Maisha Yana Maana Gani Hasa?

Maisha Yana Maana Gani Hasa?

Aliyetuumba ndiye mwenye majibu

Kwenye ecosystems, binadamu hatuna tofauti na viumbe vingine

Jambo la kuzingatia, ukipata nafasi furahia kila sekunde inayopotea

Na jizuie kukutana na makwazo, maana havichelewi kukupanua moyo na ukaondoka na miaka 30

Kwa Kila jambo, linalokukabili kama challenge sema "all is well"

Karibu Dodoma Wine tupunguze mawazo ya kuwaza kwanini tupo Duniani🍷
 
Binafsi sioni kabisa

Naona tunatokea na kupotea tu

Hivi vitu tunavyovitesekea havina thamani yoyote maana ni tunaviacha tu

Sioni maana ya uwepo kabisa.

Unazaliwa then una kufa tu

Sasa si bora tu usinge kuwepo?

What the hell are we doing here?

Hebu na nyie Semeni bwana humu duniani kuna nini cha maana?

Kutafuta wealth? Ili zije zinifanye kuwa mtumwa? Ku please mwanamke mwenye mwili na akili kama mimi?

Huu ni udwanzi jamani, yaani najuilizaga hii dhana ya kufanikiwa ina maana ipi kama mwisho ni mauti?

Hebu elezeeni na nyie maana sioni maana yoyote ya haya maisha. Bado Sija ona kwakweli. Una amka asubuhi kwenda kazini unarudi umechoka then unakula una lala kesho tena unarudia yale yale, je wewe ni mashine?

Huu ujinga sitaki tena, huu,


Mapenzi nayo yamekuwa magumu, tu hakuna wa kukuthamini na kukupenda,

Aisee, watu wana jaribu kutafuta namna ya kukutumia tu. Ujinga na kuzushiana maneno ndo habari za mjini.

Binafsi nataka niachane na kucheza huu mchezo wa kijinga. Maana it's too much now.
Hilo swali wamelitafakaribwatu wengi tangu kuimbwa kwa ulimwengu, wanafalsafa wengi wamehamasika nalo. dini nazo zikaingilia iia bado kwa wengi ni kitendawili. Soma kitabu cha Ayubu katika biblia uone majibu yake, huenda yakakuangazia kidogo
 
Aliyetuumba ndiye mwenye majibu

Kwenye ecosystems, binadamu hatuna tofauti na viumbe vingine

Jambo la kuzingatia, ukipata nafasi furahia kila sekunde inayopotea

Na jizuie kukutana na makwazo, maana havichelewi kukupanua moyo na ukaondoka na miaka 30

Kwa Kila jambo, linalokukabili kama challenge sema "all is well"

Karibu Dodoma Wine tupunguze mawazo ya kuwaza kwanini tupo Duniani🍷
Hakika. Mkuu..

Mimi pia ni mapenzi wa wine ila niko mjini Dar na maisha yamenichapa hatari

Je, ni naweza kukupa taarifa zangu ili uweze kunitumia wine na mimi nipate kupoza maumivu haya ya existential crisis??
 
Miaka 80-90 na unaondoka, ni mda mfupi sana, huna la maana la kufurahia. Bora nyakati za zamani kina Methusela waliishi 900+ yrs.
 
Maisha hayawahi wala hayatokuwa na maana..
Kila mtu anajitafutia maana kivyake...
Wale wenye influence kubwa ndo wamewatengenezea wenzao "maana ya maisha"...
Unaambiwa pigania ndoto yako,, then what?
Unaambiwa uache alama duniani, ikusaidie nini na wapi?
Ndoto na mapigano ya binadamu ndo jela yake mwenyewe..
 
Back
Top Bottom