Hayati Magufuli alikuwa Nabii katika angle zifuatazo

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
15,103
22,551
Salaam, Shalom!!

Tunapoelekea katika kumbukumbu ya kukumbuka miaka 3 ya Mzalendo Magufuli,

Tujikumbushe misimamo yake iliyolivusha Taifa huku akiwaacha mbali viongozi wa Dini na Viongozi wa Vyama vya siasa na Dunia Kwa ujumla.

Sisi tusiokuwa na vyama tulikaa katikati na kupima upi Hasa ulikuwa ushauri wenye maslah ya Wananchi.

Viongozi wa Dini walikuwa tayari KUFUNGA nyumba za Ibada kuogopa corona, Magu akasema HAPANA msifunge, twendeni tukamwombe Mungu atatusaidia, na Kweli tukavuka salama.

Wanasiasa wa Upinzani walishauri tupigwe LOCKDOWN, Magu akagoma, akatoa HOJA kuwa wananchi wengi ni deiwaka, wasipotoka, familia haijala, na huo ndio ulikuwa UKWELI, maana Nchi zingine, watu walivunja Sheria ya lockdown Ili wakatafute chakula wakidai ni Afadhali kufa Kwa korona Ukiwa umeshiba, kuliko kufa Ukifa njaa umefungiwa.

Mwanasiasa mmoja, Mwenyekiti wa chama Cha upinzani akatoa wazo na kutaka wanaokaidi Chanjo, wakamatwe, wapingwe pingu na kuchanjwa Kwa lazima.

Wazo la kuhamisha IKULU Toka Dar Magogoni kwenda Dodoma, yalikuwa ni maono makubwa.

Kuanza mradi wa JNHP pia yalikuwa ni maono mema Kwa Taifa.

Kwa uchache, Itoshe kusema, Kwa Muda Mchache Mungu aliompa Magu kuwa Rais, Kweli alifanya KAZI iliyotukuka, mapungufu yake kama mwanadamu tuhakikishe hatuyafuati.

Ahsante Mungu Kwa zawadi ya Nabii Magufuli.

Amen
 
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni kwenye sakata la Corona/COVID-19 jamaa alikuwa mwamba na jemedari aliyeshinda vita mapema sana duniani. Dunia itamkumbuka katika hili.
Rabbon hafungwi na pingu za uchama linapokuja suala lenye maslah mapana ya Taifa.

Kwa Kweli mlipuko wa corona uliikuta Tanzania ikiwa strong chini ya Magufuli.

Mtu yule aliipenda nchi yake.

Katika hili la Corona nitasimama na UKWELI.

Mungu alimsaidia atuvushe.
 
Si Kweli,

Aliyetamgaza kifo chake, alisema kitu tofauti na Corona.

Hivyo acha uongo.
Huwa unafanya makosa sana kumpa mtu kichwa chako akuwazie badala yako. Hao hao unaowaamini ndio hao hao waliowatangezieni kuwa malaika wenu yuko fiti na anachapa kazi kumbe Bwana ashatwaa siku mingi sana. Tumia kichwa chako vizuri na sio ukigeuze kama kifaa cha kubebea meno!
 
Huwa unafanya makosa sana kumpa mtu kichwa chako akuwazie badala yako. Hao hao unaowaamini ndio hao hao waliowatangezieni kuwa malaika wenu yuko fiti na anachapa kazi kumbe Bwana ashatwaa siku mingi sana. Tumia kichwa chako vizuri na sio ukigeuze kama kifaa cha kubebea meno!
Ripoti ya daktari inasemaje?
 
Back
Top Bottom