Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944

MHE. TARIMBA ABBAS - MABORESHO MKABATA WA BANDARI YAZINGATIE MAONI YA WANANCHI

"Serikali ifanye utafiti ni kwanini Tandale mahali ambapo pana Shule tatu za msingi na bado wanashindwa kuweza kupata Shule ya Sekondari" - Mhe. Tarimba Abbas, Mbunge wa Jimbo la Kinondoni.

"Elimu ya dai risiti toa risiti haitusaidii tangu VAT ianzishwe mwaka 2010 mpaka leo tunaimba wimbo huo huo na watu hawatoi risiti" - Mhe. Tarimba Abbas, Mbunge wa Jimbo la Kinondoni.

"Kuboresha mkataba wa utekelezaji wa bandari lazima tuyazingatie maoni ya wananchi, siyo kila anayechangia anakuwa ni mpinzani wa serikali hapana, wapo watu wazalendo ambao wanachangia kwa manufaa ya nchi, tuchukue mawazo yao ya msingi yaingie kwenye huo mkataba wa utekelezaji tusione ni watu wanaopinga" - Mhe. Tarimba Abbas, Mbunge wa Jimbo la Kinondoni

FzPDqKkaEAE5O9O.jpg
 
Watu wenye akili ndogo ndo Wana kawaida ya kutukana watu walio tofautiana mawazo...
Utashangaa watakuja kukutukana kisa unasapoti Dpworld...
 
Sidhani kama kuna mtu anapinga uwekezaji, anayepinga atakuwa na matatizo ya akili. Shida ni kwamba huu mkataba hauna utofauti ni ile mikataba ya bandari ambayo ufalme wa China ulisainishwa kinguvu na ufalme wa Uingereza karne ya 19 baada ya Opium War kuisha (Treaty Ports/ Treaty of Nanking) ambapo Uingereza alijimegea Hong-Kong tokea mwaka 1842 na kuja kuirudisha mwaka 1996.

Nchi haiongozwi kama Saccos ya familia, kuna sheria, kanuni na taratibu ambavyo vinatakiwa kufuatwa. Sheria, kununi na taratibu visipofuatwa na watu wakaanza kuuliza maswali makasiriko yanatoka wapi ? Mbona kipindi cha Raisi Magufuli tulihoji mengi na kusema sana humu, ati iwe nongwa kwasababu Raisi Samia anakosolewa na watu fulani fulani hawapendi.

Yaani, mnataka kusema kwamba Dr Tulia, Dr Feleshi na Johari wao ndiyo wenye akili kupita watanzania wengine ambao wamesoma sheria na kufahamu madhara ambayo yako kwenye mkataba wa bandari ? Tena mambo mengine yako wazi kabisa ila watu wameshupaza shingo hawataki kujibu wanatishia watu. Kama mna nia njema na nchi kwanini muogope mijadala na kufanyia mambo gizani ?
 
Watu wenye akili ndogo ndo Wana kawaida ya kutukana watu walio tofautiana mawazo...
Utashangaa watakuja kukutukana kisa unasapoti Dpworld...
Halafu hawa watukanaji wengi wao ndio hua wapo mstari wa mbele kudai freedom of speech!
Fellas, what you're doing here is cherry-picking facts and spinning the topic off the course.......

Hivi ndugu zangu kwamba watanzania wote wakiwemo Prof Shivji, Prof Lipumba na Prof Tibaijuka wanachukia uwekezaji au wanamuonea wivu Raisi Samia ??? Mbona mambo yako wazi kabisa. Wameuliza maswali kuhusu vipengele vya mkataba ambayo serikali haijatoa majibu yanayoeleweka zaidi ya kutishia na kutuma watu wapige propaganda mitandaoni.

Sheria zipo wazi kabisa na zinatoa utaratibu ambao serikali iliuvunja kwenye huu mkataba. Sasa watu wanapohoji makasiriko yanatoka wapi ???

Fellas, what you're doing here is cherry-picking facts and spinning the topic off the course.......

Hivi ndugu zangu kwamba watanzania wote wakiwemo Prof Shivji, Prof Lipumba na Prof Tibaijuka wanachukia uwekezaji au wanamuonea wivu Raisi Samia ??? Mbona mambo yako wazi kabisa. Wameuliza maswali ambayo serikali haijatoa majibu yanayoeleweka zaidi ya kutishia na kutuma watu wapige propaganda mitandaoni. Sheria zipo wazi kabisa na zinatoa utaratibu ambao serikali iliuvunja kwenye huu mkataba. Sasa watu wanapohoji makasiriko yanatoka wapi ???

Kwani hatuwezi Ku agree to disagree??
Lazima kitu akiongea Shivji ndo kiwe msahafu wa Taifa??
Lazima tusiokubaliana na kina Shivji tunyamaze?tusiweze sema hatukubaliani??
 
Kwani hatuwezi Ku agree to disagree??
Lazima kitu akiongea Shivji ndo kiwe msahafu wa Taifa??
Lazima tusiokubaliana na kina Shivji tunyamaze?tusiweze sema hatukubaliani??
Ndugu The Boss!
Of all the things in the world I ascribe, prescribe, subscribe and describe are facts, nothing else.

Binafsi nakubaliana kabisa na usemi wako kwamba tunapopishana ni lazima tujifunze uungwana wa kukubali tofauti zetu. Wote hapa tunafahamu umuhimu wa uwekezaji wa nje hasa kupitia shirika kubwa kama DP World, ila ambacho hatukikubali ni vipengele vya ule mkataba. Wengi mmechanganya mambo kwamba wanaopinga vipengele vya mkataba basi wanampinga Raisi Samia, jambo ambalo siyo kweli. Mkataba umekaa vibaya mno na tunasema hivi kwasababu ya uzoefu wa kisheria. Kama tutajibiwa hoja basi zijibiwe kiutaalamu siyo vinginevyo.​
 
Hakuna anaye kataa uwekezaji, tunacho kataa Ni mkataba ulivyo sukwa.
Nivizuri MTU akaupitia kwanza ndio atoe maoni.
Nina uhakika wabunge wote including speaker hawakuusona.
 
Fellas, what you're doing here is cherry-picking facts and spinning the topic off the course.......

Hivi ndugu zangu kwamba watanzania wote wakiwemo Prof Shivji, Prof Lipumba na Prof Tibaijuka wanachukia uwekezaji au wanamuonea wivu Raisi Samia ??? Mbona mambo yako wazi kabisa. Wameuliza maswali kuhusu vipengele vya mkataba ambayo serikali haijatoa majibu yanayoeleweka zaidi ya kutishia na kutuma watu wapige propaganda mitandaoni.

Sheria zipo wazi kabisa na zinatoa utaratibu ambao serikali iliuvunja kwenye huu mkataba. Sasa watu wanapohoji makasiriko yanatoka wapi ???

Tumia akili unapoquote comment zangu na sio kukurupuka hovyo tu,nimeongelea wanaowachukia wenzao kisa wanatoa maoni ambayo hayawapendezi wao,halafu wewe unaniquote na ngonjera zingine kabisa! Nani amekataa watu wasihoji?

Uwe unasoma na kuelewa kwanza kabla ya kukurupuka na vingereza vyako vya google hapa.
 
Watu wenye akili ndogo ndo Wana kawaida ya kutukana watu walio tofautiana mawazo...
Utashangaa watakuja kukutukana kisa unasapoti Dpworld...
Kwani anayeipinga Dpw ni nani nitajie mmoja na sababu zake
 
Tumia akili unapoquote comment zangu na sio kukurupuka hovyo tu,nimeongelea wanaowachukia wenzao kisa wanatoa maoni ambayo hayawapendezi wao,halafu wewe unaniquote na ngonjera zingine kabisa! Nani amekataa watu wasihoji?

Uwe unasoma na kuelewa kwanza kabla ya kukurupuka na vingereza vyako vya google hapa.
Bwahahaha, dude are you ok ?

Wewe ustaadh bwana huwa na makasiriko ya ajabu ajabu tu. Hapo juu nimeuliza kitu gani kibaya ?
The Boss tumeelewana naye vizuri tu, ila wewe umefika hadi kusema viingereza vya google.
 
Punguza ujinga wewe,ni wapi nimepinga watu kutoa maoni yao? Au mradi tu na wewe ucomment ili usisahauliwe kua nawe umo humu JF?
 
Wewe mchungaji acha kujichekesha chekesha hovyo,tutaanza kukutilia mashaka.
Yaani mtu anayependa mipasho na kusutana anitilie mimi mashaka kwasababu nimemwambia ukweli. Wewe ni nani hadi usiambiwe ukweli ? Mazee, wewe ukitaka tukana uwezavyo, lakini ukweli nishakwambia. Achana na hizi pigo za kupenda kusutana na mipasho. Mtoto wa kiume ukishasema NDIYO au HAPANA inatosha, hayo mengine ya mara kiingereza cha google, mara mjinga ni AMETEURISH.
 
Back
Top Bottom