Tangia lini,mbona numuona na ford ranger rangi ya machungwa flani hivi anazurula tu!?
 
Hii kila kitu michezo tu, ndio maana hata tunaongozwa na mtu anayetudharau lkn bado tunambabakia
 
Mahakama ya Kinondoni leo Jumanne imetoa amri ya kutangazwa gazetini, nyumba aliyoishi Masaki na au kijijini kwao Kolomije kwa aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ili apate taarifa za kesi iliyofunguliwa dhidi yake na Mwandishi wa Habari, Saed Kubenea. Kesi itatajwa 2 Machi 2022.

Pia soma > Paul Makonda ashindwa kufika Mahakamani katika kesi inayomkabili. Kesi yaahirishwa hadi 08 Feb 2022

Shauri hilo limetajwa kufuatia Mahakama hiyo kushindwa kusikiliza hapo awali baada ya shughuli kuingiliana.

----

Akizungumza mahakamani hapo Leo Wakili wa upande wa waleta maombi Nyaronyo Kicheere, ameeleza kwamba wameshindwa kumpata mjibu maombi namba 3 ambaye ni Paul Christian Makonda kwa kuwa Masaki alikokuwa anakaa amekwishahama na namba yake ya simu haipatikani na hivyo kuiomba Mahakama hiyo iwapatie hati ya kumsaka maeneo mbalimbali.

Aidha wameomba kupewa hati za wito ambazo zitapelekwa alipokuwa akifanyia kazi kwa mara ya mwisho, kwenye nyumba aliyokuwa anaishi kwa mara ya mwisho, maeneo anayotembelea mara kwa mara na nyingine iwekwe katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, nyingine ipelekwe bandarini, Kolomije, Misungwi mkoani Mwanza na ya mwisho ipelekwe kwenye gazeti la Kiswahili na la kingereza.

Wakili ameongeza kuwa lengo la kufanya hivyo ni kutaka mjibu maombi hayo ambaye ni Paul Makonda apate taarifa juu ya uwepo wa kesi hiyo mahakamani.

Kwa upande wake Hakimu wa mahakama hiyo Aron Ryamuya, ameeleza kuwa hoja ya kwenda kubandika hati hizo katika viwanja vya ndege na bandarini ni kinyume cha sheria na ni uchafuzi wa mazingira na badala yake akakubali matangazo hayo yapelekwe kwenye nyumba yake ya Masaki aliyokuwa akiishi, kwenye gazeti na kijijini kwao Koromije pekee.

Kesi hiyo namba 1 ya mwaka 2022, imeahirishwa hadi Jumatatu ya Machi 2, 2022.

Chanzo: EATV
 
Notice sio swala la kuku na yai; kipi kimetangulia.

Unasajili kesi kwanza, mahakama inaamua kama kuna kesi ya kujibu na kutoa notice.

Wakili awezi kujitapa tu tunamtaka mtu aje mahakamani kusikiliza upumbavu wao. For their own amusement ya kuona Makonda kapigwa picha akiingia mahakamani na kuchapisha kwenye magazeti yao au kurusha kwenye social media.

Ni sawa jirani ampige mkewe, aliepigwa agome kufungua mashtaka. Nyumba ya pili ivalie njuga kumshitaki mpigaji una uhusiano gani na tukio? Hana.

Mtu anaeweza shitaki kwa lazima ni jamuhuri, umepeleka umbea wako kwao. Wamemwita victim ameshauri waachane na case na wao wametii.

We jirani bado kihehere unashtaki kwa lazima, unaunganisha na ofisi ya DPP kwa kutoshitaki.

Hi case ya Makonda inatengeneza bad precedent mahakamani; kwa kuendekeza siasa za kishamba na ujinga ujinga.

Kama mimi ndio Makonda siendi, huyo Kubenea he might as well include Clouds Media kwa kutoshitaki.

Clearly motive ya case ni personal vendetta. Na hii case ikisikilizwa inafungua Pandora Box ya NGO kufungua mashtaka kwa niaba ya victim mbali mbali kama jamuhuri aitofanya na ndio mwanzo wa kusikilizwa case za ovyo ovyo kama hii ya Makonda.

It is a for a reason case civil dispute zinataka kuona relation la mshitaki na mshitakiwa vinginevyo kila mtu akikwera na tukio atafungua case.
naamini atajitokeza ! labda hajapata samansg.h
 
Machadema cjui yakoje yanapenda chuki sana!!!
Mboe aliwafundisha tabia za kihalifu kama vile; ukaidi, UVUTAJI wa bangi, ukorofi, ujambazi, ubishi na kila aina ya uhalifu.
ndio maana nasema mboe lazima afungwe kifungo cha maisha gerezani ili iwe fundisho kwa hawa nyumbu wake.
 
Hakuna mtu anayemficha Makonda, kwa kuwa aliyekuwa anamtuma kufanya uovu ni Mwendazake ambaye ametangulia Jehanam.

Makonda atakuwa kisha kimbia Nchi au kama yupo ata commit suicide tu, hamna namna atakubali kushtakiwa kama Ole Sabaya
Kesi inaendeleaje?
 
Mahakama ya Kinondoni leo Jumanne imetoa amri ya kutangazwa gazetini, nyumba aliyoishi Masaki na au kijijini kwao Kolomije kwa aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ili apate taarifa za kesi iliyofunguliwa dhidi yake na Mwandishi wa Habari, Saed Kubenea. Kesi itatajwa 2 Machi 2022.
 

Attachments

  • Screenshot_20220305-075111_Gallery.jpg
    Screenshot_20220305-075111_Gallery.jpg
    130.4 KB · Views: 10
Back
Top Bottom