RIWAYA: HIsia zangu (TEST)

Man Jau

JF-Expert Member
Apr 8, 2011
461
682
Nimeanza tabia mbaya tangu nikiwa shule ya msingi, nimefanya na watu wengi sanaa tena sanaa. Lakini kwanini naandika kitabu hiki?? Ni kwa sababu ninataka ufahamu kitu; kuwa tangu nianze kuwa na tabia mbaya mpaka sasa sijapata faida yoyote ile, si kwa Mungu wangu mbinguni, wala kwa wanadamu duniani.

Nakumbuka ilikuwa darasa la pili, yes, nina kumbukumbu yenye nguvu sana, na nakupa siri hii, ukitaka kuwa na tabia mbaya kama za kungwi na mwenye kuyaweza mambo ni lazima uwe na memory nzuri na yenye nguvu.

Ninakumbuka darasa la pili, nilikuwa mwanafunzi ninayefanya vizuri sana darasani, sio maarufu lakini ninafanya vizuri mno. Enzi zangu masomo ya vipindi yalikuwa machache, kiswahili, kiingereza, imla, kuchora, hesabu na mwandiko. Madaftari tunaandikia mojamoja, kila somo na daftari lake. Daftari langu la mwandiko nalikumbuka vizuri sana kwa sababu nilikuwa nasifiwa saana katika kuumba maandishi vizuri, yaani ukitazama herufi Aa, Bb, Cc na Dd zangu, haadi raha, unasisimka kuziona.

Mwalimu wangu simkumbuki vizuri ila alikuwa ananisimamisha ubaoni, niwaandikie wanafunzi wengine. Enzi zile tulikuwa tunapewa Boonge moja la rula, alafu unalinyoosha kisha unachora mistari miwili kama vile kwenye daftari la Mwandiko, na kisha ukianza kuumba herufi, zinajitokeza vizuri sanaa mpaka raha.

Sasa mara nyingi huwaga wanakuja wanafunzi wa madarasa yaliyotuzidi kisha wanakuja kutuchorea na kutuandikia, ila kwangu mimi, hali ilikuwa tofauti, na nakumbuka vizuri kuwa tuliwahi kuchorewa na mwanafunzi wa darasa la tatu mara moja tuu, na hio ndio ilikuwa mara ya kwanza na ya mwisho kwa darasani kwetu kuchorewa somo la mwandiko na waliotuzidi kidato, na hii ndio ilikuwa mara yangu ya kwanza kuonekana kuwa ninajua sana kuandika vizuri.

Kisa chake kilikuwa hivii;

Nilikuwa na rafiki yangu anaitwa Riziki, tulikuwa watundu sana, watundu balaa darasani, yaani ni wale wanafunzi ambao hatuvumi lakini tumo. Sisi tulikuwa tunajifanya vimwinyi vitoto, yaani tunaingia darasani na hela, tunakula na kunywa, hatuandiki, hatusomi, tunapiga kelele weeeeeh, mpaka tunachoka sie, muda wa kulala tunalala, tukiamka tunaondoka. Huu ndio ulikuwa mchezo wetu tangu vidudu, well, unakumbuka nilikuambia kuwa nina memory nzuri? Well, story nyingi za vidudu nilisimuliwa na wazazi wetu, picha, etc, but its all good.

Sasa, katika masomo yote, somo la hesabu ndio somo pekee ambalo tulikuwa kimya sana, hatuongei chochote wala kupiga kelele, wala kuleta utundu. Tulikuwa kimya mno. Hatuna ujanja. Hii ni kwa sababu mwalimu wetu wa hesabu alikuwa anaogopeka na wote, maana alikuwa mpole sana lakini ukikosa hesabu zake utachezea bakora mpaka ulie. Maana wanawake walikuwa wanachapwa mkononi mpaka wanalia na kwa wanaume walikuwa wanachapwa matakoni tuu, hadi wale masugu tunaowajua na kuwakubali kuliko maelezo walikuwa wanatoa kilio shuu, kiasi kwamba wote badala ya kumcheka mwenzetu tunakuwa kimyaaa kwa woga. Na hii tulikuwa tunaaminika kuwa labda huenda sisi tulikuwa watundu ndio tungekuwa na namna ya kucheat ila haikuwa hivyo..hadi sisi tulikuwa kimya. Na hali hii haikuwa kwetu sisi tuu, bali kwa darasa zima...mwalimu yeye alikuwa hajui cha mtoto wa mwalimu wala diwani, yeye ni bakora tuu..huyu mwalimu aliwahi kumchapaga mwanafunzi mpaka akazimia, akamchapa tena fimbo ingine moja tuu tena ile kubwa kuliko, mpaka akazinduka, ukatuni na uchalechale wa mwanafunzi huyo ukamuisha hapoapo, wa kumuita juma kereke.

