Maisha Yana Maana Gani Hasa?

Maisha Yana Maana Gani Hasa?

Binafsi sioni kabisa

Naona tunatokea na kupotea tu

Hivi vitu tunavyovitesekea havina thamani yoyote maana ni tunaviacha tu

Sioni maana ya uwepo kabisa.

Unazaliwa then una kufa tu

Sasa si bora tu usinge kuwepo?

What the hell are we doing here?

Hebu na nyie Semeni bwana humu duniani kuna nini cha maana?

Kutafuta wealth? Ili zije zinifanye kuwa mtumwa? Ku please mwanamke mwenye mwili na akili kama mimi?

Huu ni udwanzi jamani, yaani najuilizaga hii dhana ya kufanikiwa ina maana ipi kama mwisho ni mauti?

Hebu elezeeni na nyie maana sioni maana yoyote ya haya maisha. Bado Sija ona kwakweli. Una amka asubuhi kwenda kazini unarudi umechoka then unakula una lala kesho tena unarudia yale yale, je wewe ni mashine?

Huu ujinga sitaki tena, huu,


Mapenzi nayo yamekuwa magumu, tu hakuna wa kukuthamini na kukupenda,

Aisee, watu wana jaribu kutafuta namna ya kukutumia tu. Ujinga na kuzushiana maneno ndo habari za mjini.

Binafsi nataka niachane na kucheza huu mchezo wa kijinga. Maana it's too much now.
Usiumize kichwa mkuu,Aliyekuumba lengo lake kubwa ni hili na amelielezea ndani Quran tukufu na haya ndiyo majibu ya unachouliza:

KWA NINI TUMEKUJA DUNIANI?

Allah muumbaji ametuumba kwa kusudio maalumu, si kwa bahati wala bure.
1. Kumuabudu yeye Mungu muumbaji.

وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ

“Sikuwaumba majini na watu isipokuwa waniabudu.” (Adh-Dhaariyaat 51:56)

2. Kujaribiwa kwa matendo yetu

الَّذِي خَلَقَ الْمَوْتَ وَالْحَيَاةَ لِيَبْلُوَكُمْ أَيُّكُمْ أَحْسَنُ عَمَلًا

“Yeye ndiye Aliyeumba mauti na uhai ili akujaribuni ni nani miongoni mwenu mwenye matendo mazuri zaidi.” (Al-Mulk 67:2)

3. Hatukuumbwa bure kimzaha

أَفَحَسِبْتُمْ أَنَّمَا خَلَقْنَاكُمْ عَبَثًا وَأَنَّكُمْ إِلَيْنَا لَا تُرْجَعُونَ

“Je, mlidhani kwamba tuliwaumba bure tu, na kwamba hamtarudishwa kwetu?” (Al-Mu’minuun 23:115)

4. Kutafuta Akhera bila kusahau dunia

وَابْتَغِ فِيمَا آتَاكَ اللَّهُ الدَّارَ الْآخِرَةَ وَلَا تَنسَ نَصِيبَكَ مِنَ الدُّنْيَا

“Tafuta kwa yale aliyokupa Allah makazi ya Akhera, wala usisahau sehemu yako katika dunia.” (Al-Qasas 28:77)

5. Surat Al-Baqarah 2:156: Innaa lillaahi wa innaa ilayhi raaji'uun.
Maana: “Hakika sisi ni wa Allah, na hakika kwake Yeye tutarejea.”

KIUFUPI:

Tupo duniani ili tumuabudu Mungu muumbaji (Allah), tujaribiwe kwa matendo yetu, na tujiandae kwa maisha ya Akhera baada ya kufa. Tusijenge dunia tukaisahau Akhera, wala tusitafute Akhera kwa kusahau wajibu wetu wa duniani.
Hela unazitafuta ila utaziacha tu,na unaowaachia nao wataziacha tu.
Katika tukio la uhakika ambalo kila mtu atakutana nalo ni kifo.
Katika pumzi zako hapa Duniani Muabudu Mola wako kwa njia maalum alizoelekeza yeye na usifuate mafundisho na maelekezo yaliyotengenezwa na Watu.

Nakukaribisha katika uislam,njia ya kweli na uhakika,dini pekee ya Muumba wa mbingu na Ardhi.
Soma UISLAM(usiwasome waislam),jifunze UISLAM maswali yote unayotatizika majibu yake yapo katika UISLAM...kule mambo yapo wazi kabisa.
Nje ya hapa,ndugu yangu nakuhakikishia katu hautakuja kupata jibu wala kuelewa kwanini upo hapa Duniani na utabaki na hilo fumbo mpaka unafukiwa kaburini kumbe jibu alishaliweka hapa Duniani.
 
