Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, kwa hakika Magufuli anaweza sana kuwa waziri chini ya Raisi mtendaji, lkn magufuli hafiti/hatoshi kuwa Rais wa nchi kwa jinsi alivyo.
Nadhan hii si tu kwakuwa sasa kasimamishwa na CCM la hasha, ila mara nyingi imejadiliwa hapa hata kabla haijajulikana atakuja kuwa mgombea wa uRais kuwa huyu hatoshi.
Ni sawa na useme Chadema apewe Tundu lissu agombee Urais kwa haraka utajua tu lisu anaweza kuwa mtendaji mzuri lakn asifae kuwa kiongozi mkuu wa viongozi wengine.
Hii na kwa magufuli ni ivo ivo, anaweza uwaziri, akiongea kwa style yake ile ya comedic na data za uongo flan basi watu wanafurai na wizara inaenda, lakn sio kuwa Rais wa nchi.
Rais inahtaji mtu makini, anaesoma sana na kuelewa mambo mbali mbali ya ndani na nje, Diplomasia, Uchumi, Siasa, asiekurupuka kusema ili tu apate popularity au watu wajue pia yupo eneo husika.
Magufuli kwa hayo au sifa hizi ana pwaya, lakn namvisha Lowasa Urais, namuona akitenda kwa haiba ya pekee sana, kwanza lowasa anaonekana anajisomea sana na kusoma habari za Dunia ya nje, anajua mambo mengi, ana uzoefu na serikali na uongozi, ni mtulivu sana.
mara nyingi E. Lowasa akiongea katika mahojiano au hotuba yeyote (fatilia) lazima utamsikia akitoa nukuu mbalimbali au akinukuu kauli za viongozi kama Tony Blair, Magreth Thatcher, Frank D loosevet, nk nk
Hii tu inaonesha ni mtu alie na uwanda mpana wa kujua Mambo ya nje, na Diplomatic protocol /issues.
Magufuli si mtulivu hata kidogo, anaongea mara nyingi ili aonekane anajua, au asifiwe kwa kuwa na tarakimu kichwani, na wengi mkifatilia nyingi ni mbwembwe tu si kweli kuwa ndiyo ilivyo.
Magufuli hana exposure nje ya nchi na mambo ya kigeni. Asije akafanya mambo ya Tshangrai aliekutana na Waziri mkuu wa Germany na kuchemsha kila hatua aliopiga.