Maisha: Changamoto za kuzaa nje ya ndoa

MeruA

JF-Expert Member
Aug 9, 2017
1,391
2,123
Poleni na changamoto za kujikinga na corona,kwa kuzingatia maelekezo ya wataalamu wa afya tutashinda hili janga,na hili nalo litapita.

Naomba nijielekeze kwenye mada,
Nimekaa na hili moyoni kwa miaka mitatu lakini leo nimeona niwashirikishe wanaJF ili kubadilishana mawazo, hii ni baada ya kupigiwa simu na mzazi mwenzangu nikiambiwa mwanangu anaumwa lakini utata wa gharama za matibabu nimejikuta nawaza matukio ya nyuma kidogo.

Huyu mzazi mwenzangu nilikutana naye mwaka 2016 nikiwa katika harakati zangu za maisha ya hapa na pale huko wilayani Biharamlo. Binti nilimuelewa maana ni kisu balaa; kwa wakware wenzangu shingo lazima uigeuze.

Mwaka huo nilikuwa napiga harakati za migodini huko Nzega mkoani Tabora, binti hakuchomoa tukaanza mahusiano ile kumegana kisela. Nilimjuza kama nina familia lakini sikuweza kumwambia wapi familia yangu iliko jambo ambalo leo naiona faida yake.

Basi bwana mimi nikamaliza mishemishe zangu zilizonipeleka Biharamlo nikamuaga nikaondoka tukaendelea kuwasiliana. Baada ya mwezi mmoja akaniambia amenasa mimba nilipochekecha takwimu sikupinga nikasema sawa nitakuhudumia.

Tukaendelea kuwasiliana na kumtumia kila akihitaji huduma za hapa na pale. Ukafika wakati wa kujifungua, akajifungua salama mtoto wa kike. Baada ya muda akaniambia mtoto analia sana kwa tamaduni zetu nilijua pengine analilia jina basi nikamweleza cha kufanya na nikamwambia ampe jina la mama yangu mzazi, akafanya hivyo na tatizo la kulia likakoma mara moja.

Baada ya miezi mitatu akataka sana nikamuone mtoto basi bila hiyana nikaweka ratiba vizuri nikatembea mpaka huko kwao. Kwa kuwa nilishatambulishwa kwa baba yake wala haikuwa shida kufikia kwao, japo nilikuwa sijawahi kufika nyumbani kwao kwa muda ambao tulifahamiana.

Basi bwana nimefika kwao wakafanya kila liwezekanalo kuhakikisha napata mapokezi mazuri kama mkwe na mgeni. Hali ya kiuchumi pale nyumbani ilikuwa ya chini sana yaani maisha ya tabu kidogo na ni kijijini nikawa najiuliza mbona mama mtoto wangu anaonekana wa kishua sana kumbe huku nyumbani anaishi maisha haya!!

Kwangu haikuwa changamoto kwa kuwa nimetokea maisha duni pengine kuliko hata yale sema ilikuwa suprise tu kulingaa na alivyo baby mama. Kwa kuwa pesa nilikuwa nayo na nilipewa mapokezi mazuri huku nilikuwa sijawahi hata kujitambulisha basi nikashawishika kufanya mambo makubwa kidogo ili nikitoka angalau niache heshima pale nyumbani na hapo kijijini.

Mzee alikuwa anaishi kwenye nyumba ya udongo ila imeezekwa kwa bati(16) mgogo wa tembo.Nyumba ilikuwa imechanika na ilikuwa haijapigwa lipu na mzee alikuwa mgonjwa wa TB basi kwa mazingira yale nikiona kama ni hatari kwa afya yake nikashawishika kumboreshea kidogo.

Nikaenda sentani (mjini) nikahemea mazagazaga kibao kama ngano, sukari, mafuta, mahindi na mchele kisha nikaongea na shemeji yangu (kaka wa baby mama)akatafuta mafundi na tofari kiasi ile nyumba ikafumuliwa sehemu ilipochanika ufa kisha ikajengwa vizuri ikasakafiwa nje ndani, baada ya kumalizika mzee alishukuru sana.

Jioni moja nikiwa natembea tembea kubarizi upepo na kuona mazingira nikamuona kijana mmoja nikamshawishi kwa kumpa 10,000/= ili anipe dondoo kidogo kuhusu mwenendo wa baby mama wangu. Jamaa kwanza akaniuliza kama nimempenda huyo dada kiukweli kutoka moyoni baada ya kumjibu ndipo akanishushia full data kuhusu baby mama.

Kwanza akanieleza huyo dada ni miongoni mwa warembo wanaozunguka kila mkoa kufuata mabwana, akimpata wa Singida basi ataenda mpaka huko, akimpata dereva atatembea naye safari zote yaani kwa kifupi husafiri kwenda kujiuza popote nchini na alikuwa ameolewa na askari ambaye amezaa naye watoto wawili (wapo kwa baba yao) lakini kwa tabia za umalaya wa yule binti askari alichomoa.

Jamaa alinieleza mengi mpaka mwili ukaishiwa nguvu lakini nikajikaza kiume nikamshukuru yule kijana kisha akaahidi kunipa data kadri inavyowezekana na akanisihi sana kama nina mpango kumuoa nisitishe kabisa. Nikarudi hapo nyumbani jioni ile, sikuonesha dalili za chochote nilichoelezwa. Usiku ule nikamtaarifu kwamba ningeliondoka kesho yake, kulipokucha nikaanza safari ya kurudi.

Nikamwachia pesa ya matumizi baby mama wangu nikaondoka. Tukaendelea kuwasiliana kama kawaida. Baada ya miezi kadhaa siku moja akanipigia simu kwamba wamezinguana na mzee wake amemtimua na yupo kwa kaka yake.

Mzee aliwakatia plots watoto wake wote akaniambia kama naweza nimjengee hata kislop kwenye plot yake. Nikajishauri sana pamoja na mawazo ya wadau na nilipomfikiria mwanangu ataishi mazingira gani basi nikafikia uamzi wa kukubali kumjengea. Nikamwambia atafute mafundi niongee nao nikawambia watafute tofari za kununua, mawe na material mengine nikawatumia 1.2M nyumba ikanyanyuka slop ya bati 10. Ilijengwa kwa wiki moja tu na ikakamilika kabisa kila kitu.

Katika mafundi wale walioijenga kuna fundi mmoja nilimuona ni mstaarabu basi kwa kuwa nina dondoo za hapo awali za baby mama nikamshawishi kunipa kila kinachoendelea huko. Baada tu ya mwezi mmoja tangu nyumba yake iishe kisha kuhamia baby mama akapata bwana mwingine kijana mmoja mponda kokoto akaanza kujilia mzigo tena na kulala hapohapo kwenye geto nililomjengea. Habari zote nilipewa na yule jamaa yangu fundi pamoja na yule kijana wa mwanzo.

Basi nikapanga safari ya kushtukiza ili nikajionee na kwa muda wote huo baby mama sikuwahi kumuuliza chochote. Nikasafiri kimyakimya mpaka huko nikafika jioni saa moja moja jioni. Kufika kwanza akastuka sana hapo jamaa yake hakuwepo labda alikuwa bado yupo kwake maana alikuwa na mji pia. Nikafika nikamuomba simu yake nikaizima then nikampa ya kwangu amulikie, akapika tukala tena nikiwa happy nikamsifia kwamba nyumba yake imejengwa vizuri.

Usiku baada ya kula ndipo nikaanza kumuuliza kuhusu huyo bwana yake akagoma kunipa ushirikiano. Nikamuomba namba za huyo bwana yake akagoma nikamzaba kibao kimoja cha kimataifa akaona nyotanyota akaniambia jina la namba lilivyoseviwa. Nikampigia jamaa kiustaarabu sana kwanza nikajitambulisha kwamba mimi ni nani kwa huyo mwanamke wake na nikamweleza namna ninavyomfahamu yeye mshikaji kwa kila kitu (nilikuwa na data zote)kuhusu yeye. Jamaa kafunguka bila kuacha hata nukta na akasema kipindi kijumba hicho kinajengwa aliambiwa pesa alipewa na mjomba wake mstaafu alikuwa mtumishi wa serikali ndiyo zimejenga hicho kijumba. Yote hayo jamaa aliongea simu ikiwa loud speaker, nilimshukuru kwa ushirikiano.

Usiku ule nilimpiga nusura nimuue, badaye nikaona nitapata kesi hivyo kulipokucha nikawapigia mafundi waje wabomoe hicho kijumba wakisambaze kabisa. Kweli asubuhi na mapema mafundi wakafika, kabla hawajaanza kubomoa baby mama akatoka muda kidogo akarudi na maaskali wawili. Ile wamefika wakaamuru mafundi washuke chini(walikuwa wameshaanza kutoa misumali ya bati).

