Maisha: Changamoto za kuzaa nje ya ndoa

Maisha: Changamoto za kuzaa nje ya ndoa

Sometimes Taarifa ni muhimu.. Umeamua kufanya unavyotaka, niambie Putin nmepata MTU ,mie nawewe basi.


Masuala ya kufanya upotezaji wa muda na hali ,hutia Hasira sana.

Sasa huoni matokeo yake yanamfanya mtoa mada awe ktk njia panda, asijue mtoto niwake au lah?



Kwa maelezo ya upande mmoja alotoa mtoa mada...nikwamba, Demu ni Muhuni .
Mkuu,na nimetoa machache tu ningeeleza kila kitu pangehitaji episode kama tatu au nne za namna hii,na nilijua naweza kumbadili kwa kumpa mahitaji mhimu pale nilipoambiwa story zake kwa mara ya kwanza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa kuna kitu cha kujifunza sisi wanaume.Kuna kufanywa wewe kuwa mtumwa ni bora kutulia kwako.
 
Yaani nimemaliza kukutengenezea mazingira ya kujihifadhi ndani ya mwezi mmoja hujui nitakuja lini?real???
Na nimetoka kufanya jambo jingine ndani ya miezi mitatu kwa baba yako mzazi??harafu usijue nakuja lini??
Dah tuwe waungwana jamani japo kidogo basi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa hiyo ulipanga kumfanya mtoto wa watu mchepuko wa kudumu?
 
Mkuu ulikuwa na haha gani ya kunishambulia hivyo?? Hapa ni MMU tunaaswa kupendana kuwa marafiki wakati wote. Neno dogo linatumika kama utani tu na pengine kujenga mahusiano tu kwa kuwa hatudahamiani.

We ni baba wa watoto watatu uwe na adabu basi. Asante.
"Dogo" kwa wengine ni dharau kubwa sana Sababu hunijui hata kidogo!! mimi nimechukulia ni dharau kubwa sana!! Huo utani unaweza tania Unao waona huko mtaani kwako sio usiemjua
 
Mkuu,na nimetoa machache tu ningeeleza kila kitu pangehitaji episode kama tatu au nne za namna hii,na nilijua naweza kumbadili kwa kumpa mahitaji mhimu pale nilipoambiwa story zake kwa mara ya kwanza.

Sent using Jamii Forums mobile app
Watakao kuelewa ni wachache mzee ila huyo mwanamke hafai,kwa jitihada ulizo zieleza nimeamini kabisa kuwa huyo ni cha wote na wala hafai kuwa mke wala hawala zaidi ya mengine ni kukuletea matatizo.
Wanawake wazuri wana matatizo sana,ila huruma huwa inakuja tu pale unapobaini kuwa ana kiumbe chako tumboni.

Hayo mambo ya kuwa na michepuko tusilaumiane hasa kwa sisi wanaume,Haya mambo yapo na yataendelea,kikubwa mwangalie mtoto na pale akihitaji kitu msaidie kwa kumtazama mtoto,Hawa viumbe wana matatzo yao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watakao kuelewa ni wachache mzee ila huyo mwanamke hafai,kwa jitihada ulizo zieleza nimeamini kabisa kuwa huyo ni cha wote na wala hafai kuwa mke wala hawala zaidi ya mengine ni kukuletea matatizo.
Wanawake wazuri wana matatizo sana,ila huruma huwa inakuja tu pale unapobaini kuwa ana kiumbe chako tumboni.

Hayo mambo ya kuwa na michepuko tusilaumiane hasa kwa sisi wanaume,Haya mambo yapo na yataendelea,kikubwa mwangalie mtoto na pale akihitaji kitu msaidie kwa kumtazama mtoto,Hawa viumbe wana matatzo yao

Sent using Jamii Forums mobile app
Amina sana mkuu,yule mtoto nampenda sana,ukizingatia ndiyo mtoto wa kike pekee maana nina watoto watatu wa kiume kwa mke wangu.
Natamani nimchukue nimpeleke kwa mama yangu sema bado kadogo only three yrs,angalau afikishe mitano basi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Poleni na changamoto za kujikinga na corona,kwa kuzingatia maelekezo ya wataalamu wa afya tutashinda hili janga,na hili nalo litapita.

Naomba nijielekeze kwenye mada,
Nimekaa na hili moyoni kwa miaka mitatu lakini leo nimeona niwashirikishe wanaJF ili kubadilishana mawazo, hii ni baada ya kupigiwa simu na mzazi mwenzangu nikiambiwa mwanangu anaumwa lakini utata wa gharama za matibabu nimejikuta nawaza matukio ya nyuma kidogo.

