Madhumuni ya Rais yalikuwa kuifanya bandari ya DSM kuwa ya Mwendo kasi ya kisasa kama SGR. Watekelezaji wamechemsha kwa kuanza na International Treaty

Dr Akili

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
4,953
4,326
1. Madhumuni (vision) na malengo (objectives) mazuri ya Rais wetu, ambayo aliyatangaza wazi hadharani, yalikuwa ni kuifanya bandari ya DSM kuwa ya kiwango cha mwendo kasi, cha kisasa na cha viwango vya kimataifa (international standards) kama zilivyo bandari hususani zile za Singapore na Taiwan. Alitaka kuacha legacy yake kwa watanzani kama ile aliyoacha JPM kwa reli ya umeme ya SGR na JNHPP.

2. Inasikitisha sana kuona watalaam wetu wa mipango, wachumi, wanasheria, wahandisi na watendaji wengineo serikalini kushindwa kuyawekea mipango rahisi ya utekelezaji kufanikisha vision na objectives hizo za rais wetu mpendwa. Badala yake, kabla ya mengine yo yote, wakakurupuka na kuja na hii International treaty na kuliburuza bunge letu kuridhia (retify) faster faster kuwa sheria ya nchi yetu kuhusiana na bandari zetu zote za maji na zile kavu. Kwa tafsiri ya mwanasheria mbobezi, Prof. Shivji, intergovernmental agreement (IGA) maana yake ni International Treaty, sawa na zile za Human Rights, MIGA, International Court ya Hauge etc. Tumeambiwa kuwa baada ya hiyo Treaty kitakachofuata ni Host Government Agreement (HGA), host government hapa ikiwa ni serikali ya Tanzania. Yaani ni sarakasi juu ya sarakasi!

3. Wanasheria na wachumi wetu wabobezi (wakiwemo akina Jaji Waryoba, Prof Shivji, TLS, Prof. Tibajuka na Prof Lipumba) baada ya kuipitia hiyo Treaty yote na kuichambua kipengele kwa kipengele, wamebainisha bila kuacha shaka kwamba hiyo treaty ni sawa na kuziuza bure au kuwapa bure (donate) bandari zetu zote kwa kampuni ya DP World ya emirate ya Dubai; yaani yaliyomo kwenye vipengere vya hiyo Treaty ni zaidi ya ubinafishaji. Yaani kama hiyo Treaty itatekelezwa basi tutakuwa tumepoteza umiliki na udhibiti wa hizo bandari zetu kwa kiwango kinachozidi 90%. Zitakuwa ni mali za Emirate ya Dubai na kuzirudisha litakuwa ni jambo lililo next to impossible. Mapato watakayoyapata hao DP World hatutayajua na yatakuwa none of our business. Hata gharama halisi ya kile watakacho wekeza hatutakijua. Sana sana watatukatia ka murahaba watakoona kanatufaa. Sisi tutabaki tu kutoa ulinzi wa shughuli yao hiyo tukiwa nje.

4. Wananchi walimshuhudia Spika wetu bungeni (ambaye ndiye refree wa bunge asiyepaswa kuegemea upande mmoja), akipoka kazi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali wa kutetea misuada ya serikali inayofikishwa bungeni. Spika alionekana wazi wazi kutetea huo mswada na kuwanyima fursa ya kujieleza vizuri wabunge walioonekana kutaka kuupinga.

Wananchi wameshuhudia kwa nguvu kubwa mawaziri wa serikali pamoja na Mwanasheria mkuu wa serikali pamoja na Spika wa bunge letu, wakijiumauma kutetea hiyo Treaty. Mara eti hayo yaliomo kwenye hiyo Treaty (IGA) siyo mkataba bali ni makubaliano tu (yaani MoU) na kwamba mikataba bado haijaandaliwa. Wanasema mikataba itakuja kuandaliwa huko mbeleni baada ya kusaini kitu kingine kinachoitwa Host Government Agreement (HGA)!

5. Hapo sasa ndipo ngoma hii inavyozidi kuchanganya na kunoga zaidi. Kwani Host Government Agreement maana yake ni maridhio ya serikali mwenyeji kuruhusu nchi yake au sehemu ya nchi yake kutumiwa kwa shughuli fulani ya nchi ya nyingine ya nje. Kwa mfano tulisaini HGA na nchi ya Uganda kuiruhusu Uganda kutumia sehemu ya nchi yetu kupitisha bomba lao la mafuta na sehemu ya bandari yetu ya Tanga kuhifadhi na hatimaye kuyasafirisha hayo mafuta yao ughaibuni. Hilo bomba na hayo mafuta siyo mali zetu wala hayatuhusu. Lakini tuliwataka kwenye hiyo HGA wawe wanatulipa kiasi kidogo cha thamani ya mafuta yanayopita kwenye hilo bomba lao. Eneo tulilowapa hao Uganda ni kwa muda wa milele au hapo watakapomaliza kabisa mafuta nchini kwao. Wanapata pesa kiasi gani kwenye shughuli yao hiyo ya mafuta sisi halituhusu, it is none of our business. TRA na wengineo eneo hilo haliwahusu kwani litakuwa ni la Uganda, sisi tunapaswa tu kulilinda tukiwa nje ya shughuli. Kwa hiyo HGAs zitakazofanyika kwa serikali ya Dubai nazo zitamaanisha hivyo. Mbaya zaidi Dubai Emirate bayou siyo sovereign state kama ilivyo Uganda, mambo ya ushirikiano na nchi za nje uko chini ya UAE (United Arab Emirates) kama sisi huku ilivyo kwa serikali ya Zanzibar masuala hayo ni ya URT (United Republic of Tanzania).

6. Kwa nini basi haswa hawa wapanga mipango yetu ya maendeleo wameu complicate sana huu mradi wa kuboresha bandari yetu kuu ya DSM kuwa bandari ya viwango vya kisasa vya kimataifa vya mwendo kasi wa upakuaji na upakiaji wa meli unaofanyika digitally na kwa remote control ukiwa mbali na eneo?

Mbona mradi wa aina hiyo ni rahisi tu na gharama yake haiwezi hata kufikia nusu ya mradi wa bwawa la umeme (wa trillion saba) lilijengwa kwa viwango vya kimataifa na waarabu wa Egypt bila cha IGA, HGA wala sarakasi ya aina hiyo. Ni mradi mdogo sana ukilinganishwa na mradi wa SGR (wa trillion zaidi ya ishirini) unaojengwa na makampuni kutoka nchi za Utruki na China kwa muda wa miaka minne tu na mkataba wake haukuwa na IGA wala HGAs. Ni mradi mdogo sana ukilinganishwa na mradi wa LNG (wa trillion karibia mia moja) uliopewa makampuni makubwa ya nchi kadhaa za bara la Ulaya bila cha IGA kwa miaka milele bila hata ya wananchi kuambiwa kama ile fifty fifty win win situation ya sheria yetu ya nchi ya maliasili zetu imo kwenye mkataba huo wa muda wa milele au wa hapo gesi yetu yote itakapomalizika kuchotwa. Wala waziri wetu wa nishati haukupeleka mkataba huo bungeni kuridhiwa kwa sababu kwa makusudi haukuufanya uwe wa wa kiwango cha International treaty yaani IGA kwani angalifanya hivyo angelazimika kuupeleka bungeni ukaridhiwe. Kwani kwa mjibu wa katiba yetu ya nchi mikataba ya hadhi ya IGA aka International Treaty inapaswa kuridhiwa na bunge kwa niaba ya wananchi. Mikataba mingine ikiwamo ya HGA wabunge wetu hawapaswi kuiridhia wala hata kuiona kwani huwa ni confidential.