Somo la Mwandiko ndio somo langu pendwa. Nalipenda mpaka basi, nimekuwa nikipenda kuandika tangu chekechea na nahisi ndio linahusika katika kunipa hamu ya kuwahadithia haya na mengine mengi zaidi kwa njia ya maandishi. Haya, chai na yenyewe isiwe nyingi, acha niendelee.

Baada ya yule mwanafunzi wa darasa la tatu kuandika vizuri kwenye ubao, nakumbuka alikuwa mwanamke, maana shule yetu ilikuwa na wasichana wengi sana kuliko maelezo, darasani kwetu tuu kulikuwa na wasichana arubaini kati ya watu hamsini, kitu ambacho si cha kawaida kwa shule nyingi za msingi...ila kwetu ilikuwa ni kawaida kwa wadada kutuongoza kwa kila kitu. Kwa wanaoifahamu shule yetu watakubaliana na mimi kwamba imekuwa ikipokea waalimu wa kike wengi na bora zaidi kuliko maeneo mengine, wanafunzi wa kike wengi zaidi kuliko maeneo mengine na hata attendance yetu ilikuwa na falsafa ya wanawake wengi zaidi kuliko wanaume. Ingawa ilikuwa ni shule ya mchanganyiko lakini wanawake walikuwa wengi sana, zaidi ya robo tatu shule nzima

Unaweza kudhania kuwa kwanini shule hii haikufanywa kuwa shule ya wasichana pekee, ni kwa sababu katika uanzilishi, bodi ya shule ilikuwa na viongozi wasichana wengi na mwanaume mmoja tuu, na yeye ndie aliefanikisha kila jambo ingawa alikuwa haongei, wala kuchangia mada ya mazungumzo katika harakati za awali za uanzilishi wa shule, so hii ikapelekea uamuzi uliokuja kutolewa ni kuwa na muongozo wa jinsia ya kike kwa asilimia kubwa sana, zaidi ya wanaume.

Shule yetu kwanza ilianza kwenye miaka ya tisini, enzi hizo kabla ya siasa ya vyama vingi. Miaka ya tisini utawala wa nchi ulikuwa unahusisha kujijua na kujitambua zaidi, kutambua fursa mpya na ndio maana mzee rukhsa alin’gara kwelikweli kwa sababu kila kitu kipya kilipewa kibali na kipaumbele.

Haya

Turudi kule kwa mwanafunzi wa darasa la tatu.

Mwanafunzi huyu aliitwa Haida, ni mrefu na mwenye umbo kubwa mno. Akisimama darasani umbo lake ni sawa na kusema mwalimu amesimama darasani. Hii ilipelekea kuwa endapo akiwa anaelezea kitu, watu woote kunyamaza kimya kumsikiliza, kwa sababu akisema, we ni nani mpaka upinge? Enzi hizo ukiwa na mwili mkubwa unaonekana mbabe, unasikilizwa na hata kuogopwa. Tulikuwa wadogo sana, hatuna hisia wala utambuzi, ila kwangu, hali ilikuwa tofauti. Nilimuona kana kwamba ni mtu wa pekee, ule upole wake anavyotabasamu, au kukohoa kwa huruma, au akishika rula kubwa ya mbao darasani kana kwamba inataka kumuanguka, kulinifanya nimuangalie kwa makini mno kuliko maelezo, kiasi cha kukazania details zingine nyingi tuu ndogondogo.

Nilimtanzama tangu alipoingia na kuweka rula yake pembeni ya ubao, mwalimu nakumbuka aliongea na kutusemesha kuhusu yeye akimtambulisha ila mi sikusikiliza chochote, nilikuwa aniangalia ile rula tuu na yule aliyeishika ile rula na kuiweka pembeni ya ubao. Umakini wa kumuangalia yeye uliongezeka kwa sababu baada tuu ya kuiweka rula hio pembeni ya ubao, alikuwa akiona aibu na kuamua kuzuga kwa kuichezea rula ile kwa kuigongagonga ukutani, kitu ambacho kilikuwa kinanihamisha umakini kwa mbaaali, hadi kuamua kuituliza akili yangu kwa kumuangalia yeye huku mawazo madogo kwa mbali yakinijia na kuondoka, “hivi yeye ni nani? I ina maana anajua sana kuandika? Ina maana huyu ni bora kuliko wote? Mh! Hapana, mwalimu amesema ni darasa la tatu, hawezi kuwa bora kuliko darasa la nne, la tano, la sita na la saba” huyu atakuwa wa kawaida tuu.” Lakini kuandika hakuhitaji akili, mbona mimi ninafaulu sana darasani na ninaandika vizuri kuliko wote lakini hesabu sipatagi mia. Riziki pia ziiro, kila somo anafeli na kuandika anajua, ingawa hanifikii mimi, lakini anajua.”

Nimejiuliza maswali haya mengi namengine majibu sijapata, hadi nikaamua kunyamaza kimya.

Baada tuu ya utambulisho, mwalimu alizugazuga kidogo kisha akakaa nje. Mwalimu wetu huyu alikuwa hapendi kufundisha, muda wote yeye anaona uvivu, anasinzia, hata ongea yake imekaa kizembezembe, hadi walimu wenzie walikuwa wanamuita jina la utani sleepy sasa kwa vile sisi tunapenda kushika kiherehere tukitumwaga tukawa tunasema silipi. Mwalimu silipi anataka hiki, mwalimu silipi anaitwa, na kwa vile alikuwa sio mtu wa kutumia, muda wote yeye analala tuu, jina lake likavuma shule nzima, ila cha ajabu mkuu hakujua kaitwa hivyo kwa sababu gani, maana alikuwa analala sana na hajawahi hata siku moja kumuona akilala kwani mara nyingi analala darasani, nyuma kabisaa, na darasa letu alikuwa analipenda sana kwa sababu tulimtunzia sana siri yake hii...ila kama unavyojua tenaa shule, kila mtu ana tabia zake tofautitofauti, Haikutuchukua muda kwa wanafunzi makini kama mimi kujua kuwa mwalimu huyu ni mvivu. Maana tuliandika sana ubaoni, sanaaa. Yeye alikuwa anapenda kumtumia mwanafunzi huyu hadi kwenye madarasa mengine kwa sababu ya umbo lake, coz anavyoonekana mkubwa hata mkuu akipita kwa mbali anakuwa anaona kana kwamba ni mwalimu anafundisha, mpaka alipokamatwaga miaka kadhaa baadae na kusimamishwa shule baada ya wanafunzi kumripoti kuwa anawafanyisha sana kazi yake kuliko wao kujisomea. Si unajua tena shule zikiwa na wanawake wengi, umbeaumbea unatoka hapa, unaenda pale, unakuzwakuzwa weeh mpaka unafika kule, mwisho wa siku inakuwa kesi. Ingawa kwa upande wa mwalimu wangu wa mwandiko alizingua lakini kwa kiasi fulani najikuta namtetea kidogo kwa sababu ya mapenzi yangu ya kuandika.

Haya, turudi kwa Haida, ilikuwa mara yake ya kwanza kuingia darasani kwetu, na kwa hali ilivyo, mzubao wangu haukuleta athari yoyote kwake, maana hata sidhani kama aliuzingatia.

Aliangalia darasa zima, kisha hakusema kitu, kila mtu alikuwa anapiga kelele, mwalimu alikuwa amevuta zake kiti nyuma kabisaa ya ubao, alafu akaanza kulala. Watu walikuwa wanaendelea kuongea, na kunongona, mi nilikuwa makini namuangalia Haida kwa umakini. Riziki nakumbuka alikuwa ananisemesha kitu, lakini sikumsikiliza, si unajua tena wanafunzi wa shulke ya msingi, tunapenda kelele tuna buzzing kama nini sijui. Haida aliliangalia darasa zima, kisha akaanza kuongeza mapozi fulani hivii ambayo kwa wakati ule sikuyaelewa. Kisha akaanza kuchora mstari.

Nilikuwa na hamu mno, ya kuandika kama yeye alivyokuwa anaandika ubaoni, nilikuwa makini kumfuatisha kila hatua anayofanya, yeye akifanya ubaoni, mimi nilikuwa naifuatisha kwa rula na penseli yangu tena kwneye daftari ambalo limeshachorwa tayari mistari.

Naomba nikukumbushe tuu kuwa ninapenda sana muandiko, kiasi kwamba sikosi rula kwenye begi langu. Kuna muda naandikaga somo la muandiko, mpaka daftari langu linajaa, na kwa vile tulikuwa tuna daftari la kuchora lakini hatulitumii sana kwa sababu mwalimu wetu wa kuchora alikuwa hapendi kuchora kwa sababu hajui kuchora vizuri, kuna siku alituchorea ndege vibaya tukacheka darasa zima, akakasirika na kutuchapa woote, wanafunzi wote tukamchukia, mwalimu mkuu aliliona tukio zima na kuamua kumhamisha kazi mwalimu kwa kukosa umakini akiwa kazini. Hii imetufanya tukae muda mrefu bila kulitumia daftari hili. Kwa hio daftari la mwandiko likijaa au nikiwa nimelisahau nyumbani au mahali pengine, natumia daftari langu la kuchora kuandikia, na kwa sababu nina rula, ninachora vizuri sana na nakuwa naenda sawa na ubao jinsi ulivyo, so, kuna wakati nagandamizia kwenye daftari la muandiko, na kuna wakati nachora upya kwenye daftari la kuchora.

Sasa wakati Haida anaanza kuchora nilikuwa natumia daftari langu la mwandiko, na lilikuwa linakaribia kujaa. Nikaanza kuchora mstari wa kwanza na wa pili, kisha nikaandika herufiza mwanzo alizoandika ubaoni. Kumbuka kuwa hili lilikuwa daftari la Mwandiko so kila mstari nilikua nachora tena upya kwa kugandamizia. Haida yeye aliandika Aa Bb Cc na Dd kwa kwenda chini, ili kila herufi tuifuatilizie kimshazari kwa kuirudia, mi nilivyoona nikaacha, nikaamua kulitoa daftari langu la Kuchora kisha nikaanza kuchora na kuandika vile alivyokuwa anaandika yeye. Sijui ni ushindani au kwenda sambamba..ila nilijikuta tuu nafanya hivi…sijui kuwa nilihisi ninataka kufaidi..ila ndio hivyo. Huenda Nilifanya hivi kwa sababu niliona kila kitu anachoandika ni rahisi mno.

Kumbe wakati nahangaika kutoa daftari la Mwandiko, Haida aligeuka na kuniona, kisha akanyamaza kimya akawa ananiangalia. Mi wakati sijui hili wala lile, wala sijaangalia tena ubaoni, nikawa naendelea na harakati zangu za kuandika, darasa zima lilikuwa linaendelea kuongea, kisha wakawa wanapunguza makelele taratibu na baadae kuwa kimya. Kwa vile mimi nilikuwa napenda ninachokifanya, na ninakaa siti za mbele pembeni ilikuwa rahisi kidogo kuonekana na Haida, Ndio, najua utakuwa unajiuliza nimewezaje kupiga kelele nikiwa siti ya mbele? Ndugu, mimi ni mmoja wa wale vingunge, vimwinyi vitoto, siti yangu ilikuwa mbele pembeni, na waalimu wengi wakiingia darasani wanasimamaga katikati ili walione darasa lote, ila mimi nipo siti ya pili ukutani pembeni, na kulikuwa na njia nje ya darasa, so hata mwalimu akisikiaga kelele huwa tunamwambiaga kuwa kuna wapita njia huko, na sisi tulikuwa na taimingi moja nzuri sana, tukitaka kuongea tunamuangalia kwanza mwalimu kama anatuona, na tulikuwa na taimingi nzuri sana, sanaa, kiasi kwamba ilikuwa vigumu mno kutustukia.

Haida alianza kwanza kuniangalia, kisha akasogea kwa ukaribu mpaka nilipokuwa. Kwa vile nilitoka uwepo na akili yangu yote ilikuwa kwenye kuandika, nilijiona ni kana kwamba nipo kwenye dunia nzuuuri sana na ya kipekee, na kadri nilivyozidi kuandika ndipo maua maua mazuri yenye harufu nzuri na ya kuvutia ndio yalivyozidi kutoka kwenye yale maandishi niliokuwa naandika. Nilikuwa naandika vitu ambavyo navijua mwenyewe, na wala sio vilivyokuwa vinaandikwa ubaoni, niliacha kabisa kuangalia mbele, nilinogewa hasa na mwandiko ndio maana Haida alinishangaa na kunisogelea taratibu, sauti zote zilijichuja na kuwa kimya.

Wakati Haida aliposimama jirani yangu ile harufu ya manukato mazuri ilizidi, nikahisi kana kwamba mwandiko wa herufi b ndogo imenisimamia kwa kugeuka, na nikawa kama najisogeza karibu ya hio herufi, kwa mahaba mazito, na kuikumbatia, kumbe kiuhalisia nilikuwa nimemsogelea Haida na kumkumbatia bila mikono, maana alikuja na kusimama pembeni yangu na nilikuwa naihisi harufu nzuri kwa sababu ya manukato ambayo alikuwa nayo kwenye nguo zake za shule.

