Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,499
- 113,610
Wanabodi,
Kama kawaida yangu kila nipatapo fursa huja na makala zangu za kwa Maslahi ya Taifa. Makala ya leo ni pongezi kwa Jaji Stella Mugasha wa Mahakama ya Rufani Tanzania, kusimama kidete, kupinga uvunjifu wa katiba uliofanywa na Rais wa JMT, kumuongezea muda wa kuhudumu katika nafasi ya Jaji Mkuu, baada ya kutimiza umri wa miaka 65 kama ilivyoripotiwa humu Profesa Ibrahim Juma kuendelea kuwa Jaji Mkuu, Rais Samia anavunja Katiba ya JMT?
Naomba ku declare Interest
Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Juma ni Mwalimu wangu wa sheria nilipokuwa Mwanafunzi wa LL.B UDSM.
Nilipomaliza mwaka wa 4, Dr. Ibrahim Juma (as then was), ndio alikuwa Dean wangu pale Fol.
Na nilipopata uwakili, ni Prof. Ibrahim Juma aliyeniapisha kuwa Wakili kipindi hiki cha Ujaji Mkuu wake, hivyo nikitetea uvunjifu huu wa katiba wa Rais Samia kumuongezea muda Jaji Mkuu kinyume cha katiba, simtetei Dr. Juma kwasababu ni Mwalimu wangu, wala simtetei kwa sababu ni Dean wangu, au kwasababu alinipa uwakili, namtetea Dr. Ibrahim Juma kuongezewa muda kidogo kwa katiba kuvunjwa kidogo tuu for logical reasoning, kama katiba yetu imeisha vunjwa sana mara kibao kwa mambo makubwa ya msingi na yenye madhara makubwa kwa taifa na tulikaa kimya!, why isivunjwe kwa hili dogo ambalo halina madhara yoyote?.
Rais Samia vunja tuu katiba kwa haya madogo madogo, hata watangulizi wako wote walivunja!, tena wengine wetu akina sisi pia tulikuwa washauri wa bure kumshauri rais wetu avunje katiba Kama sio udikteta, Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria, ongoza kwa 'presidential decrees'! hivyo hili, mwacheni Mama avunje katiba as long as anavunja kwa nia njema na dhamira safi!, na uvunjwaji wenyewe, hauna madhara!.
Nimependekeza Jaji Mugasha apewe maua yake kwa sababu hii ndio mara ya kwanza katika historia ya Mahakama Tanzania, mtu mwenye cheo cha juu kiasi hicho, cheo cha Jaji Rufani kupinga hadharani tena kwa waraka wenye vifungu, kupinga kitendo cha Rais wa JMT kumuongezea muda Jaji Mkuu baada ya kutimiza umri wa miaka 65 ni uvunjifu wa katiba ya JMT ya mwaka 1977 kuhusu ukomo wa Jaji Mkuu kuhudumu.
Hii ndio mara ya kwanza katika historia ya Tanzania, ofisa yoyote wa serikali kupinga uvunjifu wa katiba unaofanywa na Rais wa JMT.
Hili ni jambo zuri na la afya sana, katiba ndio sheria Mama, hakuna aliye juu ya katiba, hata rais wa JMT hayuko juu ya katiba, katiba ni lazima iheshimiwe na wote, hivyo kitendo hiki cha Jaji Stella Mugasha, ni kitendo cha kishujaa sana na ni cha kishujaa zaidi kufanywa na Jaji Mwanamke, hivyo kuthibitisha sometimes wanawake ni mashujaa kuliko wanaume!, hivyo Jaji Mugasha apewe maua yake na jina lake liandikwe kwa herufi za dhahabu katika list ya mashujaa wa nchi hii.
Pamoja na ushujaa wote huu kwangu mimi, hili la Rais wa JMT kuvunja katiba kwa nia Njema ili taifa lisiwe na ombwe la uongozi wa Mahakama wakati mchakato wa kumpata Jaji Mkuu mpya ukiendelea mimi naliona kama ni dogo tuu, yaani nakubali na kuridhia kabisa katiba ivunjwe tuu katika yale madogo madogo yasiyo na madhara!.
Jana nimemsikia Wakili senior Alex Mgongolwa Clouds TV akimtetea Rais Samia kuvunja katiba kwa kumuongezea muda Jaji Mkuu, Wakili Mgongolwa hoja yake ni Kifungu cha ambacho Rais ana mamlaka ya kumuongezea muda Jaji Rufani baada ya kutimiza umri wa miaka 65, Wakili Mgongolwa, aliteleza kifungu cha kinachomzua CJ, CAG, CDF, DIS, na wakubwa wengine kuteuliwa nafasi za kiutendaji baada ya kufikisha umri wa kustaafu Wakili Mgongolwa: Katiba inamruhusu Rais kumuongezea muda Jaji Mkuu
Sababu yangu ni moja tuu, using logical reasoning, jee kuna ubaya gani kumuongezea muda kidogo tuu Jaji Mkuu aliyepo, ambaye ametimiza umri wa miaka 65 kwa ghafla tuu kabla mchakato wa kumpata Jaji Mkuu mwingine?.
Hii maana yake kuna udhaifu kwenye utendaji wa Mahakama, kwasababu kwa mujibu wa Standing Orders za serikali, mtendaji yoyote wa serikali anapobakiza miaka miwili kabla ya tarehe yake ya kustaafu, anakumbushwa kwa barua ili aanze kujipanga. Anapobakiza 6 months anatumiwa reminder, na anapobakiza mwezi mmoja, anapewa likizo ya lazima ya kustaafu wakati akiandaliwa mafao yake, akitoka likizo ni kuaga tuu na kuagwa!. Inaonekana hili halikufanyika kiasi kwamba inaonekana it's as if Jaji Mkuu ametimiza miaka 65 ghafla!. Turuhusu Uvunjifu huu wa katiba kwa nia Njema ila pia watu wawajibike!.
Swali kwa Jaji Stella Mugasha na wana tasnia nzima ya sheria, walikuwa wapi siku zote Rais wa JMT alipokuwa anavunja katiba ya JMT kwenye mambo makubwa ya msingi?!. Mfano mzuri ni Rais wa JMT alipozuia mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa!, hili ni jambo kubwa na la msingi sana, lenye madhara makubwa!, majaji watetezi wa katiba ya JMT, walikuwa wapi?!, mbona walikaa kimya?.
Kwenye hili, angalau mimi nililulizia, japo sikumbuki nilijibiwa nini, lakini watetezi wa katiba wa aina hii walikuwa wapi?, mbona walinyamaza kimya?.
Juzi kati hapa nimeipongeza TLS kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa katiba hili la Bandari Kwa la Bandari, Pongezi TLS. Katiba yetu imenajisiwa. Bunge limetunga Sheria batili. Haki za Watanzania zimeporwa. Kwanini TLS wamenyamaza kimya? lakini nao pia niliwauliza maswali haya haya ninayouliza leo.
Sheria Kuu kuliko zote nchini kwetu ni katiba, katiba ndio sheria Mama, sheria nyingine yoyote inayokwenda kinyume cha katiba ni sheria batili!. Kinachoibatilisha hiyo sheria yoyote kinyume cha katiba, ni katiba yenyewe!.
Nimalizie kwa pongezi tena, kwa Jaji Stella Mugasha kwa hili la utetezi wa katiba ya ila kuna makubwa kuliko hili la kumuongezea muda Jaji Mkuu.
Natoa wito kwa Rais wetu Mama Samia, kwa vile wewe ni Mwanamke na ni mtetezi Mkuu wa wanawake, na kwa vile Jaji Mkuu Prof. Ibrahim Juma amefikisha muda wa ukomo wa kuwa Jaji Mkuu, na kwa vile Jaji Stella Mugasha ana sifa zote za kuwa Jaji Mkuu, ila amebakiza miaka 3 kutimiza umri wa miaka 65, hivyo hawezi kuteuliwa kuwa Jaji Mkuu , lakini anaweza kuteuliwa kuwa Kaimu Jaji Mkuu, wakati mchakato wa kumpata Jaji Mkuu mpya ukiendelea na tena Samia endelea kuandika historia mpya ya Tanzania kwa kututeulia Jaji Mkuu wa kwanza Mwanamke!.
Mungu Mbariki Jaji Stella Mugasha
Mungu Mbariki Rais Samia atuteulie Jaji Mkuu Mwanamke!
Mungu Ibariki Tanzania
Paskali
Rejea
1. Sheria ya Uchaguzi Ni Bad Law! Kuendelea Kuitumia ni Ujinga? Kuwabebesha Masikini Gharama za Uchaguzi ni Dhambi!
2. Shurti la kudhaminiwa na chama kugombea uchaguzi, ni shurti batili kwa mujibu wa Katiba, linatutia hasara, tulifute!.
3. Mgombea Kudhaminiwa na Chama ni Ubatili Uliochomekwa Kiubatili na Bunge Letu Ndani ya Katiba Yetu!. Tuache Ubatili Huu Uendelee Ndani ya Katiba Yetu?
4. Madudu haya ya ajabu ya kisheria yaliweza kufanyika vipi wakati tuna Wanasheria?

- Serikali yetu ime draft sheria batili, inayokwenda kinyume cha katiba, ikaipeleka Bungeni kutungwa kuwa sheria!, Majaji na wanasheria watetezi wa katiba kama hawa walikuwa wapi?, mbona walikaa kimya?!.
- Bunge letu likaitunga hiyo sheria batili inayokwenda kinyume cha katiba, Majaji na wanasheria watetezi wa katiba kama hawa walikuwa wapi?, mbona walikaa kimya?!.
- Rais wa JMT akaisaini hiyo sheria batili kuwa ni sheria!, Majaji na wanasheria watetezi wa katiba kama hawa walikuwa wapi?, mbona walikaa kimya?!.
- Mahakama Kuu kupitia kesi ya Mchungaji Mtikila, (RIP), ikatamka sheria hiyo ni batili na kuitaka serikali iifute, Majaji na wanasheria watetezi wa katiba kama hawa walikuwa wapi?, mbona walikaa kimya?!.
- Ubatili wa sheria batili yoyote unabatilishwa na katiba, Mahakama Kuu ikiisha tamka sheria fulani ni batili kwa kwenda kinyume cha katiba, automatically sheria batili hiyo inakuwa imebatilika from there and then. Kazi ya serikali ni procedures tuu za kuifuta!. Kwanini Majaji na wanasheria watetezi wa katiba kama hawa walikaa kimya?!.
- Serikali yetu ikakata rufaa kupinga uamuzi huo wa Mahakama Kuu, ikashidwa!, kwanini Majaji na wanasheria watetezi wa katiba kama hawa walikaa kimya?!.
- Serikali yetu baada ya kubwagwa, ikafanya kubwa kuliko, ikapeleka Bungeni mabadiliko ya katiba kwa hati ya dharura, batili ile ikachomekewa kiubatili ndani ya katiba yetu!. Kwanini Majaji na wanasheria watetezi wa katiba kama hawa walikuwa wapi?, mbona walikaa kimya?!.
- Bunge letu likafanya mabadiliko ya batili ya katiba na kuichomeka kiubatili, hiyo batili ndani ya katiba yetu!. Hivyo katiba yetu imenajisiwa kwa kuchomekewa ubatili!, kwanini Majaji na wanasheria watetezi wa katiba kama hawa walikuwa wapi?, mbona walikaa kimya?!.
- Mchungaji Mtikila hakukubali katiba yetu inajisiwe, akafungua shauri jingine kupinga mabadiliko hayo ya katiba, Mahakama Kuu ikampa ushindi na kutangaza mabadiliko hayo ni batili!, kwanini Majaji na wanasheria watetezi wa katiba kama hawa walikuwa wapi?, mbona walikaa kimya?!.
- Serikali yetu ikakata rufaa Mahakama ya Rufani kupinga uamuzi huo wa Mahakama Kuu, serikali ikashinda, kwanini Majaji na wanasheria watetezi wa katiba kama hawa walikuwa wapi?, mbona walikaa kimya?!.