Mradi wa LNG kwa namna muundo wake ulivyo ulipaswa kuwa na hadhi hiyo ya International Treaty. Huu wa DP World muundo wake ni sawa na ule wa makontena wa TICTS ambao haukuwa na IGA wala HGAs. TICTS walikuwa ni kama waajiriwa tu wa TPA (makuli wa kupakua na kupakia meli) kwa mkataba wa miaka 20. Walikuwa chini ya uongozi wa TPA na hivyo ilikuwa rahisi kuwatimua wakiboronga wakati wo wote bila ya kupelekana kwenye mahakama za kimataifa.

7. Mpango wa utekelezaji wa dhamira nzuri ya rais kwa bandari ya DSM ulipaswa kuwa rahisi tu, rahisi kuliko ule wa SGR na wa JNHPP. Tayari kina cha bandari ya Dar tulikuwa tumesha kamilisha mradi (usio na IGA wala HGA) wa kuongeza kina chake hadi kufikia kina kinacho wezesha meli ya ukubwa wo wote duniani kutia nanga kwenye bandari ya DSM. Mradi huu wa DP World wa uboreshaji wa bandari hii ulipaswa kuwa wa kununua na kufungwa mitambo (cranes) ya kisasa ya upakuaji na upakiaji wa meli zinazofika hapo DSM.

Mitambo hiyo ilitakiwa kuwa ya automated artificial intelligence system yenye uwezo wa kutambua hata thamani ya kilichoko kwenye kila container na kiasi kodi zinazopaswa kulipwa serikalini (TRA etc) ambazo hata Rais wetu na ye yote mwenye password yake ataweza kuziona akiwa mahali po pote duniani. Ni kama zile alizoziona Bw. Msukuma, mbunge wa Chato, huko Dubai akabaki anashangaa kwani ni mitambo inayoendeshwa kwa kubonyeza remote control hata na mtoto wa miaka saba kama inavyofanyika kwa smartphone au television. Mitambo ya aina hiyo ingaliziba kabisa janja janja ya baadhi ya watumishi wa TPA na TRA wanayotumia kutupiga pale bandarini na kuchelewesha mizigo.

8. Hivyo mpango wa mradi huo ulitakiwa kuandaliwa na wahandisi wetu wa bandari (Port Engineers) wakishirikiana na maafisa mipango wetu. Timu yetu hii ya senior port engineers na senior planning officers wetu tungaliweza kuiongezea nguvu za kiutalaamu kwa kuwapatia Consultant Port Engineers wa kukodi kutoka nchi zenye uzoefu huo eg kwa rafiki zetu wa Dubai. Timu hii ingebainisha aina na kiasi cha mitambo inayohitajika na gharama yake. Hivyo timu hii ya watalaamu ingalitayarisha BQ (bill of quantities) na kuiachia serikali kutafuta source ya ku finance huo mradi ambao ungaliweza kutoka kwa mapato yetu ya ndani au kutoka kwa mikopo yenye riba nafuu kutoka mahali po pote hususani kwa rafiki zetu wa Emirate ya Dubai. Rais alichofanya huko Dubai na kwingineko duniani alikokwenda na atakakoendelea kwenda ni kututafutia marafiki ambao tutaweza kuwakopa au kutupa misaada (grants) tunapokuwa na uhitaji. Haendi huko kufanya International Treatises za aina ye yote bali MoUs tu za ushirikiano wa kiurafiki.

9. Baada ya serikali kupata source of finance wa mradi huo, competitive tender ingalitangazwa ya kupata kampuni ya uhandisi ya kusimika mitambo hiyo katika bandari ya DSM. Tender hiyo ya miaka isiyozidi mitatu ingalijumuisha usimamizi wa uendeshaji wa mitambo hiyo na kuwafundisha watanzania kuiendesha mitambo hiyo ndani ya kipindi hicho cha miaka mitatu kama itakavyokuwa kwa miradi yetu ya SGR na JNHPP. Ugumu uko wapi hapo? Kwa nini wanasheria wa serikali ndiyo wamekuwa wa kwanza katika utayarishaji mpango wa mradi huu, badala ya wahandisi na wanamipango wetu? Wanasheria hawa walipaswa kuhusika mwishoni kabisa wakati wa kuwekeana mkataba na huyo mkandrasi wa kusimika hiyo mitambo ya kisasa pale bandari ya DSM. Wanasiasa wetu kwa maana ya cabinet yetu ndiyo wa hatua ya mwisho kabisa ambao kwa niaba ya wananchi wanapaswa kujiridhisha na kuridhia kuwa kilichofanywa na hao watalaam wetu hakina dosari yo yote kwani mambo yakija kuharibika at the end the back stops at them!

Kilichofanyika kwenye mpango wa mradi huu ni vice-versa, yaani waliopaswa kuwa wa mwisho wakawa wa kwanza na wale waliotakiwa kuwa wa kwanza watakuwa ndiyo wa mwisho. Hiyo sasa ni sarakasi, kichwa chini miguu juu. Na hii ndicho sarakasi bado inayoendelea kwa wanasiasa kuwa wanasheria wa kudadavua vifungu vya sheria vilivyomo kwenye mkataba huo huku wanasheria wa serikali wakiwa wame mute. Kulikuwa hakuna sababu ya kujumulisha bandari zote za majini na za nchi kavu za Tanzania bara kwa pamoja kwenye mradi huu. Tungeanza na bandari moja ya DSM. Hizo zingine zingalifuata baadaye moja moja kwani hata mahitaji yake ya maboresho yanatofautiana na ni madogo. Sasa bandari kama ya Ukerewe inahitaji maboresho gani ambayo yanatushinda hadi tumwachie Mwarabu wa Dubai kuyafanya?

10. Kwenye miradi ya kimkakati kwa Taifa si jambo la busara kuiweka miradi hii kwenye umiliki ya uendeshaji wa watu binafsi au kampuni binafsi au nchi nyingine ya nje. Miradi hii ya kimkakati kwa taifa letu ni pamoja na ya miundombinu ya nishati, reli, barabara, bandari na usafiri wa anga. Miradi ya aiana hii ni roho na mishipa ya damu ya uchumi wa taifa letu. Si busara hata kidogo kubinafisha, kukodisha au kupangisha miundo mbinu hii. Na tunapaswa kuiijenga na kuiboresha kwa pesa yetu ya ndani au ya mikopo nafuu ya serikali yetu. Hili ndilo jukumu kuu (core function) la serikali yetu la kuleta maendeleo ya nchi yetu. Pia ni kwa ajili ya usalama na utulivu wa kijamii wa nchi yetu. Tunaweza kupangisha au kukodisha au kubinafisha au kuuza mbuga zetu za wanyama pori, mashamba ya mpunga, mahindi, karafuu etc lakini siyo hii miundombinu ya kimkakati ya taifa letu. Uwekezaji kwa natural resources za nchi nao lazima uzingatie sheria yetu nzuri ya natural resources inayozingatia not less than 50 % win-win situation.

