Machangudoa wa UK kiboko,tahadhari kwa wana JF

Wa Ndugu,

Kama wiki moja hivi iliyopita nilikuwa Liverpool,UK kwa dhumuni la kumuwakilisha mteja wangu kwenye baraza(tribunal) moja la migogoro juu ya biashara ya pamba, nilipofika Heathrow Airport nilikutana na binti mmoja umri wake kama 17-19 akiwa na bango lenye jina langu la kunikaribisha,akajitambulisha kuwa anaitwa Cassie na ni mhudumu wa hotel niliyopanga kufikia:

Kwa kuwa ilikuwa week end nilipanga kukaa London muda wote hadi jumatatu ambayo ilikuwa siku ya kesi, nikaongozana nae moja kwa moja hadi hotelini,tulipofika reception tukaulizwa mko pamoja?? akajibu "oooh, yes! akanisindikiza hadi chumbani kwangu na akaniomba aingie ili aweke mizigo yangu,kwa kuwa nilijua labda ndiyo British hospitality nikakubali.............kumbe ilikuwa janja ya nyani[ili ionekane kama tuko pamoja,yaani nimekuja nae] alipofikisha mizigo akaniaga na kuondoka.

Baadae niliondoka mpaka Sussex kuonana na ndugu yangu mmoja na kula bata kiaina,niliporudi usiku reception wakaniambia funguo anazo mwenzangu.....nikaduwaa lakini sikutaka kuwashtua ili nijue nini kinaendelea in case mambo yakienda kombo niwa sue(niwashtaki kwa usumbufu ili wanilipe fidia)...basi ile kuingia chumbani,nikamkuta Cassie akiwa na night dress ameketi kwenye kijimeza,amewasha mishumaa huku akinywa mvinyo akanipokea kwa mahaba mazito kwa maneno ya ulaghai.......AT YOUR SERVICE P'SE,nikamuuliza what service?? akaanza kusaula,nikasema yaleyale ya STRAUSS KAHN!!!! nikachukua simu ili kupiga reception na polisi akanisihi nisifanye hivyo kwani yupo kazini,nilipomuuliza kwa nini hakusema akaniambia yeye sio HO, bali anatafuta pesa za kwenda mapumzikoni tu........nilipomsamehe aliniporomoshea matusi makubwa eti mi nyani tu................

Hayo ndo yaliyonisibu,kwa hiyo mkuwe makini jamani wale mnaopenda kutembelea pande hizo........

Kwa kiasi fulani huu mtiririko umekosa mshiko............aidha mkuu mvua ya kiangazi unasema kweli lakini ni mzembe (tusi kama wewe ni mwanasheria) ama unachangamsha kijiwe tu!
1. Aliyekupokea umesema ni mhudumu wa hoteli tena unafika hoteli eti anasema mko wote?? Masuala yanaanza kunitanza, hivi hapo reception hawamjui mhudumu wao?
2. Umesema msichana ni miala 17-19? Well, in UK hotel reps wao wengi wanaopokea wageni ni kuanzia miaka 30, kwa sababu mimi nimeshawahi kuifanya hii kazi na kuipata kwake, mbali ya mambo mengine wanataka pia lazima uwe na uzoefu kwenye udereva (at least miaka 3 bila points kwenye leseniya udereva) na uwe walau kuanzia miaka 25 (kwa sababu ya bima) Huyo msichana leseni alipata akiwa na miaka mingapi? ama unataka kutwambia mulikodi gari? Kwa huduma ya mapokezi wakifanya hivo ni hasara.
3. Uliondoka London J3 siku ya kesi? inawezekana kama ulipanda domestic flight ila haijakaa vema kwamba unasafiri siku ya kesi yenyewe, ukizingatia usafiri na hata kama ulienda na ndege bado kuna morning traffic jam toka J. Lennon airpot kwenda City. wacha niishie hapa.
 
