Super Handsome

JF-Expert Member
Jul 16, 2013
3,846
6,439
Mahakama ya Kinondoni leo Jumanne imetoa amri ya kutangazwa gazetini, nyumba aliyoishi Masaki na au kijijini kwao Kolomije kwa aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ili apate taarifa za kesi iliyofunguliwa dhidi yake na Mwandishi wa Habari, Saed Kubenea. Kesi itatajwa 2 Machi 2022.

Pia soma > Paul Makonda ashindwa kufika Mahakamani katika kesi inayomkabili. Kesi yaahirishwa hadi 08 Feb 2022

Shauri hilo limetajwa kufuatia Mahakama hiyo kushindwa kusikiliza hapo awali baada ya shughuli kuingiliana.

makonda.jpg

----

Akizungumza mahakamani hapo Leo Wakili wa upande wa waleta maombi Nyaronyo Kicheere, ameeleza kwamba wameshindwa kumpata mjibu maombi namba 3 ambaye ni Paul Christian Makonda kwa kuwa Masaki alikokuwa anakaa amekwishahama na namba yake ya simu haipatikani na hivyo kuiomba Mahakama hiyo iwapatie hati ya kumsaka maeneo mbalimbali.

Aidha wameomba kupewa hati za wito ambazo zitapelekwa alipokuwa akifanyia kazi kwa mara ya mwisho, kwenye nyumba aliyokuwa anaishi kwa mara ya mwisho, maeneo anayotembelea mara kwa mara na nyingine iwekwe katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, nyingine ipelekwe bandarini, Kolomije, Misungwi mkoani Mwanza na ya mwisho ipelekwe kwenye gazeti la Kiswahili na la kingereza.

Wakili ameongeza kuwa lengo la kufanya hivyo ni kutaka mjibu maombi hayo ambaye ni Paul Makonda apate taarifa juu ya uwepo wa kesi hiyo mahakamani.

Kwa upande wake Hakimu wa mahakama hiyo Aron Ryamuya, ameeleza kuwa hoja ya kwenda kubandika hati hizo katika viwanja vya ndege na bandarini ni kinyume cha sheria na ni uchafuzi wa mazingira na badala yake akakubali matangazo hayo yapelekwe kwenye nyumba yake ya Masaki aliyokuwa akiishi, kwenye gazeti na kijijini kwao Koromije pekee.

Kesi hiyo namba 1 ya mwaka 2022, imeahirishwa hadi Jumatatu ya Machi 2, 2022.

Chanzo: EATV
 
Mahakama ya Kinondoni leo Jumanne imetoa amri ya kutangazwa gazetini, nyumba aliyoishi Masaki na au kijijini kwao Kolomije kwa aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ili apate taarifa za kesi iliyofunguliwa dhidi yake na Mwandishi wa Habari, Saed Kubenea. Kesi itatajwa 2 Machi 2022.

Shauri hilo limetajwa kufuatia Mahakama hiyo kushindwa kusikiliza hapo awali baada ya shughuli kuingiliana.

C2522067-9FDB-46F7-93B6-5EAE6F22A8AD.jpeg
 
Ha ha ha ha .maigizo haya,yaani mahakama imeshindwa kumpata ,Hadi waombe gazeti liwatafutie makonda.maigizo haya,ukiona hivyo hapo hakuna kesi ni Kiki tu!!

Tatizo hujui, kuna utaratibu wa mtu kumpelekea wito wa Mahakama, moja wapo ni kumkabidhi mkononi mhusika kama hapatikani unapeleka kwa mwajiri ama nyumbani kwake na hapo nyumbani kama hamna wa kupokea unabandika kwenye mlango wake.

Njia zote zikishindikana, sheria inasema inabidi litolewe tangazo la huo wito kwenye magazeti angalau mawili hadi matatu yanayo sambazwa nchi nzima, so hapo hamna cha ajabu.
 
Mahakama ya Kinondoni leo Jumanne imetoa amri ya kutangazwa gazetini, nyumba aliyoishi Masaki na au kijijini kwao Kolomije kwa aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ili apate taarifa za kesi iliyofunguliwa dhidi yake na Mwandishi wa Habari, Saed Kubenea. Kesi itatajwa 2 Machi 2022.

Pia soma > Paul Makonda ashindwa kufika Mahakamani katika kesi inayomkabili. Kesi yaahirishwa hadi 08 Feb 2022

Shauri hilo limetajwa kufuatia Mahakama hiyo kushindwa kusikiliza hapo awali baada ya shughuli kuingiliana.

Ukitaka kujua kwa nini magufulists hawampendi samia ni kwa mambo kama haya. Wapwani ndio wafanyaji wakubwa wa madawa ya kulevya.
Mama anaacha aliyekua mtumishi mwakilishi wa rais mkoa wa dar kunyanyasika na kubakia katika hali ya mashaka kwa kazi aliyofanya kupambana na dawa za kulevya. Ni kisasi tu wala sio lingine.
 
Back
Top Bottom