Mafuriko makubwa yaikumba Dar es Salaam

Mafuriko makubwa yaikumba Dar es Salaam

Poleni sana hapo Dar. Huku kwetu milimani licha ya mvua kubwa namna hii lakini hamna mafuriko.
 
Kinondoni mkwajuni nyumba zimefunikwa na maji na watu kadhaa wameokolewa.
 
Si kipindupindu pekee Mkuu bali pia kuhara damu na malaria kwa ongezeko la Mbu na Dar ilivyo chafu!!

Sasa tutazamie kipindupindu na magonjwa mengine ya milipuko
 
Poleni sana mliokumbwa na mafuriko, hameni mabondeni jamani njooni huku nje ya mji, sisi watu wa mbezi ya kimara hatuna shida ya mafuriko, kuishi huku kunaraha yake bwana japo ni mbali tu kutoka mjini tunapofanyia kazi
 
Ohoo mara mwaka huu mvua Hanna,ohoo mara imeshuka ikapanda ...haya sasa mipango ya Mungu ndo inatimia kama alivyopanga mwenyewe iwe
 
Sina cha kusema
Miaka 50 ya uhuru hatuna Engineer hata mmoja wa kutuokoa?
Alafu tunasema maisha bora yataletwaje?
 
Mungu tuepushe na madhara ya miili, nafsi na roho zetu!.


Lawama zote ziiendee Ccm na serikali yake kwa kushindwa kuwa proactive wala reactive. Serikali ina wataalam wa miundombinu wengi ambao wamesoma vizuri wakahitimu (achana na wale wakupasishwa wa sasa), wameajiriwa na wanalipwa mishahara - kodi zetu kwa kazi hiyo.

Ni nini kinaifanya serikali ishindwe kuwatumia katika kuhakikisha miundo mbinu yetu iko vizuri ili kuepusha fedheha hii ya kurudia rudia kwa majanga ambayo yamepoteza uahi wa ndugu zetu, mali, na kuleta magonjwa ya milipuko yanayotugharimu fedha nyingi za kigeni na kudidimiza uchumi wetu? Ninaamini wataalam wana majibu sahihi ya kuboresha na kuimarisha miundo mibnu ili watanzania tuishi kwa amani na tuone mvua ni baraka na si laana ila serikali haitaki kuwatumia ama kwa kutokujali shida za wananchi ama kwa kutokujua thamani na maana halisiya utaalamu.

Ujenzi holela ambao ndio chimbuko kubwa linasopelekea athari za mvua kuwa mbaya na kwa kiwango kikubwa, unalelewa na serikali kutokuzingatia na kumaanisha kufanya kazi kwa ufanisi na kwa malengo ya kuboresha ustawi wa taifa.

Tuna mipango miji, upimaji na ramani wanalipwa mishahara kila mwezi january to december, na hadi marehemu wako kwenye payrolls za serikali. Lakini hawa watu, wanakuwa desk officers ama private dealers!.
Kuna ugumu gani wa kusurvey viwanja na maeneo kwa wingi ili anayehitaji kujenga aonyeshwe eneo lake kama vile route za magari ya abilia?
Ajabu hawa wataalam, kazi yao ni kwenda kupima maeneo kwa maombi ya watu binafsi baada ya ujenzi holela bila considerations za mahitaji muhimu ya general public, wanalipwa fedha sawa na private surveyors, kitu kinachokithirisha ukosefu wa miundo mbinu sahihi na mwisho ni kama tunavyoona.

Ni jambo lisilofikirika kwamba watu wanajenga mchana, serikali inaona haichukui hatua yoyote, badala yake inakwenda kuweka namba kwenye zile nyumba holela, inachukua kodi, wakati huo huo, umeme wanawekewa, na maji ya serikali wanapelekewa, bills wanalilpa kwa serikali kila mwezi, na soko wanajengewa, local Governments wanachukua levy, kodi wengine wanalipa na baraka zote za serikali kama vile hakuna kosa lolote lipo. Ni jambo la ajabu mvua zinaanza kunyesha, mafuriko yanaanza, serikali inawageuka eti wahame wamejenga mabondeni, mara wamejenga bila mifereji, mara eneo walilojenga si la makazi, mara walipo ni mkondo wa mto hivyo wameziba mto na hadhithi nyingi kibao.

SWALI LA KUJIULIZA, NIA THABITI YA SERIKALI KULINDA NA KUSIMAMIA MASLAHI NA USTAWI WA UMMA IKO WAPI?
KWA UZEMBE HUU, BILA KUBADILISHA UTAWALA, TANZANIA ITAKUWA BADO IPO KWA MIAKA MICHACHE IJAYO?
TAFAKARI!.
Aaah una hasira kwelikweli. Ninaungana nawe kwa mipango miji. Nina kesi kwangu jirani yangu kujenga ukuta bila kuacha nafasi kuyoka kwenye mpaka wa kisanja unaotutengamisha kwa kuzingatia mipango miji inavyotaka, nimelalamina hakuna kinachofanyika kwa vile jamaa kuwahi kwa wanasiasa wanaopita wakuu wa wilaya ni tatizo kweli. Dar ni tabu mtu a kidogo tu wengi wataokotwa India. Dar na Kuala Lumpur vinafanana sana lakini ni mara chache Kuala Lumpur kupata mafuriko!
 
Wakuu vipi foleni kutoka mjini,kupitia moroco mpaka sayansi,inatembea?
 
Tatizo kujenga ovyo bila mpangilio, kujenga mabondeni na ukosefu wa miundo mbinu ya kutolea maji wakati wa mvua,,,

Kinacho nishangaza tuko karibu na bahari tunaweza kuwa na miundo mbinu iliyo imara ya kupeleka maji baharini lakini tumekosa viongozi wenye upeo na uwezo wa elimu ya infrastructure
 
Njia ya Masana kuelekea Goba, imekatwa na maji mahali pawili!. Kutoka Tegeta kwenda Mwenge, foleni imeanzia Lugalo, ila kutoka Mwenge kwenda Tegeta, hakuna foleni, nikilinganisha na jana, nilitoka town saa 11 jioni, nikafika home saa 5 usiku, leo nimetoka saa 7 saa hizi niko home!, hadi watoto wanashangaa, dogo anashangaa kumuona dady saa hizi!, hivyo mvua hizi sio kila kitu ni balaa tupu,pia imesaidia!.

Pasco

Ukijarulibu kuaangalia kweli hii mvua ni janga, je hakuna uzembe wa miundo mbinu kwa hapo? Maana hapo Dar kukuta chemba ya choo inavuja katikati ya mji sio ajabu na nyinyi wakazi wa hapo mko happy tu huku mkiwa watanashati. Tupe feedback ukiachia kwamba ni janga, uzembe wa miundo mbinu umechangia kwa kiasi gani na nini kifanyike? Kumbuka hapa jf viongozi wetu wanapita huenda wakabeba chochote kwenye mapendekezo yetu.
 
Cheza mechi ya kirafiki mpwa siyo kama zile za mashindano kombe uwanjani 🙂🙂

Hahahahaaaa ndio narudi sasa! Naam ushauri wako na wa Mpwa MANI ulizingatiwa. Napata sasa kikombe cha chai ya tangawizi.
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom