Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 1,968
- 955
MHE. TARIMBA ABBAS - MABORESHO MKABATA WA BANDARI YAZINGATIE MAONI YA WANANCHI
"Serikali ifanye utafiti ni kwanini Tandale mahali ambapo pana Shule tatu za msingi na bado wanashindwa kuweza kupata Shule ya Sekondari" - Mhe. Tarimba Abbas, Mbunge wa Jimbo la Kinondoni.
"Elimu ya dai risiti toa risiti haitusaidii tangu VAT ianzishwe mwaka 2010 mpaka leo tunaimba wimbo huo huo na watu hawatoi risiti" - Mhe. Tarimba Abbas, Mbunge wa Jimbo la Kinondoni.
"Kuboresha mkataba wa utekelezaji wa bandari lazima tuyazingatie maoni ya wananchi, siyo kila anayechangia anakuwa ni mpinzani wa serikali hapana, wapo watu wazalendo ambao wanachangia kwa manufaa ya nchi, tuchukue mawazo yao ya msingi yaingie kwenye huo mkataba wa utekelezaji tusione ni watu wanaopinga" - Mhe. Tarimba Abbas, Mbunge wa Jimbo la Kinondoni