Mabadiliko ya katiba kutoa ukomo wa raisi kuongoza miaka kumi tuu na kumpa nafasi Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan kugombea tena 2030

Ndugu zangu watanzania katiba yetu imeweka ukomo wa muhula mmoja wa viongozi akiwamo rais na wabunge kuchaguliwa kila baada ya miaka mitano. Hii ni nzuri ila tatizo kubwa ni kwamba katiba imeweka ukomo wa raisi kuwa miaka 10 tuu kitu ambacho sio sahihi.

Ni muda muafaka kifungu hicho kifanyiwe marekebisho haraka ili raisi aweze kukaa madarakani zaidi ya miaka kumi na kuendelea. Miaka mitano au kumi ni michache sana kumpatia mama atuvushe. Kwaiyo mfano katiba mpya ikija iwe na option kama raisi akitaka kugombea agombee tena na sio miaka kumi ikiisha ndiyo basi.

Hii imekaa poa manake kuna katiba za vyama watu wanaruhusiwa kugombea nafasi hadi miaka 20 na kuendelea .

Pamoja tuungane na tujenge taifa letu

utakuwa umepagawa na huyo uliyemtaja si bure. Wakati tunatamani miaka iende haraka tupate mwingine wewe unataka kumuongezea muda? seriously??
 
Kifupi Uchaguzi ni kupoteza muda na pesa za nchi kirahisi rahisi.

Ila umejiandaaje litakapo ingia jiwe jingine?
Ili Nchi hii na Nchi hizi za Africa zinahitaji kuongozwa na watu Kama Jiwe ndio zinaweza kupata maendeleo ya kweli kweli !!

Wanatakiwa kama wale waliobatizwa majina na mabeberu kwamba ni madikiteta ndio watawale hizi Nchi ndipo bara hili litaondokana na huu umasikini wa kujitakia !!
Kwa kifupi wanatakiwa madikiteta waadilifu !! Mark my words !!
 
Amini amini nawaambieni mada hii siyo kwaajili ya shekeli wala vipande vya dhahabu na fedha bali kuzuia vurugu za wale wenye tamaa ya 2030
Baada ya uchaguzi tunafikiria uchaguzi mwingine !! Salaalleh !! 😅😅🙏🙏
 
Hili tuliliongea mkalikataa. Tuliwaambia mama anamalizia awamu ya 5 ya Magufuli kikatiba mkakataa mkasema hii ni awamu ya 6. Sasa awamu unayosema siyo ya Samia ni ipi? ya 5, au ya 6 kwa maana awamu ya ya Magu ilikuwa ya 5.
Nipeni faida ya kubadilisha badilisha maRais kila baada ya miaka kumi katika hizi Nchi zinazoitwa masikini !!

Hizi demokrasia za miaka kumi kumi au minne minne hizi zinawafaa Wazungu ambao Nchi zao zilishatengeneza taasisi imara kabisa ambazo hazitetereki wala kutetereshwa na kitu chochote kile katika Nchi ndizo zilizo shika hatamu ya kuiongoza Nchi wapi ielekee !!
Na ndio maana leo unaona hata Trump yupo Mahakamani kujibu mashitaka !!
Hii miaka kumi kumi ni kazi bure tu kwetu Africa ! Tunatakiwa kwanza tutengeneze Taasisi zetu imara kabisa kabisa kama za wazungu ndipo tunaweza tukaweka hata ukomo wa Rais kutawala ukawa ni miaka minne tu !! 😅😅🙏🙏 Tafakari !!
 
Back
Top Bottom