Maandamano ya wanahabari Sept 11, 2012

Maandamano ya wanahabari Sept 11, 2012

acha ujinaga wako wewe, PhD na maamuzi ya mtu vinahusiana nini? hujawahi ona prof au dr bingwa wa wanawake anabaka?!! phweeeeeeeeeeeee

Well said though you failed to avoid immotions. PHD na maamuzi ya ajabu havina uhusiano maana hata UDSM wapo PH hoders au waliozipata PHD zao pale lakini matendo na maamuzi yao yanatia shaka. Mmoja yule wa REDET na yeye PHD yake Mzumbe? Mwingine amekuwa mkuu wa wilaya juzi, mwingine alipingana na wasomi wenzie akakataa hoja ya mgobea binafsi. Mwingine alisema anajenga barabara ili CDM waandamane vizuri na yeye PHD yake mbichi tena ya UDSM kwenye chemistry. List ni ndefu lakini itoshe kusema kama ulivyomwambia kuwa PHD au cheti na maamuzi havina ushusiano. Wapo wenye navyo lakini delivery/output contrasting ownership
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Hivi yule RPC aliyekuwa Mwanza yupo wapi jamani? Maana nahisi ndiye role model ya ma RPC
 
acha ujinaga wako wewe, PhD na maamuzi ya mtu vinahusiana nini? hujawahi ona prof au dr bingwa wa wanawake anabaka?!! phweeeeeeeeeeeee

Kama ungetafuta neno lingine badala ya hili, ningekubaliana na wewe. otherwise bado nina wasiwasi na Elimu ya Mzumbe kuanzia 2010
 
Safi sana waandishi wa habari. Kama kuna mikoa imekataza maandamano haya wakati jana waliruhusiwa basi ina lake jambo. Ila serikali kama mna masikio mnavyodai basi sikieni na macho yaone!!!! Ndugu wananchi serikali yenu ni sikivu.... aaaah wapi?
 
Naunga mkono maandamano, kama haki ya msingi ya kila raia kutoa maoni yake. Siungi mkono kitendo cha kuzomea waziri, kwa kuwa tendo la mauaji, si dhamira ya serikali wala chama chochote cha siasa, bali ni utendaji kazi mbovu wa mtu mmoja na wala si jeshi la polisi.

Mangaline
Unachosema ni kweli kwa kiasi fulani kwa kuwa unahamasisha heshima kwa viongozi wetu. Lakini kiongozi kuheshimika nae anawajibika ili heshima imfuate. Yeye kama mwakilishi wa serikali hajachukua hatua zinaoashiria kuwajibika kwake kama Waziri wa Mambo ya Ndani. Kwa mfano, hajatamka lolote kulaani kitendo cha polisi kumwua Mwangosi, hajawapa hata pole ya mdomo ndugu wafiwa na wakazi wa sehemu tukio lilippotokea, hajamchukulia hatua yoyote RPC Iringa, na mapungufu mengine mengi tu!! Sasa ataheshimiwa kwa lipi anaonekana kama kalewa madaraka vile? Pamoja na hayo kama nakosea nieleweshwe mbona viongozi wakuu wa serikali Rais na Waziri Mkuu hawajasema lolote kuhusu hili jambo la mauaji katika mikutano ya kisisasa? Hapo tuipimeje dhamira ya serikali kwa hili?
 
sijapenda walivyomfukuza nchimbi.. ni ukosefu wa adabu !.. wangemsikiliza kaja kusema nini.. !

Nchimbi alifuata nini? maandamano ya waandishi wa habari yanamhusu nini? Kama alitaka kuwaambia au kuongea na waandishi si angeita viongozi wa vyama vya waandishi wa habari? Alisubiri waitishe maandamano ndio aende kujikomba aonekane mwema na yupo upande wao!Kama serikali yake haikutuma hata mwakilishi katika msiba wa Mwangosi ama kutoa rambirambi kama walivyoshikilia kidedea msiba wa Kanumba,Yeye alikwenda kufanya nini? acha kutetea ujinga,Nchimbi na viongozi wengine wenye dhamana na jeshi la Polisi nao ni wahusika katika mauaji ya Mwangosi ndio maana hakuna hata aliyethubutu kutoa kauli iliyonyooka kuhusu kuwachukulia hatua askari waliofanya mauaji haya akiwemo RPC Kamuhanda na wewe kama ndio wale wale ni bora unyamaze tu!
 
[h=3]Katika hali ya isiyokuwa kawaida kutokea katika nchi hii wanahabari jijini Dar es Salaam wamemzomea na kumfukuza katika maandamano yaliyoandaliwa kulaani mauaji ya mwanahabari Daudi Mwangosi Leo jijini Dar.[/h] Hatua hiyo imetokea baada ya Waziri huyo wa wizara ya mambo ya ndani ya nchi kufika katika viwanja vya jangwani kwa ajili ya kujipa jukumu la kupokea maandamano bila mwaliko wowote toka kwa waandaaji wa maandamano hayo.
Kutokana na zomea zomea hiyo ya wanahabari dhidi ya waziri Nchimbi hali ilionekana kuwa si shwari na kupelekea waziri huyo kuondolewa na rais wa UTPC Keneth Simbaya na viongozi wengine wakiwemo askari polisi.
Habari zaidi kuhusiana na tukio hilo utaipata vizuri hapo baadae.
meena.jpg

Katibu Mkuu wa Jukwaa la Wahariri akiongea mara baada ya kuhitimisha maandamano hayo katika uwaja wa Jangwani Jijini Dar.

CHANZO: GUMZO LA JIJI
 
huyo mtu unaomsema kafikishwa mahakamaani ndani ya masaa 24 au bado na kwa nn. jibu swali
Suala la kufikishwa mahakamani ndani ya masaa yasiyozidi 24, ni ya kiraia. kumbuka, mtuhumiwa ni Polisi, na upo uwezekano wa kufuata taratibu za kijeshi, ambapo mtuhumiwa hufikishwa mahakamani baada ya kusimamishwa kazi.
 
Hivi yule RPC aliyekuwa Mwanza yupo wapi jamani? Maana nahisi ndiye role model ya ma RPC

Anaitwa Commissioner Simon Sirro acha usitukumbushe mwanza bila yeye mwanza pangechuka damu, lakini yule sirro alisema aliyeshinda atangazwe watu kaondoka mapeeeema kwenda kufungua mvinyo na kujipongeza.Yule ni kat ya graduate wachache ndani ya jeshi la polisi, lakini pia msingi wake wa elimu sipendi kuutaja kwani afundihswa jamaa akadaka mambo, lakini katiwa kapuni
 
WANAHABARI WAMTIMUA WAZIRI NCHIMBI KATIKA MAANDAMANO YAO.

kamwe Waziri Nchimbi hatasahau waandishi jinsi walivyomfanya.
fundisho kwako na viongozi wengine wanaofika bila kupata mwaliko
 
mbona rpc iringa hakumsikiliza yule muandishi aliyekwenda kumgongea dirisha, baada ya kuona mauti yanamnyemelea mwangosi! angemsikia na kumuokoa, hata wao leo wangemsikiliza nchimbo! uwe unafikiri kidogo kabla ya kumwaga vapour zako, inasaidia sana!

shukran kwa ushauri nitaufanyia kazi...

lakini nchimbi ni kiongozi wa serikali ilitakiwa wamsikilize amekuja na ujumbe gani kutoka serikalini.. maandamano hayatakuwa na tija yoyote kama watahitimisha na yale mabango wa malalamiko while mtu mbaye alikuwa na uwezo wa kuwajibu papo kwa hapo wamefukuza ...

Nchimbi alifuata nini? maandamano ya waandishi wa habari yanamhusu nini? Kama alitaka kuwaambia au kuongea na waandishi si angeita viongozi wa vyama vya waandishi wa habari? Alisubiri waitishe maandamano ndio aende kujikomba aonekane mwema na yupo upande wao!Kama serikali yake haikutuma hata mwakilishi katika msiba wa Mwangosi ama kutoa rambirambi kama walivyoshikilia kidedea msiba wa Kanumba,Yeye alikwenda kufanya nini? acha kutetea ujinga,Nchimbi na viongozi wengine wenye dhamana na jeshi la Polisi nao ni wahusika katika mauaji ya Mwangosi ndio maana hakuna hata aliyethubutu kutoa kauli iliyonyooka kuhusu kuwachukulia hatua askari waliofanya mauaji haya akiwemo RPC Kamuhanda na wewe kama ndio wale wale ni bora unyamaze tu!

sasa hayo maswali.. wangempa nafasi nchimbi angeyajibu vizuri .. mimi si msemaji wa nchimbi so sijui alikwenda kufanyanini...
 
