Maandamamano ya Kenya kuhamia Tanzania?

Asha Abdala

JF-Expert Member
Mar 21, 2007
1,130
44
Na Muhibu Said
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetangaza azma ya kufanya maandamano ya amani hadi ubalozi wa Kenya nchini hapa, kulaani matokeo tata ya Uchaguzi Mkuu yaliyompa ushindi Rais Mwai Kibaki na kusababisha vurugu na mauaji ya raia nchini humo.
Mbali na kulaani matokeo hayo na mauaji, maandamano hayo yatakayovishirikisha vyama vya CUF, TLP na NCCR-Mageuzi pia yanalenga kumshinikiza Rais Kibaki kuachia ngazi na wadau wengine kuchukua hatua mbalimbali ili kuokoa mtafaruku wa kisiasa ulioikumba nchi hiyo.
Kwa mujibu wa Chadema, maandamano hayo yanatarajiwa kufanyika kesho sambamba na mkutano wa hadhara utakaohutubiwa na viongozi wa vyama na wanaharakati mbalimbali na kuhitimishwa na ujumbe wa mshikamano utakaowasilishwa katika Ubalozi wa Kenya nchini.
Azma hiyo ilitangazwa na Chadema kupitia barua yake ya Januari 3, mwaka huu, iliyoelekezwa kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa chama hicho, Erasto Tumbo.
"Tunakusudia kuandaa maandamano ya amani siku ya Jumamosi tarehe 5 Januari mwaka 2008 kuunga mkono harakati za wapenda demokrasia na maendeleo, kulaani matokeo mabaya ya uchaguzi, mauaji yanayoendelea na kueleza na kushinikiza hatua mbalimbali zinazotakiwa kuchukuliwa na Rais Kibaki na wadau wengine ili kuondoa machafuko Kenya.
"Tunaamini kwamba matokeo ya uchaguzi wa Kenya na hali ya kisiasa ambayo imetokana na matokeo hayo ni masuala ambayo yanawagusa pia Watanzania na wapenda demokrasia wote kutokana na uhusiano wa kisiasa, kiuchumi na kijamii baina ya raia wa nchi hizi," ilieleza sehemu ya barua hiyo ya Chadema.
Kwa mujibu wa barua hiyo ambayo Mwananchi imepata nakala yake, maandamano hayo yataanzia Urafiki katika eneo la soko la ndizi kesho saa 4:00 asubuhi na yatapita katika Barabara ya Morogoro na kuelekea katika Uwanja wa Manzese Bakhressa ambako yatasimama kwa muda kwa ajili ya mkutano huo.
Baada ya mkutano huo, maandamano hayo yataendelea kwa kupita katika barabara hiyo na kuingia katika Barabara ya Kawawa kisha Barabara ya Kinondoni na kuishia katika Ubalozi wa Kenya ambako ujumbe huo utawasilishwa saa 9:00 alasiri.
"Pamoja na Chadema, vyama vya CUF, TLP na NCCR-Mageuzi navyo vitaalikwa kushiriki kwenye maandamano hayo ambayo yatakuwa pia wazi kwa umma kushiriki.
 
Salaam toka Kenya
Vyanzo vyangu vya habari vinasema kwamba Tibagiana amepiga marukufu maandano ya kesho . Kasema Wapinzani wakijaribu watakiona cha moto. Je kuna mkono wa JK kwenye hili ? Serikali inaogopa nini maandamano ya amani ya kupinga watu kufa na kura kuibiwa ama wasi wasi ndiyo umesha watanda kabla ya siku ?Mwenye habari kamili anipe na anieleze sababu alizozitoa Tibaigana .
 
Sababu hiz nimepewa na mtu wa Darisalama anasema mambo yalikuwa kama hivi na Chacha Wangwe .

sababu yake kwamba hali ya usalama wa nchi yetu sisalama kwani askari wote wapo kwenye ulinzi wakuangalia na kupokea wakenya.Pili,Maandamano yataleta vurugu kwasababu maandamano ya wapinzani yamelenga kutetea kikundi kimoja cha kambi ya odinga hivyo kikundi kingine cha mwai kibaka kinaweza kuja kutuvamia. 3.Kuandamana hadi kwenye ubalozi wa kenya ni kuvunja sheria za kimataifa kwani kila ubalozi unaendeshwa kwa sheria zake. Na leo Tobaigana aliwaita wawakilishi wa vyama hivyo kwaajili ya majadiliano kwamba anakataa maandamano hayo wamemwambia wataandamana na wakamkejeli kwamba afanye kazi ya jeshi siyo kuvamia kazi ya siasa.msemaji wa wapinzani alikuwa Chacha Wangwe ameonge kwa kujiamini kabisa nilikuwa namuangalia hapa chanel ten, sina mbavu nimecheka, na mkuu wa oganaizesheni wa chadema kasema wataandamana kwa amani ila polisi wakianza kuwapiga polisi ndiyo watakuwa wameanzisha vurugu, ujue wtz sikuhizi wamefyatuka akili kwani wamekuwa wasema ovyo kupita kiasi.
 
Hivi CHADEMA wametoa tamko gani kuhusu:

MAHUJAJI na ATC

SMZ KUTUMIA WANAJESHI KUFANYA SHEREHE ZA IDDI

BREACH ON NATIONALSECURITY NA ILE HELICOPTER YA JESHI KUANGUKA

WATANZANIA WALIOKWAMA HUKO KENYA

 
Ni kujibu swali la mwisho ndugu Game theory, ni kuwa watanzania waliokwama huko kenya kesho ndio naaamini watatoa tamko lao juu ya jambo hilo.

Niko nchi fulani na nimekutana na wakenya waliokuwa wanamuunga mkono Kibaka nimeshangazwa na jinsi wanavyosema kuwa MONGIKI ni kikundi kilichoundwa na wakikuyu wakijua kuwa kama matokeo yakimwangusha basi wangefanya kazi yao na tayari wamesambaza nyaraka Nairobi kuonya kuwa kama machafuko yakiendelea basi wao watajitokeza hii ni hali ya hatari sana sana .

Nawatakia CHADEMA maandamano mema kwani hii itakuwa ni kuonyesha solidarity na wenzetu wa kenya.
 
Haya maandamano si ya lazima ni sawa na kupulizia moto machafuko ya huko Kenya. Kama wanafikiri wanasaidia mimi sijui lakini binafsi siungi mkono maandamano hayo jinsi yalivyosasa, na badala yake viongozi wa upinzani wangeenda huko huko Kenya na kujaribu kuwashawishi rafiki zao kutafuta njia muafaka za kutatua matatizo ya watu wa Kenya.
 
Salaam toka Kenya
Vyanzo vyangu vya habari vinasema kwamba Tibagiana amepiga marukufu maandano ya kesho . Kasema Wapinzani wakijaribu watakiona cha moto. Je kuna mkono wa JK kwenye hili ? Serikali inaogopa nini maandamano ya amani ya kupinga watu kufa na kura kuibiwa ama wasi wasi ndiyo umesha watanda kabla ya siku ?Mwenye habari kamili anipe na anieleze sababu alizozitoa Tibaigana .

MAJIRA 5/1/08

•
Wapinzani Tanzania kama ODM
*Serikali yawazuia kuandamana Dar wang'ang'ania
*Wadai wanataka kushinikiza Kibaki aachie ngazi
*Polisi yasema si muafaka kwa hali ilivyo sasa

Na Rabia Bakari

LICHA ya Jeshi la Polisi nchini kuzuia maandamano ya umoja wa vyama vinne vya upinzani nchini, vyama hivyo vimesisitiza kuendelea na maandamano hayo leo kwa lengo kuu la kulaani mauaji na wizi wa kura uliotokea Kenya.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, kwa niaba ya vyama hivyo, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Bw. Chacha Wangwe, alisema maandamano hayo ni ya amani yenye lengo la kulaani wizi wa kura, vifo vinavyoendelea nchini Kenye na kumshinikiza Rais Mwai Kibaki ajiuzulu.

