Asha Abdala
JF-Expert Member
- Mar 21, 2007
- 1,130
- 44
Na Muhibu Said
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetangaza azma ya kufanya maandamano ya amani hadi ubalozi wa Kenya nchini hapa, kulaani matokeo tata ya Uchaguzi Mkuu yaliyompa ushindi Rais Mwai Kibaki na kusababisha vurugu na mauaji ya raia nchini humo.
Mbali na kulaani matokeo hayo na mauaji, maandamano hayo yatakayovishirikisha vyama vya CUF, TLP na NCCR-Mageuzi pia yanalenga kumshinikiza Rais Kibaki kuachia ngazi na wadau wengine kuchukua hatua mbalimbali ili kuokoa mtafaruku wa kisiasa ulioikumba nchi hiyo.
Kwa mujibu wa Chadema, maandamano hayo yanatarajiwa kufanyika kesho sambamba na mkutano wa hadhara utakaohutubiwa na viongozi wa vyama na wanaharakati mbalimbali na kuhitimishwa na ujumbe wa mshikamano utakaowasilishwa katika Ubalozi wa Kenya nchini.
Azma hiyo ilitangazwa na Chadema kupitia barua yake ya Januari 3, mwaka huu, iliyoelekezwa kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa chama hicho, Erasto Tumbo.
"Tunakusudia kuandaa maandamano ya amani siku ya Jumamosi tarehe 5 Januari mwaka 2008 kuunga mkono harakati za wapenda demokrasia na maendeleo, kulaani matokeo mabaya ya uchaguzi, mauaji yanayoendelea na kueleza na kushinikiza hatua mbalimbali zinazotakiwa kuchukuliwa na Rais Kibaki na wadau wengine ili kuondoa machafuko Kenya.
"Tunaamini kwamba matokeo ya uchaguzi wa Kenya na hali ya kisiasa ambayo imetokana na matokeo hayo ni masuala ambayo yanawagusa pia Watanzania na wapenda demokrasia wote kutokana na uhusiano wa kisiasa, kiuchumi na kijamii baina ya raia wa nchi hizi," ilieleza sehemu ya barua hiyo ya Chadema.
Kwa mujibu wa barua hiyo ambayo Mwananchi imepata nakala yake, maandamano hayo yataanzia Urafiki katika eneo la soko la ndizi kesho saa 4:00 asubuhi na yatapita katika Barabara ya Morogoro na kuelekea katika Uwanja wa Manzese Bakhressa ambako yatasimama kwa muda kwa ajili ya mkutano huo.
Baada ya mkutano huo, maandamano hayo yataendelea kwa kupita katika barabara hiyo na kuingia katika Barabara ya Kawawa kisha Barabara ya Kinondoni na kuishia katika Ubalozi wa Kenya ambako ujumbe huo utawasilishwa saa 9:00 alasiri.
"Pamoja na Chadema, vyama vya CUF, TLP na NCCR-Mageuzi navyo vitaalikwa kushiriki kwenye maandamano hayo ambayo yatakuwa pia wazi kwa umma kushiriki.