ITAMKUMBUKA KAMA DIKITEITA ALIYETOKEA TANZANIA KAMA ILIVYO HISTORIA YA AMINI HAITAFUTIKANi wazi kuwa hata ungefanya mema mangapi kwa wanadamu kamwe usitegemee kupata sifa,pongezi au kutiwa moyo na wote, NASEMA KAMWE.
Tumeshuhudia viongozi kama Gaddafi licha ya kuwapenda sana watu wake na kutumia rasilimali za nchi kwa manufaa ya wananchi, lakini wapi mwisho wa siku alichukiwa hadi kuuwawa kinyama, LEO WANAJUTA na mifano mingine lukuki kama hiyo.
Kwa Tanzania kama ilivyo kwa nchi za wanadamu wengine wenye hulka fanani,usitegemee fadhila wala pongezi kutoka kwao hata kidogo.Ila ukweli ni kuwa:
- Mengi mazuri rais ameyafanya na wote ni mashahidi ila kwa sababu ya UCHAMA basi hakuna anayeona kitu chochote kimefanyika.
-Ni nani aliyeweka mwiko mkubwa huu wa vyama pinzani kutosifia utendaji wa rais hata kwa yale yanayolenga maslahi ya kizazi chetu na kijacho?.au chama tawala kutosifia upinzani hata pale wanapofanya mema yanayohusu maslahi mapana ya nchi hii?
Je huu uzalendo unaoimbwa kuchwa kutwa una maana gani ikiwa yale yanayoguza maslahi ya taifa yanabezwa na kutupwa kama vitu visivyofaa.Kwa hali hii napata kigugumizi ikiwa wale wale wanaoimba uzalendo ,hawayataki yahusuyo uzalendo .Je si unafiki huu?.
Basi nasema ikiwa uzalendo ndio nguzo ya maendeleo ya taifa letu, MH.MAGUFULI KAZA UZI HISTORIA ITAKUKUMBUKA.