11. Kwa lugha ya kawaida, mwekezaji halisi (original) ni yule anayekuja na mtaji wake tunampa eneo (ardhi) lililo tupu la kufanyia uwekezaji wake. Uwekezaji huo unaweza kuwa wa kujenga kiwanda chake, kilimo au shughuli nyingine zikiwamo za huduma hususani hospitali au shule. Mazao ya uwekezaji wake atayauza ndani au nje ya nchi jinsi atakavyo amua yeye kwani ni mali yake. Na bei atapanga anayotaka yeye, hatutamwingilia isipokuwa kwenye hiyo ataongeza VAT yetu; yaani atakuwa wakala wetu wa kutukusanyia VAT kutoka kwa wateja watakaonunua bidhaa au huduma zake.

Mwekezaji feki ni yule anayekuja tukampatia mali yetu hususani Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Bwawa la Kuzalisha Umeme la Nyerere au SGR yetu kwa madhumuni ya kuiendesha yeye na kuiboresha ili performance (ufanisi) yake iwe bora zaidi kwa sababu tu eti sisi tumeshindwa kuongeza performance. Mwekezaji wa aina hii anaweza akawa wala hana mtaji wo wote wa maana akitegemea kuupata hapa hapa kwenye mradi wetu. Mbaya zaidi kama tutaingia naye mkataba unaompa protection kubwa ya kutomwingilia au kumgusa kwenye shughuli zake ikiwamo mapato atakayovuna kutoka kwenye miradi yetu nyeti ya kitaifa. Mwekezaji wa aina hii anaweza akawa hata taperi (brief case investor), haijalishi anatoka nchi gani. Tulishuhudia akina Richmond toka USA walichotufanyia wakati ule wa awamu ya nne ya JK!

Sasa huyu DP World wananchi wengi wanashindwa kujua yuko kundi gani la wawekezaji. Jee ni kweli DP World anakuja kama muwekezaji kama ambavyo baadhi ya wanasiasa wanasema? Au anakuja kama mkandrasi wa kuboresha bandari yetu ya DSM? Alipaswa kuja kama mkandrasi na sisi ndio tutakuwa tunamlipa ujira wa kazi tutakazompa kufanya kwa kipindi tutakachoona kinafaa kukamilisha kazi hiyo. Wala serikali isiogope kukopa kwa ajili ya kutekeleza miradi kama hii ya kimkakati ya maendeleo. Dunia inampenda sana rais wetu na ingependa afanikiwe kwa kiwango kikubwa kuipaisha kimaendeleo Tanzania; ili kuwa mfano kwa nchi zingine hasa za kiafrika zilizong'ang'ania kuwa cheo cha urais ni cha wanaume tu na hasa wanaume waliokuwa wanajeshi.

Sijasoma hata hii risala mpaka mwisho ila kwa uvyotaka kumtetea rais,unatupa ujumbe yakwamba rais hayupo makini...na hasomi mikaba nyeti tena inahusu rasilimali ya taifa..sasa kazi yake nini?

Ni hivi wakati kiongozi anataka kufanya maamuzi dhidi ya rasilimli ya nchi awasikilize wananchi ndio bunge la kwanza kabla ya wale machawa wanaozunguka dodoma

Mtoto wa form six akisoma ule mkataba hawezi kuukubali

Huyu mwanamke kaupitisha ule mkataba wa ovyo na kuuza loliondo kwasababu anachuki kubwa sana na watanganyika na anawapenda wanzazibari na waarabu.
 
Ule mkataba ukiusoma vipengele vyake, moja ya kipengele kinazungumzia "Instrument of Full Powers", ambapo kwenye kipengele hicho, Samia kama kiongozi mkuu, amekaimisha majukumu yake kwa Waziri Prof. Mbarawa, atie saini yake kwenye ule mkataba wa hovyo.

Sasa ukimaliza kusoma hicho kifungu, halafu urudi ujisome ulichoandika hapo juu, kwamba Samia alikuwa na nia nzuri, nia nzuri ipi hiyo iliyompelekea Samia akamruhusu Mbarawa kuweka saini yake kwenye ule mkataba wa hovyo namna ile?

Msihangaike kumsafisha Samia, kwa ule mkataba wa hovyo hakwepi lawama, yeye ni msaliti, kwani aliujua, akauona, na kuruhusu kutiliwa saini usaliti huo.
 
Sio kweli.

Rais ndio alienda kwenye saba saba za Dubai na kuwakabidhi matapeli bandari.

Tusisingizie wengine.

Mbarawa amefanya makosa mangapi kwenye ile wizara na bado yupo?

Kisa Mzanzibari?

Angekuwa mnyakyusa angeachwa pale mpaka leo?

Mama kahusika moja kwa moja kwenye kugawa bandari ya Tanganyika

Zile treat amesaini na Dubai ni za nini kama sio ndio hizi za kuuza nchi?
 
Mungu akubariki sana yani umeonngea kitaalaamu sana hii itasaidia kuamsha hisia upya kwawale waliokuwa wameanza kupumbazwa na propaganda za waovu,,
Kwanini una upeo mdogo? Umeshindwa hata kujua nini kipo kwenye mkataba uoanishe kama kinafanana na kile mleta mada alichoandika hapa, ili uone kama vinaendana?

Kwa kifupi, terms za kwenye ule mkataba wa hovyo wa bandari, hazifanani kabisa na kile mleta mada alichoandika, mfano mmojawapo nimekupa clause ya Instrument of Full Powers, ambapo Samia kwa makusudi, amemkaimisha majukumu yake Prof. Mbarawa aweke saini kwenye ule mkataba wa hovyo..

Sasa kwa mazingira hayo utasema vipi Samia hahusiki? kama kweli hahusiki kwanini amuache Prof. Mbarawa ofisini mpaka leo licha ya kumuharibia kazi?

Jiongeze.
 
Yeye ndokasema Rais hahusiki ila ukisoma alichoandika kaikaanga serikali nzima maana alichozungumza amemaanisha serikali ilikuwa likizo,
 
Sa100 kaingiza Nchi mkenge kwa kujua alichokuwa amekusudia kufanya!
Jambo kubwa kama hilo huwezi kulifanya kienyeji na kimangungo kama alivyofanya!
Watetezi wake hawana hoja!
Yaani tuache kumsikiliza Profesa Shivji, Process Anne Tibaijuka, Dr.Rugemeleza Nshala, Tundu Lissu, Boniface Mwabukusu n.k na Tumsikilize Majaliwa, Sa100, Zebwela, Steve Nyerere, Maulidi Kitenge, Shehe Ubwabwa Mwaipopo na Mbumbumbu Mizungu ya Reli mingine!?
Tujaribuni kuwa serious kwenye mambo ya msingi kwa Taifa.
Sa100 ameuza Bandari zetu kupitia Bogus Treaty !
 
1. Madhumuni (vision) na malengo (objectives) mazuri ya Rais wetu, ambayo aliyatangaza wazi hadharani, yalikuwa ni kuifanya bandari ya DSM kuwa ya kiwango cha mwendo kasi, cha kisasa na cha viwango vya kimataifa (international standards) kama zilivyo bandari hususani zile za Singapore na Taiwan. Alitaka kuacha legacy yake kwa watanzani kama ile aliyoacha JPM kwa reli ya umeme ya SGR na JNHPP.

