Maandamano ya wanahabari Sept 11, 2012

Maandamano ya wanahabari Sept 11, 2012

[h=2]WAZIRI NCHIMBI ATIMULIWA NA WAANDISHI WA HABARI[/h]
via starikaMkali blog -- WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Emmanuel Nchimbi, amekumbana na fadhaa ambayo haikutarajia wakati alipotimuliwa katika maandamano ya waandishi wa habari ya kupinga mauaji ya mwandishi mwenzao wa kituo cha televisheni cha Channel Ten, David Mwangosi, wakati alipozuka bila mwaliko.

Huku wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe tofauti, waandishi waliandamana kuanzia kwenye ofisi za Channel Ten katikati ya jiji la Dar es Salaam na kutembea hadi katika viwanja vya Jangawani lakini walipofika mwisho wa maandamano yao walipigwa na butwaa baada ya kumkuta Waziri Nchimbi akiwa wa kwanza kufika katika eneo hilo tayari kupokea maandamano.

Wakati Nchimbi akijiandaa kuanza kuzungumza mbele ya wanahabari, upinzani mkali ukazuka kwa waandishi dhidi ya kiongozi huyo wa serikali wakitaka aondoke mahala hapo kwani maandamano hayo yalikuwa hayamuhusu.

"Atokee.... aondokee.... hatumtakiiii.... nani kamleta hapa?" yalikuwa ni baadhi ya maneo yaliyokuwa wakitolewa kwa sauti kubwa kupinga uwapo wa waziri Nchimbi mahala hapo.

Huku akizomewa, Waziri Nchimbi alijaribu kuvumilia aibu hiyo kwa takriban dakika tano huku pengine akitumai kwamba watamruhusu kuzungumza kilichompeleka mahala hapo.

Mwandishi wa habari mkongwe, ambaye pia ni mwanasheria, Nyaronyo Kicheere, alisogea mbele ya umati wa waandishi na kusimama jirani na alipokuwapo waziri Nchimbi na kusema: "Tumeambiwa tunakuja hapa kwa ajili ya mkutano wa waandishi wa habari na utapokewa na jukwaa la wahariri, inakuwaje tupokewe na mtu mwingine. Hatumhitaji mtu mwingine hapa, aondoke."

Baada ya kauli hiyo, waziri Nchimbi aliondoka mahala hapo na kuzua shangwe kubwa kwa waandishi ambao pia walimsindikiza kwa kumzomea mpaka alipoingia katika gari lake la wizara. Hakuja na gari lake la waziri.

Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari walizungumza na kukemea mauaji hayo na bila ya kuuma-uma maneno walisema kwamba Mwangosi aliuawa kwa kulipuliwa na polisi na kwamba waliohusika wote wachukuliwe hatua za kisheria.

"Waandishi na wafanyakazi wengine wanalipa kodi ilipolisi wapate magwanda, wapate bunduki, wapate mabuti na wanalipwa ili walinde raia na sio kuua raia, vitendo kama hivi havikubaliki," alisema Jesse Kwayu, mhariri mkuu wa gazeti la NIPASHE.

Mwandishi mkongwe, Masoud Sanani, aliongeza: "Waarabu wanasema 'wal kiswaswa haq' yaani 'kisasi ni haki', lakini sisi kwa busara tunasema kwamba hatuna kisasi ila tunataka mambo haya yawe mwisho, waandishi waachwe wafanye kazi zao kama askari wanavyoachwa wafanye kazi zao."

"Tumeshasikia askari akitingishwa kidogo, mtu anashitakiwa kwa kumzuia askari kufanya kazi yake, tunataka waandishi nao waachwe wafanye kazi yao," alisema.

Waandishi walitaka familia ya marehemu Mwangosi ilelewe na watoto wasomeshwe mpaka watakapofikia.

Miongoni mwa mabango yaliyokuwapo katika maandamano hayo yalisomeka: "Bunduki na mabomu hayatazuia kalamu zetu kuandika ukweli," "Hatuogopi vitu vizito wala vitu vya ncha kali."



