Lukansola
JF-Expert Member
- Sep 5, 2010
- 5,435
- 1,611
Mnapoeza muda wa watu kufanya kazi. Watu wanataka barabara, hospitali, shule bora n.k. Hawataki maandamano.
Acheni uzushi, kahamasisheni shughuli za maendeleo.
Hamjawahi kuhamasisha hata ujenzi wa shule ya kata, kazi yenu kuandaa maandamano tu. Huo ni unafiki wa kisiasa, hamna moyo wa kweli wa kuleta maendeleo Tanzania.
Cha msingi sio kujua theme bali ni kujiuliza jamii itanufaika vipi na maandamano hayo na je, jitihada zinazotumika kuandaa maandamano zisingeweza kutumika kuleta manufaa zaidi? Hawa wote wanafiki tu!
Kwa hiyo unadhani baada ya maandamano hayo uchwara bajeti ya nchi itabadirishwa?
Nothing will be achieved by those maandamano other than media attention!
Kwa hiyo maandamano ndio yataleta hospitali?
Vyama vinavyojifanya kujali kwa nini visihamasishe foundations zitakazofanya miradi ya maendeleo kwa mfano?
Maandamano feki ni unafiki tu!
Jamani huyu Marco****o hana lolote la maana someni hapo juu, yeye ndio anayepoteza muda wake mwenyewe kwa kudhihirisha jinsi alivyo na mawazo mafupi kama mkia wa mbuzi, hivi kuna watu mazoba kiasi hicho looh! siamini huyu lazima ametumwa, kwa hiyo yeye anajali muda wa wote walihudhuria maandamano kuliko wao wenyewe,kwa hiyo yeye anazijua shida zao kuliko wao wenyewe, yeye ana uchungu zaidi kuliko walioamua kusimamisha shughuli zao wenyewe na kushiriki maandamano, yeye hasomi magazeti wala kuangalia tv wala kusikiliza radio, maana angefanya hivyo angeijua nguvu ya maandamano. Kwako marcopolo kama wewe unadhani maandamano ni kupoteza muda, wenzio wako matumbo joto saa hizi amini usiamini kwa hiyo endelea kusinzia. thread kama hizi hakuna hata haja ya kuzichangia tunampa umaarufu asio stahili. :A S 13::A S 13::A S 13::A S 13::A S 13::hand: