Magufuli: Saddam alikuwa rais wa Kuwait!!

Saddam alikwisha wahi kuiteka Kuwait na ndiyo mwanzo wa kilichompelekea kushambuliwa na mataifa makubwa yote duniani mpaka kuuliwa.

Hivi mleta mada hiyo shule ulienda kusomea ujinga?
 
Moja kati ya maswali muhimu ambayo wagombea wa Urais duniani kote wamekuwa wakiulizwa ni kuhusu; sera za kimataifa "foreign policy".

Rais anabidi ajue mambo ya nje na ndani ya nchi yake ili aweze kujua athari nchi yake inaweza kukumbana nazo kutokana na sera hizo za kimataifa.

Kwa JPM ameonesha kwamba,

1.Hamjui Saddam. Hili lipo wazi.
2.Haijui nchi ya Kuwait.
3.Haijui Iraq
4.Haijui vita ya Iraq vs USA

Hii ni hatari sana kwa dunia ya leo.

Ni kwamba haujui huo ukanda mzima Persian gulf ...kwa hiyo sasa atawezaje kujua conflicts za huo ukanda na mataifa ya magharibi, zinazotokana na issue ya mawese na mambo mengine??
Chembechembe za gulf war2, bado zinawaumiza watu wa hiyo region... sasa ukimuuliza hilo atajua? Wenzake waliropoka na kutia chumvi mambo yaliyokuwa kwenye dosier moja hivi ku speed up vita- 'WMD within 45 minutes...' Sasa na yeye mwache tu aendelee kuropoka mambo asiyoyajua.

Kinachowagusa watawala wetu wengi- wa huku wakisikia conflicts kama hizo, ni the fact kwamba, mtawala mmoja wa miaka mingi ameangushwa...hili ndo muhimu zaidi kwao kuliko mambo mengine yoote yanayosababisha hizo conflicts.
 
hiyo tunaita "error" na sio mistake, so ni kawaida kukosea ilihali unajua au kupitiwa in somehow
 
Nimenukuu ukurasa wa 22 wa Gazeti la mwananchi la leo 16/09/2015
para ya Kwanza; naomba ninukuu" Msifanye mabadiliko kwa pupa kama watu wa Libya. walimwondoa madarakani rais Saddam , hapana rais Gaddafi maana Saddam alikuwa rais wa Kuwait"

"Magufuli , na Lowassa nani atatufaa kwa Siasa za nje" ni kichwa cha habari cha article yenyewe.

Magufuli huyu anayejua kila barabara ya nchi hii ameshindwa kujua vitu vya darasa la nne vinavyotokea nje ya mipaka ya Tanzania sembuse siasa za kimataifa atazijulia wapi. Kuna uwezekano akashindwa kujua hata majina ya nchi tulizopakana nazo, au kushindwa kujua Marekani, india Uk nk zipo mabara gani. Kama ni hivyo je atajuaje trouble makers na marafiki wa kweli anaoweza kushirikiana nao katika siasa za dunia. Au ushindi kwanza mengine yatajipa?. Ukiona rais hajui kinachoendelea upande mwingine wa dunia ujue kazi tunayo hivyo tusifanye makosa katika uchaguzi wa mwaka huu la sivyo watanzania woote tutaonekana mambumbumbu.
Huyu jamaa atakua anakariri na haelewi anazungumza nn kukosea mara mbili ni kosa kubwa
 
Kumbe gazetini nilizania umemsikia na mdomo ake akitamka hivyo...

siamini
 
Saddam alikwisha wahi kuiteka Kuwait na ndiyo mwanzo wa kilichompelekea kushambuliwa na mataifa makubwa yote duniani mpaka kuuliwa.

Hivi mleta mada hiyo shule ulienda kusomea ujinga?

Kwa hy ina justify kuwa saddam ni rais wa kuwait kisa aliiteka
This rediculous
 
Uwaziri miaka 20, PhD yake lakini swali la darasa la tatu au la nne linamshinda sasa siasa za nje ndo hajui kabisa. Hatufai.
 
Back
Top Bottom