2. Inasikitisha sana kuona watalaam wetu wa mipango, wachumi, wanasheria, wahandisi na watendaji wengineo serikalini kushindwa kuyawekea mipango rahisi ya utekelezaji kufanikisha vision na objectives hizo za rais wetu mpendwa. Badala yake, kabla ya mengine yo yote, wakakurupuka na kuja na hii International treaty na kuliburuza bunge letu kuridhia (retify) faster faster kuwa sheria ya nchi yetu kuhusiana na bandari zetu zote za maji na zile kavu. Kwa tafsiri ya mwanasheria mbobezi, Prof. Shivji, intergovernmental agreement (IGA) maana yake ni International Treaty, sawa na zile za Human Rights, MIGA, International Court ya Hauge etc. Tumeambiwa kuwa baada ya hiyo Treaty kitakachofuata ni Host Government Agreement (HGA), host government hapa ikiwa ni serikali ya Tanzania. Yaani ni sarakasi juu ya sarakasi!

3. Wanasheria na wachumi wetu wabobezi (wakiwemo akina Jaji Waryoba, Prof Shivji, TLS, Prof. Tibajuka na Prof Lipumba) baada ya kuipitia hiyo Treaty yote na kuichambua kipengele kwa kipengele, wamebainisha bila kuacha shaka kwamba hiyo treaty ni sawa na kuziuza bure au kuwapa bure (donate) bandari zetu zote kwa kampuni ya DP World ya emirate ya Dubai; yaani yaliyomo kwenye vipengere vya hiyo Treaty ni zaidi ya ubinafishaji. Yaani kama hiyo Treaty itatekelezwa basi tutakuwa tumepoteza umiliki na udhibiti wa hizo bandari zetu kwa kiwango kinachozidi 90%. Zitakuwa ni mali za Emirate ya Dubai na kuzirudisha litakuwa ni jambo lililo next to impossible. Mapato watakayoyapata hao DP World hatutayajua na yatakuwa none of our business. Hata gharama halisi ya kile watakacho wekeza hatutakijua. Sana sana watatukatia ka murahaba watakoona kanatufaa. Sisi tutabaki tu kutoa ulinzi wa shughuli yao hiyo tukiwa nje.

4. Wananchi walimshuhudia Spika wetu bungeni (ambaye ndiye refree wa bunge asiyepaswa kuegemea upande mmoja), akipoka kazi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali wa kutetea misuada ya serikali inayofikishwa bungeni. Spika alionekana wazi wazi kutetea huo mswada na kuwanyima fursa ya kujieleza vizuri wabunge walioonekana kutaka kuupinga.

Wananchi wameshuhudia kwa nguvu kubwa mawaziri wa serikali pamoja na Mwanasheria mkuu wa serikali pamoja na Spika wa bunge letu, wakijiumauma kutetea hiyo Treaty. Mara eti hayo yaliomo kwenye hiyo Treaty (IGA) siyo mkataba bali ni makubaliano tu (yaani MoU) na kwamba mikataba bado haijaandaliwa. Wanasema mikataba itakuja kuandaliwa huko mbeleni baada ya kusaini kitu kingine kinachoitwa Host Government Agreement (HGA)!

5. Hapo sasa ndipo ngoma hii inavyozidi kuchanganya na kunoga zaidi. Kwani Host Government Agreement maana yake ni maridhio ya serikali mwenyeji kuruhusu nchi yake au sehemu ya nchi yake kutumiwa kwa shughuli fulani ya nchi ya nyingine ya nje. Kwa mfano tulisaini HGA na nchi ya Uganda kuiruhusu Uganda kutumia sehemu ya nchi yetu kupitisha bomba lao la mafuta na sehemu ya bandari yetu ya Tanga kuhifadhi na hatimaye kuyasafirisha hayo mafuta yao ughaibuni. Hilo bomba na hayo mafuta siyo mali zetu wala hayatuhusu. Lakini tuliwataka kwenye hiyo HGA wawe wanatulipa kiasi kidogo cha thamani ya mafuta yanayopita kwenye hilo bomba lao. Eneo tulilowapa hao Uganda ni kwa muda wa milele au hapo watakapomaliza kabisa mafuta nchini kwao. Wanapata pesa kiasi gani kwenye shughuli yao hiyo ya mafuta sisi halituhusu, it is none of our business. TRA na wengineo eneo hilo haliwahusu kwani litakuwa ni la Uganda, sisi tunapaswa tu kulilinda tukiwa nje ya shughuli. Kwa hiyo HGAs zitakazofanyika kwa serikali ya Dubai nazo zitamaanisha hivyo. Mbaya zaidi Dubai Emirate bayou siyo sovereign state kama ilivyo Uganda, mambo ya ushirikiano na nchi za nje uko chini ya UAE (United Arab Emirates) kama sisi huku ilivyo kwa serikali ya Zanzibar masuala hayo ni ya URT (United Republic of Tanzania).

6. Kwa nini basi haswa hawa wapanga mipango yetu ya maendeleo wameu complicate sana huu mradi wa kuboresha bandari yetu kuu ya DSM kuwa bandari ya viwango vya kisasa vya kimataifa vya mwendo kasi wa upakuaji na upakiaji wa meli unaofanyika digitally na kwa remote control ukiwa mbali na eneo?

Mbona mradi wa aina hiyo ni rahisi tu na gharama yake haiwezi hata kufikia nusu ya mradi wa bwawa la umeme (wa trillion saba) lilijengwa kwa viwango vya kimataifa na waarabu wa Egypt bila cha IGA, HGA wala sarakasi ya aina hiyo. Ni mradi mdogo sana ukilinganishwa na mradi wa SGR (wa trillion zaidi ya ishirini) unaojengwa na makampuni kutoka nchi za Utruki na China kwa muda wa miaka minne tu na mkataba wake haukuwa na IGA wala HGAs. Ni mradi mdogo sana ukilinganishwa na mradi wa LNG (wa trillion karibia mia moja) uliopewa makampuni makubwa ya nchi kadhaa za bara la Ulaya bila cha IGA kwa miaka milele bila hata ya wananchi kuambiwa kama ile fifty fifty win win situation ya sheria yetu ya nchi ya maliasili zetu imo kwenye mkataba huo wa muda wa milele au wa hapo gesi yetu yote itakapomalizika kuchotwa. Wala waziri wetu wa nishati haukupeleka mkataba huo bungeni kuridhiwa kwa sababu kwa makusudi haukuufanya uwe wa wa kiwango cha International treaty yaani IGA kwani angalifanya hivyo angelazimika kuupeleka bungeni ukaridhiwe. Kwani kwa mjibu wa katiba yetu ya nchi mikataba ya hadhi ya IGA aka International Treaty inapaswa kuridhiwa na bunge kwa niaba ya wananchi. Mikataba mingine ikiwamo ya HGA wabunge wetu hawapaswi kuiridhia wala hata kuiona kwani huwa ni confidential.

Mradi wa LNG kwa namna muundo wake ulivyo ulipaswa kuwa na hadhi hiyo ya International Treaty. Huu wa DP World muundo wake ni sawa na ule wa makontena wa TICC ambao haukuwa na IGA wala HGAs. TICC walikuwa ni kama waajiriwa tu wa TPA (makuli wa kupakua na kupakia meli) kwa mkataba wa miaka 20. Walikuwa chini ya uongozi wa TPA na hivyo ilikuwa rahisi kuwatimua wakiboronga wakati wo wote bila ya kupelekana kwenye mahakama za kimataifa.

7. Mpango wa utekelezaji wa dhamira nzuri ya rais kwa bandari ya DSM ulipaswa kuwa rahisi tu, rahisi kuliko ule wa SGR na wa JNHPP. Tayari kina cha bandari ya Dar tulikuwa tumesha kamilisha mradi (usio na IGA wala HGA) wa kuongeza kina chake hadi kufikia kina kinacho wezesha meli ya ukubwa wo wote duniani kutia nanga kwenye bandari ya DSM. Mradi huu wa DP World wa uboreshaji wa bandari hii ulipaswa kuwa wa kununua na kufungwa mitambo (cranes) ya kisasa ya upakuaji na upakiaji wa meli zinazofika hapo DSM.

