Ukiwa kijana na afya njema uwezi kuona umuhim wa ndoa, lakini ninavyozidi kuwa mtu mzima naona kabisa maamuzi yangu ya ujanani hayakua sahihi, kuna baadhi ya wanawake hawakua smart ila walinipenda kweli ningetuliaga na mmoja kwa sababu nakiri hakuna mwanamke mkamilifu. Mwanamke wa kuwa nae uzeeni na ukiwa na mafanikio ni mashaka sana, hapo hakunaga mapenzi ya kweli ukifilisika ama ukiumwa vizuri wanakimbia.. so kama una nafasi ya kuoa ndoa ni muhimu, watoto sio muhimu saana. Cha msingi hakikisha kama huna watoto una akiba ya kutosha, jiwekeze sawasawa, mpunga ukiwepo huwezi kosa wa kukuuguza