Wangemkamata na kumkata "Biology" yake ndio angetia akili, yaani wamemwacha hivhivi tu?? no haiwezekani
 
shukran kwa ushauri nitaufanyia kazi...

lakini nchimbi ni kiongozi wa serikali ilitakiwa wamsikilize amekuja na ujumbe gani kutoka serikalini.. maandamano hayatakuwa na tija yoyote kama watahitimisha na yale mabango wa malalamiko while mtu mbaye alikuwa na uwezo wa kuwajibu papo kwa hapo wamefukuza ...

sasa hayo maswali.. wangempa nafasi nchimbi angeyajibu vizuri .. mimi si msemaji wa nchimbi so sijui alikwenda kufanyanini...

Huo ujumbe kutoka serikalini mpaka wakiandamana ndio unakuja sio? wasingeandamana? Nchimbi alidandia meli isiyomuhusu na yote ilitaka kujikosha na kujifanya mwema kwa waandishi ili aonekane mwema,2015 is near. Kama ana ujumbe ama hana kutimuliwa ilikuwa lazima sasa ajipange jinsi ya kufikisha ujumbe katika namna ambayo walengwa wa kupokea huo ujumbe watairidhia..OTHERWISE ame fail na wewe pia una fail kumtetea hapa
 
JANGWANI

Wakati maandamano yakiingia Uwanja wa Jangwani, waziri wa Mambo ya Ndani Emmanuel Nchimbi alifika uwanjani na kusimama jukwaa kuu. Hatua hii ilisababisha waandishi kupiga kelele na kumzomea na kutaka aondoke.

Hivyo alianza kuondoka na waandishi kumuimbia aondoke aondoke....

Aliondoka kwa aibu.

Chanzo: Mabadiliko Forum

427950_350111055074844_379961017_n.jpg

Waandishi wa HABARI wakiigiza TUKIO hilo LEO
 
Huo ujumbe kutoka serikalini mpaka wakiandamana ndio unakuja sio? wasingeandamana? Nchimbi alidandia meli isiyomuhusu na yote ilitaka kujikosha na kujifanya mwema kwa waandishi ili aonekane mwema,2015 is near. Kama ana ujumbe ama hana kutimuliwa ilikuwa lazima sasa ajipange jinsi ya kufikisha ujumbe katika namna ambayo walengwa wa kupokea huo ujumbe watairidhia..OTHERWISE ame fail na wewe pia una fail kumtetea hapa

1 ) sikuzote watu wanapoandama inamaana wanaonyesha / dhihirisha hisia zao kwa jambo fulani ...

2) Maandamano hayana tija yanapomalizika bila ya itifaki yeyote ... maswali mliyonayo yanapokosa majibu etcl ..

3)si mtetei nchimbi najaribu kusema ukweli msiotaka kusikia baadhi yenu waandishi wamekosa adabu kwa kumfukuza kiongozi wa serikali ambaye angekuwa na majibu ya maswali yao ... end of the day wamerudi makwao na maswali yasio kuwa na majibu

Nchimbi alifuata nini? maandamano ya waandishi wa habari yanamhusu nini? Kama alitaka kuwaambia au kuongea na waandishi si angeita viongozi wa vyama vya waandishi wa habari? Alisubiri waitishe maandamano ndio aende kujikomba aonekane mwema na yupo upande wao!Kama serikali yake haikutuma hata mwakilishi katika msiba wa Mwangosi ama kutoa rambirambi kama walivyoshikilia kidedea msiba wa Kanumba,Yeye alikwenda kufanya nini? acha kutetea ujinga,Nchimbi na viongozi wengine wenye dhamana na jeshi la Polisi nao ni wahusika katika mauaji ya Mwangosi ndio maana hakuna hata aliyethubutu kutoa kauli iliyonyooka kuhusu kuwachukulia hatua askari waliofanya mauaji haya akiwemo RPC Kamuhanda na wewe kama ndio wale wale ni bora unyamaze tu!

Huyu hapa wakati anaingia uwanjani

418859_413389955389748_619602570_n.jpg

Hapa akiwa tayari katimuliwa anaondoka kwa aibu kichwa chini

427870_413390608723016_1858638376_n.jpg
 
Back
Top Bottom