Bw. Wangwe alisema hawawezi kunyamaza kwa sababu wanaokufa ni majirani wa Tanzania na vitendo vilivyotokea Kenya vinaweza pia kutokea nchini.

“Sisi tulitoa taarifa Polisi juu ya maandamano yetu, na leo (jana), Kamishna wa Polisi, Bw. Alfred Tibaigana, alituita tukazungumza naye na katika mazungumzo hayo, alituzuia kuandamana, wakati ni haki yetu ya msingi.

“Sasa tunasema maandamano yako pale pale, tulikwenda Polisi kutoa taarifa na si kuomba kibali, nia yetu ilikuwa tupate ulinzi ili waandamanaji wasidhuriwe. Cha kushangaza Tibaigana alizungumza kisiasa badala ya kuzungumza kama chombo cha Dola,” alisema Bw. Wangwe.

Aidha, aliongeza kuwa pamoja na Bw. Tibaigana kuzuia maandamano hayo, lakini wenyewe wataendelea nayo, hivyo Polisi inatakiwa kutoa ulinzi na na isipotaka kufanya hivyo iache, lakini haina haki ya kuzuia maandamano hayo.

“Tunaomba polisi wasitumike kama chombo cha siasa, bali watumike kama chombo cha Dola kwa ajili ya kuwalinda wananchi,” aliongeza.

Alisema endapo leo polisi watajitokeza katika maandamano hayo, basi watajua kwamba wako kwa ajili ya kuwalinda na si kuzuia maandamano.

Maandamano hayo yanatarajiwa kuanzia viwanja vya Urafiki Ubungo na kuishia Manzese, ambako kutakuwa na mkutano na baada ya hapo watapeleka ujumbe wao Ubalozi wa Kenya nchini.


Polisi yapiga nyundo


Jeshi la Polisi Kanda Maalumu Mkoa wa Dar es Salaam, limesitisha maandamano ya amani ya vyama vya CHADEMA, CUF, TLP na NCCR-Mageuzi, yanayotarajiwa kufanyika leo kuhusu mgogoro wa kisiasa nchini Kenya anaripoti Rehema Mohamed.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Kamanda Tibaigana, alisema hatua hiyo imekuja ikiwa na lengo la kuweka nchi katika hali ya usalama zaidi ili kuepusha vurugu zinazoweza kutokea.

Kamanda Tibaigana alisema kuruhusu maandamano hayo ni sawa na kushabikia kikundi kimoja nchini humo, ilhali nchini kukiwa na baadhi ya Wakenya wanaoweza kuwa wa upande mwingine usioshabikiwa na kusababisha vurugu kubwa.

"Hatuwezi kudai nchi yetu iko salama kwa hali iliyopo Kenya sasa, ni kweli kwamba vitendo vyovyote vya kuonesha uchochezi wa kushabikia kikundi kimoja Kenya vitakavyofanywa nchini, vitaliingiza Taifa katika vurugu kubwa pengine kuliko hata iliyopo Kenya kwenyewe, kwa mantiki hiyo maandamano hayo hayatafanyika," alisema Kamanda Tibaigana.

Alisema hata hivyo vyama hivyo vinaonesha maandamano hayo hayatakuwa ya amani kwa kile wanachodai kuwa hata wao waliwahi kuibiwa kura katika uchaguzi mbalimbli uliowahi kufanyika nchini.

Kamanda Tibaigana alisema Jeshi la Polisi Mkoa wa Dar es Salaam, litahakikisha kuwa maandamano hayo hayafanyiki na kuwataka wananchi kulitilia maanani amri hiyo ili kuepukana madhara yanayoweza kutokea baadaye.

Alisema hata hivyo vyama hivyo vinaweza kukata rufaa kwa Waziri wa Usalama wa Raia, Bw. Bakari Mwapachu, kwa mujibu wa sheria kama wanaona hawatendewi haki, kwa kuzuiwa maandamano yao.

Awali, Januari mosi mwaka huu, umoja wa vyama hivyo kupitia Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CHADEMA, Bw. Erasto Tumbo, walimwandikia barua ya kuomba kufanyika kwa maandamano hayo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Bw. Jamal Rwambow.

