Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,499
Wakuu!
Baada ya msanii chipukizi wa Singeli, Dogo Patten, kususia mahojiano kwenye kipindi cha Gen Talk cha Mjini FM, gumzo limeibuka mitandaoni likihusisha watangazaji na mashabiki. Tukio hilo limezua hisia kali baada ya vipande vya mahojiano kuonyesha watangazaji wakimshinikiza msanii huyo kuzungumzia masuala ya shule badala ya muziki wake, jambo lililowafanya mashabiki wengi kuhisi ni dharau na “kubully” kwa msanii mdogo mwenye umri chini ya miaka 18.
Haji Manara, mkongwe kwenye tasnia ya utangazaji, alilaani tukio hilo akisema:
"Mmeonyesha dharau kubwa kwa muziki wa Singeli na kumfanya kijana ajione ni nothing. Tokeni hadharani kumuomba radhi na muache kujipa uungu mtu hewani."