Maisha yangu na baada ya miaka 50

Maisha yangu na baada ya miaka 50

Kunradhi Baba Desi , Mwalimu aliyenipiga kibao miaka hiyo na amefariki several years ago ni Mwl Nsibu(sio Mwl Nkane).My apologies and sorry for any inconveniences not intended.
Hata hivyo nimekumbuka waalimu kadhaa:
Mr Ntanga
Mrs Mwanza
Mrs Kahemele
Mrs Mwansasu
na wa zamani zaidi(asians)
Miss Figuiredo(later Mrs Fernandes)
Miss Killochia
Mrs Walji

na wazungu
Mr Brown
Mr Dalton mwalimu wa Dini
Miaka mingi imepita hapo naongelea 1964-68 sijui kwa sasa hivi wako wapi,
Mwenye habari tafadhali.

...Mwalimu Nsibu nakumbuka alikuwa mkali wa mambo ya kwaya na bendi ya shule yeye mwenyewe akiwa hodari wa kupiga filimbi!
Huyu Miss Figuiredo alikuwa na uhusiano na akina Roy na Endrico Fiquiredo ambao walikuwa tulikuwa tunakaa nao mitaa ya maghorofa ya keko lakini sisi tukiishi kwenye zile nyumba za NHC zilizoungana kama treni na ambao sasa ndio wanamiliki Studio ya kurekodia Muziki na Bendi ya Inafrica? Nadhani wote ama mmoja wao bado wanaishi pale.
 
Baba Desi

Kwanza Shikamoo na Pili Hongera sana kwa kufikisha 50yrs.Mungu akubariki ili uweze kuishizaidi na zaidi.

Hongera sana Baba Desi

...Marahaba na Asante sana mkuu!! 🙂🙂
 
...Mwalimu Nsibu nakumbuka alikuwa mkali wa mambo ya kwaya na bendi ya shule yeye mwenyewe akiwa hodari wa kupiga filimbi!
Huyu Miss Figuiredo alikuwa na uhusiano na akina Roy na Endrico Fiquiredo ambao walikuwa tulikuwa tunakaa nao mitaa ya maghorofa ya keko lakini sisi tukiishi kwenye zile nyumba za NHC zilizoungana kama treni na ambao sasa ndio wanamiliki Studio ya kurekodia Muziki na Bendi ya Inafrica? Nadhani wote ama mmoja wao bado wanaishi pale.

Hawa kina Figuiredo..ndio wale waliokuwa wanakaa pale keko bora-magorofani?
Walikuwa na ndugu yao mwingine anaitwa Jackson (alisoma Forodhani Primary)? Kama ni hao..nakumbuka hawa jamaa walikuwa ni waGOA. BabaDesi..wewe ulikuwa unakaa mitaa ile ya duka la mchina?
 
...Ndio hao hao. walikuwa pia na dada yao anaitwa Vero. Sina hakika na hilo Duka la mchina, kama ni lile lililo katikati pale ya magorofa na zile nyumba basi ndio hapo ila enzi hizo pale palikuwa na muembe mkubwa sana ndio kilikuwa kijiwe chetu. Mimi nilikuwa nakaa nyumba ya kwanza kwenye 'treni' iliyokuwa opoziti 'treni' na waliyokuwa wakiishi akina Roy. Nyumba yetu ilikuwa No 98 Mtaa wa Ngorongoro unaoanzia pale keko bora kuelekea Chang'ombe sijui kama mpaka leo unaitwa hivyo!
 
Last edited:

Ule muembe naukumbuka. Duka la mchina kama sikosei lilikuwepo mtaa wa majimaji!! Huu mtaa ulikuwa sambamba na ngorongoro..nao pia ulikuwa unaelekea Chang'ombe!!Kipindi sana mkuu!!
 
...Ndio hao hao. walikuwa pia na dada yao anaitwa Vero. Sina hakika na hilo Duka la mchina, kama ni lile lililo katikati pale ya magorofa na zile nyumba basi ndio hapo ila enzi hizo pale palikuwa na muembe mkubwa sana ndio kilikuwa kijiwe chetu. Mimi nilikuwa nakaa nyumba ya kwanza kwenye 'treni' iliyokuwa opoziti 'treni' na waliyokuwa wakiishi akina Roy. Nyumba yetu ilikuwa No 98 Mtaa wa Ngorongoro unaoanzia pale keko bora kuelekea Chang'ombe sijui kama mpaka leo unaitwa hivyo!
Namkumuka sana Vero sijui yuko wapi sasa, not seen her for the last 37-40 years!
 
Baba Desi mbona mie ujanitafuta au kwa kuwa tulikutana miaka ya 2000? (Joke)
Hongera sana kaka kwa kutimiza miaka hiyo MUNGU akujalie mingine ili uwaone wajukuu wa Desi

(Dadako Dommy!!)
 
...Kwanza una kesi! juhudi zangu zote za kukutafuta zimegonga mwamba ambao 'umeupanda' wewe! Siamini kama bado upo hapo ulipokuwa! Bila shaka upo nje ya Bongo??? 😛
 
Amah!! kesi tena? Nipo kaka maisha yanagonga!! Acha tu. Yes nipo Bongo niende wapi.
 
baba desi ....nami nakukumbuka sana........nilikuwa nakaa kule mtaa wa chamwenyewe.....kwa nyuma ukitokea pale maduka mawili.....nakumbuka kulikuwa na mihogo ya kukaanga mitamu sana pale michichani karibu na bakwata.........dah.....zamani raha kweli.....manake unatembea pekupeku toka changombe kupita toroli,kekomwanga mpaka kariakoo bila wasiwasi.....dah sasa nipo ughaibuni 30years ninamisi sana home...
 
...Kweli Bongo yetu sasa Kubwa! Tuko humu humu halafu hatuonani? Nashukuru sana lakini kwa hili la kunishitua kwamba bado upo na kunitakia heri. Ubarikiwe!
 
baba desi ....nami nakukumbuka sana........nilikuwa nakaa kule mtaa wa chamwenyewe.....kwa nyuma ukitokea pale maduka mawili.....nakumbuka kulikuwa na mihogo ya kukaanga mitamu sana pale michichani karibu na bakwata.........dah.....zamani raha kweli.....manake unatembea pekupeku toka changombe kupita toroli,kekomwanga mpaka kariakoo bila wasiwasi.....dah sasa nipo ughaibuni 30years ninamisi sana home...

Hii mihogo pia kulikuwa na mzee mmoja anaileta pale shuleni Chang'ombe ndani ya tenga alilokuwa amefunga kwenye kiti cha nyuma cha baiskeli yake halafu anakuwekea chachandu la pilipili, vitunguu na nini tena sijui, tukaipa jina la 'Likembe' maana wakati huo Morogoro Jazz chini ya Soloist Mbaraka Mwishehe na mtindo wao wa Likembe ndio wanavuma kweli!
 
BabaDesi nimefurahi sana kwa kuwa utatimiza 50th birthday. Ni jambo la kumtukuza Mungu. Nafurahi pia sasa utapata wageni wengi siku hiyo maana naamini wengi mtatafutana sana following your thread. Kama uko Dar sijui utakuwa unaishi eneo lipi,ila Chan'gombe siku hizi kumebadilika kiasi. Zile nyumba za uhindini wahindi wengi waliziuza na pia zinanuniliwa sana siku hizi, wanabomoa wanajenga magorofa. Miundo mbinu (barabara za mitaa) ni zilezile tangu enzi hizo, ni mashimo hazina ukarabati hata kidogo, yaani manispaa wamezembea sana wilaya ya Temeke. Ule uwanja wa Mchichani palipokuwa panalimwa mchicha ndipo Manji alinunua na kupauza wameshaweka fence na sijui developments gani zinategemewa pale. Nyumba za treni bado zipo, nafikiri watu walishauziwa.

Katika mpango miji ya manispaa ya Temeke eneo lote la uhindini lipo katika mpango wa kubadilishwa kabisa kwa kujengwa business/residential complexes za magorofa, hivyo ukinunua nyumba au zile zilizopo zinatakiwa zivunjwe na kujenga ghorofa. Pengine itabadili uso wa Chango'ombe maana inaonekana ipo katika old stone age!!!! Yale magofu ya uhindini sasa yanauzwa kuanzia 200-300m. Unaweza wahi moja pale, it isa a potential area kwa sasa japo zamani ukimwambia mtu naishi wilaya ya Temeke anaduwaa kidogo maana wengi tunaamin ukiishi Dar ni Kinondoni na Ilala!!!!
 
Maana kwa kweli kuna aina ya mandhari fulani humu yanaweza kufukuza watu wazima, and I put the blame squarely on babadesi himself, Invisible that is, maana ana very high tolerance na watu wa mizaha mizaha na mambo ya kitoto humu.

ebu tuambia hayo yako ya kikubwa
 
...Maane, Asante kwa taarifa hii. Mimi bado nabanana humu humu Daslam wilaya ya kinondoni. hayo mabadiliko yote uliyosema ndio maendeleo yenyewe! Hapo mchichani upande wa klabu ya Sigara na eneo lote la hiyo sekondari iliyopo hapo palikuwa ni kifusi cha kutupia makapi ya mpunga! Nakumbuka wanafunzi walikuwa wakiungua sana pale kwa sababu kama unavyojua kifusi kinavyowaka. unaona majivu juu yametulia unatia mguu kumbe ndani moto unawaka vibaya! Nakumbuka kuwa baadae ilibidi ipigwe marufuku kuchoma makapi ya mpunga hapo kwa jinsi wanafunzi walivyokuwa wakiunguzwa na moto!!
 
Maana kwa kweli kuna aina ya mandhari fulani humu yanaweza kufukuza watu wazima, and I put the blame squarely on babadesi himself, Invisible that is, maana ana very high tolerance na watu wa mizaha mizaha na mambo ya kitoto humu.

ebu tuambia hayo yako ya kikubwa

...Steven, mbona umebadilisha hio post ya watu?? aliyeipost alitaja JK hapo wewe ulipoweka babaDesi! Kuna ujumbe unataka kunipa labda, sijauelewa? 🙄
 
Hongera sana na nakutakia miaka mingi yenye positive contribution kwa Taifa letu hili.
 
Baba Desi heri ya maadhimisho ya siku ya kuzaliwa.

Nahakika kama wapo humu wataku pm, assuming wanataka ku re-establish contacts with any piece of you!

Lakini sidhani kama hili jamvi lina watu wengi wa demographics yako. Nimegundua wengi aidha si watu wazima au hawa act their age. Ningefurahi sana kama mpo kina Baba Desi wengi mtuletee mitazamo ya angle yenu. Mnahitajika sana, and that's one thing I miss in this baraza. Watu mnaokumbuka foleni za kununua sukari na kadi za mgao wa petroli.

I gotta tell you one thing though. Inahitaji uvumilivu kuwepo hapa watu wa rika lako, na nashukuru uwepo wenu mtu ka wewe na wengine wanao sound matured and responsible, the Rev. Kishoka's of the forum, the Kichuguu's, JokaKuu's, Mwawado's, Jasusi's, QM, Mama's, Mzee Mwanakijiji's, Augustine Mosha's, SteveD, WomenofSubtanc, Blueray, Painkiller, the BubuAK's, Halisi, the Fundi Mchundo's of the jamvi and a handful others, I don't care how old you are, but I read you guys as sooo matured and full of gravitas. And of course, the illustrious FMES types, when he acts his age.

Maana kwa kweli kuna aina ya mandhari fulani humu yanaweza kufukuza watu wazima, and I put the blame squarely on Jakaya Kikwete himself, Invisible that is, maana ana very high tolerance na watu wa mizaha mizaha na mambo ya kitoto humu.

Again, hongera na heri ya siku ya kuzaliwa Baba Desi.

...angalia loser hili,who are you to judge?
 
Baba Desi mbona mie ujanitafuta au kwa kuwa tulikutana miaka ya 2000? (Joke)
Hongera sana kaka kwa kutimiza miaka hiyo MUNGU akujalie mingine ili uwaone wajukuu wa Desi

(Dadako Dommy!!)

...Kwanza una kesi! juhudi zangu zote za kukutafuta zimegonga mwamba ambao 'umeupanda' wewe! Siamini kama bado upo hapo ulipokuwa! Bila shaka upo nje ya Bongo??? 😛

Why can't you PM each other?

BWT.....Nimependa mnavyojikumbusha maenzi yenu...hongereni!
 
Back
Top Bottom