Maisha Yana Maana Gani Hasa?

Maisha Yana Maana Gani Hasa?

Binafsi sioni kabisa

Naona tunatokea na kupotea tu

Hivi vitu tunavyovitesekea havina thamani yoyote maana ni tunaviacha tu

Sioni maana ya uwepo kabisa.

Unazaliwa then una kufa tu

Sasa si bora tu usinge kuwepo?

What the hell are we doing here?

Hebu na nyie Semeni bwana humu duniani kuna nini cha maana?

Kutafuta wealth? Ili zije zinifanye kuwa mtumwa? Ku please mwanamke mwenye mwili na akili kama mimi?

Huu ni udwanzi jamani, yaani najuilizaga hii dhana ya kufanikiwa ina maana ipi kama mwisho ni mauti?

Hebu elezeeni na nyie maana sioni maana yoyote ya haya maisha. Bado Sija ona kwakweli. Una amka asubuhi kwenda kazini unarudi umechoka then unakula una lala kesho tena unarudia yale yale, je wewe ni mashine?

Huu ujinga sitaki tena, huu,


Mapenzi nayo yamekuwa magumu, tu hakuna wa kukuthamini na kukupenda,

Aisee, watu wana jaribu kutafuta namna ya kukutumia tu. Ujinga na kuzushiana maneno ndo habari za mjini.

Binafsi nataka niachane na kucheza huu mchezo wa kijinga. Maana it's too much now.
Mfalme Sumani aliandika, Mhubiri 12:8 "
8 Mhubiri asema, Ubatili mtupu; mambo yote ni ubatili!". Mzee Mwinyi alisema, "Maisha ni hadithi tu, basi ishi uwe hadithi nzuri".
 
Nionavyo mimi maisha ni zawadi ambayo Mungu alitupa yaani tuishi tule na tumuabudu haijalishi kwa njia ipi, na ndio maana alitupa wanyama mimea na matunda. Ila sisi binadamu ndio tukaleta complications kibao badala yake tumekuwa na chuki za kila namna na kila mahali sababu tunayoyafanya hayakuwa makusudi ya Mungu maana yake miongoni mwetu kuna watu sasa inabidi waabudiwe na watukuzwe ili wewe upate kuishi maana wao ndio wameshika mpini, riziki yako na hatma yako.

Hii kitu Mungu hapendi ndio maana wote hamuwez kuwa na amani mnabaki kuchukiana tu na kuombeana mabaya. Fuatilia maisha ya jamii ambayo hazikufikiwa na ukoloni au usasa kama wa Adzabe ndio utaelewa mfumo wa mausha ya binafamu upoje. Rizki ya binadamu Mungu alishaiweka wazi ndio maana kila mwaka mvua inanyesha m, wanyama wanazaliwa na matunda yanazaa, asili inapatikana. Haikuhitaji wew kuwa na jembe ili upate rizki.
Kumbe life is just simple, we just need to live.. 😂
 
Halafu hapa duniani unaweza ukakuta niko peke angu na kila ninachokiona kinatokea ni uongo mtupu.. Halafu unaweza ukakuta hakuna hata mpuuzi yoyote anaitwa Mama Samia..
 
Fikra za mkosaji mtu aliekata tamaa, kwa ushauri wangu, jikite zaidi kwa utafutaji issue za kufa mwachie israel mtoa roho anafanye kazi yake.
Aliye Kata tamaa? 😂
Mpaka wa kina Elon musk, wanatafuta maana mpaka wanakwenda sayari tofauti, mpaka wanatengeneza neural link kwa ajili ya kuongeza lifespan alaf wewe unasema nini?
 