Huyu mzazi mwenzangu nilikutana naye mwaka 2016 nikiwa katika harakati zangu za maisha ya hapa na pale huko wilayani Biharamlo. Binti nilimuelewa maana ni kisu balaa; kwa wakware wenzangu shingo lazima uigeuze.

Mwaka huo nilikuwa napiga harakati za migodini huko Nzega mkoani Tabora, binti hakuchomoa tukaanza mahusiano ile kumegana kisela. Nilimjuza kama nina familia lakini sikuweza kumwambia wapi familia yangu iliko jambo ambalo leo naiona faida yake.

Basi bwana mimi nikamaliza mishemishe zangu zilizonipeleka Biharamlo nikamuaga nikaondoka tukaendelea kuwasiliana. Baada ya mwezi mmoja akaniambia amenasa mimba nilipochekecha takwimu sikupinga nikasema sawa nitakuhudumia.

Tukaendelea kuwasiliana na kumtumia kila akihitaji huduma za hapa na pale. Ukafika wakati wa kujifungua, akajifungua salama mtoto wa kike. Baada ya muda akaniambia mtoto analia sana kwa tamaduni zetu nilijua pengine analilia jina basi nikamweleza cha kufanya na nikamwambia ampe jina la mama yangu mzazi, akafanya hivyo na tatizo la kulia likakoma mara moja.

Baada ya miezi mitatu akataka sana nikamuone mtoto basi bila hiyana nikaweka ratiba vizuri nikatembea mpaka huko kwao. Kwa kuwa nilishatambulishwa kwa baba yake wala haikuwa shida kufikia kwao, japo nilikuwa sijawahi kufika nyumbani kwao kwa muda ambao tulifahamiana.

Basi bwana nimefika kwao wakafanya kila liwezekanalo kuhakikisha napata mapokezi mazuri kama mkwe na mgeni. Hali ya kiuchumi pale nyumbani ilikuwa ya chini sana yaani maisha ya tabu kidogo na ni kijijini nikawa najiuliza mbona mama mtoto wangu anaonekana wa kishua sana kumbe huku nyumbani anaishi maisha haya!!

Kwangu haikuwa changamoto kwa kuwa nimetokea maisha duni pengine kuliko hata yale sema ilikuwa suprise tu kulingaa na alivyo baby mama. Kwa kuwa pesa nilikuwa nayo na nilipewa mapokezi mazuri huku nilikuwa sijawahi hata kujitambulisha basi nikashawishika kufanya mambo makubwa kidogo ili nikitoka angalau niache heshima pale nyumbani na hapo kijijini.

Mzee alikuwa anaishi kwenye nyumba ya udongo ila imeezekwa kwa bati(16) mgogo wa tembo.Nyumba ilikuwa imechanika na ilikuwa haijapigwa lipu na mzee alikuwa mgonjwa wa TB basi kwa mazingira yale nikiona kama ni hatari kwa afya yake nikashawishika kumboreshea kidogo.

Nikaenda sentani (mjini) nikahemea mazagazaga kibao kama ngano, sukari, mafuta, mahindi na mchele kisha nikaongea na shemeji yangu (kaka wa baby mama)akatafuta mafundi na tofari kiasi ile nyumba ikafumuliwa sehemu ilipochanika ufa kisha ikajengwa vizuri ikasakafiwa nje ndani, baada ya kumalizika mzee alishukuru sana.

Jioni moja nikiwa natembea tembea kubarizi upepo na kuona mazingira nikamuona kijana mmoja nikamshawishi kwa kumpa 10,000/= ili anipe dondoo kidogo kuhusu mwenendo wa baby mama wangu. Jamaa kwanza akaniuliza kama nimempenda huyo dada kiukweli kutoka moyoni baada ya kumjibu ndipo akanishushia full data kuhusu baby mama.

Kwanza akanieleza huyo dada ni miongoni mwa warembo wanaozunguka kila mkoa kufuata mabwana, akimpata wa Singida basi ataenda mpaka huko, akimpata dereva atatembea naye safari zote yaani kwa kifupi husafiri kwenda kujiuza popote nchini na alikuwa ameolewa na askari ambaye amezaa naye watoto wawili (wapo kwa baba yao) lakini kwa tabia za umalaya wa yule binti askari alichomoa.

