Rufani dhini ya Mbunge Pauline Gekul yatupiliwa mbali, wapanga kufungua kesi ya madai kwa wote waliomchafua

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,327
24,232
Mfumo wa haki jinai ni mbovu pia hata teuzi za majaji zinatia shaka asema wakili kiongozi wa jopo la mteja wao aliyefungua kesi dhidi ya mbunge Pauline Gekul

Kesi hiyo ni rufaa ya jinai namba 577 ya mwaka 2024 leo 15 April 2024 mbele ya jaji wa Mahakama Kuu kanda ya Manyara, kuhusu shambulio la kudhuru mwili, linalomhusu Pauline Gekul, akituhumiwa kumfanyia ukatili .... ambapo aliyefanyiwa ukatili alifungua kesi namba 577 ya kupinga Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali - DPP aliyefuta kesi dhidi ya Gekul hapo Jumatano, Desemba 27, 2023 dhidi ya mtuhumiwa Mbunge wa Babati Mjini, Pauline Geku.
---
Mahakama Kuu Kanda ya Manyara imetupilia mbali rufaa iliyokuwa imefunguliwa dhidi ya Mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul baada ya kukubaliana na hoja moja ya pingamizi kati ya tatu zilizowasilishwa na mbunge huyo.

Uamuzi huo umetolewa jioni hii na Jaji Devotha Kamuzora aliyekuwa akisikiliza rufaa hiyo iliyokuwa imefunguliwa na Hashim Ally.

Jaji huyo amesema Mahakama baada ya kupitia hoja za pande zote mbili kuhusiana na pingamizi hilo la awali, amekubaliana na hoja moja ya pingamizi hilo, kwamba mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza rufaa hiyo.

Amesema uamuzi wa hoja hiyo moja unatosha kumaliza rufaa hiyo kwa kuitupilia mbali na kwamba, haoni sababu ya kuangalia hoja nyingine mbili za pingamizi hilo la awali lililowasilishwa na mjibu rufaa.

Hata hivyo, Jaji Kamuzora ameeleza kuwa upande ambao haujaridhika na uamuzi huo unaweza kukata rufaa.

Akizungumzia uamuzi huo, Wakili Peter Madeleka anayemwakilisha Hashim, amesema hawajaridhika nao na wanatarajia kukata rufaa Mahakama ya Rufani kuupinga.

Wakili Madeleka ameongeza kuwa wakikosa haki katika mahakama hiyo, watakata rufaa Mahakama ya Haki za Binadamu ya Afrika.

Katika rufaa hiyo mrufani alikuwa na sababu sita za rufaa hiyo akipinga uamuzi wa Mahakama ya Wilaya ya Babati kuifuta kesi aliyokuwa amemfungulia mbunge huyo.

PIA SOMA

Naibu Waziri na Mbunge Pauline Gekul adaiwa kumfanyia Ukatili wa Kimwili Mtoto

Breaking News: - Rais Samia Suluhu atengua uteuzi wa Pauline Gekul saa chache baada ya kutuhumiwa kufanya unyanyasaji

Pauline Gekul ajibu tuhuma za kumdhuru na kumdhalilisha kijana

Pauline Gekul anastahili kuvuliwa uanachama na kufikishwa mahakamani haraka sana. Amekichafua na kukipaka matope chama

CCM Manyara yakutana kumjadili Pauline Gekul, kutoa tamko Novemba 27, 2023

Audio: Emmanuel Gekul akitoa vitisho vya kutaka kumdhuru anayedaiwa kusambaza Video ya kijana aliyefanyiwa ukatili na Pauline Gekul

Mbunge Pauline Gekul akamatwa na Jeshi la Polisi akijaribu kutoroka nchini kuelekea nchini Kenya

Mbunge Pauline Gekul ahojiwa Polisi na kupewa dhamana, karudi nyumbani kwake

Peter Madeleka kusikiliza kesi ya Gekul mahakama ya Wilaya kwa tuhuma alizonazo dhidi ya Hamis

Mbunge Pauline Gekul atakiwa kufika Mahakamani Disemba 27, 2023 kujibu tuhuma dhidi yake

