Mahakama Kuu Divisheni ya Uhujumu Uchumi na Rushwa yatupilia mbali mapingamizi 2 kesi ndogo ya Mbowe na Wenzake. Jaji Siyani ajitoa kuendelea na kesi

Katiba Mpya umekuwa ni wimbo. Je, hiyo Katiba Mpya itamzuia mtu kufanya uhalifu au mwalifu kutokushughulikiwa? Au, kwa agenda ya siri ya wanasiasa, itawaingiza madarakani watimize mambo yao binafsi?

Wewe tobiasi unaathirika vipi na Katiba iliyopo?
Wajinga wengi sana.
 
Oct 20 katika Mahakama ya Makosa ya uhujumu uchumi pale law school:

1. Mheshimiwa Jaji Kiongozi aliyatupilia mbali mapingamizi yaliyowekwa na upande wa utetezi kwa kujiridhisha pasi na shaka kuwa:

(a) Maelezo ya mshitakiwa wa pili yalikuwa yametolewa Dar Central Police, ndani ya muda wa masaa 4 baada ya kukamatwa na makando kando yake, kama ilivyo elekezwa kisheria.

(b) Maelezo ya mshitakiwa wa pili yalikuwa yametolewa kwa ridhaa yake mwenyewe pasipokuwa na shinikuzi lolote.

Ni wazi kuwa Mheshimiwa Jaji Kiongozi aliukubali ushahidi wote wa upande wa mashtaka kama ulivyo kuwa, pasipo na kuzingitia lolote kutokea katika ushahidi wa upande wa utetezi.

2. Wengine tuliokuwapo kuwakilisha mahakani ni kama tulivyo pichani:





Kuhudhuria mahakamani ni haki yetu.

Bila kujali kitakacho tokea tutakuwapo pia kesho na tutafuatilia hadi dakika ya mwisho.

Mungu uwabariki na kuwasimamia watuhumiwa hawa ili haki ikatendeke.

Mikononi mwako ukawalinde.
 
Naww kwa akili zako unaelewa nini kumhusu huyo unayemtetea...? Ulikuwa nae wapi hadi uone mmoja kaonewa na mwingine katendewa sawa. Binadam lazima tujifunze kuwa wavumilivu, leo kw mwenzio kesho kwako... wanasiasa tunawatetea sana lakini mwisho wa siku ndo hao hao wanaotufanya tunaendelea kusota mtaani.

Mimi nikushauri pambania ugali wako achana na mambo ya siasa. Aliyekuwepo ndo tunaenda nae, akija unayempenda ni majaliwa. Chuki zetu na mihemko ya kisiasa isitufanye tukagawanyika kama Taifa. Daima ni lazima tuwe wamoja na wapenda amani.

RIP JPM
Kazi iendelee.
Tumwombee mama akaze hili nidhani ya kazi serikalini iimarike zaidi.
 
Mmmh,

Chumvi ikiisha ukali wake haiitwi chumvi Tena. Ama chakula kikitoka tumboni kupitia utumbo mpana hauitwa kinyesi Ila kikipitia mdomoni huitwa matapishi. Vyote vikitoka havifai kuwa chakula Tena.

Sasa usisifie matapishi kwamba ni chakula kwa sababu kinafanana na chakula. Wala kinyesi hata kifanane na mayai yaliyopikwa vyema bado ni kinyesi tu. Hivyo Sifia panapohitaji kusifiwa na kosoa pale inapobidi ndio manaa Mungu alikupa ubongo.

Mbowe sio Gaidi na hajawahi kufanya njama za kigaidi.

Usiwe Kama chichidodo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…