Next time fikia kwa ndugu zako Sussex, uwasaidie kupunguza umasikini na bills
 
Yes tahadhari ni kitu muhimu sana...... ila if it was me, hiyo ni strauss kahn case and I was going to make sure she is outta my room the next second. If I needed a ho, then let me go find her by myself.....pole lakini... halafu euro mia 2 parefu pia duh.
 
Aisee Moskwito........... me nilifikiri unabite them human beings usiku.......... kumbe hata mchana unafyonza tu.......... khaaa!

BTW Moreno O'campo alikuwa natafauta wasaidizi, nimtumie contacts zako?

...lol...huyu bro kwa hii simulizi yake, jurors wote mpaka sasa tunamuona 'guilty until proven innocent!'
 
JF raha tupu!
1. Lawyer anakubali kuwa yuko pamoja na msichana wa umri mdogo, isitoshe mwongo.
2. Lawyer anatoa pounds 200 baada ya kuitwa nyani
3. Lawyer bado anauchuna anapoulizwa ataje jina la hoteli.
4. Hoteli hawawajui wahudumu wao.
5. Hoteli za London, kama vile wanavyofanya guest house za Sinza, hawadai passport na/au vitambulisho vya wateja wao
 
twenty-pounds-notes.jpg
mikwara mingine! So you have paid him!
 
Kwa kiasi fulani huu mtiririko umekosa mshiko............aidha mkuu mvua ya kiangazi unasema kweli lakini ni mzembe (tusi kama wewe ni mwanasheria) ama unachangamsha kijiwe tu!
1. Aliyekupokea umesema ni mhudumu wa hoteli tena unafika hoteli eti anasema mko wote?? Masuala yanaanza kunitanza, hivi hapo reception hawamjui mhudumu wao?
2. Umesema msichana ni miala 17-19? Well, in UK hotel reps wao wengi wanaopokea wageni ni kuanzia miaka 30, kwa sababu mimi nimeshawahi kuifanya hii kazi na kuipata kwake, mbali ya mambo mengine wanataka pia lazima uwe na uzoefu kwenye udereva (at least miaka 3 bila points kwenye leseniya udereva) na uwe walau kuanzia miaka 25 (kwa sababu ya bima) Huyo msichana leseni alipata akiwa na miaka mingapi? ama unataka kutwambia mulikodi gari? Kwa huduma ya mapokezi wakifanya hivo ni hasara.
3. Uliondoka London J3 siku ya kesi? inawezekana kama ulipanda domestic flight ila haijakaa vema kwamba unasafiri siku ya kesi yenyewe, ukizingatia usafiri na hata kama ulienda na ndege bado kuna morning traffic jam toka J. Lennon airpot kwenda City. wacha niishie hapa.

Kama kweli kiangazi ni mwanasheria nileze vizuri hayo mazingira kwenye red yamekaaje???
Vinginevyo wewe ni walewale wa ikataba feki wasiojua wanachokifanya!
 
Mama D, ni kweli sijawahi kupokewa na hotelier hata mara moja, na sijui utaratibu wao wa kuajiri,pia miaka 17-19 hakuniambia ila ni makadirio yangu kwa jinsi kalivyokuwa kanaonekana,bahati mbaya,sikumtilia shaka hata kidogo,na hata reception alivyouliza MKO WOTE???(Mimi nilitafsiri kuwammekuja pamoja kutoka airport) hilo nalo katika mazingira yale halikumaanisha hawamfahamu(kwa tafsiri yangu) ila tumefika pale wote???

kwa hiyo,katika mazingira hayo yote,kilichonishtua ni pale nilipoambiwa mwenzangu yupo chumbani(sikuogopa maana kiulinzi nilishajiandaa) kwa mazingira hayo ndo maana nimetoa tahadhari katika forum hii,labda mama D kwa kuwa umeshafanya kazi huko,unaweza kushare uzoefu na wana jf japo kwa mengine ambayo aidha yanafanana na hili au ya namna hii........................
 
Back
Top Bottom