Mitambo hiyo ilitakiwa kuwa ya automated artificial intelligence system yenye uwezo wa kutambua hata thamani ya kilichoko kwenye kila container na kiasi kodi zinazopaswa kulipwa serikalini (TRA etc) ambazo hata Rais wetu na ye yote mwenye password yake ataweza kuziona akiwa mahali po pote duniani. Ni kama zile alizoziona Bw. Msukuma, mbunge wa Chato, huko Dubai akabaki anashangaa kwani ni mitambo inayoendeshwa kwa kubonyeza remote control hata na mtoto wa miaka saba kama inavyofanyika kwa smartphone au television. Mitambo ya aina hiyo ingaliziba kabisa janja janja ya baadhi ya watumishi wa TPA na TRA wanayotumia kutupiga pale bandarini na kuchelewesha mizigo.

8. Hivyo mpango wa mradi huo ulitakiwa kuandaliwa na wahandisi wetu wa bandari (Port Engineers) wakishirikiana na maafisa mipango wetu. Timu yetu hii ya senior port engineers na senior planning officers wetu tungaliweza kuiongezea nguvu za kiutalaamu kwa kuwapatia Consultant Port Engineers wa kukodi kutoka nchi zenye uzoefu huo eg kwa rafiki zetu wa Dubai. Timu hii ingebainisha aina na kiasi cha mitambo inayohitajika na gharama yake. Hivyo timu hii ya watalaamu ingalitayarisha BQ (bill of quantities) na kuiachia serikali kutafuta source ya ku finance huo mradi ambao ungaliweza kutoka kwa mapato yetu ya ndani au kutoka kwa mikopo yenye riba nafuu kutoka mahali po pote hususani kwa rafiki zetu wa Emirate ya Dubai. Rais alichofanya huko Dubai na kwingineko duniani alikokwenda na atakakoendelea kwenda ni kututafutia marafiki ambao tutaweza kuwakopa au kutupa misaada (grants) tunapokuwa na uhitaji. Haendi huko kufanya International Treatises za aina ye yote bali MoUs tu za ushirikiano wa kiurafiki.

9. Baada ya serikali kupata source of finance wa mradi huo, competitive tender ingalitangazwa ya kupata kampuni ya uhandisi ya kusimika mitambo hiyo katika bandari ya DSM. Tender hiyo ya miaka isiyozidi mitatu ingalijumuisha usimamizi wa uendeshaji wa mitambo hiyo na kuwafundisha watanzania kuiendesha mitambo hiyo ndani ya kipindi hicho cha miaka mitatu kama itakavyokuwa kwa miradi yetu ya SGR na JNHPP. Ugumu uko wapi hapo? Kwa nini wanasheria wa serikali ndiyo wamekuwa wa kwanza katika utayarishaji mpango wa mradi huu, badala ya wahandisi na wanamipango wetu? Wanasheria hawa walipaswa kuhusika mwishoni kabisa wakati wa kuwekeana mkataba na huyo mkandrasi wa kusimika hiyo mitambo ya kisasa pale bandari ya DSM. Wanasiasa wetu kwa maana ya cabinet yetu ndiyo wa hatua ya mwisho kabisa ambao kwa niaba ya wananchi wanapaswa kujiridhisha na kuridhia kuwa kilichofanywa na hao watalaam wetu hakina dosari yo yote kwani mambo yakija kuharibika at the end the back stops at them!

Kilichofanyika kwenye mpango wa mradi huu ni vice-versa, yaani waliopaswa kuwa wa mwisho wakawa wa kwanza na wale waliotakiwa kuwa wa kwanza watakuwa ndiyo wa mwisho. Hiyo sasa ni sarakasi, kichwa chini miguu juu. Na hii ndicho sarakasi bado inayoendelea kwa wanasiasa kuwa wanasheria wa kudadavua vifungu vya sheria vilivyomo kwenye mkataba huo huku wanasheria wa serikali wakiwa wame mute. Kulikuwa hakuna sababu ya kujumulisha bandari zote za majini na za nchi kavu za Tanzania bara kwa pamoja kwenye mradi huu. Tungeanza na bandari moja ya DSM. Hizo zingine zingalifuata baadaye moja moja kwani hata mahitaji yake ya maboresho yanatofautiana na ni madogo. Sasa bandari kama ya Ukerewe inahitaji maboresho gani ambayo yanatushinda hadi tumwachie Mwarabu wa Dubai kuyafanya?

10. Kwenye miradi ya kimkakati kwa Taifa si jambo la busara kuiweka miradi hii kwenye umiliki ya uendeshaji wa watu binafsi au kampuni binafsi au nchi nyingine ya nje. Miradi hii ya kimkakati kwa taifa letu ni pamoja na ya miundombinu ya nishati, reli, barabara, bandari na usafiri wa anga. Miradi ya aiana hii ni roho na mishipa ya damu ya uchumi wa taifa letu. Si busara hata kidogo kubinafisha, kukodisha au kupangisha miundo mbinu hii. Na tunapaswa kuiijenga na kuiboresha kwa pesa yetu ya ndani au ya mikopo nafuu ya serikali yetu. Hili ndilo jukumu kuu (core function) la serikali yetu la kuleta maendeleo ya nchi yetu. Pia ni kwa ajili ya usalama na utulivu wa kijamii wa nchi yetu. Tunaweza kupangisha au kukodisha au kubinafisha au kuuza mbuga zetu za wanyama pori, mashamba ya mpunga, mahindi, karafuu etc lakini siyo hii miundombinu ya kimkakati ya taifa letu. Uwekezaji kwa natural resources za nchi nao lazima uzingatie sheria yetu nzuri ya natural resources inayozingatia not less than 50 % win-win situation.

11. Kwa lugha ya kawaida, mwekezaji halisi (original) ni yule anayekuja na mtaji wake tunampa eneo (ardhi) lililo tupu la kufanyia uwekezaji wake. Uwekezaji huo unaweza kuwa wa kujenga kiwanda chake, kilimo au shughuli nyingine zikiwamo za huduma hususani hospitali au shule. Mazao ya uwekezaji wake atayauza ndani au nje ya nchi jinsi atakavyo amua yeye kwani ni mali yake. Na bei atapanga anayotaka yeye, hatutamwingilia isipokuwa kwenye hiyo ataongeza VAT yetu; yaani atakuwa wakala wetu wa kutukusanyia VAT kutoka kwa wateja watakaonunua bidhaa au huduma zake.

Mwekezaji feki ni yule anayekuja tukampatia mali yetu hususani Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Bwawa la Kuzalisha Umeme la Nyerere au SGR yetu kwa madhumuni ya kuiendesha yeye na kuiboresha ili performance (ufanisi) yake iwe bora zaidi kwa sababu tu eti sisi tumeshindwa kuongeza performance. Mwekezaji wa aina hii anaweza akawa wala hana mtaji wo wote wa maana akitegemea kuupata hapa hapa kwenye mradi wetu. Mbaya zaidi kama tutaingia naye mkataba unaompa protection kubwa ya kutomwingilia au kumgusa kwenye shughuli zake ikiwamo mapato atakayovuna kutoka kwenye miradi yetu nyeti ya kitaifa. Mwekezaji wa aina hii anaweza akawa hata taperi (brief case investor), haijalishi anatoka nchi gani. Tulishuhudia akina Richmond toka USA walichotufanyia wakati ule wa awamu ya nne ya JK!