Source: wavuti - wavuti
 

Attachments

  • 1109585_orig.jpg
    1109585_orig.jpg
    57 KB · Views: 64
  • 1151242_orig.jpg
    1151242_orig.jpg
    77.5 KB · Views: 57
  • 2894940_orig.jpg
    2894940_orig.jpg
    113.7 KB · Views: 50
  • 4302458_orig.jpg
    4302458_orig.jpg
    57.2 KB · Views: 56
  • 5406829_orig.jpg
    5406829_orig.jpg
    70 KB · Views: 50
  • 6266262_orig.jpg
    6266262_orig.jpg
    70.4 KB · Views: 48
  • 6316198_orig.jpg
    6316198_orig.jpg
    48.7 KB · Views: 46
  • 6359719_orig.jpg
    6359719_orig.jpg
    119.5 KB · Views: 47
Nchimbi bureeeeeeeeee kabisa waziri unazamia msosi ambao hujaalikwa hawa ndio mawaziri wa serikali YA CCM, huwezi kuwatambua wakati gani wanafanya kazi za chama wakati gani wanafanya kazi za serikali/AU WAKATI GANI WAKO SERIOUS??HUYU JAMAA NI MAFIAA WAANDISHI KAENI NAE CHONJO SANA ANATEKELEZA AMRI YA ALIYEMWEKA NDIO MAANA ANAKATAA KUJIUZLU KWA KEJELI KUWA HATUWEZI PATA WAZIRI KAMA YEYE BORA ANGESEMA DR.HARRISON MWAKYEMBE NA DR.MAGUFULI HUYU MIMI KWANZA SIWEZI KUMWITA DR.NTAKUWA MWEHU, upumbavu mtupu,yaani wanakera hawa jamaa mpaka kinyaaa!!!!!!!!!!!!!!

(KUTOKA FACEBOOK MDAU MMOJA ANASEMA)
Nawapongeza sana WAANDISHI WA HABARI KWA KUMTIMUA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI EMMANUEL NCHIMBI NAWAPONGEZA SANA kwa kuonyesha hisia zenu kwa kitendo kiovu kabisa ambacho kimefanywa NA POLISI wetu DHIDI YA MWANDISHI WA HABARI DAUDI MWANGOSI ,lakini nataka niwaambie EMANUEL NCHIMBI WAZIRI WA MAMBO YA NDANI,kuvamia maandamano yenu YA WANAHABARI NA KUTAKA KUHUTUBIA bila kualikwa sio bahati mbaya anajua mtaandika zaaaidi k
uhusiana na YEYE kutimuliwa kwake na kuacha kuandika maaovu na ujumbe mliokusudia,Haingii akilini kwa mtu mwenye ngazi ya WAZIRI KUVAMIA KWA MFANO SHEREHE AMBAYO HANA KADI YA MWALIKO??KWA HIYO HAWA JAMAA INABIDI MUENDELEE KUWAKOMALIA TU HIVIHIVI!!!!!!!!!!!!!!!HAWA NDIO MAWAZIRI WA TANZANIA HUWEZI KUJUA WAKATI GANI YUKO SERIOUS!!!!!!!!!!!!!!!!!!!VIVA SAIZI HAKUNA KUWABEBA HAWA MABWEGE MMEWABEBA SANA WAMEISHIA KUWAUA MKIWACHEKEA WATAWAMALIZA HAO SAIZI WAMEKUWA WAZEE WA VITU VIZITO/FLYING OBJECTS,TAZAMA BILA PICHA KUWAAUMBUA WALISHAANZA KUSEMA BOMU WALIKUWA NALO WAANDISHI WA HABARI,UJINGA MTUPU!!!!!!!
na wana mpango hata wa kunutrilize baadhi ya waandishi ili washughulike na wale wenye msimamo mkali waandishi mkae chonjo na watu wa habari leo tbc uhuru,hoja,sauti huru, fahamu na vyombo km hivyo
 
Mbona mmetembe km chache sana DTV na Jangwani Hata km 5 hazifiki,mmeshindwa hata na yule jamaa wa mafinga aliyetembea km56? @lst mngetembea hadi viwanja vya chuo kikuu mkafanye mkutano ili ujumbe ufike kwa wengi.
Sidhani kama umbali wa kutembea una shida sana. Cha muhimu ni nini wanataka kukifikia katikam tukio hilo
 
Una ugomvi na waandishi wa habari? Au na wewe ni mmojawapo wa wale askari waliomsulibisha Yesu??/
msamehe bure tu huyu anatumia masaburi muda mwingi akili yake alishatumbukiza chooni siku nyingi!!
 
Nchimbi alitaka kupima hali ya hewa. huo mwanzo tuendako watafukuzwa wengi au watabaki wenyewe wanahutubiana. waandishi wamechoka wananchi ndo kabisaa.

  • :spy:
    • :flypig:


 
Nchimbi si waziri wa habari umefwata nini hapa jangwani we na polisi wako si ndo mmesababisha tufikie hapa kwendaaaa
 
hivi baba rizmoko yupo wapi jemeni?? au kaenda kufanya featuring na wakina boyz 2 men??? kwani kuna nchi yoyote imefiliwa?? labda yupo msibani! rubbish!
 
Hao ni waandishi, waziri aibu debe je siku CHADEMA wakaitisha ile yenyewe?

"Mabadiliko yana tabia....hayana mjadala wala mbadala.....wenye hekima huyapokea kwa amani...." Mwl. J.K. Nyerere
 
Kama ni uzembe wa mtu mmoja tu na siyo taasisi wala serikali, kwanini asiwajibishwe?. na wanalindwa na nani kufanya uovu wao?.
Majibu Tafadhari!.
Polisi aliyefanya uhalifu huo, tayari amekwisha kamatwa na anahojiwa kwa hatua zaidi za kisheria. Kwani ulipenda awajibishwe vipi zaidi ya hivyo?????????
 
"Vox Populi Vox Dei"

Sauti ya Watu ni Sauti ya Mungu"

Mungu kasikia KILIO CHENU atawajibu



Huko mara waandishi wamekataliwa hata kutoka nje kwenye jengo la press club yao mkuu wa polisi amewaonya ajaribu hata kupiga picha source channel 10


attachment.php

attachment.php

attachment.php

attachment.php

attachment.php
[/QUOTE]
 
Polisi aliyefanya uhalifu huo, tayari amekwisha kamatwa na anahojiwa kwa hatua zaidi za kisheria. Kwani ulipenda awajibishwe vipi zaidi ya hivyo?????????

Afikishwe mahakamani, kwani wanangoja nini? Mbona yule Mkenya feki alipandishwa kizimbani faster ili kuwaziba wateteahaki midomo? Na kwanini hawataki tume huru, wanajiundia vikamati ambavyo havitambuliki kikatiba/kisheria?
 
sijapenda walivyomfukuza nchimbi.. ni ukosefu wa adabu !.. wangemsikiliza kaja kusema nini.. !
 
Matamshi toka kwa ma CCM yanaonyesha kwamba CCM na Serikali wanaua watu .Kila mara angalia mauaji ya Nyamongo, Songea , Morogoro, Igunga , Ndago na sasa Iringa daima kuna statements za kisiasa na watu wanapoteza maisha mbele ya Serikali ya CCM .Wewe unasemaje ?
Nakubaliana na wewe kuwa yapo mauaji ambayo wakati mwingine yangeweza kuzuilika, kama busara zingetumika. Kuzuia maandamano ya amani, wakati mwingine si lazima kutumia silaha za moto. Askali hupewa silaha za moto, ili zitumike pale tu inapolazimu. Matumizi ya silaha za moto katika tukio la Iringa, haukuwa wa lazima, na ndiyo maana wahusika wanashikiliwa na polisi. Naungana na wewe, kuwa hakuna lugha nzuri kwa aliyefiwa, ndiyo maana hatuwezi kulaumu zomea zomea ya waandishi wa habari kwa waziri, kwani kila mtu huwa ni kichaa hasira zinapopanda. kwa hilo, hasira za waandishi zilitawala busara.
 
sasa kama waandishi wana pa kusemea, madaktari wana pa kusemea... Wale wa Moro na Singida na Arusha waliouawa nani atawasaidia kupaza sauti zao hivi?
 
Ficha upumbavu wako japo kwa sekunde,serikali na jeshi unalolitetea vimebaki uchi kwa kupiga sarakasi huku wamevaa taulo!Wenye mawazo kama yako na Tendwa ni HATARI kwa nchi.Shame on you
Sikuhukumu kwa matumizi ya maneno makali, kwani najua hakuna lugha nzuri wakati wa kifo. Ila kwa great thinkers, daima busara hutawala hasira hata wakati wa machungu kama haya. Najua si wewe peke yako uliye na machungu, bali kwa kila mpenda haki, kitendo kilichofanywa na polisi huko Iringa kinasikitisha sana, na hakuna anayekiunga mkono. Pamoja na hayo, tujifunze kutawala hasira wakati wa matatizo kama haya. kila mtu awe na uhuru wa kutoa maoni yake bila kukashfiwa na wengine. Pole kwa yaliyotokea.
 
sijapenda walivyomfukuza nchimbi.. ni ukosefu wa adabu !.. wangemsikiliza kaja kusema nini.. !
mbona rpc iringa hakumsikiliza yule muandishi aliyekwenda kumgongea dirisha, baada ya kuona mauti yanamnyemelea mwangosi! angemsikia na kumuokoa, hata wao leo wangemsikiliza nchimbo! uwe unafikiri kidogo kabla ya kumwaga vapour zako, inasaidia sana!
 
Back
Top Bottom