Kwa kutii sheria nikawaambia maaskari wakae niwape picha kwa ufupi. Wakashauri maelekezo nikawape kituoni, tukapanda pikipiki kuelekea kituoni tulipofika kabla ya yote nikawaomba wamuweke ndani kwanza mwanamke kabla ya yote maana yeye ndiye alistahili kukaa ndani na siyo mimi. Nikawapa dokezo kisha wakamtia ndani ndipo nikawapa mkanda mzima maafande walishangaa sana, wakatuma wapelelezi kule kijijini ili kujiridhisha ukweli wa maelezo yangu. Kukuta ni kweli tupu basi baby mama wakampa kipondo na kumtukana sana kwa kuhatarisha maisha maana nilingeliweza kufanya chochote cha hatari kama bwana yake ningemkuta ndani na kwa bahati nzuri hiyo siku hakuja sijui nani alimtonya.

Basi ilipofika saa kumi na moja jioni yule mkuu wa kituo akanisihi sana nimwachie tu na yote niliyafanya kwa kipindi chote ibaki kumbukumbu kwa mwanangu. Kweli nikawambia wamuachie cha ajabu anatoka ndani na majeraha yake akaomba hela ya mboga, na ikumbukwe kipindi nampiga usiku alikiri kosa na kuomba nimsamehe tu kila mara "baba Mai nisamehe nakupenda ni umalaya tu"

Jioni hiyo niliwaaga ndugu zake na walinishukuru kwa moyo huo wa uvumilivu nikaondoka jioni ileile hata sikulala hapo tena. Baada ya hapo sikuwasiliana naye kwa mwaka mzima, nilimpiga block kila sehemu kwa bahati mbaya hakuwa anajua kwangu wala sehemu ninayofanyia kazi.

Alikuja kunitafuta baada ya mtoto kuugua degedege sijui namba alipata wapi, nikamtumia hela akamtibu mtoto na ukawa mwanzo wa mawasiliano lakini alikuwa akinitafuta pale tu mtoto akiwa anaumwa.

Mpaka hii juzi baada ya kunipa summery ya matibabu ambayo kiuhalisia yalikuwa feki. Kutongoza tongoza huku kumenipitisha kwenye changamoto lukuki na huyu baby mama. Kuzaa nje wadau mnatatuaje hizi changamoto na hawa wazazi wenzenu?

NB: Nimefupisha mambo mengi na kuweka baadhi ya code maana dunia kijiji.

Asanteni.
 
Pole....kisa chako kizuri na unajua kusimulia pia uandishi hauchoshi kusoma

Hakukuwa na haja ya kumpiga wakati we mwenyewe una familia sasa ulitaka yeye akatulizie wapi mihemko na wewe muda mwingi upo kwa mkeo? We endelea kumtumia matumizi baby mama sababu ya mtoto wenu hata kwa Mara moja baada ya kila week 8.
 
Duh! Basi hawa watu ndio walivyo kumbe! Yaani ungesema ni Ushirombo halafu ukasema ni Mtoto wa kiume hahahaha ningekutajia jina kabisa. Yote uliyoyaandika yanafanana kabisa na huyo Dada. Labda kama umebadili hizo taarifa mbili.

Wanawake ndio walivyo, yaani jamaa alinisimulia hivyo hivyo, tofauti ni hizi tu na kwamba yeye hakwenda polisi aliamua kukaa kimya tu.

Mshkaji alikua anafunga safari kabisa anaenda ushirombo Kahama huko anakaa hapo kumbe demu ni mke wa MTU. Akabeba mimba akajifungua duh jamaa analea na huyu nae analea.

Wanaume tuna majanga aiseeee. UKIMWI utatumaliza, jamaa alinitumia hadi picha ya demu, ni mkali, ni chombo, akiniruhusu nitaitafuta niiweeke hapa.
 
Aiseeh mimi nipo makini Broo!! Kwanza Siwezi Kujenga Ukweni Hiyo ni never iwe kwa mke au kwa mtu niliyezaa nae pembeni!! kama walishindwa kujenga kipindi hicho Mimi ni mwema kiasi gani mpaka niwajengee hata iwe choo sijengi.Maana nina mifano Mingi ya watu waliokua wema waliofanya makubwa ukweni au kwa michepuko au wake wadogo mwisho wa siku wamekua Fu**ked😀 pamoja na wema wote walioonesha!! Hivo ni vitu ambavo sitakuja kufanya ni big mistake!! Hiyo hela wekeza kwa Ajili ya watoto wako Tu( wapate elimu bora,wapeleke national parks, wafurahi kuna baba) sio sijui kumjengea mke au mchepuko huko ni matumizi mabaya sana ya fedha!!