Hii kitu nilishaiwaza kitambo binafsi naonaga maisha hayana maaana. Unajikuta unatafuta hela mwisho wake unakufa. Na hata kuowa sijui kuwa na familia mtu anakwambia jitahidi upate waalu mtoto uache jina sasa mimi nikishakufa hilo jina litanisaidia nini mimi na tayari sipo duniani
 
Mungu katika Quran tukufu anasema:
( 29:64)
"Wa maa haadhihil-hayaatud-dunyaa illaa lahwun wa la'ib, wa innad-daaral-aakhirata lahiyal-hayawaan, law kaanuu ya'lamuun"

Kwa kiswahili:

“Na maisha haya ya dunia si chochote ila ni mchezo na pumbao. Na hakika nyumba ya Akhera ndiyo maisha halisi, laiti wangekuwa wanajua.”
 
Mungu anasema kupitia Quran tukufu:
(3:185)

"Wa mal-hayaatud-dunyaa illaa mataa'ul-ghuruur."

Maana:
“Na maisha ya dunia si chochote ila ni starehe ya udanganyifu.”
 
Sijui kuhusu Umri wako, sijui kuhusu Dini Yako ila kama hiki ulichoandika linatoka ndani ya Moyo wako mwenyewe...! Soon you will have encounters with God....!

Kabla Mungu kukutana na Watu wake Huwa anaanza kupandikiza mawazo aina hii ndani ya mind zao.
Ki ukweli kama tunazaliwa tunajua, tunaoa then tunakufa hafu basi, ujue haya Maisha hayana maana ya yoyote, lakini kama baada ya kufa Kuna Maisha mengine, hapo ndipo unapata maana nzima ya Maisha.

Rasta Huwa wanaamini Binadamu hafi, Wakristo wanaamini japo Binadamu Kuna siku atakufa lakini baada ya kufa Kuna Maisha mengine, na wengine Binadamu hafi ila anabadirisha makazi, baada ya miaka yakuishi hapa Duniani ikiisha, yule mtu wa ndani ambaye hasa ndiye wewe, anataka kwenye Mwili wako (Kitendo kinachoitwa kufa japo mtu wa ndani Huwa hafi) na kwenda kuendelea kuishi kwenye Ulimwengu mwingine, na Matendo yake akiwa hapa Duniani ndiyo yataamua kwenda Kuzimu kusubiria Hukumu ama kwenda Paradiso kusubilia siku ya Mwisho.
Kuzimu unapajua mkuu? Na Paradiso je?
 
Alitetuumba anasema kupitia Quran tukufu
(87:16:17)
"Bal tu'thiruunal-hayaatad-dunyaa.Wal-aakhiratu khayrun wa abqaa."

Maana:
“Bali nyinyi mnapendelea maisha ya dunia, hali ya kuwa Akhera ni bora na inadumu zaidi.”
 
Halafu hapa duniani unaweza ukakuta niko peke angu na kila ninachokiona kinatokea ni uongo mtupu.. Halafu unaweza ukakuta hakuna hata mpuuzi yoyote anaitwa Mama Samia..
Hahahaha mama Samia ni muunganiko wa celi tu mkuu nazo ikawa mwili wa mifupa na nyama, plus brain activity inayo fanya awe mama samia
 
Hoja unayo, almuradi Usiwe “suicidal”

Maana conclusion yake kubwa ni kijiuwa, hilo usifanye. Lakini hoja yako ni fikirishi sana.

Majibu yake utapewa lazima yatakuwa “spiritual”,

Na hiyo sintofahamu ya kuhusu dhumuni la maisha, ndo maana kumetokea ama kupelekea uwepo wa dini na imani mbali mbali kwamba kuna maisha baada ya haya hapa duniani.
Na ni dini pekee ndio itakupa kusudio la kwanini tupo hapa duniani

Je,unadhani tuliuumbwa kwa mchezo mchezo tu tufanye hii daily routine daily?

Hapana kuna big purpose zaidi ya hii,kuna maisha mengine ambayo ni tifauti na haya na kikubwa zaidi hayo maisha yajayo foundation yake inaanzia hapa
 
Hoja unayo, almuradi Usiwe “suicidal”

Maana conclusion yake kubwa ni kijiuwa, hilo usifanye. Lakini hoja yako ni fikirishi sana.