Wanafunzi wote walikuwa kimya kwa sababu walishangaa kuniona nikimkumbatia Haida mapajani mwake, ndio maana walikuwa kimya. Haida naye alikuwa kimya. Kila mtu alikuwa kimya, sauti ingine iliokuja kusikika ni ya mwalimu wetu wa darasa kule nyuma akikoroma, na hii ndio iliomstua kila mtu na kufanya darasa zima wacheke kwa kicheko. Ndipo nikastuka, naangalia hivi, naona nimejiegeza kwenye mapaja ya Haida nikiwa katikati ya kumbatio.

Niliogopa sana, kisha nikaona aibu sana, kwamba imekuwaje nimesinzia ghafla na kujikuta namkumbatia Haida? Tena nilikuwa nina mawazo tofauti kabisa na yeye, kiasi cha kwamba Mwandiko huu huu ndio...yaani mwandiko huuhuu ndio...aaah, ona sasa hadi nakosa neno la kusema,

Haida aliniangalia kisha akanipa pole, na kuniuliza kama ninaweza kuandika ubaoni. Nilikuwa dhaifu kifikra na nina kauwoga flani hivii kasikoelezeka, nadhani alielewa hilo na kuniacha nitulie kwanza. “Usiogope, ni kawaida tuu. Utakuwa sawa.” Haya maneno sijui yalikuwa na maajabu gani, nikatulia na kujikaza, kisha nikaenda hadi pale mbele, na kisha nikachukua rula na kuangalia ubao. Kwa jinsi alivyokuwa anaichezesha ile rula kubwa kwa madaha, iliniongezea sana hamu na msukumo kwa kuandika vizuri ubaoni. Kahofu kote kakaondoka, nikamuomba chaki, akanipa na mkono mwingine, kisha nikaanza kuandika tuu kidogo kwa wepesi kwenye kona, na kufuta, kisha nikamuomba rula.

Alichofanya, aliihamisha rula na mkono mwingine kisha akanipa, na nikaipokea na kuiegemeza kwenye ubao. Darasani watu walicheka kidogo kisha wakanyamaza kimya. Wakawa wanaendelea kuangalia ni nini kitakachotokea mbele ya ubao. Haya yote yalivyokuwa yanaendelea, kama ungekuja darasani kwetu siku hiyo kwa bahati mbaya ungeweza kudha ni kuwa mwalimu na mwanafunzi wanafundishana, na kuna ‘mkaguzi’ nyuma ya ubao amelala. Maana kila akikoroma kwa nguvu kama darasa liko kimya sana watu wanaanza kucheka na kuongea kidogo, kisha wananyamaza.

Nilianza kuchora mistari sawa na ile aliochora Haida, ilikuwa midhaifu kidogo, ila ilionekana. Haida yeye alitabasamu tuu, hasemi neno. Nilipomaliza kuichora yote miwili ndipo alinipa daftari ili niweze kuandika. Yalikuwa ni maelekezo ya kwenye daftari lake la shule ya msingi. Oh, my, najua nilikuwa najiamini sana kuwa naandika kuliko wote, ila damn, huyu mtu anajua kuandika mnoo, yaani kwa kuandika, ananikimbiza, ananifikia, ananipita na anapunguza spidi na bado simpati yaani yupo vizuri sana zaidi ya sana. Nilikuwa namchukulia poa ila ni noma aisee. Ana mwandiko mzuri balaa.

Nilijikaza kisabuni kisha nikaanza kuandika. Herufi za mwanzo kila mtu alinisifu, na darasa zima walinipigia makofi, Haida aliwaangalia, kisha hakusema neno, kisha walipomaliza kupiga makofi ndio akaniambia, “Kumbe unajua, Hongera.” Hata asante nilishindwa kusema maana aibu inanitembelea jirani, na huku kuna ka kitete fulani cha kuwa its official, nimeandika ubaoni kama mwalimu, kimenijaa kinamwagika. Na huku nimetoka kumkumbatia yeye mapajani, yaani, aah. Ila yote kwa yote, kitete cha kuandika ubaoni ndio kilikuwa na nguvu kuliko.

Niliendelea kuandika kidogo kwa ajili ya somo na kisha Haida akasema inatosha mpaka hapo. Kiu ya kuendelea kuandika ilikuwa imenijaa, ila Mwalimu alistuka, na kutuona tushamaliza kuandika.

Mwalimu alisema, “Darasa zima, mmemaliza kuandika?” darasa zima liliitikia, “Ndioooo” Mwalimu alisema tena, “ Haya wapigieni makofi” palepale tukapigiwa makofi na kila mtu darasani...kisha nikarudi kukaa. Riziki alinikumbatia ile kiutundu flani hivii kwa kunishuhudia kuwa nimeandika vizuri sana. Mi niliitikia tuu kwa furaha ila muda huo niligeuza macho yangu kumuangalia Haida, na kweli, niliuona uzuri wake. Niliona kana kwamba ni mwanamke mzuri sana kuliko wote duniani, yaani mwanamke ambaye ananielekeza kuandika vizuri namna hii na bado sina cha kumlipa. Mwanamke ambaye ananivutia kila kitu chake, maana uzuri wa mtu una maana gani kama haujui namna ya kuutumia?

Haya,

tuliendelea na masomo, na Haida akawa rafiki yangu mzuri na mkubwa sana, tulikutana mara nyingi na maeneo mbalimbali tukizungumza, kucheza na kuandika pamoja. Tuliandika sana, kila tulichokiona, tuliandika kwenye kalenda, kwenye manila, kwenye mbao, na hata majaladio ya watu. Nakumbuka tuliunda ka-timu flani hivii ambacho kalikuwa na nguvu balaa, combo, ambayo kila mtu shuleni aliipenda.

Kumbuka shule yetu ilikuwa ya pekee sana hivyo wanafunzi walioletwa kwetu walikuwa ni wa hali fulani hivii ya tofauti na mazingira ya tofauti, wapo waliokuwa na uwezo haswa, na wapo waliokuwa na uwezo wa kunjunga, nadhani hapa mnanielewa, na wapo wa kawaida na wengine wale akina mie, ambao hatukua wengi sana. Sasa, kwenye shule yetu ilikuwa na utamaduni wa usupastaa, yaani, kwa mfano mtu akiwa maarufu shuleni anapata huduma nyingi za ziada, ni sawa na kusema anakuwa mtawala flani hivii asiye rasmi, si unao naga watu maarufu wanakuwaga wanapata misereleko maeneo tofautitofauti, hawakai foleni an kadhalika? Basi na sie shuleni kwetu mambo yalikuwa hivyoivyo. Kulikuwa na ka-utamaduni ka watu kuwa couples hawa walikuwa wanakula bure canteen, hawakai foleni, hawachapwi na muda mwingi wanakaa pamoja. Hii hali ilianza tangu shule inaanzishwa, na ilikuwa haitiliwi sana maanani na uongozi wa shule ila mkuu wa shule wa pili alikuwa amechanganyikiwa nayo na kuikuza sana kiasi kwamba alitengeneza kaubao flani hivii ofisini mwake na kuziandika couples za kila mwaka. So, ilikuja kutokea kuwa na kaushindani flani hivii kwa kila mwaka lazima iwepo the best, na kila darasa ziwepo, ila iliyokuwa inapata Premium Service ni moja tuu, haijalishi ipo darasa lipi, kubwa au dogo..hii shule nzima ndio walikuwa wanaikubali.

Haya, urafiki ulianza, kati ya mwanafunzi wa darasa la pili na la tatu. Hiki sasa kilikuwa kitu cha kawaida lakini kipya shuleni. Kwa jinsi tulivyokuwa tunazurula pamoja baada ya madarasa, na kusubiriana, ndio
Haya, urafiki ulianza, kati ya mwanafunzi wa darasa la pili na la tatu. Hiki sasa kilikuwa kitu cha kawaida lakini kipya shuleni. Kwa jinsi tulivyokuwa tunazurula pamoja baada ya madarasa, na kusubiriana, ndio ilivyotufanya kuwa maarufu shule nzima. Maana ni rahisi kuonekana. Hilda mrefu, mimi mfupi. Hapo sasa, kila mtu alikuwa anatuangalia. Mimi binafsi nilikuwa sipo smart sana, ila Hilda alikuwa Super Smart yaani ana muonekano nadhifu mno. Kila tulipokuwa pamoja alikuwa ananikumbatia na kunigusa kwa ukaribu, na kwa vile wote tulikuwa watoto ilikuwa si rahisi kutuhisi kwa matamanio maana tulikuwa tunacheza muda mwingi na kuandika pamoja. Kuna siku tuliwahi kutumia trick ya kugombana na watoto fulani na tukawapiga kwa kuwachangia, walipoenda kushtaki kwa mwalimu, alipokuja kutukamata mwalimu alitukuta tumekaa wawili, mimi na Hilda tunaandika..mwalimu alipotuona akaghairi, na kuwashika wao watoto na kuwachapa tena, maana tulikuwa ni kama vi malaika vitoto hasa tukiwa tunaandika Mwandiko.