Hilo swali wamelitafakaribwatu wengi tangu kuimbwa kwa ulimwengu, wanafalsafa wengi wamehamasika nalo. dini nazo zikaingilia iia bado kwa wengi ni kitendawili. Soma kitabu cha Ayubu katika biblia uone majibu yake, huenda yakakuangazia kidogo
Anasemaje ayubu kwa ufupi?
 
Eti ukipata zile dejavu maana yake hiyo experience ulishaipitiaga kwenye past life Yako😆
Uongo tupu ni mambo ya kufikiria tu hayo, hakuna cha past life hapa,

Mbona wanyama hawana reincarnation?

Binadamu tumejua sana kujipa sifa, eti kuna Mungu, sijui alimuumba binadamu kwa mfano wake??

Wanachekesha sana
 
Miaka 80-90 na unaondoka, ni mda mfupi sana, huna la maana la kufurahia. Bora nyakati za zamani kina Methusela waliishi 900+ yrs.
Duuh, mbona wanasema shida sio umeishi miaka mingapi, ila ni umeishi vipi. Kukaa kwingi sio kigezo

Ila kufa kiko pale pale
 
Maisha hayawahi wala hayatokuwa na maana..
Kila mtu anajitafutia maana kivyake...
Wale wenye influence kubwa ndo wamewatengenezea wenzao "maana ya maisha"...
Unaambiwa pigania ndoto yako,, then what?
Unaambiwa uache alama duniani, ikusaidie nini na wapi?
Ndoto na mapigano ya binadamu ndo jela yake mwenyewe..
Kumbe jela ni imposition ya idea zisizo na mashiko? Kwamba tunazaliwa na kufa
 
Weka objectives kila mwaka alafu uzi meet, life will be exciting, ukikaa kiboya bila malengo unaamka, unazurura unakunya unalala, utajiuliza hayo maswali
Duuh kwa hiyo ukiwa busy ndo maana ya maisha? Je hiyo si kwamba ni distraction tu ya kukimbia huku na huku ukisubiria wakati wa kufa
 
Usipokuwa busy utakufa pia, umejikuta upo duniani unaishi, find a purpose otherwise utatumika kuwafikishia watu wengine purpose zao
So what's a purpose kama hiyo purpose inaishia kufutika katika uso wa Dunia within a few years ukisha kufa, mfano wewe Saizi unadhani kuna mtu una jali kuhusu maisha yako duniani? Vivyo hivyo ukisha kufa ndo imepita hiyo
 
So what's a purpose kama hiyo purpose inaishia kufutika katika uso wa Dunia within a few years ukisha kufa, mfano wewe Saizi unadhani kuna mtu una jali kuhusu maisha yake duniani? Vivyo hivyo ukisha kufa ndo imepita hiyo
Thinking yako inachanganya vitu viwili, kwamba unakubali kuwepo na maana ila hiyo maana inakua diluted kwasababu tunakufa.

Aliyeyatengeneza maisha ndiyo ameamua yafikie ukomo wakati fulani. Wengine wanawahi na wengine wanachelewa.

Umaana wa maisha unapatikana kwa namna utakavyoyaishi, pamoja na ufupi wake.

Watu waliofanikiwa kuweka maana kwenye maisha yao, wanaacha legacy, siku ya vifo vyao wasifu/nyasifu zao zinakuthibitishia namna walivyoweka maana kwenye maisha yao.

Watu kama, Isaac Newton, Nikola Tesla, Albert Einstein na Mixologist.

Ila kuna watu wengine wanakuwa wamekuja kuzurura tu hapa duniani
 
Watu kama, Isaac Newton, Nikola Tesla, Albert Einstein na Mixologist.

Ila kuna watu wengine wanakuwa wamekuja kuzurura tu hapa duniani
Hii ndo illusion kubwa sana, ambayo naizungumzia unafikiri babu zako hawakuacha legacy?

Unafikiri walikuja kuzurura?

Hapa ndipo mnapochanganya maana ya maisha na self accomplishments ambazo ni either zinakuwa recognized au laah, wale ambao hawako recognized sio kwamba hawakufanya makubwa, tena it's those who aren't singed ndo huwa wame ishi vyema. Ila yote kwa yote kuishi kwao na michango yao hupotea pale wanapofutika katika uso wa dunia
 
Back
Top Bottom