone watililikaji coment
 
  • Kicheko
Reactions: EEX

Similar Discussions

Back
Top Bottom