Sasa huyu DP World wananchi wengi wanashindwa kujua yuko kundi gani la wawekezaji. Jee ni kweli DP World anakuja kama muwekezaji kama ambavyo baadhi ya wanasiasa wanasema? Au anakuja kama mkandrasi wa kuboresha bandari yetu ya DSM? Alipaswa kuja kama mkandrasi na sisi ndio tutakuwa tunamlipa ujira wa kazi tutakazompa kufanya kwa kipindi tutakachoona kinafaa kukamilisha kazi hiyo. Wala serikali isiogope kukopa kwa ajili ya kutekeleza miradi kama hii ya kimkakati ya maendeleo. Dunia inampenda sana rais wetu na ingependa afanikiwe kwa kiwango kikubwa kuipaisha kimaendeleo Tanzania; ili kuwa mfano kwa nchi zingine hasa za kiafrika zilizong'ang'ania kuwa cheo cha urais ni cha wanaume tu na hasa wanaume waliokuwa wanajeshi.

1. Mwanasheria mkuu wa serikali aliusoma mkataba huu?
2. Mwanasheria mkuu wa serikali aliusaini mkataba huu?
3, Saa100 aliusaini aliusoma? Aliuelewa?
 
Attachments

  • 8E2228FF-FA0F-4CB5-8958-2BA8438E8F27.jpeg
    8E2228FF-FA0F-4CB5-8958-2BA8438E8F27.jpeg
    58 KB · Views: 5
  • 35783522-0FA6-48E1-BF84-B5643E324343.jpeg
    35783522-0FA6-48E1-BF84-B5643E324343.jpeg
    79.5 KB · Views: 5
  • 91BF14CF-46DF-4A3E-AECD-9E6B5A0A8507.jpeg
    91BF14CF-46DF-4A3E-AECD-9E6B5A0A8507.jpeg
    32 KB · Views: 6
  • FB036C43-51ED-47CE-BB2F-9FA051223AB4.jpeg
    FB036C43-51ED-47CE-BB2F-9FA051223AB4.jpeg
    55.3 KB · Views: 3
  • A6A31E0A-08A0-4D9A-A1E7-3AD2E5382E99.jpeg
    A6A31E0A-08A0-4D9A-A1E7-3AD2E5382E99.jpeg
    131.1 KB · Views: 3
  • D9AF1813-2F9D-4DDC-914F-7357EF074BC9.jpeg
    D9AF1813-2F9D-4DDC-914F-7357EF074BC9.jpeg
    150.5 KB · Views: 3
  • D025A1A0-DEE7-4DBE-8AEC-21DD062AD9C5.jpeg
    D025A1A0-DEE7-4DBE-8AEC-21DD062AD9C5.jpeg
    75.7 KB · Views: 4
  • 47128FC2-0EE8-4359-914A-F9B87DA15233.jpeg
    47128FC2-0EE8-4359-914A-F9B87DA15233.jpeg
    55.1 KB · Views: 3
Binafsi sijasoma hili gazeti lote kwasababu naona ni utetezi juu ya rasi kuwa alikuwa na mipango thabi. Shida ya hii nchi yetu ni kuwa chombo tunachokitegemea kutuwakilisha na kujadili juu ya maoni yetu washika dau wao wanaunda hoja wenyewe na kuzipeleka wenyewe kwa mitazamo yao. Democrasi haipo ya kuwapa watu uhuru wa kutoa mawazo yao. Nchi yenyewe wasomi na watafiti wa kitaalam tena wamesomeshwa na serikali wengine kwenye nchi ambazo leo hii zinakuja kutunyonya ima maana walienda kufunzwa namna ya kujiibia?, wapo wapi mataalam wetu?, je wanashirikishwa katika michakato mbali mbali ya maendeleo ya kiuchumi? mawazo watunge wao tena kwa kupeana posho za kutumia kodi zetu kisha hatuna uhuru wa kuchangia mawazo wanatuona mazuzu wakiharibu wanatafuta wa kumfunga paka kengele. Fungu la kukosa sisi maana dereva kavunja gia kuna nini tena?
 
Mnapofeli ndio hapo.. Kwanini haujataka kusoma hili andiko lote... Kuna aina tofautitofauti za uandishi, mimi nakuomba rudia tena kulisoma andiko lote. Mama katetewa kwani nia ya aondoke mwenyewe bila kufukuzwa.
 
1. Madhumuni (vision) na malengo (objectives) mazuri ya Rais wetu, ambayo aliyatangaza wazi hadharani, yalikuwa ni kuifanya bandari ya DSM kuwa ya kiwango cha mwendo kasi, cha kisasa na cha viwango vya kimataifa (international standards) kama zilivyo bandari hususani zile za Singapore na Taiwan. Alitaka kuacha legacy yake kwa watanzani kama ile aliyoacha JPM kwa reli ya umeme ya SGR na JNHPP.

2. Inasikitisha sana kuona watalaam wetu wa mipango, wachumi, wanasheria, wahandisi na watendaji wengineo serikalini kushindwa kuyawekea mipango rahisi ya utekelezaji kufanikisha vision na objectives hizo za rais wetu mpendwa. Badala yake, kabla ya mengine yo yote, wakakurupuka na kuja na hii International treaty na kuliburuza bunge letu kuridhia (retify) faster faster kuwa sheria ya nchi yetu kuhusiana na bandari zetu zote za maji na zile kavu. Kwa tafsiri ya mwanasheria mbobezi, Prof. Shivji, intergovernmental agreement (IGA) maana yake ni International Treaty, sawa na zile za Human Rights, MIGA, International Court ya Hauge etc. Tumeambiwa kuwa baada ya hiyo Treaty kitakachofuata ni Host Government Agreement (HGA), host government hapa ikiwa ni serikali ya Tanzania. Yaani ni sarakasi juu ya sarakasi!

3. Wanasheria na wachumi wetu wabobezi (wakiwemo akina Jaji Waryoba, Prof Shivji, TLS, Prof. Tibajuka na Prof Lipumba) baada ya kuipitia hiyo Treaty yote na kuichambua kipengele kwa kipengele, wamebainisha bila kuacha shaka kwamba hiyo treaty ni sawa na kuziuza bure au kuwapa bure (donate) bandari zetu zote kwa kampuni ya DP World ya emirate ya Dubai; yaani yaliyomo kwenye vipengere vya hiyo Treaty ni zaidi ya ubinafishaji. Yaani kama hiyo Treaty itatekelezwa basi tutakuwa tumepoteza umiliki na udhibiti wa hizo bandari zetu kwa kiwango kinachozidi 90%. Zitakuwa ni mali za Emirate ya Dubai na kuzirudisha litakuwa ni jambo lililo next to impossible. Mapato watakayoyapata hao DP World hatutayajua na yatakuwa none of our business. Hata gharama halisi ya kile watakacho wekeza hatutakijua. Sana sana watatukatia ka murahaba watakoona kanatufaa. Sisi tutabaki tu kutoa ulinzi wa shughuli yao hiyo tukiwa nje.

