Kalumbesa
JF-Expert Member
- Nov 24, 2010
- 1,013
- 356
1 ) sikuzote watu wanapoandama inamaana wanaonyesha / dhihirisha hisia zao kwa jambo fulani ...
2) Maandamano hayana tija yanapomalizika bila ya itifaki yeyote ... maswali mliyonayo yanapokosa majibu etcl ..
3)si mtetei nchimbi najaribu kusema ukweli msiotaka kusikia baadhi yenu waandishi wamekosa adabu kwa kumfukuza kiongozi wa serikali ambaye angekuwa na majibu ya maswali yao ... end of the day wamerudi makwao na maswali yasio kuwa na majibu
1. Walipoandaa maandamano yao walikuwa na malengo/maazimio na Nchimbi na serikali yake hawakuhitajika kuleta ujumbe ama maelezo yoyote kama sehemu ya maazimio yao,utamshirikishaje muuaji katika mipango ya ndugu yako aliyeuawa?
2. Itifaki ya maandamano/lengo/tija ya maandamano wanaoijua ni wale waliyoyaandaa..sio lazima unapoaandaa maandamano uandae maswali yatakayohitaji kujibiwa wakati wa maandamano
3.Hayo ya kukosa adabu waandishi ndio unayaona, mbona hauoni kama Nchimbi na Serikali yake wamekosa adabu kwa kutokuchua hatua kali kwa wauaji wa mwandishi kinyume na sheria za nchi na pia kutokupeleka uwakilishi wa serikali katika mazishi yake?