Magufuli: Saddam alikuwa rais wa Kuwait!!

Nimenukuu ukurasa wa 22 wa Gazeti la mwananchi la leo 16/09/2015
para ya Kwanza; naomba ninukuu" Msifanye mabadiliko kwa pupa kama watu wa Libya. walimwondoa madarakani rais Saddam , hapana rais Gaddafi maana Saddam alikuwa rais wa Kuwait"

"Magufuli , na Lowassa nani atatufaa kwa Siasa za nje" ni kichwa cha habari cha article yenyewe.

Magufuli huyu anayejua kila barabara ya nchi hii ameshindwa kujua vitu vya darasa la nne vinavyotokea nje ya mipaka ya Tanzania sembuse siasa za kimataifa atazijulia wapi. Kuna uwezekano akashindwa kujua hata majina ya nchi tulizopakana nazo, au kushindwa kujua Marekani, india Uk nk zipo mabara gani. Kama ni hivyo je atajuaje trouble makers na marafiki wa kweli anaoweza kushirikiana nao katika siasa za dunia. Au ushindi kwanza mengine yatajipa?. Ukiona rais hajui kinachoendelea upande mwingine wa dunia ujue kazi tunayo hivyo tusifanye makosa katika uchaguzi wa mwaka huu la sivyo watanzania woote tutaonekana mambumbumbu.

Chagua Magufuli.
 
Magufuri ni mtu wa kukariri,sio kuelewa, mtu anaekariri muda flani husahau, hata sasa ukimshtukiza barabwra ya bagamoyo mwenge atakwambia ina kilomita 1000.

Mawaziri wa kikwete ni mzigo,vihiyo. Mulugo alisema Tanzania inatokana na zimbabwe na zanzibar. Pia akasema mbeya ina ukubwa wa kilomita 29 za mraba.

Saddam alikua rais wa kuwait?
Kwenye mkutano wa kampeni morogoro alisema kutoka morogoro mjini mpaka bigwa ni kilomita 70
 
Nimenukuu ukurasa wa 22 wa Gazeti la mwananchi la leo 16/09/2015
para ya Kwanza; naomba ninukuu" Msifanye mabadiliko kwa pupa kama watu wa Libya. walimwondoa madarakani rais Saddam ,
hapana rais Gaddafi maana Saddam alikuwa rais wa Kuwait"

"Magufuli , na Lowassa nani atatufaa kwa Siasa za nje" ni kichwa cha habari cha article yenyewe.

Magufuli huyu anayejua kila barabara ya nchi hii ameshindwa kujua vitu vya darasa la nne vinavyotokea nje ya mipaka ya Tanzania sembuse siasa za kimataifa atazijulia wapi. Kuna uwezekano akashindwa kujua hata majina ya nchi tulizopakana nazo, au kushindwa kujua Marekani, india Uk nk zipo mabara gani. Kama ni hivyo je atajuaje trouble makers na marafiki wa kweli anaoweza kushirikiana nao katika siasa za dunia. Au ushindi kwanza mengine yatajipa?. Ukiona rais hajui kinachoendelea upande mwingine wa dunia ujue kazi tunayo hivyo tusifanye makosa katika uchaguzi wa mwaka huu la sivyo watanzania woote tutaonekana mambumbumbu.

Tatizo chemistry imejaa kichwani.
 
Kwenye mkutano wa kampeni morogoro alisema kutoka morogoro mjini mpaka bigwa ni kilomita 70

Magufuri urais hauwezi, hajui siasa za nje, hajui viongozi wa nje hata waliopita, mwenzake Lowassa hadi anawanakili misemo yao, yeye hata ukimuuliza iddi amin alikua rais wa wapi anaweza kusema congo na mobutu akasema kenya.
 
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, kwa hakika Magufuli anaweza sana kuwa waziri chini ya Raisi mtendaji, lkn magufuli hafiti/hatoshi kuwa Rais wa nchi kwa jinsi alivyo.

Nadhan hii si tu kwakuwa sasa kasimamishwa na CCM la hasha, ila mara nyingi imejadiliwa hapa hata kabla haijajulikana atakuja kuwa mgombea wa uRais kuwa huyu hatoshi.

Ni sawa na useme Chadema apewe Tundu lissu agombee Urais kwa haraka utajua tu lisu anaweza kuwa mtendaji mzuri lakn asifae kuwa kiongozi mkuu wa viongozi wengine.

Hii na kwa magufuli ni ivo ivo, anaweza uwaziri, akiongea kwa style yake ile ya comedic na data za uongo flan basi watu wanafurai na wizara inaenda, lakn sio kuwa Rais wa nchi.

Rais inahtaji mtu makini, anaesoma sana na kuelewa mambo mbali mbali ya ndani na nje, Diplomasia, Uchumi, Siasa, asiekurupuka kusema ili tu apate popularity au watu wajue pia yupo eneo husika.

Magufuli kwa hayo au sifa hizi ana pwaya, lakn namvisha Lowasa Urais, namuona akitenda kwa haiba ya pekee sana, kwanza lowasa anaonekana anajisomea sana na kusoma habari za Dunia ya nje, anajua mambo mengi, ana uzoefu na serikali na uongozi, ni mtulivu sana.

mara nyingi E. Lowasa akiongea katika mahojiano au hotuba yeyote (fatilia) lazima utamsikia akitoa nukuu mbalimbali au akinukuu kauli za viongozi kama Tony Blair, Magreth Thatcher, Frank D loosevet, nk nk

Hii tu inaonesha ni mtu alie na uwanda mpana wa kujua Mambo ya nje, na Diplomatic protocol /issues.

Magufuli si mtulivu hata kidogo, anaongea mara nyingi ili aonekane anajua, au asifiwe kwa kuwa na tarakimu kichwani, na wengi mkifatilia nyingi ni mbwembwe tu si kweli kuwa ndiyo ilivyo.

Magufuli hana exposure nje ya nchi na mambo ya kigeni. Asije akafanya mambo ya Tshangrai aliekutana na Waziri mkuu wa Germany na kuchemsha kila hatua aliopiga.

Huyu magufuri hata kauli za mentor wake kikwete za ukitaka kula lazima uliwe hazijui sembuse hao unaomtajia.

Kauli za kina kenyata za kutembea kufua mbele makalio nyuma hazijui, sembuse kuna Magreth,Lincolin,Franklin au hata za wanasayansi kina Newton au Albert?

Huyu mpe kukariri mabarabara na kusalimua kimakabila ya tanzania, hakuna kitu pale.
 
Kwa hy ina justify kuwa saddam ni rais wa kuwait kisa aliiteka
This rediculous

Hakusema rais wa Kuwait, nilimsikiliza, alisema yule "Saddam wa Kuwait".

Nikisema cityhunter yule wa JF nnamaana wewe ni rais wa JF?

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
 
Last edited by a moderator:
Magufuli tatizo kubwa katika hizi kampeni kawa mropokaji...

Ile hulka yake ya kuwa mtu mwenye matamshi ya hakika imemtoka kwa sasa...

Anabwabwaja tu kiasi kwamba kuna makosa mengi ya kimatamshi kashayafanya...
 
Hakusema rais wa Kuwait, nilimsikiliza, alisema yule "Saddam wa Kuwait".

Nikisema cityhunter yule wa JF nnamaana wewe ni rais wa JF?

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?

Acha kumlisha maneno
Alisema wazi shahiri kuwa saddam rais wa kuwait

Kukubali kukosea ni busara zaid
 
Last edited by a moderator:
Hakusema rais wa Kuwait, nilimsikiliza, alisema yule "Saddam wa Kuwait".

Nikisema cityhunter yule wa JF nnamaana wewe ni rais wa JF?

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?

Ff mfano wako kwa cityhunter hauna maana. Kubali magufuli si tu kakosea, HAJUI
 
Last edited by a moderator:
Hakusema rais wa Kuwait, nilimsikiliza, alisema yule "Saddam wa Kuwait".

Nikisema cityhunter yule wa JF nnamaana wewe ni rais wa JF?

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?

Mama si tuseme tu ulimi hauna mfupa, kuliko kutetea hili pia.....!!!

Aliteleza tu...!!
 
Last edited by a moderator:
Hakusema rais wa Kuwait, nilimsikiliza, alisema yule "Saddam wa Kuwait".

Nikisema cityhunter yule wa JF nnamaana wewe ni rais wa JF?

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
Ukipenda Siyo lazima useme ni kengeza! Unawaponda wenzako kuhusu elimu zao Kwa kitu ambacho kinaweza kukupunguzia elimu yako pia. Kuwa mkereketwa wa chama siyo lazima kutetea au kuponda kila kitu. Kama Magufuli akikosea kitu kidogo hicho Ni ubinadamu, tumkatae au kumkubali kwa sera za chama chake. Hoja hii ni ya USHABIKI na nyepesi sana. Hata hivyo #kurayangukwaenl
 
Last edited by a moderator:
Si kwasababu anachoongea ni cha uongo ndo maana anajichanganya na nafsini kwake anajua tuu kua adadanganya ila atafanyaje sasa hana namna
 
Mama si tuseme tu ulimi hauna mfupa, kuliko kutetea hili pia.....!!!

Aliteleza tu...!!

Ameteleza nini?

Labda kwa mtu kama finyu kama wewe ndiyo unaweza kumuona hivyo.

Lakini kwa msomi kama Magufuli nnamuelewa anasema nini.

Labda wewe huelewi kuwa Saddam alitangaza kuwa Kuwait ni yake na alitangaza mpaka kuibadilisha jina na kuiita Qadhima.

Kwa hiyo Magufuli kukumbusha Saddam wa Kuwait wala hajakosea. Magufuli alikuwa anaongelea kuhusu watu kukurupuka na "mabadiliko" na Saddam alikurupuka na kuibadilisha Kuwait na ndipo umaarufu wake mkubwa ulipoanzia na ndipo kulimpelekea mpaka kukosa yote.

Labda ulikuwa huelewi yote hayo, si kulaumu kwa kuwa nnajuwa ujinga upo kwenye damu yako. Au...

Hizo shule mlienda kusomea ujinga?
 
Back
Top Bottom