Yap best nakubaliana na wewe, lakini ukweli ni kwamba viwanja watu wanauziana kyenyeji kwa bei nafuu, na wengi hukwepa gharama za upimaji, ni watu wangapi wanaishi kwenye nyumba hata miaka 10 nyumba kiwaja hakija pimwa wala haijui hati???????????? mbona oysterbay, masaki hakuna mafuriko?????????
Yan sasa hivi huku mbezi beach ni mvuaa balaaaa
wa mjini tokeni mapema mtalala njiani kama mimi jana
Dar Tambararee - Serikali sikivu.
Samahani dada, umemaliza darasa la ngapi? Nata nikufowardie jinsi mipango miji inavyotengenezwa na mafuriko ni ya kawaida wala yasingetokea.
By the way. Kwa kifupi ukishindwa kuelekeza maji pa kupita maji yenyewe yanakulazimisha kupita na fidia juu. Sasa dada hilo siyo jukumu la mtu mmoja mwenye kaploti ya mita 60 kwa mita 40. Kuna mamlaka husika inayoitwa mipango miji na wizara yenye waziri, naibu waziri, katibu mkuu, wakurugenzi, wataalam wa kupima na kuratibu miundo mbinu za miji na majiji....nk...nk....sasa hawa ndo tunawatupia lawama ambao ndo inaitwa "serikali"
Serikali ipo kwa ajili yetu sote ila haiwajibiki kwetu. Kwa mujibu wa katiba pendekezwa.
Serikali lazima ilaumiwe kwani hata ile sheria ya kujenga mita sitini kutoka baharini haaifuati. Kutokujenga sehemu za wazi hawazifuati (huko ndiko maji yanapumulia). Kuna sheria ya kutokujenga mabondeni watendaji wanaruhusu! Mikondo ya maji haitakiwi kuzibwa lakini wananchi wanaziba na serikali inaangalia tu!
Tunahitaji serikali ya kisayansi na kama ni kuhamisha watu wahamishwe kwa gharama, waliojenga sehemu za wazi wavunjiwe mifereji ijengwe sehemu husika nchi nzima.
Ukiwa na miundo mbinu mizuri hata mafuriko yakija huwa yanaondoka baada ya muda mfupi.
Ni nani anayejenga au kupanga Jangwani huku akiwa hafahamu kwamba pale Jangwani kila mwaka ni mafuriko? Serikali inaweza kulaumiwa lakini wananchi wenyewe ni wapumbavu tena wapumbavu kweli kweli! Kwa wanaoishi Dar es salaama wanafahamu ugomvi usioisha kati ya serikali na wananchi wa mabondeni hususani Jangwani! Lakini leo hii ukipita mkong'oto pale na kuwalazimisha watu kuhama, baadae ni nyinyi ndio mtarudi tena hapa na kuja na hoja za haki za binadamu!!ndugu yangu Eli79. Huyo mwehu anayetetea serikali anamaanisha kuwa raia mwenyewe afanye hizo hesabu zoote, achore mchoro, aprove mwenyewe, mwenye kiwanja adesign sewage system ya jiji zima drainage system ya mtaa, jiji, nk......
NAKUPINGA KABISA % 100! Dar haijawahi na wala haitawahi kuwa ama kukumbwa na mafuriko ya maji ya mvua.
ILA Miaka yote Dar imeshuhudia MAFURIKO ya nyumba kwenye mikondo na njia za maji.