Jamaa alinieleza mengi mpaka mwili ukaishiwa nguvu lakini nikajikaza kiume nikamshukuru yule kijana kisha akaahidi kunipa data kadri inavyowezekana na akanisihi sana kama nina mpango kumuoa nisitishe kabisa. Nikarudi hapo nyumbani jioni ile, sikuonesha dalili za chochote nilichoelezwa. Usiku ule nikamtaarifu kwamba ningeliondoka kesho yake, kulipokucha nikaanza safari ya kurudi.

Nikamwachia pesa ya matumizi baby mama wangu nikaondoka. Tukaendelea kuwasiliana kama kawaida. Baada ya miezi kadhaa siku moja akanipigia simu kwamba wamezinguana na mzee wake amemtimua na yupo kwa kaka yake.

Mzee aliwakatia plots watoto wake wote akaniambia kama naweza nimjengee hata kislop kwenye plot yake. Nikajishauri sana pamoja na mawazo ya wadau na nilipomfikiria mwanangu ataishi mazingira gani basi nikafikia uamzi wa kukubali kumjengea. Nikamwambia atafute mafundi niongee nao nikawambia watafute tofari za kununua, mawe na material mengine nikawatumia 1.2M nyumba ikanyanyuka slop ya bati 10. Ilijengwa kwa wiki moja tu na ikakamilika kabisa kila kitu.

Katika mafundi wale walioijenga kuna fundi mmoja nilimuona ni mstaarabu basi kwa kuwa nina dondoo za hapo awali za baby mama nikamshawishi kunipa kila kinachoendelea huko. Baada tu ya mwezi mmoja tangu nyumba yake iishe kisha kuhamia baby mama akapata bwana mwingine kijana mmoja mponda kokoto akaanza kujilia mzigo tena na kulala hapohapo kwenye geto nililomjengea. Habari zote nilipewa na yule jamaa yangu fundi pamoja na yule kijana wa mwanzo.

Basi nikapanga safari ya kushtukiza ili nikajionee na kwa muda wote huo baby mama sikuwahi kumuuliza chochote. Nikasafiri kimyakimya mpaka huko nikafika jioni saa moja moja jioni. Kufika kwanza akastuka sana hapo jamaa yake hakuwepo labda alikuwa bado yupo kwake maana alikuwa na mji pia. Nikafika nikamuomba simu yake nikaizima then nikampa ya kwangu amulikie, akapika tukala tena nikiwa happy nikamsifia kwamba nyumba yake imejengwa vizuri.

Usiku baada ya kula ndipo nikaanza kumuuliza kuhusu huyo bwana yake akagoma kunipa ushirikiano. Nikamuomba namba za huyo bwana yake akagoma nikamzaba kibao kimoja cha kimataifa akaona nyotanyota akaniambia jina la namba lilivyoseviwa. Nikampigia jamaa kiustaarabu sana kwanza nikajitambulisha kwamba mimi ni nani kwa huyo mwanamke wake na nikamweleza namna ninavyomfahamu yeye mshikaji kwa kila kitu (nilikuwa na data zote)kuhusu yeye. Jamaa kafunguka bila kuacha hata nukta na akasema kipindi kijumba hicho kinajengwa aliambiwa pesa alipewa na mjomba wake mstaafu alikuwa mtumishi wa serikali ndiyo zimejenga hicho kijumba. Yote hayo jamaa aliongea simu ikiwa loud speaker, nilimshukuru kwa ushirikiano.

Usiku ule nilimpiga nusura nimuue, badaye nikaona nitapata kesi hivyo kulipokucha nikawapigia mafundi waje wabomoe hicho kijumba wakisambaze kabisa. Kweli asubuhi na mapema mafundi wakafika, kabla hawajaanza kubomoa baby mama akatoka muda kidogo akarudi na maaskali wawili. Ile wamefika wakaamuru mafundi washuke chini(walikuwa wameshaanza kutoa misumali ya bati).

Kwa kutii sheria nikawaambia maaskari wakae niwape picha kwa ufupi. Wakashauri maelekezo nikawape kituoni, tukapanda pikipiki kuelekea kituoni tulipofika kabla ya yote nikawaomba wamuweke ndani kwanza mwanamke kabla ya yote maana yeye ndiye alistahili kukaa ndani na siyo mimi. Nikawapa dokezo kisha wakamtia ndani ndipo nikawapa mkanda mzima maafande walishangaa sana, wakatuma wapelelezi kule kijijini ili kujiridhisha ukweli wa maelezo yangu. Kukuta ni kweli tupu basi baby mama wakampa kipondo na kumtukana sana kwa kuhatarisha maisha maana nilingeliweza kufanya chochote cha hatari kama bwana yake ningemkuta ndani na kwa bahati nzuri hiyo siku hakuja sijui nani alimtonya.

Basi ilipofika saa kumi na moja jioni yule mkuu wa kituo akanisihi sana nimwachie tu na yote niliyafanya kwa kipindi chote ibaki kumbukumbu kwa mwanangu. Kweli nikawambia wamuachie cha ajabu anatoka ndani na majeraha yake akaomba hela ya mboga, na ikumbukwe kipindi nampiga usiku alikiri kosa na kuomba nimsamehe tu kila mara "baba Mai nisamehe nakupenda ni umalaya tu"

Jioni hiyo niliwaaga ndugu zake na walinishukuru kwa moyo huo wa uvumilivu nikaondoka jioni ileile hata sikulala hapo tena. Baada ya hapo sikuwasiliana naye kwa mwaka mzima, nilimpiga block kila sehemu kwa bahati mbaya hakuwa anajua kwangu wala sehemu ninayofanyia kazi.

Alikuja kunitafuta baada ya mtoto kuugua degedege sijui namba alipata wapi, nikamtumia hela akamtibu mtoto na ukawa mwanzo wa mawasiliano lakini alikuwa akinitafuta pale tu mtoto akiwa anaumwa.

Mpaka hii juzi baada ya kunipa summery ya matibabu ambayo kiuhalisia yalikuwa feki. Kutongoza tongoza huku kumenipitisha kwenye changamoto lukuki na huyu baby mama. Kuzaa nje wadau mnatatuaje hizi changamoto na hawa wazazi wenzenu?

NB: Nimefupisha mambo mengi na kuweka baadhi ya code maana dunia kijiji.

Asanteni.
mimi nimezaliwa nje ya ndoa cha moto nilikiona isee,yani nimetoboa kimungumungu tu
 
Sasa wewe mkuu unamlaa mkeooo alafu mchepukooo akae na ugwaduuu tuu[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji23][emoji23] Pesa sio kila kitu mkuuu hata kama ungempa Bil 1 keshoo angetafutaa wa kumtoa genyeee tuuu yaniii its nature mzee...!! Ukimfanyia mazuri fanya kwa manufaa ya mtoto wako zaidi sio yeye maana huyo sio wakooo...

Sent using Jamii Forums mobile app
Sikupingi brother.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alafu basi nenda ugongewe huko, wewe unagongewa kabisa kwa Nyumba ya Mzazi mwenzio , tena aliye hai, na unayemtegemea kuja kwako kadiri ya Mahitaji yenu.???



Dharau zilizopitiliza.
Ni ajabu sana,basi olewa kabisa funga hicho kijumba basi lakini hata mwezi haujaisha unaweka mwanaume ndani huku unajua muda wowote jamaa sponsor anaweza kuja? ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Meru A, kwanza nikushukuru kwa kutushirikisha mkasa huu, tunapata cha kujifunza wana MMU. Nimejifunza kwamba;

1. Kuchepuka kunakuletea matatizo, fadhaa na kukosa raha

2. Mbwa kala mbwa maana na wewe ulikuwa unatembea nje ya ndoa so akitembea nje ya mahusiano ni ngoma droo. Unaona jinsi inavyouma?? Je wewe mbona unamsaliti mkeo??
3. Jana nilitoa thread inayoonesha madhara ya kutelekeza watoto.... wewe umekuwa mfano wa kweli na jinsi inavyotesa hasa unapoona mwanao yuko mafichoni huko na huthubutu kumwonesha kwa ndigu na jamaa.

4. Si kila king'aacho ni dhahabu...ulimuona demu akiwa mzuri kumbe anakotoka ni hohehahe na anaishi kwa kuuza nyapu kwa mtu yeyote na popote. Mwanzo ulimuona ni kifaa.

5.Tutulie ndani ya ndoa zetu ndiko kuna furaha na raha ya kweli. Hizo gharama ulizotumia kusafiri na kujenga kuhudumia ....fikiria ungempa mkeo akazitumia angekulipa fadhila kiasi gani?? Achilia mbali hiyo nyumba ya slop kumi ungeijenga kula Chamanzi Mbagala ingekuwa kitega uchumi cha kudumu.

Yangu ni hayo tu.
Sikupingi mkuu,upo sahihi na nimejifunza kwa kweli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom