Maeneo muhimu ambayo serikali zetu zinapaswa kuzingatia wakati wa mazungumzo yao na makampuni ya mafuta ya mafuta na gesi

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
6,318
8,229
Uvumbuzi wa mafuta na gesi huleta msisimko mkubwa sana katika taifa. Mara nyingi mataifa haya yenye utajiri wa rasilimali za mafuta na gesi hutafuta ushiriki wa makampuni ya kimataifa yenye rasilimali za fedha na utaalamu ili kusaidia kuzalisha na kuyauza mafuta na gesi katika mataifa hayo ili tu kuweza kuinua uchumi wa mataifa hayo.

Mara nyingi serikali na makampuni ya mafuta na gesi huweka juhudi kubwa katika kuelewa masuala ya kiufundi na kibiashara ya kuendeleza miradi ya mafuta na gesi. Kwa kweli, hata hivyo, changamoto kubwa katika miradi hii ya mafuta na gesi kwa serikali huwa ni swala zima la mazungumzo zidi ya kampuni za mafuta na gesi zinazowekeza.

Hata hivyo, mara tu wataalamu wa mataifa hayo wanapoanza kufanya mazungumzo ya kujadili mikataba itakayotumika, hujikuta kwamba makampuni makubwa ya mafuta na gesi yanakua na rasilimali nyingi za kifedha, ujuzi bora wa kutafuta maeneo yenye mafuta au gesi, na zaidi uzoefu katika mazungumzo ya mikataba.

Kiukweli nchi nyingi ambazo makampuni ya mafuta na gesi huingia kuwekeza huwa na rasilimali chache kuliko makampuni ya mafuta na gesi yenyewe. Kwa mfano, mapato ya Exxon Mobil ya dola bilioni 371 yalizidi pato lote la Saudi Arabia lililokua na utajiri wa mafuta la dolla bilioni 281. Hivyo mazungumzo na kampuni kama hiyo yenye utajiri lazima yawe magumu.

Lakini kiukweli makampuni ya mafuta na gesi huhamasika sana wakati wa mazungumzo ya mikataba ya mafuta na gesi. Mara nyingi huzingatia gharama na uwekezaji waliofanya kwenye utafutaji wa mafuta na gesi na idadi ya visima vikavu vilivyopatikana. Hivyo wao macho yao yote wakati wa mazungumzo hutafuta kurejesha kwa haraka gharama hizo za nje ya mfuko katika mazungumzo yoyote watakayofanya.

Pia makampuni ya mafuta na gesi hukiri kwamba hupaswa kufanya kazi katika hali na mazingira magumu sana ya ufisadi na rushwa, ambayo huhitaji taasisi za kimataifa na serikali ambazo kampuni za mafuta na gesi zinakuazimewekeza wakati fulani ili kutoa msaada wa "kisiasa". Rais wa kampuni fulani huru ya mafuta na gesi alisema: "Tunapaswa kukabiliana na machafuko lakini kisha tunabasamu hivyo tunapata pesa katika machafuko."

Kampuni za mafuta na gesi mara nyingi hurekebisha mtindo wao wa mazungumzo kulingana na tafsiri zao za mazingira ya kisiasa ambayo hufanya kazi. Wakiwa wamezoea kushughulika na serikali za kimabavu au katika nchi zilizokumbwa na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe, kampuni za mafuta na gesi mara nyingi huleta ulinzi binafsi, mtazamo usio na maelewano na wa kiburi kuelekea mazungumzo.

Je ni masuala gani muhimu hupaswa kuzingatiwa wakati wa mazungumzo ya mikataba ya mafuta na gesi?

(1) Masuala ya kiufundi na biashara
Wakati wa mazungumzo ya mikataba ya mafuta na gesi, masuala ya kiufundi na biashara ni mambo ambayo hutakiwa huzingatiwa sana. Mara nyingi hili ndilo eneo ambalo huwa na mgogoro wakati wa majadiliano. Kampuni nyingi za mafuta na gesi hutaka kulimiliki eneo hili. Na katika eneo hili mara nyingi kampuni huajili wataalamu waliohitimu katika eneo hili. Kiukweli asilimia 90-95% ya juhudi za majadiliano hutumika hapa kwenye eneo la kiufundi na biashara.

(2) Maswala ya kimazingira, kijamii, kiuchumi na kisiasa
Maswala ya kimazingira, kijamii, kiuchumi na kisiasa ni mambo ambayo hupuuzwa kwa kiasi wakati wa mazungumzo. Lakini masuala hayo ni muhimu sana pia wakati wa kujadili mikataba ya mafuta na gesi.

Imewahi kusisitizwa na mtendaji mkuu wa kampuni ya mafuta ya zamani ya kimataifa kwamba muda na juhudi kidogo sana hutumika kwa upande wa "watu" wa mchakato wa kuendeleza mafuta na gesi, na matokeo yake ni kwamba hatari nyingi muhimu zaidi za mazungumzo na makubaliano yanayofuata hupuuzwa.

Hivyo mara nyingi kujadili mgawanyo sawa wa mali za mafuta na gesi na makampuni haya ya kimataifa huwa ni changamoto kubwa na huhitaji uwekezaji mkubwa wa muda na pesa katika kukusanya timu ya wataalam wa kufanya mazungumzo. Hivyo wataalamu wa upande wa serikali wanatakiwa kujua masuala muhimu ya kujadiliana na makampuni haya kabla ya kuanza mazungumzo.

Kiukweli macho mengi huwa kwenye mazungumzo ya mikataba ya mafuta na gesi, sio tu yale ya pande mbili kuu yaani serikali na kampuni za mafuta na gesi zinazowekeza. Wamiliki wa ardhi pia mara nyingi jamii za wakazi ambao ardhi yao huathiriwa wao pia hudai fidia kwa matumizi na usumbufu wa mali zao katika ardhi yao ambayo mradi utapita. Hili pia hutakiwa lizingatiwe sana, hata kama vikundi vya watu hao sio sehemu ya mchakato rasmi wa mazungumzo.

Wenyeji wa mahali mafuta na gesi ilipo gunduliwa ambao hawawi kwenye orodha ya mambo ya kuzingatia kwenye mkataba wa mafuta na gesi, mara nyingi wao hudai sehemu yao kwa njia ya ajira na malipo ya fidia kwasababu ya mradi kuanzishwa kwenye eneo lao. Madai haya yatalazimika kushughulikiwa, na kutatuliwa kwa njia bora, kupitia mchakato wa kisiasa wa ndani ya nchi, na, ikiwezekana, kama sehemu ya mazungumzo ya jumla ya mkataba wa mafuta na gesi.

Hivyo makampuni ya mafuta na gesi mara nyingi hutoa ahadi maalum za kutoa mafunzo na kuajiri wazawa, na pia kusaidia jamii kwenye miradi ya maendeleo na mshikamano. Na hili ndilo la mwisho katika kile kinachoitwa maswala laini (au ya kijamii). Kwa mapana zaidi, mijadala ya kisiasa kuhusu jinsi ya kutumia mali ya mafuta na gesi ambayo kiukweli bado haijapatikana huendelea kutawala haraka masikioni na midomoni mwa watu ndani ya taifa, na hata kusababisha kuenea habari zisizo za kweli. Mashinikizo ya kisiasa hupelekea kudhoofika kwa mazungumzo yanayotarajiwa zidi ya makampuni ya kimataifa ya mafuta na gesi kwa kuanzisha kwa hila ratiba isio sahihi, ambayo ni ya haraka ili kuharakisha mazungumzo. Mazungumzo yatakuwa, hata hivyo kama historia ndio mwongozo yatakuwa makali na yatachukua muda.

Lakini kuna maeneo muhimu ambayo serikali zetu zinapaswa kuzingatia wakati wa mazungumzo yao zidi makampuni ya mafuta ya mafuta na gesi. Lakini kuna maeneo muhimu ambayo serikali zetu zinapaswa kuzingatia wakati wa mazungumzo yao zidi makampuni ya mafuta ya mafuta na gesi. Kwanza: ni nani anayepaswa kujadiliana, juu ya masuala gani, na mazingira gani ya taarifa, na kwa wakati gani. Vipengele kama vile muundo wa mkataba wa mafuta na gesi pia vinapaswa kuzingatiwa sana na serikali. Pia maswala ya viwango vya uhasibu; jukumu la kusaidia miradi ya kijamii; masuala ya afya na mazingira; vifungu muhimu vya sheria vilisivyoweza kuingiliwa na mabadiriko ya kisiasa au mabadiriko ya sheria au sera na maswala ya masharti ya kusitisha mkataba wa mafuta na gesi.

Nitaendelea...

Hitimisho: Pamoja na kuongezeka kwa ushindani wa kimataifa wa kuchukua na kumiliki rasilimali za mafuta na gesi hasa kutoka kwa makampuni ya mafuta na gesi ya serikali, ambayo hutoa msaada wa serikali kwa urahisi kwa makampuni yanayotaka kuwekeza kwenye sekta ya mafuta na gesi na pia kutokana na wasiwasi mkubwa wa usalama wa nishati, haswa katika bara la Ulaya na Amerika, ni muhimu zaidi kuliko hapo awali kwa mataifa yanayo miliki rasilimali za mafuta na gesi kuwa na ujuzi wa kitaalamu wa kujadili mikataba na makampuni ya mafuta na gesi ya kimataifa ambayo yatakubaliwa na kuheshimiwa baadaye na serikali zijazo za mataifa hayo.

Lakini pia mazingira haya mapya ya ushindani pia yatahitaji zaidi, uwazi kutoka kwa makampuni ya mafuta na gesi ya kimataifa katika mchakato mzima wa mazungumzo. Bila hivyo, mataifa yanayozalisha mafuta na gesi hayatakuwa na njia ya kujua ikiwa yanatendewa haki.
 
Back
Top Bottom