Kuna siku wakati nipo darasani kilikuja kikaratasi kimeandikwa Haida. Mimi nakumbuka nilikuwa darasa la nne. Nilikifungua na kukisoma, “Mambo? Leo usiondoke, naomba nisubirie twende wote nyumbani” nilikisoma kisha nikamuangalia alienipa kikaratasi. Alikuwa Riziki, yeye anachekacheka tuu, haelewi kitu. “kuna nini? Mbona kama unazubaa?” nikamjibu, “hamna kitu” Riziki akauliza huku anataka kuniputa mkononi “embu nione” aliniputa kikaratasi wakati anakikunjua ili asome nikampora kwa haraka sana pia kisha kwa spidi ya ajabu nikakidumbukiza mdomoni na kukitafuna! Riziki akakasirika, “ ah, nimesoma Mambo, leo usi..(akasita) usifanyeje? usije? Kakutataza usiende kumfuata? (Anaendelea kujiuliza, mi namshangas kimya ila sijibu kitu) Usinifuate? Kwani kakuf’kuza? Niambie basiii” sikumjibu kitu, nimebaki namshangaa tuu. Nilimshangaa kuwa amewezaje kubeba kikaratasi vile asikisome, mpaka pale na kunipa bila shida yoyote, alafu nilipomaliza kukisoma ndio ajawe na shauku nzito hivyo kiasi cha kunipora kikaratasi chenyewe.

Kwanza nimemsifu kwa kuwa mjumbe mzuri, Mesenja bora, amepewa ujumbe na umefika bila ya kuusoma. Kuhusu tabia yake ya kuuliza maswali lukuki akiwa na shauku nishamzoea na huwaga inanikeraga sana, ila sasa ndio rafiki, nitafanyaje, najikuta nishamzoea tena.

Nilijinyamazia kimya kisha nikawa nasubiri tuu muda ufike, sina wazo lolote na wala sitarajii chochote, ila sikuwa kama siku zingine. Siku zingine tulikuwa tunachukuana tuu na kwenda maeneo mbalimbali mazurimazuri, yenye maua au kimvuli kizuri na kukaa, kucheza au kuandika, na sikuwa na waza chochote ila siku hio nilikuwa najihisi tofauti hivii, hali fulani hivii isiyoelezeka.

Unajua hizi roho zinazungumza, eenh, hata kama ni kwa maandishi, roho huzungumza. Mtu anaweza sema neno moja tuu, nakupenda, na mtu akahamisha milima kisa anapendwa. Hope hapo unanielewa.

Haya. Muda ukafika, darasa langu la nne, Haida yupo darasa la Tano.nikaenda zangu hadi getini, nikamsubiri. Haida akafika, nikaongozana nae mpaka kwao. Sio mbali sana na kwetu, ila palikuwa na kamwendo.

Nyumbani wanamjua sana Haida, sijawahi lala kwao, ila hata nikisema kwetu kuwa nataka nikalale kwa akina Haida, hawapingi. Mi maisha yangu yote nimekua na mama. Baba na mama walizinguanaga kitambo kila mtu akawa na maisha yake. Wanaelewana vizuri tuu, ila ndio hivyo tena, ya wazee yanabaki kuwa ya wazee. Hivyo. Sasa mama yupo bize sana na mambo zake mobb, na hana muda na watoto, sisi tunajilea wenyewe. Ndio, tunakula, tunavaa, tunalala, ila masuala ya ukaguzi na kadhalika, ni juu yetu wenyewe. Dadaangu mkubwa yeye ndie incharge wa kila kitu. Sijui kesi za kupigana, kununua nguo na mahitaji, na kadhalika ni yeye. Nilikua na broo wangu mtata sana, yeye ngumi mkononi muda wote, dada yangu ndio msuluhishi wa familia na anampa kichapo cha maana kakaangu anayenifuatia mimi lakini hakomi, kwa hio jamii nzima ikawa inanijua kuwa mimi ni mpole sana na broo wangu alikuwa anapenda kunibeba mimi kwenye maugomvi yake hayo, ili aonekane kuwa hajaanzisha ugomvi..na kadhalika..lakini, anyway, umepata idea.

Sasa sifa ya mwandiko ilienea hadi tunapokaa maana shule yetu ni mojawapo ya shule maarufu katika mji huu, so ilikuwa rahisi sana kwa wanafunzi kupeana taarifa na kuwasiliana. Wapo waliokuwa wakali wa hesabu na masomo mengine lakini sisi tulikuwa tunasifika kuwa tuna akili sana na tunapenda mno kuandika. Na kiuhalisia masomo mengine tulikuwa tunafanya vizuri sana ila mwandiko ndio hautuambii kitu.

