Tatizo la bandari ya Dar ni ufisadi uliokubuhu. Dubai hawana tatizo hili, sasa IGA inakujaje? Hata HGAs ni batili

Dr Akili

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
4,953
4,326
Hauhitaji kuwa mwanasheria kufahamu maana na dhana ya haya maneno ya IGA na HGA.

Makubaliano ya taifa moja na taifa moja jingine au zaidi yenye nguvu za kisheria (legal binding), yanayohusu kushirikiana kutatua matatizo fulani yanayozikumba nchi zote husika yanaitwa Treaty. Maneno mengine yanayotumika badala ya neno treaty ni convention, protocol, pact au accord. Sisi waswahili tuanaita mkataba wa kimataifa. Kwa kiingereza, a treaty is a legally binding agreement between two states or more than two states.

Ikiwa ni nchi mbili tu ndizo zinahusika mkataba huo unaitwa Bilateral International Treaty, kwa kifupi BIT ambayo wengine wa kisasa wanaiita IGA. Ikiwa nchi husika ni zaidi ya mbili, mkataba huo unaitwa Multilatera International Treaty au kwa ufupi MIT.

Jambo la muhimu ni kwamba tatizo (problem) linalohitaji ushirikiano wa pamoja wa namna ya kulitatua ni lazima liwe ni tatizo linapatikana kwenye nchi zote zilizo kwenye mkataba huo na kwamba bila ushirikiano wao wa pamoja tatizo hilo halitakwisha nchini kwao. It must be a mutual problem. Na kwa sheria ya kimataifa hizi BIT aka IGA na MIT ni lazima ziridhiwe na mabunge ya nchi husika. Zinaweza kuridhia with reservations kwa baadhi ya vipengele vya mikataba. Kwa mfano hiyo Vienna Convention on the Law of Treaties (1969) sisi Tanzania hatukuridhia hiyo article 66 inayohusu procedures for judicial settlement, arbitration and conciliation.

Sasa tatizo la bandari yetu ya Dar es Salaam ni ufisadi uliokubuhu na sugu, miaka nenda miaka rudi. Kwenye awamu ya JPM ulipungua kwa kiasi kikubwa kutokana na very close monitoring ya rais mwenyewe in person na tumbua tumbua yake. Nchi ya Dubai haina tatizo la namna hiyo nchini kwao. Hili tatizo la ufisadi pale Dar port ni la kwetu pekee wala Dubai hawahusiki. It is not a mutual problem of Tanzania and Dubai Emirate. Sasa IGA inakujaje hapa? Mkataba huu wa IGA ni batili kabisa by definition of IGA aka BIT.

HGA ni maridhio (yenye nguvu za kisheria) ya nchi mwenyeji (Host Government) kuruhusu sehemu ya nchi yake itumike kufanyia shughuli au mradi wa nchi nyingine. Kwa mfano tuliwaruhusu Uganda kupitisha bomba lao hadi bandari ya Tanga. Pia tuliwapa sehemu ya nchi huko Tanga ya kuhifadhia mafuta yao kabla ya kusafirishwa kwenda ughaibuni. Mkataba huo wa HGA kwa Uganda ni wa milele au hadi pale Uganda watakapomaliza mafuta yao. Lakini hatukuwaruhusu bure: tulikubaliana nao kwamba watakuwa wanatulipa senti 12 za USD kwa lita ya mafuta yanayopita kwenye bomba hilo, pia watatoa ajira kadhaa kwa watanzania, na sasa tutawapelekea na kuwauzia gesi yetu kupitia bomba hilo.

Yaani dhana ya HGA ni kuwa shughuli au mradi unaofanywa ndani ya nchi mwenyeji ni mali ya huyo wa nchi nyingine. Hakuna takwa la sheria za kimataifa la mabunge husika kuridhia mikataba ya HGA. Hilo bomba litakalopita nchini kwetu ni la Uganda, mafuta ni ya kwao, shughuli zote ni za Waganda na hatupaswi kuwaingilia kwa vyo vyote vile isipokuwa kuwalinda. Sasa hawa Dubai Emirate na DP World wao ndivyo nao wanataka hivyo kwamba baada ya IGA tutasaini pia HGAs mbali mbali za kuruhusu sehemu ya nchi yetu wafanyie shughuli zao? Yaani hayo maeneo ya bandari yawe ya kwao sawa na tulivyowapa Waganda? Hili halikubaliki na ni batili by definition. Wao waanzie tu kwa projects tutakazo ziandaa, kuzitangaza (tender) na kama watashinda tenda tutawapa. Mbona huyo TICS wa kutoka China hatukuwa naye na IGA wala HGA.
 
Hii bilateral international treaty ndiyo ya kwanza kufanyika na kuridhiwa na bunge letu. Tumeridhia multilateral international treaties nyingi ikiwamo hiyo ya MIGA (Multilateral Investment Guarantee Agency), ICSID (International Center for Settlement of Investment Disputes), Vienna Convention on the law of Treaties minus its article 66, the Geneva convention on war crimes na kadhalika.
 
Back
Top Bottom