Majibu yake utapewa lazima yatakuwa “spiritual”,

Na hiyo sintofahamu ya kuhusu dhumuni la maisha, ndo maana kumetokea ama kupelekea uwepo wa dini na imani mbali mbali kwamba kuna maisha baada ya haya hapa duniani.
OK, na siko suicidal kabisa mkuu

Spiritual aspect inasaidia sana, japo nayo haikupi majibu ya moja kwa moja
 
Na ni dini pekee ndio itakupa kusudio la kwanini tupo hapa duniani

Je,unadhani tuliuumbwa kwa mchezo mchezo tu tufanye hii daily routine daily?

Hapana kuna big purpose zaidi ya hii,kuna maisha mengine ambayo ni tifauti na haya na kikubwa zaidi hayo maisha yajayo foundation yake inaanzia hapa
Unaweza kuelezea kwa mapana kuhusu mafia yako mkuu?
 
Hii kitu nilishaiwaza kitambo binafsi naonaga maisha hayana maaana. Unajikuta unatafuta hela mwisho wake unakufa. Na hata kuowa sijui kuwa na familia mtu anakwambia jitahidi upate waalu mtoto uache jina sasa mimi nikishakufa hilo jina litanisaidia nini mimi na tayari sipo duniani
Quran imasema"
"Al-maalu wal-banuuna ziinatul-hayaatid-dunyaa, wal-baaqiyaatus-swaalihaatu khayrun 'inda Rabbika thawaaban wa khayrun amala."

Maana:
“Mali na watoto ni mapambo ya maisha ya dunia. Na matendo mema yenye kubaki ndiyo bora mbele ya Mola wako kwa malipo na bora kwa matumaini.”
 
OK, na siko suicidal kabisa mkuu

Spiritual aspect inasaidia sana, japo nayo haikupi majibu ya moja kwa moja
Majibu ya moja kwa moja yapo kaka na yapo wazi kabisa.
Tatizo tunachagua vitabu vya kusoma,
Kiukweli me sifahamu imani yako ila nakushauri,tenga muda thn tafuta ule msahafu wa Quran wenye tafsiri ya kiswahili,kaa utulie soma hicho kitabu,hayo unayoyawaza yote utashangaa ulichelewa wapi kuyajua.
YAle ni maneno halisi ya Mungu,so kule Mungu ndo ametoa jibu kwanini tupo hapa na baada ya hapa wapi tunaenda...usiumize kichwa mkuu kaa usome.
Me nakuunga mkono na hata Quran inaunga mkono kwamba "Maisha ya Dunia si chochote" ila yapo maisha bora zaidi ila siyo haya,haya maisha ni pumbao/upuuzi
 
Maisha ni matamu iwapo una resources. Changamoto ni resources, haya mambo ya uchumi, nchi, pesa sijui ulinzi ni uhaba wa resources otherwise maisha ni matamu mno.
 
Maisha ni matamu iwapo una resources. Changamoto ni resources, haya mambo ya uchumi, nchi, pesa sijui ulinzi ni uhaba wa resources otherwise maisha ni matamu mno.
Maisha ni matamu kwa vipindi vifupi vifupi,utamu wa vipindi...hapa Duniani hakunaga utamu wa moja kwa moja haijalishi wewe ni Tajiri kupindukia au maskini uliyepitiliza...tusidanganyane,tembea uone mkuu ili ujue mambo yalivyo,aliyeumba hii Dunia anakwambia "Hii Dunia si chochote ila ni starehe za udanganyifu"...aliyeumba ndo anasema hivyo na ukitazama ni kweli kabisa na ndicho alichokiona mtoa mada....amewaza pakubwa sana japo majibu yote yapo katika Quran tukufu.
 
Back
Top Bottom