Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Wakati fulani tunaweza kusema tatizo la ufisadi na uporaji wa rasilimali zetu linatokana na mianya ya kikatiba na kisheria, hivyo tunahitaji Katiba mpya. Lakini ukitafakari kwa makini utagundua mbona sasa mafisadi na wabadhirifu wanakiona cha " mtema kuni" na Katiba ni ile ile, kumbe tatizo halikuwa Katiba bali aina ya uongozi. Basi mwaka huu 2018 tuunganishe nguvu zetu kumsaidia Rais Magufuli kuyatokomeza mafisadi na majizi yote na kuifanya ile hadithi ya shamba la bibi kubakia historia. Najua watuhumiwa wengi wa ufisadi wako lupango kwa sasa, lakini kuna wachache wamefichamia pahala fulani na wanatetewa kweli, basi watanzania kwa umoja wetu hima tuushinde ufisadi. Nawasilisha!
Tungekuwa na katiba iliyo strong huyu Magufuli leo hii angekuwa lupango ananyea ndoo kwa ufisadi wa kivuko cha Bagamoyo pamoja na ufisadi wa nyumbani za serikali alizouza na kuwagawia awala na ndg zake.

Tungekuwa na katiba strong Mkapa, Kikwete na viongozi wengi tu waandamizi ndani ya ccm leo hii wangekuwa wananyea debe bila chenga.

Ebu twambie mafisadi gani yamepelekwa kwenye ile mahakama ya mafisadi?
 
Mkuu hata Singasinga humuoni?!!
Singasinga kiini macho tu huyo. Hana kesi. Kwani alivunja benki ipi? Waliotetea huo upuuzi kudai zile ni hela za IPTL mbona hawajakamatwa? Aliyeruhusu hizo hela zichotwe Benki kuu mbona hajakamatwa? It is just a matter of time Ruge na Singa watatoka tu maana hawana kesi. Ili kesi iwe binding lazima uianze kwenye mzizi sio matawi. Hawa wawili ni matawi tu. Kuna watu walisuka hilo deal na kuruhusu hizo pesa zitoke. Wako wapi?
 
Singasinga kiini macho tu huyo. Hana kesi. Kwani alivunja benki ipi? Waliotetea huo upuuzi kudai zile ni hela za IPTL mbona hawajakamatwa? Aliyeruhusu hizo hela zichotwe Benki kuu mbona hajakamatwa? It is just a matter of time Ruge na Singa watatoka tu maana hawana kesi. Ili kesi iwe binding lazima uianze kwenye mzizi sio matawi. Hawa wawili ni matawi tu. Kuna watu walisuka hilo deal na kuruhusu hizo pesa zitoke. Wako wapi?
Hapa ndipo pa kujiuliza wako wapi hawa wenye jukumu la Authorisation juu ya malipo hayo:

Gavanna Wa Benki kuu.
Waziri wa Fedha
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha
Waziri wa Nishati na Madini
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini
Paymaster General
Rais wa nchi (ili mabilioni hayo yatoke lazima ruhusa ya rais itoke)
 
Hapa ndipo pa kujiuliza wako wapi hawa wenye jukumu la Authorisation juu ya malipo hayo:

Gavanna Wa Benki kuu.
Waziri wa Fedha
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha
Waziri wa Nishati na Madini
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini
Paymaster General
Rais wa nchi (ili mabilioni hayo yatoke lazima ruhusa ya rais itoke)
Ndiyo maana kila kesi ikitajwa prosecutor anadai uchunguzi haujakamilika. Mara ya mwisho ruge aliwaambiwa atawasaidia kuwambia nani alichota hizo pesa. Hawa wawili ni mbuzi tu wa kafara.
 
Binafsi nimefurahishwa na kasi ya Dkt. Magufuli. Naamini wapo pia wengi wanaoungana nami katika furaha hii. Magufuli ameanza kwa kasi ambayo kama ataimaintain, Tanzania haimalizi miaka mitano itakuwa tayari ni nchi yenye kipato cha kati.

Hata hivyo wapo baadhi yetu ambao wanakejeli kasi hiyo. Hao kwangu ni watu waliozoea ubwete na bora liende!. Wanamwona Magufuli kuwa ni mtu atakayekuwa kauzibe kwao!

Wapigaji wote, wavivu wote na wazee Wa madili wote watamchukia Magufuli ila mi niseme na niwaombe tu kwamba tumpe support huyu jamaa kiukweli atatufikisha mahali Fulani!

Tuwafichue wote wanapanga kumhujumu (najua wanajulikana), tuwakatae kwani hawana nia njema na taifa letu.

By June 2018, tunatakiwa kuna na ndege mpya 6 zinatembea, ikiwemo Boeing ya abirria 260+, miracles, mimi naweza kusema...., Lakini mimi ninachoshangaa, mbona baadhi yetu haya hawayaoni?
 
sasa nyie wa humu kwenye mitandao ndio
wasomi
watoto wa mjini
mna sijui exposure
Na mawazo yenu ndio haya eti bora mtu kuliko katiba aibu kubwa je mamilioni ya watanzania walioko vijijini watatoa mawazo gani?
haya mambo anayofanya magufuli zinatakiwa kufanywa na mfumo sio kutegemea mtu mmoja .akiondoka tu tunasubiri miaka mingine 30 au 50 kabisa. Aibu kubwaaaa
 
Napata faraja sana ninapoiona Tanzania ikihamia kwenye uchumi wa kati ndani ya miaka 5 ijayo.

kwa kuwa na miundombinu bora na ya kisasa chini ya usimamizi kazi wa kamanda mkuu JP Magufuli. Isitoshe yafaa kusema Tanzania si shamba la bibi tena kwa wanyonyaji wachache kuja kuvuna madini yetu na kutuacha hohehahe.

Biashara ya meno ya tembo na madawa ya kulevya sasa Tanzania ni moto hapafai tena kwa waliozoea vya kunyonga.

Usimamizi wa rasilimali za umma, utumiaji wa teknolojia kukuza uchumi na kuongeza tija si jambo la kuhoji tena katika nchi yetu pendwa Tanzania.

Afya na Elimu kwake JPM ni vipaumbele bila kusahau maji na umeme kwa vijiji na miji yote ifikapo 2025.

Kilimo, Ajira na Viwanda ni mambo ambayo mkuu wetu yanamchoma moyo wake kwa kuwekea mipango mikakati ili atokomeze umaskini kwa vijana wetu ifikapo 2025.

Mwenyezi mungu tulindie raisi wetu huyu na umuepushe na watu fitina walioja husda kwenye vifua na nyuso zao.

Ewe mnyaazi mungu mwingi wa rehema nakuomba umrehemu na kumjaza kudra na baraka zako rais wetu mpendwa John Pombe Joseph Magufuli na chama chake pendwa CCM.

Nakuomba Mnyaazi mungu uwatie upofu wanaopingana na juhudi zake za kumkomboa mtanzania maskini kutoka kwenye lindi la umaskini ili mtanzania aweze kuishi vyema ndani ya nchi yake kwa amani, furaha na kwa riziki kubwa kubwa.

Amiiin Amiiin Amiin.
 
Ficha ujinga wako na Ccm yako, maisha yanazidi kuwa magumu wewe unaleta hoja za kingese ngese hapa.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Katika mfumo wa kiuchumi wa dunia, kuna madaraja matatu.
La kwanza ni daraja la nchi zinazojulikana kama 'Core Countries'---Hizi ni nchi ziliizoendelea kiviwanda mfano U.S. U.K. France etc.

Kundi la pili ni kundi la nchi zinazojulikana kama Semi-periphery countries---Hizi ni nchi ambazo zinafuatia baada ya zile 'core countries'. Kwa Afrika nchi zilizomo/iliyomo kwenye daraja hili ni moja tu Afrika Kusini.

Daraja lingine ni lile la nchi zinazojulikana kama 'Periphery countries'----Hizi ni nchi ambbazo ni tegemezi, na zina hali mbaya kiuchumi kiasi kwambba bila 'core countries' na 'semi-periphery countries', ukweli ni kwamba zinaenda ICU kupumulia machine.

Sasa kama kwa Afrika nchi yenye uchumi wa kati ambayo ni Afrika Kusini pekee, do you think Tanzania itafikia uchumi wa kati 'semi-periphry countries' ndani au baada ya miaka mitano? Egypt, Nigeria, ziko juu sana kiuchumi kufanananisha na sisi, na hazipo kwenye uchumi wa kati, sasa kwa hali hii unadhani Tanzania itaweza kuibuka na kuzipita nchi hizo kisha kufika kileleni ili kuungana na Mwafrika Kusini ambaye yeye ndiye hasa aliyepo kundi hili la 'Semi-Periphery' countries?

Jamani, tusiwe tunapotoshana, uongo mwingine ni dhambi kubwa. Mi nadhani ungesema, na kutoa wito kwa kila Mtanzania kufanya kazi kwa bidii ili kujenga uchumi mzuri na kuandaa mazingira mazuri ya kuchumi hapo baadaye na si kusema kwamba eti ndani ya miaka mitano tutakuwa kwenye uchumi wa kati. Hilo haliwezekani, na halitokuja kuwezekana. Mark my words!
 
Back
Top Bottom