Pili huwa sinaga garantii ya kuwa mwanamke yoyote ninaeishi nae atakua wangu nikampa asilimia zote Never hata iwe mke wangu huwa naishi nae mguu ndani mguu nje!! Kingine sitaki mwanamke aniletee shida katika maisha yangu Nikiwa na msemo kwamba sijazaliwa nae.

Tatu Maisha nitakayoyajenga ni kwa ajili ya watoto wangu na Nitafocus kwa watoto tu maana hao ndio ndugu zangu!!
Brazaa hawa wanawake ambao leo uko nao kesho yupo na mwingine Dont give a chance akusome hata awe mke wako kuwa mtu usie eleweka!! Maana thamani yako wewe ni ukiwa hai na mwenye afya ya kutafuta,si tumeona wengi tu jamaa baada ya kukata moto au yuko kitandani hajitambui Mali zile mwanamke anatapanya na masela wengine.Kila siku tunatakiwa kujifunza katika maisha.

Kwa upande wa matumizi huwa nipo na limitations sana huwa situmagi hela kizembe maana wanawake ni wazuri kwenye ku Fake vitu sana.
Ukishajua hayo mkuu mwanamke akusumbui..na utaish vizur tu maana nilijiapia kwamba sitaki stress katika maisha yangu Sitaki kufa mapema( hili namwachia Mungu Ila sio kwa sababu za wanawake never)!! Nina limit ya mwanamke kunisumbua maana nimetengeneza mazingira wasinizoee sana iwe niliezaa nae au Wife.

Furaha yangu Huwa ipo kwa watoto kwani Napenda sana Watoto na sitaki hata siku moja kuja kutelekeza mtoto!! Mwanamke akizingua huwa nina namna namtreat kisaikolojia which is more painful huwa sipigi.

Mwisho; Sitaki Stress katika maisha yangu zinazoletwa na mtu anaitwa mwanamke.Furaha yangu Ipo kwa watoto tu sio mwanamke!! So Huwa hawanisomagi hata kidogo maana nabadilika badilika...Eti mwanamke anataka kujifanya Anakujua sana kuliko Mama yako aliyekuzaa kisa umezaa nae.
 
Duh! Basi hawa watu ndio walivyo kumbe! Yaani ungesema ni Ushirombo halafu ukasema ni Mtoto wa kiume hahahaha ningekutajia jina kabisa. Yote uliyoyaandika yanafanana kabisa na huyo Dada. Labda kama umebadili hizo taarifa mbili.

Wanawake ndio walivyo, yaani jamaa alinisimulia hivyo hivyo, tofauti ni hizi tu na kwamba yeye hakwenda polisi aliamua kukaa kimya tu.

Mshkaji alikua anafunga safari kabisa anaenda ushirombo Kahama huko anakaa hapo kumbe demu ni mke wa MTU. Akabeba mimba akajifungua duh jamaa analea na huyu nae analea.

Wanaume tuna majanga aiseeee. UKIMWI utatumaliza, jamaa alinitumia hadi picha ya demu, ni mkali, ni chombo, akiniruhusu nitaitafuta niiweeke hapa.
Ukimwi utawamaliza vipi? Ukimwi mnajitafutia wenyewe. Sasa kama mtoa mada yuko na familia lkn akaamua kukitombesha nje tena kavu kabisa (story yake imethibitisha ilo).
Yan huu Uzi hapa ni mtatusema leo, Kila mtu atakuja na janga lake mnasahau na nyie ndio source ya hayo majanga
 
Aiseeh mimi nipo makini Broo!! Kwanza Siwezi Kujenga Ukweni Hiyo ni never iwe kwa mke au kwa mtu niliyezaa nae pembeni!! Hivo ni vitu ambavo sitakuja kufanya ni big mistake!!

Pili huwa sinaga garantii ya kuwa mwanamke yoyote ninaeishi nae atakua wangu nikampa asilimia zote Never hata iwe mke wangu huwa naishi nae mguu ndani mguu nje!! Kingine sitaki mwanamke aniletee shida katika maisha yangu Nikiwa na msemo kwamba sijazaliwa nae.

Tatu Maisha nitakayoyajenga ni kwa ajili ya watoto wangu na Nitafocus kwa watoto tu maana hao ndio ndugu zangu!!
Brazaa hawa wanawake ambao leo uko nao kesho yupo na mwingine Dont give a chance akusome hata awe mke wako kuwa mtu usie eleweka!!