4. Wananchi walimshuhudia Spika wetu bungeni (ambaye ndiye refree wa bunge asiyepaswa kuegemea upande mmoja), akipoka kazi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali wa kutetea misuada ya serikali inayofikishwa bungeni. Spika alionekana wazi wazi kutetea huo mswada na kuwanyima fursa ya kujieleza vizuri wabunge walioonekana kutaka kuupinga.

Wananchi wameshuhudia kwa nguvu kubwa mawaziri wa serikali pamoja na Mwanasheria mkuu wa serikali pamoja na Spika wa bunge letu, wakijiumauma kutetea hiyo Treaty. Mara eti hayo yaliomo kwenye hiyo Treaty (IGA) siyo mkataba bali ni makubaliano tu (yaani MoU) na kwamba mikataba bado haijaandaliwa. Wanasema mikataba itakuja kuandaliwa huko mbeleni baada ya kusaini kitu kingine kinachoitwa Host Government Agreement (HGA)!

5. Hapo sasa ndipo ngoma hii inavyozidi kuchanganya na kunoga zaidi. Kwani Host Government Agreement maana yake ni maridhio ya serikali mwenyeji kuruhusu nchi yake au sehemu ya nchi yake kutumiwa kwa shughuli fulani ya nchi ya nyingine ya nje. Kwa mfano tulisaini HGA na nchi ya Uganda kuiruhusu Uganda kutumia sehemu ya nchi yetu kupitisha bomba lao la mafuta na sehemu ya bandari yetu ya Tanga kuhifadhi na hatimaye kuyasafirisha hayo mafuta yao ughaibuni. Hilo bomba na hayo mafuta siyo mali zetu wala hayatuhusu. Lakini tuliwataka kwenye hiyo HGA wawe wanatulipa kiasi kidogo cha thamani ya mafuta yanayopita kwenye hilo bomba lao. Eneo tulilowapa hao Uganda ni kwa muda wa milele au hapo watakapomaliza kabisa mafuta nchini kwao. Wanapata pesa kiasi gani kwenye shughuli yao hiyo ya mafuta sisi halituhusu, it is none of our business. TRA na wengineo eneo hilo haliwahusu kwani litakuwa ni la Uganda, sisi tunapaswa tu kulilinda tukiwa nje ya shughuli. Kwa hiyo HGAs zitakazofanyika kwa serikali ya Dubai nazo zitamaanisha hivyo. Mbaya zaidi Dubai Emirate bayou siyo sovereign state kama ilivyo Uganda, mambo ya ushirikiano na nchi za nje uko chini ya UAE (United Arab Emirates) kama sisi huku ilivyo kwa serikali ya Zanzibar masuala hayo ni ya URT (United Republic of Tanzania).

6. Kwa nini basi haswa hawa wapanga mipango yetu ya maendeleo wameu complicate sana huu mradi wa kuboresha bandari yetu kuu ya DSM kuwa bandari ya viwango vya kisasa vya kimataifa vya mwendo kasi wa upakuaji na upakiaji wa meli unaofanyika digitally na kwa remote control ukiwa mbali na eneo?

Mbona mradi wa aina hiyo ni rahisi tu na gharama yake haiwezi hata kufikia nusu ya mradi wa bwawa la umeme (wa trillion saba) lilijengwa kwa viwango vya kimataifa na waarabu wa Egypt bila cha IGA, HGA wala sarakasi ya aina hiyo. Ni mradi mdogo sana ukilinganishwa na mradi wa SGR (wa trillion zaidi ya ishirini) unaojengwa na makampuni kutoka nchi za Utruki na China kwa muda wa miaka minne tu na mkataba wake haukuwa na IGA wala HGAs. Ni mradi mdogo sana ukilinganishwa na mradi wa LNG (wa trillion karibia mia moja) uliopewa makampuni makubwa ya nchi kadhaa za bara la Ulaya bila cha IGA kwa miaka milele bila hata ya wananchi kuambiwa kama ile fifty fifty win win situation ya sheria yetu ya nchi ya maliasili zetu imo kwenye mkataba huo wa muda wa milele au wa hapo gesi yetu yote itakapomalizika kuchotwa. Wala waziri wetu wa nishati haukupeleka mkataba huo bungeni kuridhiwa kwa sababu kwa makusudi haukuufanya uwe wa wa kiwango cha International treaty yaani IGA kwani angalifanya hivyo angelazimika kuupeleka bungeni ukaridhiwe. Kwani kwa mjibu wa katiba yetu ya nchi mikataba ya hadhi ya IGA aka International Treaty inapaswa kuridhiwa na bunge kwa niaba ya wananchi. Mikataba mingine ikiwamo ya HGA wabunge wetu hawapaswi kuiridhia wala hata kuiona kwani huwa ni confidential.

Mradi wa LNG kwa namna muundo wake ulivyo ulipaswa kuwa na hadhi hiyo ya International Treaty. Huu wa DP World muundo wake ni sawa na ule wa makontena wa TICTS ambao haukuwa na IGA wala HGAs. TICTS walikuwa ni kama waajiriwa tu wa TPA (makuli wa kupakua na kupakia meli) kwa mkataba wa miaka 20. Walikuwa chini ya uongozi wa TPA na hivyo ilikuwa rahisi kuwatimua wakiboronga wakati wo wote bila ya kupelekana kwenye mahakama za kimataifa.

7. Mpango wa utekelezaji wa dhamira nzuri ya rais kwa bandari ya DSM ulipaswa kuwa rahisi tu, rahisi kuliko ule wa SGR na wa JNHPP. Tayari kina cha bandari ya Dar tulikuwa tumesha kamilisha mradi (usio na IGA wala HGA) wa kuongeza kina chake hadi kufikia kina kinacho wezesha meli ya ukubwa wo wote duniani kutia nanga kwenye bandari ya DSM. Mradi huu wa DP World wa uboreshaji wa bandari hii ulipaswa kuwa wa kununua na kufungwa mitambo (cranes) ya kisasa ya upakuaji na upakiaji wa meli zinazofika hapo DSM.

Mitambo hiyo ilitakiwa kuwa ya automated artificial intelligence system yenye uwezo wa kutambua hata thamani ya kilichoko kwenye kila container na kiasi kodi zinazopaswa kulipwa serikalini (TRA etc) ambazo hata Rais wetu na ye yote mwenye password yake ataweza kuziona akiwa mahali po pote duniani. Ni kama zile alizoziona Bw. Msukuma, mbunge wa Chato, huko Dubai akabaki anashangaa kwani ni mitambo inayoendeshwa kwa kubonyeza remote control hata na mtoto wa miaka saba kama inavyofanyika kwa smartphone au television. Mitambo ya aina hiyo ingaliziba kabisa janja janja ya baadhi ya watumishi wa TPA na TRA wanayotumia kutupiga pale bandarini na kuchelewesha mizigo.

8. Hivyo mpango wa mradi huo ulitakiwa kuandaliwa na wahandisi wetu wa bandari (Port Engineers) wakishirikiana na maafisa mipango wetu. Timu yetu hii ya senior port engineers na senior planning officers wetu tungaliweza kuiongezea nguvu za kiutalaamu kwa kuwapatia Consultant Port Engineers wa kukodi kutoka nchi zenye uzoefu huo eg kwa rafiki zetu wa Dubai. Timu hii ingebainisha aina na kiasi cha mitambo inayohitajika na gharama yake. Hivyo timu hii ya watalaamu ingalitayarisha BQ (bill of quantities) na kuiachia serikali kutafuta source ya ku finance huo mradi ambao ungaliweza kutoka kwa mapato yetu ya ndani au kutoka kwa mikopo yenye riba nafuu kutoka mahali po pote hususani kwa rafiki zetu wa Emirate ya Dubai. Rais alichofanya huko Dubai na kwingineko duniani alikokwenda na atakakoendelea kwenda ni kututafutia marafiki ambao tutaweza kuwakopa au kutupa misaada (grants) tunapokuwa na uhitaji. Haendi huko kufanya International Treatises za aina ye yote bali MoUs tu za ushirikiano wa kiurafiki.