Haya, jioni ilipofika tulienda mpaka kwao. Baba yake Haida ni mwanajeshi, hivyo muda mwingi hayupo nyumbani, anasafiri sana kikazi. Kwao kwa akina Haida hakuna mama, wanaishi na mama wa kambo ambaye na yeye ni mdogo sana, so hawezi hata kujilea mwenyewe. Wapo wao tuu wawili na msichana wa kazi. So, kufika kwao maisha yao yapo vere vere veeree, yaani uzungulaizesheni flani hivii ambao unaweza usiuelewe fastafasta.

Nilipofika nilimkuta msichana wa kazi peke yake, akiwa aanaangalia tivii. Tushazoeaga kwenda kwa akina Haida kuandika jioni kuanzia saa 12 na nusu jioni mpaka saa 3 usiku nakuwa nishamaliza kila kitu naondoka zangu. Unakumbuka niilikuambia sio mbali sana? Ndio, sio mbali sana, ni kama vile mwendo wa dakika 15-20 mpaka nyumbani, ndio maana nilikuwa naruhusiwa kutembea usiku hasa kama ni muda wa kujisomea na kadhalika. Najua nilikuwa mdogo sana ila haya mazoea yalianzaga zamani, maana baba yangu mimi alikuwa na asili ya kufundisha watu kwao kijijini, hadi wanafunzi wa madarasa ya juu, na walikuwa wanamuita kisomo na alikuwa anatembea na begi hadi usiku.

Haya wakati yule mdada anaangalia tivii alipotuona tuu akampokea Haida begi, akanipokea na mimi kisha akatuandalia chakula. Ilikuwa saa kumi hivii jioni. Msichana wa kazi alishangaa kidogo kuniona ila hakuwaza sana maana aliona ni kawaida tuu. Mara nyingi naendaga kwao usiku, leo imekuwaje nimeenda jioni. Ila haikuwa inshu.

Tukala tukashiba, kisha Haida akaniambia nimsubiri anaenda chumbani. Mi nikabaki pale sebuleni. Nikasubiri weeh, mpaka nikaona jua linazama. Yule msichana wa kazi alikuwa amenogewa na Tivii, hakujali kingine.

Mimi baada ya kusubiri sana nilijiongeza, nikaanza kutoa madaftari yangu ya mwandiko nikidhani labda kutakuwa na cha kuandika, nilitoa na ya masomo mengine, kisha nikaanza kufanya mazoezi yote viporo yaliyokuwa yamebakia kwa siku hio, na kisha nikaliandaa daftari la mwandiko tayari kwa ajili ya matumizi, nikimsubiri Haida aje.

Nilisubiri, na kusubiri, na kusubiri. Tivii inawaka, msichana anendelea kuangalia, na Haida haji. Hadi nikaanza kuboreka, nilihisi kana kwamba amepata shida, au changamoto, au ana tatizo. Unakumbuka nilikuambia kuwa roho zinawasiliana? Sasa, sijui shauku ilinijia vipi, nikajikuta naendelea kutamani kwa bidii kujua yu katika hali gani. Hamu ikaongezeka, pressure ikawa inapanda taratibu, mpaka nikawa kama nimesikia sauti flani hivii yake akiwa anaugulia maumivu ambayo sikujua kama alikuwa anaumia au analia,

Nilimuangalia msichana wa kazi, yupo bize na Tivii, mchezo wa kwenye luninga umemnogea, hageuki kulia wala kushoto, hajasikia chochote, huku ile kiu ikawa inaongezeka kwa kasi, nikawa sijielewielewi tena. Nilinyanyuka alafu nikakaa tena, kisha nikanyanyuka mara ya pili, nikasikia kama vile Haida analitaja jina langu? Sina uhakika na chumba chake nakijua, naangalia kwenye dirisha la Mlango juu naona taa inawaka, ina mwanga hafifu mwekundu, ile hali ya kunizuia kubaki pale ikawa haipo tena!

Nilijikuta tuu nanyanyuka na kuanza kuelekea kule kwenye chumba cha Haida, begi nimeliacha mezani, nikafika hadi mlangoni, Sasa najiuliza nigonge au nisigonge? Wakati najishauri akili ikaniambia nisikilizie kwenye mlango, ile naushika tuu nakuta mlango upo wazi, unaniruhusu niingie hadi ndani, na jinsi ninavyousukuma, mlango haupigi hata kelele, unanipeleka tuu ndani.

Kuingia chumbani, namkuta Haida amelala kitandani, mikono yake miwili imejishika katikati huku amefumba macho. Nilishangaa sana, nikakosa neno la kusema. Huku mdomo nimeuacha wazi, nimeganda nisijue la kufanya..


*****************************************************************************************

ITAENDELEA
 
Nimeiandika sehemu ya kwanza yote, nimeshai update kwenye huohuo uzi..ipo sehemu ya kwanza complete
 
Back
Top Bottom