Mwande na Mndewa
JF-Expert Member
- Feb 26, 2021
- 949
- 2,865
Siku kama ya leo miaka 64 iliyopita alizaliwa mtoto aliyekuja kufufua matumaini ya Watanzania,shida za Watanzania zikapata ufumbuzi,matatizo ya Watanzania akayanunua na kuwa matatizo yake,ikawa kila mwenye tatizo alikwenda kwake na kutatuliwa tatizo lake,alikuwa mwenye kipaji cha Uongozi toka kwa Mungu na mwenye kaliba ya pekee,kila mahali alipopita Watanzania walimfuata mtoto huyo aliyezaliwa tarehe 29/10/1959 ,Ucheshi wake uliwapa tumaini jipya masikini na kuona yupo mtetezi wao,huruma yake ilitua mzigo mzito waliobeba Watanzania,si mwingine ni Hayati Rais John Pombe Magufuli,mcha Mungu wa kweli na mwamini aliyeamini katika jina la Yesu,rejea kipindi cha korona.
Leo nielezee mapenzi ya mwana wa Tanzania ,mwana wa Afrika,na mtu aliyeacha alama duniani kwa matendo mazuri kwa nchi yake ya Tanzania,akiwa Waziri kwa miaka 20 na hatimaye Rais wa Tanzania kwa miaka mitano,Hayati Rais John Pombe Magufuli alifanya mambo makubwa mno,alikuwa Mzalendo mwenye mapenzi ya kweli kwa nchi yake ya Tanzania,hakutaka Tanzania ichezewe na mtu yeyote iwe Mtanzania,mzungu au mwarabu,katika urais wake kwa miaka mitano Hayati Rais John Pombe Magufuli hakuijua China,Marekani wala Ulaya toka achaguliwe hadi anaondoka dunia hii, yeye alipenda kutembelea Morogoro,Arusha, Iringa,Tanga, Mbeya, Songea, Mtwara, Lindi, Rukwa, Sumbawanga anarudi Moshi,Singida anaingia Dodoma kamaliza,
Hayati Rais John Magufuli alizunguka katika mikoa ya Tanzania Ili kujua matatizo na shida za Watanzania azitatue,katika mikutano yake alitembea kwenda moja kwa moja kuongea na mtu mwenye shida,alimuangalia usoni alipata taswira ya shida na tatizo la Mtanzania yule na kulichukua yeye tatizo lake la kulitatua kama kiongozi wa nchi,alitamani yeye akinywa chai asubuhi kila Mtanzania anywe chai, yeye akila mchana kila Mtanzania ale chakula mchana,yeye akila chakula usiku basi kila Mtanzania ale chakula usiku,hakula chakula mezani kwake bila kusoma mafaili mezani kwake na kutatua shida za Watanzania,alikuwa msikivu, mvumilivu, mwenye huruma,upendo,rafiki wa wanyonge na wanaoonewa,alisimama kwa waliovunjika moyo ili kuwapa tumaini jipya,hakuona shida kutoa mpaka senti ya mwisho mfukoni mwake kuwapa wenye uhitaji,yeye aliishi ufukara kama sisi ili kujua shida zetu,na kwa hakika siku ya mazishi yake Watanzania walilia hadi tone la mwisho,hii ilioneshwa kuondokewa kwao, Watanzania walilia sababu walijua walichopoteza,na Sasa tunaona kamwe tulichopoteza hakiwezi kurudi.
Japokuwa alikuwa mwenye mamlaka ya juu kuliko Mtanzania yeyote lakini alishuka kwa unyenyekevu na kula na Wananchi chakula wanacho kula wao,hakujitenga wala kunyanyapaa watu wa hali yoyote,masikini,mgonjwawote aliwapa sababu ya kupata tabasamu,faraja na tumaini jipya kwa maana hakusahau alipotoka,alijawa huruma na upendo,alijawa na msamaha na kumsamehe Nape aliyekwenda Ikulu kuomba msamaha,vijana wa enzi yake aliocheza nao akanywa nao kahawa,kila alipopita alitenda mema,akawafuta walioonewa machozi yao,akawafungua wafugwa wao,aliingia magerezani kuwasalimu wafugwa,ubinadamu ndio hisia zake,akawasamehe waliokosea,Wimbo wa upendo uliibwa machoni pake,rohoni na kwenye utumishi uliotukuka,hakujilimbikizia mali,alijua tulikuja tupu tutaondoka tupu,alikuwa mwenye utani,matani kidogo,alisalimia kwa lugha ishirini kabla ya kuanza kuhutubia mkutano wake,masihara kidogo ili tu kuwaonyesha ni Mimi yule yule sikubadilika,Usingizi hakupata akiiwazia Tanzania,asubuhi aliamka na saa mbili asubuhi alianza kuzindua miradi aliyoagiza ijengwe kwa manufaa ya Watanzania wa leo,kesho na kesho kutwa,alikuwa Baba mwema sana.
Wananchi wengi walikiri kuwa Rais John Magufuli ndiye rais waliyemsubiri kwa miaka mingi sana,nilisikia watu wakisema tulichoka dharau kutoka kwa vijinchi vidogovidigo Hayati Raisi John Pombe Magufuli aliturudisha kwenye chati ya Afrika na kuturudishia heshima,we are a big nation a Great Tanzania,rejea siku ya Msiba wake,Rais wa Botswana,Mh Mokgweetsi Masisi alisema,nanukuu "Tanzania you have a big shoes to wear after the departure of President John Magufuli" kila hotuba ya Rais siku ile ilimtaja Hayati Rais John Magufuli kama Mwana wa Afrika,Rais Ramaphosa alisema "Magufuli was a true son of Africa,a pan africanist" Rais Kenyatta alisema "Magufuli alikuwa ni Mwanamwema wa Afrika" mpaka hapa unaweza kujua Hayati Rais John Magufuli alitembea katika nyayo za Mababa wa Afrika,Kwame Nkrumah, Julius Nyerere,Haile Selassie,Samora Machel,Edward Mondlane,Keneth Kaunda,Jommo Kenyatta na Joachim Chisano.
Nimalizie kwa nukuu chache nilizopata kuzisoma kwenye Journal mbalimbali za kimataifa,Magufuli stands out in his humility and self-deprecation. He shuns wealth, and fame. In a country where thieves are celebrated, and murderers elevated — Dr Magufuli is the one public servant who forsook worldly possessions. Mark 8:38 asks: “For what shall it profit a man, if he shall gain the whole world and lose his own soul?” Methinks the author in the good book must have had a great leader in mind,The simplicity of this Societal and moral giant is the one thing that remains an enigma to me and many. He always roots for the little guy. He abhors hierarchy and disdains flamboyance,he’s ruthlessly self-critical. He always puts himself last,He’s a rare breed.
Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
0755078854
-Bachelor of business administration in International business.
-Master of Leadership and Management.
Recent Publications;-
-Assessment on the Effects of Micro-financing on Poverty Reduction.