Kwa upande wa matumizi huwa nipo na limitations sana huwa situmagi hela kizembe maana wanawake ni wazuri kwenye ku Fake vitu sana.
Ukishajua hayo mkuu mwanamke akusumbui..na utaish vizur tu maana nilijiapia kwamba sitaki stress katika maisha yangu Sitaki kufa mapema( hili namwachia Mungu Ila sio kwa sababu za wanawake never)!! Nina limit ya mwanamke kunisumbua maana nimetengeneza mazingira wasinizoee sana iwe niliezaa nae au Wife.

Furaha yangu Huwa ipo kwa watoto kwani Napenda sana Watoto na sitaki hata siku moja kuja kutelekeza mtoto!! Mwanamke akizingua huwa nina namna namtreat kisaikolojia which is more painful huwa sipigi.

Mwisho; Sitaki Stress katika maisha yangu zinazoletwa na mtu anaitwa mwanamke.Furaha yangu Ipo kwa watoto tu sio mwanamke!! So Huwa hawanisomgagi hata kidogo maana nabadilika badilika...Eti mwamamke anataka kujifanya Anakujua sana kuliko Mama yako aliyekuzaa kisa umezaa nae wanawake wapuuzi sana sometimes.
Hii imekaaje vizuri sana, unaweza kuja bure! Miaka ya nyuma nakumbuka kuna Jamaa walichinjana na mke wake chumbani pale Mabibo mtaa wa Mikongeni saa 12 jioni. Nilishuhudia lile tukio. Linatisha sana.

Tuko lingine lilitokea Tanga kwenye hotel ya DOLPHIN. Jamaa kampiga risasi na akajipiga na yeye. End of story
 
Ukimwi utawamaliza vipi? Ukimwi mnajitafutia wenyewe. Sasa kama mtoa mada yuko na familia lkn akaamua kukitombesha nje tena kavu kabisa (story yake imethibitisha ilo).
Yan huu Uzi hapa ni mtatusema leo, Kila mtu atakuja na janga lake mnasahau na nyie ndio source ya hayo majanga
Ndio maana nikasema UTATUMALIZA sikutaja upande mmoja Ndugu. Mi nimekumbuka tu nikaweka msisitizo!
 
Hii imekaaje vizuri sana, unaweza kuja bure! Miaka ya nyuma nakumbuka kuna Jamaa walichinjana na mke wake chumbani pale Mabibo mtaa wa Mikongeni saa 12 jioni. Nilishuhudia lile tukio. Linatisha sana.

Tuko lingine lilitokea Tanga kwenye hotel ya DOLPHIN. Jamaa kampiga risasi na akajipiga na yeye. End of story
Unaona Sasa Mifano ipo mingi tu!! Tunatakiwa tuwe wakujifunza katika maisha kila siku ila tu usimletee shida mwanamke au wewe kama utamwacha mnachana kwa amani tu!! Mnabaki kulea watoto
 
Pole....kisa chako kizuri na unajua kusimulia pia uandishi hauchoshi kusoma

Hakukuwa na haja ya kumpiga wakati we mwenyewe una familia sasa ulitaka yeye akatulizie wapi mihemko na wewe muda mwingi upo kwa mkeo? We endelea kumtumia matumizi baby mama sababu ya mtoto wenu hata kwa Mara moja baada ya kila week 8.
Umemshauri vyema sana, pia na tabia zake alishaambiwa angemuonya tu wala sio kumpiga maana hayo yote matokeo ya kutoka nje ya ndoa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nilipoona ni hapo “nikampiga karibu nimuue” na “polisi wakamshushia kipondo”

Huna moyo mkuu. Mjamzito ndo unampatia shurba hivyo? Acha ajipoze kwa mponda kokoto, atleast it seems alikuwa anamtreat gently.
 
Alikuwa ameshajifungua lkn hakukuwa na sababu ya kumpiga.
Wanaume ni wabinafsi sana, ye akiwa kwake anabanjuka vizuri tu na mke wake halafu mchepuko ndio anataka ujaze kichupa.
Mimi nilipoona ni hapo “nikampiga karibu nimuue” na “polisi wakamshushia kipondo”

Huna moyo mkuu. Mjamzito ndo unampatia shurba hivyo? Acha ajipoze kwa mponda kokoto, atleast it seems alikuwa anamtreat gently.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
35 Reactions
Reply
Back
Top Bottom