Maoni yangu juu mabadiliko ya katiba kwenye ukomo wa Urais

Salahan

JF-Expert Member
Sep 10, 2014
2,942
3,608
Habari wanajamii

Kwa mujibu wa katiba yetu inayotumika hadi sasa ukomo wa kugombea nafasi ya urais ni miaka 10 kwa kila kiongozi ikiwa ni awamu mbili yaani uchaguzi wa raisi kila baada ya miaka mitano.
Asili hii ya ukomo wa raisi imeasisiwa toka taifa la Marekani

"....Utaratibu wa kuweka ukomo wa viongozi kubaki madarakani una asili yake nchini Marekani. Nchi hiyo ambayo ndiyo kinara wa mfumo wa dunia baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia, ilifanya hivyo mwaka 1951......Walioweka vifungu hivyo kwenye Katiba ya Marekani walijiridhisha kwamba jambo ambalo kiongozi atashindwa kulifanya ndani ya miaka minane madarakani, hawezi kulifanya hata akiongozewa muda kiasi gani.....Inajulikana kwamba pamoja na kuweka mifumo hiyo, zimekuwapo sauti za kutaka kubadili utaratibu huu wa ukomo ndani ya Marekani na China pia. Mwaka 1987, kulikuwapo na kikundi cha Wamarekani waliotaka Katiba ibadilishwe ili aliyekuwa Rais wakati huo, Ronald Reagan, aendelee kubaki madarakani......BBC SWAHILI"

Maoni yangu yanaungana na wale wanaotaka kuondoa ukomo huo na kuweka utaratibu huu
1.KUWEPO NA KURA YA MAONI KILA BAADA YA MIAKA 5 YAKUAMUA AENDELEE AU ASIENDELEE

2.UKOMO WA KIONGOZI HUSIKA NI PALE TU KURA ZA MAONI ZA ASIENDELEE ZITAKAPOKUWA NYINGI KULIKO KURA ZA AENDELEE (WENGI WAPE) AMA KIFO.

3.TUME YAKUSIMAMIA KURA IWE TUME HURU ISIYO NA MUINGILIANO NA IKILU (SERIKALI ILIYOPO MADARAKANI)

Faida za kuondoa Ukomo
1.Kutekeleza miradi aliyoianzisha....Tunafahamu kwamba miradi mingi ya serikali ni miradi ya muda mrefu miaka 5-10-20 nk hivyo inahitaji ufuatiliaji na usimamiaji.Kitendo cha kuingia uongozi mwingine mambo huenda kombo ama kuzorota.Hii nipale kiongozi husika anapoliona jambo alilolianzisha mwenzake halitakuwa na manufaa nae kisiasa bali sifa huenda kwa mwasisi wake.Ama kugundua kwamba mradi huo haukuwa rafiki kwa maslahi ya nchi (hauungi mkono) hasa ikiwa mradi huo ameugundua umepitishwa kwa mikataba ya hovyo.Kila kiongozi akija na jambo lake nchi itakuwa na mipango mingi isiyotekelezeka au kubaki nusunusu.

2.Kuna viongozi hawakustahili kutoka madarakani.Kila raia anafahamu ni kiongozi gani alifaa aendelee na madaraka ila katiba ndio ilimuondoa.Kuna viongozi tunaimani nao hivyo kuendelea kushika usukani tunaamini tungefikishwa mahala pazuri.Huenda kwa maoni yako kiongozi wa namna hiyo hajatokea nchini sasa vipi akitokea je nisawa katiba ituondolee mpendwa wetu.

3.Uzoefu Na Ufahamu.Kiongozi aliyeanzisha jambo niwazi atakuwa na ufahamu nalo kwa kipindi chote awapo madarakani na atajua lipi aliwahishe na lipi alichelewe.Yani wewe kama kiongozi tayari unaramani yako njema ya mwenendo wa nchi wakati upo katika utekelezaji unaambiwa muda wako umeisha huwezi kuendelea nalo kwa mujibu wa katiba...Anakuja kiongozi mpya na ramani yake na uzoefu mpya lazima mambo yawe sivyo nawe mstaafu utayashuhudia yaendavyo.Embu fikiria mradi mmoja usimamiwe na watu watatu tofauti kila mmoja ako na maono yake au kupinga kabisa.

4.Uwajibikaji. Ukishajijua kwamba jambo ulilolianzisha ndio utaishi nalo kipindi chote ama mkataba ulioingia utaishi nao kipindi chote basi haotokubali kuharibu nafasi yako.Nasema hivi nikihisi kwamba huenda kuna viongozi wanaingia mikataba ya hovyo ambayo athari zake zinakuja kuonekana awamu nne mbele.Mfano mzuri ni kama tunavyosema kutunza rasilimali kwaajili ya kizazi kijacho,hii inafahamika kwamba tunaouwezo wa kuvuna misitu na sisi wazama hizi tukanufaika nakusaza lakini baada ya miongo kadhaa watoto wetu wakaishi katika jangwa lililotokana na sisi.Hivyohivyo kiongozi anafaa afanya jambo akiwa pia na hofu ya kuwajibika kwako sio jipu likamtumbukie aliyemfuata.

5. Miaka 10 ni michache.Ukizungumzia nchi bila shaka ni jambo kubwa sana ambalo hata mipango yake huwa niya milenia na karne ama mingo kadhaa.Sasa vipi uwambiwe unapewa miaka 10 tena ni 5 kama hukupita uchaguzi na unaambiwa ndani ya iyo miaka 5 ufanye nchi mapinduzi ya viwanda toka kwenye kilimo.Unapata picha gani zaidi tu ya kuanzisha mambo ambayo hadi unastaafu hayajatimia.Embu fikiria umeingia madarakani unakutana na agenda za miaka 60 nyuma zipatazo 100 nawe unaingia ukiwa na ajenda zako 50 ambazo pia kwa muda uliopo utakazozikamilisha kwa 100% huenda ni 5 tu.

Zingatio; Maoni hapo juu yamezingatia ajenda za kiongozi ila tunafahamu na kusikia kwamba kila kiongozi huenda kutekeleza agenda za chama chake kwamba haji na agenda zake bali zilezile alipoishia mwezake katika utekelezaji.Kama hivyo ndivyo basi ni nafuu kidogo ijapo tunafahamu kila kiongozi ako na maono ya utofauti juu ya utekelezaji huo.Na ikiwa chama ndio kinahusika na usimamiaji wa agenda izo basi kuna haja ya raia kuchagua chama kingine kitakachokuwa agenda chanya na kupendekeza mgombea mwenye maono chanya zaidi ila suala la muda wa uongozi litabaki palepale kuwaongezea muda kuweza kutekeleza majukumu yako.

Hitimisho. Haya ni maoni binafsi yasiyo na mashiko na chama chochote wala utawala wowote zaidi nimesisitiza kuongezewa muda viongozi wa kutekeleza majukumu yao (kutawala) ili kiongozi aonje tamu ya alichokianzisha na chungu ya baya alilolianzisha.Naamini hadi sasa Mheshimiwa Mwinyi angejua RUKSA inaendeleaje wapi aboreshe wapi aondoe kusudu ile RUKSA iliyo kichwani mwake ikae vyema kama alivyoitaraji.Nae hayati Mkapa angejua wapi UBINAFSISHAJI upofikia na vipi ausimamie hadi alipofikwa na umauti.Nae Mheshimiwa Kikwete angefahamu hadi sasa sera yake ya MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA hadi sasa angefikia wapi vipi aboreshe vipi abadili.Nae Hayati Magufuli angefahamu vipi TANZANIA YA VIWANDA YAKUJITEGEMEA wapi imefikia kwenye ramani yake na angefanya nini kuhakikisha kile alichokiamini kinakuwa kwa kadiri umri ungeongezeka.Naamini sera za viongozi hawa zimekwamishwa na ukomo kikatiba na kama watakiri kwamba zimetekelezeka kama walivyozipanga ndani ya muda wao wa miaka 10 basi hatuna haja ya kuulizana mana kila mtu ako na macho anaona nchi ilipofikia hivyo huenda zipo yes na no.Tunaomba raia ndio waamue uko wa uraisi sio katiba.
 
Ulishaona uchaguzi ulio huru na haki tanzania..??
Maoni yako hayana maana yoyote
Raisi ni taasisi yenye nguvu sana kwa katiba yetu hii inaweza kugeuza hata usiku kua mchana
 
Hizi ndizo mada za watu walioshiba, au kuvimbiwa. Ungekuwa na njaa, au unapitia msoto wa aina yoyote ile kutokana na aina ya watawala wabovu tulionao, kamwe usingekuja na mada ya aina hii.
 
Ulishaona uchaguzi ulio huru na haki tanzania..??
Maoni yako hayana maana yoyote
Raisi ni taasisi yenye nguvu sana kwa katiba yetu hii inaweza kugeuza hata usiku kua mchana
kwaiyo unaamini miaka mitano inatosha mapinduzi yakiuchumi
 
nimependekeza kuwepo kwa kura ya aendelee ama asiendelee mkuu
 
yawezekana ila hata wewe waweza sema vipi miaka mitano inatosha kufanya mapinduzi yakiuchumi
Kwani urais ni mtu au ni taasis tukifika huko itakuwa tumerudi kwenye uchifu, urais ni mfumo ambao mapinduzi huanywa kwa kupokezana. Hata hivyo hakina mapinduzi katika nchi ambayo yatamtegemea Rais na siyo RAIA.
 
Miaka 10 ni michache Kwa raisi Magufuli ila hao wengine hata 5 ilikuwa inawatosha
 
Kwani urais ni mtu au ni taasis tukifika huko itakuwa tumerudi kwenye uchifu, urais ni mfumo ambao mapinduzi huanywa kwa kupokezana. Hata hivyo hakina mapinduzi katika nchi ambayo yatamtegemea Rais na siyo RAIA.
ok shukran
 
Habari wanajamii

Kwa mujibu wa katiba yetu inayotumika hadi sasa ukomo wa kugombea nafasi ya urais ni miaka 10 kwa kila kiongozi ikiwa ni awamu mbili yaani uchaguzi wa raisi kila baada ya miaka mitano.
Asili hii ya ukomo wa raisi imeasisiwa toka taifa la Marekani

"....Utaratibu wa kuweka ukomo wa viongozi kubaki madarakani una asili yake nchini Marekani. Nchi hiyo ambayo ndiyo kinara wa mfumo wa dunia baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia, ilifanya hivyo mwaka 1951......Walioweka vifungu hivyo kwenye Katiba ya Marekani walijiridhisha kwamba jambo ambalo kiongozi atashindwa kulifanya ndani ya miaka minane madarakani, hawezi kulifanya hata akiongozewa muda kiasi gani.....Inajulikana kwamba pamoja na kuweka mifumo hiyo, zimekuwapo sauti za kutaka kubadili utaratibu huu wa ukomo ndani ya Marekani na China pia. Mwaka 1987, kulikuwapo na kikundi cha Wamarekani waliotaka Katiba ibadilishwe ili aliyekuwa Rais wakati huo, Ronald Reagan, aendelee kubaki madarakani......BBC SWAHILI"

Maoni yangu yanaungana na wale wanaotaka kuondoa ukomo huo na kuweka utaratibu huu
1.KUWEPO NA KURA YA MAONI KILA BAADA YA MIAKA 5 YAKUAMUA AENDELEE AU ASIENDELEE

2.UKOMO WA KIONGOZI HUSIKA NI PALE TU KURA ZA MAONI ZA ASIENDELEE ZITAKAPOKUWA NYINGI KULIKO KURA ZA AENDELEE (WENGI WAPE) AMA KIFO.

3.TUME YAKUSIMAMIA KURA IWE TUME HURU ISIYO NA MUINGILIANO NA IKILU (SERIKALI ILIYOPO MADARAKANI)

Faida za kuondoa Ukomo
1.Kutekeleza miradi aliyoianzisha....Tunafahamu kwamba miradi mingi ya serikali ni miradi ya muda mrefu miaka 5-10-20 nk hivyo inahitaji ufuatiliaji na usimamiaji.Kitendo cha kuingia uongozi mwingine mambo huenda kombo ama kuzorota.Hii nipale kiongozi husika anapoliona jambo alilolianzisha mwenzake halitakuwa na manufaa nae kisiasa bali sifa huenda kwa mwasisi wake.Ama kugundua kwamba mradi huo haukuwa rafiki kwa maslahi ya nchi (hauungi mkono) hasa ikiwa mradi huo ameugundua umepitishwa kwa mikataba ya hovyo.Kila kiongozi akija na jambo lake nchi itakuwa na mipango mingi isiyotekelezeka au kubaki nusunusu.

2.Kuna viongozi hawakustahili kutoka madarakani.Kila raia anafahamu ni kiongozi gani alifaa aendelee na madaraka ila katiba ndio ilimuondoa.Kuna viongozi tunaimani nao hivyo kuendelea kushika usukani tunaamini tungefikishwa mahala pazuri.Huenda kwa maoni yako kiongozi wa namna hiyo hajatokea nchini sasa vipi akitokea je nisawa katiba ituondolee mpendwa wetu.

3.Uzoefu Na Ufahamu.Kiongozi aliyeanzisha jambo niwazi atakuwa na ufahamu nalo kwa kipindi chote awapo madarakani na atajua lipi aliwahishe na lipi alichelewe.Yani wewe kama kiongozi tayari unaramani yako njema ya mwenendo wa nchi wakati upo katika utekelezaji unaambiwa muda wako umeisha huwezi kuendelea nalo kwa mujibu wa katiba...Anakuja kiongozi mpya na ramani yake na uzoefu mpya lazima mambo yawe sivyo nawe mstaafu utayashuhudia yaendavyo.Embu fikiria mradi mmoja usimamiwe na watu watatu tofauti kila mmoja ako na maono yake au kupinga kabisa.

4.Uwajibikaji. Ukishajijua kwamba jambo ulilolianzisha ndio utaishi nalo kipindi chote ama mkataba ulioingia utaishi nao kipindi chote basi haotokubali kuharibu nafasi yako.Nasema hivi nikihisi kwamba huenda kuna viongozi wanaingia mikataba ya hovyo ambayo athari zake zinakuja kuonekana awamu nne mbele.Mfano mzuri ni kama tunavyosema kutunza rasilimali kwaajili ya kizazi kijacho,hii inafahamika kwamba tunaouwezo wa kuvuna misitu na sisi wazama hizi tukanufaika nakusaza lakini baada ya miongo kadhaa watoto wetu wakaishi katika jangwa lililotokana na sisi.Hivyohivyo kiongozi anafaa afanya jambo akiwa pia na hofu ya kuwajibika kwako sio jipu likamtumbukie aliyemfuata.

5. Miaka 10 ni michache.Ukizungumzia nchi bila shaka ni jambo kubwa sana ambalo hata mipango yake huwa niya milenia na karne ama mingo kadhaa.Sasa vipi uwambiwe unapewa miaka 10 tena ni 5 kama hukupita uchaguzi na unaambiwa ndani ya iyo miaka 5 ufanye nchi mapinduzi ya viwanda toka kwenye kilimo.Unapata picha gani zaidi tu ya kuanzisha mambo ambayo hadi unastaafu hayajatimia.Embu fikiria umeingia madarakani unakutana na agenda za miaka 60 nyuma zipatazo 100 nawe unaingia ukiwa na ajenda zako 50 ambazo pia kwa muda uliopo utakazozikamilisha kwa 100% huenda ni 5 tu.

Zingatio; Maoni hapo juu yamezingatia ajenda za kiongozi ila tunafahamu na kusikia kwamba kila kiongozi huenda kutekeleza agenda za chama chake kwamba haji na agenda zake bali zilezile alipoishia mwezake katika utekelezaji.Kama hivyo ndivyo basi ni nafuu kidogo ijapo tunafahamu kila kiongozi ako na maono ya utofauti juu ya utekelezaji huo.Na ikiwa chama ndio kinahusika na usimamiaji wa agenda izo basi kuna haja ya raia kuchagua chama kingine kitakachokuwa agenda chanya na kupendekeza mgombea mwenye maono chanya zaidi ila suala la muda wa uongozi litabaki palepale kuwaongezea muda kuweza kutekeleza majukumu yako.

Hitimisho. Haya ni maoni binafsi yasiyo na mashiko na chama chochote wala utawala wowote zaidi nimesisitiza kuongezewa muda viongozi wa kutekeleza majukumu yao (kutawala) ili kiongozi aonje tamu ya alichokianzisha na chungu ya baya alilolianzisha.Naamini hadi sasa Mheshimiwa Mwinyi angejua RUKSA inaendeleaje wapi aboreshe wapi aondoe kusudu ile RUKSA iliyo kichwani mwake ikae vyema kama alivyoitaraji.Nae hayati Mkapa angejua wapi UBINAFSISHAJI upofikia na vipi ausimamie hadi alipofikwa na umauti.Nae Mheshimiwa Kikwete angefahamu hadi sasa sera yake ya MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA hadi sasa angefikia wapi vipi aboreshe vipi abadili.Nae Hayati Magufuli angefahamu vipi TANZANIA YA VIWANDA YAKUJITEGEMEA wapi imefikia kwenye ramani yake na angefanya nini kuhakikisha kile alichokiamini kinakuwa kwa kadiri umri ungeongezeka.Naamini sera za viongozi hawa zimekwamishwa na ukomo kikatiba na kama watakiri kwamba zimetekelezeka kama walivyozipanga ndani ya muda wao wa miaka 10 basi hatuna haja ya kuulizana mana kila mtu ako na macho anaona nchi ilipofikia hivyo huenda zipo yes na no.Tunaomba raia ndio waamue uko wa uraisi sio katiba.
Ushauri wangu kwa vijana na watu wengine, unapoandika kitu kwenye mtandao wa kijamii jitahidi utulize akili ili uandike kitu chenye kuleta maana. Huyu ndugu yetu mleta maada leo haoni upupu aliouandika hapa lkn miaka 10 ijayo ataukataa huu upupu kuwa hakuandika yeye.
 
Ushauri wangu kwa vijana na watu wengine, unapoandika kitu kwenye mtandao wa kijamii jitahidi utulize akili ili uandike kitu chenye kuleta maana. Huyu ndugu yetu mleta maada leo haoni upupu aliouandika hapa lkn miaka 10 ijayo ataukataa huu upupu kuwa hakuandika walioweka miaka 10 ni maoni yao hata wewe unaweza kuwa na maoni yako
 
Ok labda nami nikuulize, miaka 10 aliyopewa na wananchi unasema haitoshi na aongezewe. Je kwa Mungu nako ataenda kunegotiate muda wa kuishi duniani?
 
Kwa viongozi wa kiafrika hata wakipewa miaka 100 bila uchaguzi hakuna kitu cha maana watafanya, tumeyaona hayo kwa viongozi ambao hadi Leo hii Wana zaidi ya miaka 30 wako madarakani lakini nchi zao zinazidi kwenda shimoni
kwa mfano tuu huyu bibi yako ulie kuja kumpigia "chapuo* akae pale miaka 15 tuu unadhani kwenye hii nchi kuna rasilimali zitasalimika,
Kwa waafrika hata miaka 10 ni mingi, wanachofanya kwa muda wote wanao kaa madarakani ni kuiba tuu hakuna chochote cha maana wanafanya
 
basi ndio maana nikapendekeza kura ya maoni ya aendelee ama laa
 
Wananchi wataamua miaka ya mtu kuishi duniani?
hapana ni kura kuendelea na uongozi au kuitishwa uchaguzi mwingine bada ya miaka mitano...nilichoshauri kuondolewa ni ukomo wa miaka 10 na kuwepo kwa kura ya maoni kila miaka 5 ya kuendelea ama asiendelee kuongoza
 
Back
Top Bottom