Nani anamlinda Gekul? DPP asema hana mpango wa kuendelea na kesi

Ya Gekul hayajaisha, Wakili Madeleka kukata rufaa

DPP: Hakukuwa na nia ya kufungua kesi ya Jinai dhidi ya Pauline Gekul

Rufaa ya Pauline Gekul (Mbunge Babati Mjini) yapigwa kalenda

Shauri dhidi ya Mbunge Gekul lasikilizwa Mahakamani, Wakili Madeleka asema DPP hakuwa na Mamlaka ya kufuta kesi
===========================
The criminal justice system is flawed, and even the appointment of judges is questionable, according to the lead counsel of the client who filed a case against Member of Parliament Pauline Gekul.

This case is criminal appeal number 577 of 2024, taking place today, April 15, 2024, before a judge at the High Court in the Manyara Region. It involves an assault causing bodily harm, involving Pauline Gekul, who is accused of committing acts of violence... where the victim of the assault filed case number 577 to challenge the Director of Public Prosecutions who dropped the case against Gekul on Wednesday, December 27, 2023, the accused Member of Parliament for Babati Mjini, Pauline Geku.

The High Court of Manyara Region has dismissed the appeal filed against Member of Parliament for Babati Mjini, Pauline Gekul, after agreeing with one of the three objections raised by the MP.

The decision was made this evening by Judge Devotha Kamuzora, who was hearing the appeal filed by Hashim Ally.

The judge stated that after considering arguments from both sides regarding the initial objection, she agreed with one of the objections, stating that the court does not have jurisdiction to hear the appeal.

He said that the decision on that one objection is sufficient to dismiss the appeal, and he sees no reason to consider the other two objections raised by the respondent.

However, Judge Kamuzora explained that the dissatisfied party can appeal the decision.

Speaking about the decision, Lawyer Peter Madeleka, representing Hashim, said they are not satisfied and plan to appeal to the Court of Appeal to challenge it.

Lawyer Madeleka added that if they do not find justice in that court, they will appeal to the African Court on Human and Peoples' Rights.

In the appeal, the appellant had six grounds, challenging the decision of the Babati District Court to dismiss the case they had filed against the Member of Parliament.
 
TOKA MAKTABA :
29 December 2023


Wakili Mwabukusi Amvaa DPP Kufutwa kwa Kesi ya Pauline Geku

Maoni ya wadau wa mahakama kuhusu kesi ya Hashimu Ally dhidi ya mbunge Pauline Gekul, inaonesha mazingira ya mfumo wa haki jinai kuongopa kusikiliza kesi hii wasema baadhi ya wadau mawakili wasomi


View: https://m.youtube.com/watch?v=iG6WVeP1jr0
 
Mahakama Kuu Kanda ya Manyara imetupilia mbali rufaa iliyokuwa imefunguliwa dhidi ya Mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul baada ya kukubaliana na hoja moja ya pingamizi kati ya tatu zilizowasilishwa na mbunge huyo.

Uamuzi huo umetolewa jioni hii na Jaji Devotha Kamuzora aliyekuwa akisikiliza rufaa hiyo iliyokuwa imefunguliwa na Hashim Ally.

Jaji huyo amesema Mahakama baada ya kupitia hoja za pande zote mbili kuhusiana na pingamizi hilo la awali, amekubaliana na hoja moja ya pingamizi hilo, kwamba mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza rufaa hiyo.

Amesema uamuzi wa hoja hiyo moja unatosha kumaliza rufaa hiyo kwa kuitupilia mbali na kwamba, haoni sababu ya kuangalia hoja nyingine mbili za pingamizi hilo la awali lililowasilishwa na mjibu rufaa.

Hata hivyo, Jaji Kamuzora ameeleza kuwa upande ambao haujaridhika na uamuzi huo unaweza kukata rufaa.

Akizungumzia uamuzi huo, Wakili Peter Madeleka anayemwakilisha Hashim, amesema hawajaridhika nao na wanatarajia kukata rufaa Mahakama ya Rufani kuupinga.

Wakili Madeleka ameongeza kuwa wakikosa haki katika mahakama hiyo, watakata rufaa Mahakama ya Haki za Binadamu ya Afrika.

Katika rufaa hiyo mrufani alikuwa na sababu sita za rufaa hiyo akipinga uamuzi wa Mahakama ya Wilaya ya Babati kuifuta kesi aliyokuwa amemfunguli
a mbunge huyo.
 
Duniani ni sehemu ya dhiki na mateso!
Haki ipo mbinguni au pengine haipo kabisa.

Sijawahi kuamini kama mahakamani kuna haki. Binadamu tunatamaa sana.
 
Binafsi sijaelewa hoja ya mahakama na kama kuna mtu anaweza kunifafanulia kwanini Mahakama Kuu imesema haina mamlaka ya kusikiliza hiyo kesi ingawa rufaa inahusu mahalama juu ya maamuzi yaliyofanyika mahakama ya chini?

1. Kama Mahakama kuu haina mamlaka ya kusikiliza hiyo rufaa juu ya maamuzi ya mahakama ya Wilaya, hiyo mahakama ya wilaya iliwaze kufanya maamuzi?

2. Ni scenario gani zinaweza kutokea katika mahakama za chini ambazo zinaweza kupelekea mahakama kuu ishindwe kusikiliza rufaa inayotokea katika mahakama hizo za chini?
 
Huwa nina mtazamo hasi sana dhidi ya mahakama za Tanzania na taasisi zingine kwa ujumla.

Mahakama za Tanzania ni takataka tu na watendaji wake wa pande zote ni faeces tu.
 
Ndo maana jamaa aliwaambia wasiende kumaliza ishu zao mahakamani.................
 
Omba Mwenyezi Mungu akupe uhai ili uje ushughudie majaji wanaomba hizi kazi za kijaji na kufanyiwa usaili
 
1713255305775.png

Mahakama kuu Kanda ya Manyara imefutilia mbali rufaa ya Hashimu Ally, dhidi ya Mbunge wa jimbo la Babati Mjini, Pauline Gekul kwa madai kuwa imekosa na mashiko.

Maamuzi hayo, yametolewa na Jaji wa Mahakama hiyo, Devotha Kamzora huku akiwataka warufani kukata upya rufaa kama hawajaridhika na maamuzi hayo.

Kwa upande wake wakili wa Hashimu Ally, Peter Madeleka amesema hajaridhishwa na maamuzi hayo kwani kuna madudu yanaendelea kwenye kesi hiyo, hivyo ndani ya siku mbili watahakikisha wanakata rufaa, ili haki dhidi ya mteja wake itendeke.

Naye wakili wa Pauline Gekul, Efraim Kisanga amesema maamuzi yaliyotolewa na Jaji Devotha ni sahihi, hivyo muda wowote kuanzia sasa mteja wake atafungua kesi ya madai kwa wale wote waliomchafua kupitia kashfa hiyo na ukweli wote utajulikana ndani ya muda mfupi.

Pauline Gekul, alifikishwa Mahakama ya Wilaya ya Babati akikabiliwa na kesi ya jinai namba 577 ya mwaka 2023, kwa kosa la kumuingizia chupa kinyume na maumbile aliyekua Mfanyakazi wake, Hashimu Ally, kesi ambayo ilitupitiliwa mbali na Mkurugenzi wa Mashtaka kutokana na mamlaka aliyopewa.

Hata hivyo, hii inakuwa ni mara ya pili kwa Mbunge huyo Pauline Gekul kushinda kesi hiyo, licha ya mrufani wake kutaka kukata rufaa Mahakamani hapo.
 
Madereka kala hela yake, kala hela ya wana chadema, huyo anaenda kupumzika. Tena kwa kisingizio ataenda mahakama ya haki za binadamu. You dont have proof stay quite.

Kijana kajiaibisha, kwa familia yake na jamiibyake, kisa hela tu. Unaaminiwa na mtoa helq, akikufukuza kwa makosa unaona kama amekuonea unamtengenezea zengwe, blood fakn Hashim Ally.
 
Back
Top Bottom