COARTEM
JF-Expert Member
- Nov 26, 2013
- 3,622
- 3,696
Wazanzibar watakimbilia bara au oman.
wataenda Oman na Yemen
Wazanzibar watakimbilia bara au oman.
Hata huku kwetu hakuna mafuriko! Kote kwenye mafuriko ukiangalia vizuri utaona ni mkondo wa maji! Hivi pale Kimara hata ujenge shakalabaghala vipi yanaweza kutokea mafuriko kweli pale!!! Hivi huku Pugu tulivyojenga tunajua wenyewe mabona mafuriko hatuyaoni!!!mmh!! kama tatizo ni mipango miji mbona kwangu mafuriko ya hivyo hakuna ila yapo zile sehemu maarufu kwa mafuriko?? jangwani kigogo kila siku wanafurikwa lakini wapo tu
Sisi watu ni wapumbavu manake sio wajinga ni wapumbavu! Pale Jangwani hata kama ni mgeni mjini na unapita majira ya kiangazi, bado unajua kwamba lile eneo ni majanga! Na mimi tangu nipate akili, kila mwaka ni ugimvi kati ya serikali na watu wa Jangwani kwa jambo lile lile! Labda wanataka serikali ipeleke jeshi pale na kuvunja nyumba kwa nguvu lakini wakifanya hivyo, hao hao wanaojifanya kuilaumu serikali na kuufunika upumbavu wetu wenyewe ndio watakaokuja tena na kuilaumu serikali kwa kutumia nguvu.Umeona hiyo mkuu? Mvua za dar za kawaida sana tu. sasa raia wa dar watafikia hatua watalalamika nyumba zao chafu sababu serikali haiwagawii mifagio na maji ya kudekia
N kwel njoon mikoan uku izo shda hamnagan.kwa nadra sanaaaaa
Hata sisi wa Dar es salaam ambao hatuna tamaa ya kuishi karibu na Kariakoo ni raha tupu! Sema tu ikinyesha mvua, TENESKO huwa wanakata umeme vinginevyo ningesema litwange tu; na hivi nipo likizo ndo kabiaaaaasa!Sisi wa mikoani raha tupu pole sana
Labda na Kariakoo uihamishie Dodoma ndo labda watu wa Jangwani na Kigogo watahama!Serikali hamieni Dodoma.
Kuna mitaa ambayo serikali ingepiga marufuku watu kuweka makazi, lakin watz ni watu wa kusahau haraka sana
Ikiwa wewe mwenyewe unajua kabisa hili ni bonde na kila mwaka yanatokea mafuriko na bado unajenga, so why should I care about you? Hivi kuna mtoto mdogo anayejenga zile nyumba ili tumsamehe kwa kuwa hana akili? Wewe ni mtu mzima unataka kuvuka mtoni na watu wanakuambia huo mto una mamba na viboko lakini unapita tu; unaliwa na mamba halafu aje mtu mwingine aseme kwanini hamukushika ili asipite? Serikali hii sio serikali inayoongoza ng'ombe bali inaongoza wanadamu ambao Mwenyezi Mungu amewajaalia utashi wa kuelewa baya na zuri. Ikiwa serikali imeshasema mara kadhaa kwamba wananchi hameni mabondeni na watu wanajifanya vichwa maji, basi subiri watu wapoteze watu wao wa karibu kabisa kama mke au watoto, watahama tu! Au mnataka serikali itumie nguvu halafu mrudi tena hapa na simulizi za ukiukwaji wa haki za binadamu?Alafu wanakuambia serikali haihusiki na majanga haya. Wakati wanaacha watu wanajenga kiholela, wanaruhusu nyumba zijengwe mabondeni...hakuna master plan ya jiji..sewage and drainage system tunazisoma tu kwenye mitandao...serikali sikivu imekufa mpwa!!
Ya jana ilikuwa kali, nimetoka mjini posta na private car saa kumi na moja jioni, nimeingia mataa ya fire saa sita na dakika 12 usiku mbezi mwisho nikafika saa saba, saa nane kasoro ndo nilikuwa nakula chakula cha jioni. Leo sijakanyaga mjini, kama ndo na Leo itakuwa kama jana nawapa pole kwa watakao kutwa na mafoleni
hivi maji hayaingii kwenye papuchi kweli, asije akiondoka hapo anaenda kuchutama na kujaza kindoo kidogo.
Alafu wanakuambia serikali haihusiki na majanga haya. Wakati wanaacha watu wanajenga kiholela, wanaruhusu nyumba zijengwe mabondeni...hakuna master plan ya jiji..sewage and drainage system tunazisoma tu kwenye mitandao...serikali sikivu imekufa mpwa!!
Mitaa kamaa ya kigogo bondeni kule na Jangwani sio ya kusubiri serikali ile inabidi mwananchi mwenyewe ujiongeze ukisubiri serikali inakula kwenu
Ok Ok.. Ok...Ikiwa wewe mwenyewe unajua kabisa hili ni bonde na kila mwaka yanatokea mafuriko na bado unajenga, so why should I care about you? Hivi kuna mtoto mdogo anayejenga zile nyumba ili tumsamehe kwa kuwa hana akili? Wewe ni mtu mzima unataka kuvuka mtoni na watu wanakuambia huo mto una mamba na viboko lakini unapita tu; unaliwa na mamba halafu aje mtu mwingine aseme kwanini hamukushika ili asipite? Serikali hii sio serikali inayoongoza ng'ombe bali inaongoza wanadamu ambao Mwenyezi Mungu amewajaalia utashi wa kuelewa baya na zuri. Ikiwa serikali imeshasema mara kadhaa kwamba wananchi hameni mabondeni na watu wanajifanya vichwa maji, basi subiri watu wapoteze watu wao wa karibu kabisa kama mke au watoto, watahama tu! Au mnataka serikali itumie nguvu halafu mrudi tena hapa na simulizi za ukiukwaji wa haki za binadamu?