Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Informer

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2006
Messages
1,407
Points
2,000

Informer

JF-Expert Member
Joined Jul 29, 2006
1,407 2,000
Binafsi nimefurahishwa na kasi ya Rais Dkt. Magufuli. Naamini wapo pia wengi wanaoungana nami katika furaha hii. Rais Magufuli ameanza kwa kasi ambayo kama ataimaintain, Tanzania haimalizi miaka mitano itakuwa tayari ni nchi yenye kipato cha kati.

Hata hivyo wapo baadhi yetu ambao wanakejeli kasi hiyo. Hao kwangu ni watu waliozoea ubwete na bora liende!. Wanamwona Magufuli kuwa ni mtu atakayekuwa kauzibe kwao!

Wapigaji wote, wavivu wote na wazee wa madili wote watamchukia Rais Magufuli ila mi niseme na niwaombe tu kwamba tumpe support huyu jamaa kiukweli atatufikisha mahali fulani!

Tuwafichue wote wanaopanga kumhujumu (najua wanajulikana), tuwakatae kwani hawana nia njema na taifa letu.

Habari zaidi, soma =>Toka kwa Wananchi: Kero na Vitendo vya kifisadi vinavyoendelea nchini vinavyotakiwa kufuatiliwa...
 

ss3

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Messages
213
Points
195

ss3

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2015
213 195
Kweli huyu ndiye rais niliyemsubiri kwa miaka mingi sana. Sikuhizi yule jamaa yangu aliyekuwa anafanya kazi pale halmashauri ya manispaa ya kinondoni simuoni tena. Yaani yeye alikuwa anatembepea maeneo mawili tu. Kwenye ATM na BAR. Anajifanya eti yuko serikalini ndo maana hafanyi kazi. Na kama wiki hivi sijamwona alafu nikimpigia simu anasema yuko busy. ***** ngoja aje amkute hayuko apigwe chini ntacheka alafu hata hana nyumba.
Magufuli hebu mtembelee na huyu umfinye kidogo ajifunze kuishi kwa kuchubuka kama sisi
 

farajamilele

Member
Joined
Feb 12, 2014
Messages
90
Points
125

farajamilele

Member
Joined Feb 12, 2014
90 125
tutampima kwa matokeo kama vifaa vya kutosha mahospitalini, madawa ya kutosha, wafanyakazi wa kutosha hasa elimu na afya, vitendea kazi vya kutosha mashuleni, wanafunzi wenye sifa elimu ya juu wote wanapata mikopo, barabara nzuri, maji salama, umeme wa uhakika, uchumi wa mtu mmoja mmoja umekua n.k hatutampima kwa ziara maofisini
 

1954

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2006
Messages
6,465
Points
2,000

1954

JF-Expert Member
Joined Nov 14, 2006
6,465 2,000
Tumechoka dharau kutoka kwa vijinchi vidogovidigo mh. Raisi turudishe kwenye chati ya Afrika turudishe heshima we are big nation.
Ni kweli kabisa. Tuko nyuma kwa sababu ya kuleana. Hatuna nidhamu ya kazi wala nidhamu ya maisha. Tunaishi kwa kubabaisha tu. Tumekuwa wachuuzi wa bidhaa za nje ikiwemo mitumba. Hatufanyi uzalishaji wa bidhaa. Polisi barabarani wanakula rushwa kama sala yao. Nenda pale kibaha maili moja uone namna polisi wenye vitambi wanavyokimbilia mabasi ya abiria kutoka mikoani yanavyoingia stendi. Konda wanaweka rushwa kwenye ratiba za mabasi na polisi wanachukua 'posho' hizo haramu. Watu hawafanyi kazi ofisini ......eti wanakweda kunywa chai........... cai Ukiigia .....gia nyi gB
 

Rodney01

JF-Expert Member
Joined
May 14, 2013
Messages
749
Points
1,000

Rodney01

JF-Expert Member
Joined May 14, 2013
749 1,000
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli , leo mchana amefanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kukutana na hali ya kumsikitisha.

Rais amesikitishwa na kuhuzunishwa na hali ya huduma kwa wagonjwa hususan wanaolala chini. Pia amekasirishwa na hali ya kutokujali wala kushughulikia vifaa vya kufanyia kazi ambapo amekuta mashine muhimu za uchunguzi wa magonjwa kama vile MRI na CT-SCAN zikiwa hazifanyi kazi kwa muda wa miezi miwili sasa, ilihali mashine kama hizo katika Hospitali za binafsi zinafanya kazi na wagonjwa wanaelekezwa kwenda kutafuta huduma huko?. Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema na kutoa maelekezo yafuatayo :

Rais amevunja Bodi ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambayo ilishamaliza muda wake na amemteua Prof. Lawrence Mseru , kukaimu nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Muhimbili kuanzia kesho tarehe 10 Novemba, 2015.

Dkt. Hussein L. Kidanto ambaye ndiye anayekaimu hivi sasa, amehamishiwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ambako atapangiwa kazi nyingine.

Balozi Sefue pia amesema, Rais ametoa wiki moja na kwa vyovyote si zaidi ya wiki mbili kwa uongozi mpya wa Muhimbili kuhakikisha kuwa mashine zote za uchunguzi wa magonjwa ambazo hazifanyi kazi zinafanya kazi na kuhudumia wananchi kama ipasavyo.

Tayari Wizara ya Fedha imetoa shilingi bilioni 3 kwa ajili ya kazi hiyo na kulipa madeni ya ukarabati wa mashine za uchunguzi wa magonjwa nchini.

Hata hivyo Katibu Mkuu Kiongozi amesema kuanzia sasa hospitali zote nchini zinatakiwa kutenga fedha kutoka kwenye mapato yao wenyewe na kuhakikisha mashine na vifaa vyote vya kazi vinafanya kazi wakati wote (Regular Maintenance).

Balozi Sefue pia metumia nafasi hii kuwaagiza watendaji na viongozi wote katika sehemu za kazi kuhakikisha wananchi wanahudumiwa ipasavyo na kazi za umma zinatekelezwa ipasavyo.

Hakutakuwa na huruma kwa watumishi wa Umma wasiojali wananchi na mahitaji yao. Amesisitiza Balozi Sefue.

Mwisho

Imetolewa na;

Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu ? Dar es Salaam.
9 Novemba, 2015
 

William Mshumbusi

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2012
Messages
918
Points
225

William Mshumbusi

JF-Expert Member
Joined Mar 27, 2012
918 225
Ziara za magufuli na maagizo makali havikuwa vitu vipya kwangu kwani ata Mjomba alikuwa hivyohivyo.

namuona Raisi wangu anafanya maamuzi. Bila kujari yuko sahihi kiasi gani kwani ni bora kufanya maamuzi ukakosolewa na wachache kuliko kuogopa kufanya uamuzi. Ameanza kuikata kiu ya maamuzi magumu niliyoitamani kutoka kwa Lowassa.

Nashauri baada ya kuunda balaza la mawaziri Raisi wangu awapangie majukumu mazito mawaziri wake na awasisitize wawe wepesi kufanya maamuzi juu ya wizara zao na kuweka utaratibu utakaowezesha kujua na kusimamia hadi ngazi za chini kabisa ya idara zao.

Mfano waziri wa fedha aweze kuwajibishwa kwa kushindwa kuchukua hatua kwa ubadhilifu kwenye halimashauri

Au waziri wa elimu aweze kuwajubishwa kwa utoro na uzembe unaofanywa na walimu shuleni

Au Waziri wa afya awajibishwe kwa miji kujaa taka kila kona .

Hii inamaana kubwa sana hawezekani raisi agundue uozo mkubwa kwenye idara chini ya wizara unayoongozwa na waziri fulani na kuchukua hatua alafu waziri abaki salama. Waziri anasimamia wizara moja tu wakati raisi anaangalia wizara zaidi ya kumi na tano.

Hivyo hivyo waziri akigundua uozo kwenye idara iliyo chini yake sana mfano waziri wa elimu agundue shule fulani walimu hawahudhurii shuleni kabisa anatakiwa amwajibishe mkurugenzi na afisa elimu kwa tukio hilo kwani haiwezekani waziri agundue uozo chini alafu mkurugenz abaki salama wakati waziri anaangalia Tanzania nzima na mkurugenzi anaangalia halimashauri moja tu.

Pia mkurugenzi adili na wakuu wa shule.

Hivyo basi Rais wa ngu ukikuta uozo dili na mawaziri tu mawaziri ndio watajipanga, Na waziri wa kwanza kumfukuza hiyo wizara yake uisimamie wewe kwa muda ili mawaziri waone mfano.
 

1954

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2006
Messages
6,465
Points
2,000

1954

JF-Expert Member
Joined Nov 14, 2006
6,465 2,000
Naogopa wasije wakamdedisha
Rais wetu apewe ulinzi mkubwa. Wazalendo wa kweli wa nchi hii wanataka maendeleo ya kweli. Wanataka uozo uliopo katika jamii yetu utokomezwe kwa kasi. Viongozi wamekuwa kama miungu watu. Wezi ndio wanapewa nafasi katika taasisi zetu. Waadilifu katika nchi hii ni kama hawatakiwi. Wahuni tu wanapewa madaraka makubwa kwa kujipendekeza kwa viongozi. CCM kumeoza kwa sababu ya kubebana. Serikali nako kumeoza kwa kuwa CCM kumeoza. Taasisi za CCM zimeoza hazina viongozi wa maana wamejaa wababaishaji. Taasisi za serikali nazo zimeoza kwakuwa wanawekwa watu wasio na uwezo. Asilimia 90 ya wakuu wa wilaya hawana uwezo. Uozo uko pia kwenye halmashauri. Halmashauri zimekuwa kitovu cha ulaji. Nchi hii ni lazima ikombolewe kutoka kwa viongozi mafisadi. CCM ijisafishe na serikali nayo isafishwe.
 

crabat

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2012
Messages
4,268
Points
2,000

crabat

JF-Expert Member
Joined Dec 28, 2012
4,268 2,000
Wakati tuki furahia haya ya nagufuli , tuna muomba amalize ya zanzibar maalim aapishwe amsaidie naye aondoe uoza huko znz..seif hataki mzaha na kazi ...mpe haki yake Tanzania kwa ujumla ibadikike
 

Forum statistics

Threads 1,389,319
Members 527,908
Posts 34,022,815
Top