Mr.Junior
JF-Expert Member
- Sep 8, 2013
- 11,796
- 9,999
Nimenukuu ukurasa wa 22 wa Gazeti la mwananchi la leo 16/09/2015
para ya Kwanza; naomba ninukuu" Msifanye mabadiliko kwa pupa kama watu wa Libya. walimwondoa madarakani rais Saddam , hapana rais Gaddafi maana Saddam alikuwa rais wa Kuwait"
"Magufuli , na Lowassa nani atatufaa kwa Siasa za nje" ni kichwa cha habari cha article yenyewe.
Magufuli huyu anayejua kila barabara ya nchi hii ameshindwa kujua vitu vya darasa la nne vinavyotokea nje ya mipaka ya Tanzania sembuse siasa za kimataifa atazijulia wapi. Kuna uwezekano akashindwa kujua hata majina ya nchi tulizopakana nazo, au kushindwa kujua Marekani, india Uk nk zipo mabara gani. Kama ni hivyo je atajuaje trouble makers na marafiki wa kweli anaoweza kushirikiana nao katika siasa za dunia. Au ushindi kwanza mengine yatajipa?. Ukiona rais hajui kinachoendelea upande mwingine wa dunia ujue kazi tunayo hivyo tusifanye makosa katika uchaguzi wa mwaka huu la sivyo watanzania woote tutaonekana mambumbumbu.
Chagua Magufuli.