9. Baada ya serikali kupata source of finance wa mradi huo, competitive tender ingalitangazwa ya kupata kampuni ya uhandisi ya kusimika mitambo hiyo katika bandari ya DSM. Tender hiyo ya miaka isiyozidi mitatu ingalijumuisha usimamizi wa uendeshaji wa mitambo hiyo na kuwafundisha watanzania kuiendesha mitambo hiyo ndani ya kipindi hicho cha miaka mitatu kama itakavyokuwa kwa miradi yetu ya SGR na JNHPP. Ugumu uko wapi hapo? Kwa nini wanasheria wa serikali ndiyo wamekuwa wa kwanza katika utayarishaji mpango wa mradi huu, badala ya wahandisi na wanamipango wetu? Wanasheria hawa walipaswa kuhusika mwishoni kabisa wakati wa kuwekeana mkataba na huyo mkandrasi wa kusimika hiyo mitambo ya kisasa pale bandari ya DSM. Wanasiasa wetu kwa maana ya cabinet yetu ndiyo wa hatua ya mwisho kabisa ambao kwa niaba ya wananchi wanapaswa kujiridhisha na kuridhia kuwa kilichofanywa na hao watalaam wetu hakina dosari yo yote kwani mambo yakija kuharibika at the end the back stops at them!

Kilichofanyika kwenye mpango wa mradi huu ni vice-versa, yaani waliopaswa kuwa wa mwisho wakawa wa kwanza na wale waliotakiwa kuwa wa kwanza watakuwa ndiyo wa mwisho. Hiyo sasa ni sarakasi, kichwa chini miguu juu. Na hii ndicho sarakasi bado inayoendelea kwa wanasiasa kuwa wanasheria wa kudadavua vifungu vya sheria vilivyomo kwenye mkataba huo huku wanasheria wa serikali wakiwa wame mute. Kulikuwa hakuna sababu ya kujumulisha bandari zote za majini na za nchi kavu za Tanzania bara kwa pamoja kwenye mradi huu. Tungeanza na bandari moja ya DSM. Hizo zingine zingalifuata baadaye moja moja kwani hata mahitaji yake ya maboresho yanatofautiana na ni madogo. Sasa bandari kama ya Ukerewe inahitaji maboresho gani ambayo yanatushinda hadi tumwachie Mwarabu wa Dubai kuyafanya?

10. Kwenye miradi ya kimkakati kwa Taifa si jambo la busara kuiweka miradi hii kwenye umiliki ya uendeshaji wa watu binafsi au kampuni binafsi au nchi nyingine ya nje. Miradi hii ya kimkakati kwa taifa letu ni pamoja na ya miundombinu ya nishati, reli, barabara, bandari na usafiri wa anga. Miradi ya aiana hii ni roho na mishipa ya damu ya uchumi wa taifa letu. Si busara hata kidogo kubinafisha, kukodisha au kupangisha miundo mbinu hii. Na tunapaswa kuiijenga na kuiboresha kwa pesa yetu ya ndani au ya mikopo nafuu ya serikali yetu. Hili ndilo jukumu kuu (core function) la serikali yetu la kuleta maendeleo ya nchi yetu. Pia ni kwa ajili ya usalama na utulivu wa kijamii wa nchi yetu. Tunaweza kupangisha au kukodisha au kubinafisha au kuuza mbuga zetu za wanyama pori, mashamba ya mpunga, mahindi, karafuu etc lakini siyo hii miundombinu ya kimkakati ya taifa letu. Uwekezaji kwa natural resources za nchi nao lazima uzingatie sheria yetu nzuri ya natural resources inayozingatia not less than 50 % win-win situation.

11. Kwa lugha ya kawaida, mwekezaji halisi (original) ni yule anayekuja na mtaji wake tunampa eneo (ardhi) lililo tupu la kufanyia uwekezaji wake. Uwekezaji huo unaweza kuwa wa kujenga kiwanda chake, kilimo au shughuli nyingine zikiwamo za huduma hususani hospitali au shule. Mazao ya uwekezaji wake atayauza ndani au nje ya nchi jinsi atakavyo amua yeye kwani ni mali yake. Na bei atapanga anayotaka yeye, hatutamwingilia isipokuwa kwenye hiyo ataongeza VAT yetu; yaani atakuwa wakala wetu wa kutukusanyia VAT kutoka kwa wateja watakaonunua bidhaa au huduma zake.

Mwekezaji feki ni yule anayekuja tukampatia mali yetu hususani Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Bwawa la Kuzalisha Umeme la Nyerere au SGR yetu kwa madhumuni ya kuiendesha yeye na kuiboresha ili performance (ufanisi) yake iwe bora zaidi kwa sababu tu eti sisi tumeshindwa kuongeza performance. Mwekezaji wa aina hii anaweza akawa wala hana mtaji wo wote wa maana akitegemea kuupata hapa hapa kwenye mradi wetu. Mbaya zaidi kama tutaingia naye mkataba unaompa protection kubwa ya kutomwingilia au kumgusa kwenye shughuli zake ikiwamo mapato atakayovuna kutoka kwenye miradi yetu nyeti ya kitaifa. Mwekezaji wa aina hii anaweza akawa hata taperi (brief case investor), haijalishi anatoka nchi gani. Tulishuhudia akina Richmond toka USA walichotufanyia wakati ule wa awamu ya nne ya JK!

Sasa huyu DP World wananchi wengi wanashindwa kujua yuko kundi gani la wawekezaji. Jee ni kweli DP World anakuja kama muwekezaji kama ambavyo baadhi ya wanasiasa wanasema? Au anakuja kama mkandrasi wa kuboresha bandari yetu ya DSM? Alipaswa kuja kama mkandrasi na sisi ndio tutakuwa tunamlipa ujira wa kazi tutakazompa kufanya kwa kipindi tutakachoona kinafaa kukamilisha kazi hiyo. Wala serikali isiogope kukopa kwa ajili ya kutekeleza miradi kama hii ya kimkakati ya maendeleo. Dunia inampenda sana rais wetu na ingependa afanikiwe kwa kiwango kikubwa kuipaisha kimaendeleo Tanzania; ili kuwa mfano kwa nchi zingine hasa za kiafrika zilizong'ang'ania kuwa cheo cha urais ni cha wanaume tu na hasa wanaume waliokuwa wanajeshi.

hapa alikuwa anaongelea mkataba ule wa juzi tuliolipa bilioni zaidi ya 200, hii tutaiita kesi ya Prof.Mruma. ajabu yake, dhambi zetu sisi wenyewe yeye pia ndio kaingia mkataba wa ajabu kuliko hata ule tuliolipa mamia ya mabilioni.
 
Mnapofeli ndio hapo.. Kwanini haujataka kusoma hili andiko lote... Kuna aina tofautitofauti za uandishi, mimi nakuomba rudia tena kulisoma andiko lote. Mama katetewa kwani nia ya aondoke mwenyewe bila kufukuzwa.
Nishafeli
 
Umeandika kisomi San yaani
 
Back
Top Bottom