Maandamano ya wanahabari Sept 11, 2012

Maandamano ya wanahabari Sept 11, 2012

Huyo Nchimbi siku zote alikua wapi asiyatoe aliyotaka kuyatoa leo? Safi waandishi kwa kumtimulia mbali na kumzomea! Gomeni kuandika habari zote za serikali na policcm.
 
Hiyo radio nayo inabidi wanaharakaki wote tuanze kuisusia, kwani radio hiyo na TBC, ni kama mapacha, vyombo hivyo vinaendeshwa kwa propaganda, kwa lengo la kuibeba CCM!
mimi sikujua kama kraudz ina waandishi wa habari maana kuripoti matukio kama ya fiesta na khanga party taaluma yake inakuwa tofauti kidogo
 
Walichokionyesha Leo Wanahabari wetu katika Viwanja vya Jangwani kukataa kwao kwa Kuwepo Waziri Muhusika kupokea Hoja zao ni Udhaifu, Ujinga na Akili za Kitoto, Inaelekea wamefanya Maandamano hayo bila kujua Malengo na Makusudi ya kweli ya kufanya hivyo. Kwa hiyo inayakinisha kuwa wengi wao walikuwa hapo walikuwa Bendera fuata Upe[o!
 
Serikali ya CCM ina mgogoro na madaktari, mgogoro na walimu na sasa imejinyakulia mgogoro mwingine na waandishi wa habari! Wale ma-consultants wa CCM wameenda wapi? au ndio re-branding yenyewe?
 
Nimeipenda sana hii ya kumtimua huyo waizir maana angekua na maana angechukua hatua had sasa hiv kwa walioua mwaandish mwangosi maana kila kitu kipo wazi ukizingatia picha wahusika zipo clear kuliko maelezo tangu magazetin had mitandaoni leo anapeleka miguu jangwani tena wamemheshim wangempiga mawe na kumrushia michanga.
 
Watu wanasema watanzania wengi hawana kazi nimegundua hata wenye kazi hawana la kufanya: nauliza hivi kwani Waziri Nchimbi alifuata nini?? Nani alimwalika jangwani?? Hana kazi ya kufanya kwa hivyo akaenda jangwani kufanya mambo yasiyomhusu, anatakiwa kuondoka hatufai. Kikwete Rais wangu Mawaziri wako hawajui mipaka ya kazi zao wala majukumu yao futilia mbali hawa they are letting you down.
Hongera waandishi wa Habari kwa kazi nzuri.
 
Naunga mkono maandamano, kama haki ya msingi ya kila raia kutoa maoni yake. Siungi mkono kitendo cha kuzomea waziri, kwa kuwa tendo la mauaji, si dhamira ya serikali wala chama chochote cha siasa, bali ni utendaji kazi mbovu wa mtu mmoja na wala si jeshi la polisi.
Kama ni uzembe wa mtu mmoja tu na siyo taasisi wala serikali, kwanini asiwajibishwe?. na wanalindwa na nani kufanya uovu wao?.

Majibu Tafadhari!.
 
asubuhi hii wakati waandishi wa habari wakiandamana kupinga mauaji yaliyotekelezwa na polisi dhidi ya mwanahabar mwenzao ndugu mwangos wazir alijitokeza viwanja vya jangwan akidai ameenda kuwasaport.. hata hivyo waandish walimkataa wakisisitiza kuwa hawajatoa mwaliko kwa kiongoz huyo na kumtaka aondoke mara moja..wazir aliondoka eneo hilo.
 
kama kawea waandishi hakuna kurudi nyuma tena ingewezekana waziri nchimbi angepigwa na mayai vinza hatutaki ubishoo kwa hili suala
 
Naunga mkono maandamano, kama haki ya msingi ya kila raia kutoa maoni yake. Siungi mkono kitendo cha kuzomea waziri, kwa kuwa tendo la mauaji, si dhamira ya serikali wala chama chochote cha siasa, bali ni utendaji kazi mbovu wa mtu mmoja na wala si jeshi la polisi.

Matamshi toka kwa ma CCM yanaonyesha kwamba CCM na Serikali wanaua watu .Kila mara angalia mauaji ya Nyamongo, Songea , Morogoro, Igunga , Ndago na sasa Iringa daima kuna statements za kisiasa na watu wanapoteza maisha mbele ya Serikali ya CCM .Wewe unasemaje ?
 
Walichokionyesha Leo Wanahabari wetu katika Viwanja vya Jangwani kukataa kwao kwa Kuwepo Waziri Muhusika kupokea Hoja zao ni Udhaifu, Ujinga na Akili za Kitoto, Inaelekea wamefanya Maandamano hayo bila kujua Malengo na Makusudi ya kweli ya kufanya hivyo. Kwa hiyo inayakinisha kuwa wengi wao walikuwa hapo walikuwa Bendera fuata Upe[o!
Hata hujielewi!
 
ajiuzula huyu. Kumbe hana kazi zingine ofisini.. Si awawajibishe hao wauaji? Anakuja kufanya nini? Ccm bwana
 
Tatizo madhara ya maandamano yanagusa wachache, watz wengi wanayaona/chukulia kama maigizo flani ya ucheshi..
Ni kweli lakini utakubaliana na mimi kuwa miaka kadhaa iliyopita hukuwa na mawazo kama uliyonayo sasa! hivyo basi nao watafika kipindi wataelewa somo!. Kwakuwa kayumba zimetapakaa nchi nzima, waelewa nao watatapakaa nchi nzima
 
Back
Top Bottom