Katika barua hiyo ilionesha kuwa lengo la maandamano hayo ni kuunga mkono harakati za wapenda demokrasia na maendeleo Kenya, kulaani wizi wa kura na mauaji yanayoendelea.

Kamanda Tibaigana alisema mara baada ya Kamanda wa polisi wa Kinondoni kupata barua hiyo alimpa taarifa na yeye kuamua kuitisha kikao na wawakilishi wa vyama hivyo, ili kujadili juu ya suala hilo.

Alisema katika kikao hicho, aliwaambia kuwa hali ya Kenya si nzuri hivyo wengi wao wanakimbilia nchini kupitia njia mbalimbali na hivyo suala la usalama wa nchi si zuri, pia Polisi kuruhusu maandamano hadi ubalozi wa nchi nyingine bila ridhaa ya Ubalozi husika ni kukiuka sheria za kimataifa.

Alisema kuwa pamoja na mengi yaliyojitokeza katika kikao hicho lakini wawakilishi wa vyama hivyo hawakuweza kufikia muafaka pamoja na maafisa wake kwakuwa hawakuona kwamba suala la usalama wa nchi yetu na kwamba maandamano yao kwa sasa yangeweza kuleta vurugu na uvunjaji wa amani.

 
Haya maandamano si ya lazima ni sawa na kupulizia moto machafuko ya huko Kenya. Kama wanafikiri wanasaidia mimi sijui lakini binafsi siungi mkono maandamano hayo jinsi yalivyosasa, na badala yake viongozi wa upinzani wangeenda huko huko Kenya na kujaribu kuwashawishi rafiki zao kutafuta njia muafaka za kutatua matatizo ya watu wa Kenya.

NAAFIKI 100%
 
Mimi nadhani serikali ya Tanzania ndio ingekuwa kwenye nafasi nzuri ya kusaidia kuleta amani huko Kenya. Mfano, Rais Kikwete angeweza kujitolea kuwa mpatanishi aitishe mkutano na pande zote zinazopingana hapo Arusha wajaribu kutuliza haya machafuko au labda they are already working on it!
 
Haya maandamano si ya lazima ni sawa na kupulizia moto machafuko ya huko Kenya. Kama wanafikiri wanasaidia mimi sijui lakini binafsi siungi mkono maandamano hayo jinsi yalivyosasa, na badala yake viongozi wa upinzani wangeenda huko huko Kenya na kujaribu kuwashawishi rafiki zao kutafuta njia muafaka za kutatua matatizo ya watu wa Kenya.

Mwanakijiji,

Watu kama wana muda wa kupoteza kuandamana, waache waandamane. Wajibu wa serikali ni kulinda usalama wa raia na wala sio kuzuia maandamano.

Watu mkiwaachia wafanye watakacho baada ya muda inachuja na hawafanyi tena. Si mnaona jinsi CUF walivyokuwa kila siku wanapambana na serikali ili waandamane? Sasa wameachiwa waandamane, je wameandamana mara ngapi?

Watu wameandamana London, Europe na kwingineko.

Mimi sioni kama haya maandamano ya nje yatasaidia lakini pia sioni sababu ya kuyapiga vita.
 
Cha msingi ni kuwa kuandamana kwa amani ni haki ya msingi katika nchi yeyote inayojiita demokrasia. Haya maandamano hayatakiwi kuwa na maana yeyote ndiyo yakubalike. Nakumbuka Mwalimu kabla ya vyama vingi aliwauliza makada pale Shinyanga kama wanajiamini na wao wakajibu kwa sauti kubwa ndio, naye akawauliza tena "sasa kwa nini hamtaki vyama vingi?" Waache waandamane, watafika kwenye ubalozi , watakabidhi risala, na kutoa hotuba na kwenda nyumbani. Si serikali hao, tuwaachie tu. Uoga wa nini?
 
Watanzania wanayo haki ya kuandamana na kutoa maoni yao juu ya umwagaji damu na uvunjaji wa haki za binadamu nchini Kenya. Wasikatazwe kuandamana ati kwa sababu mambo hayo yametokea Kenya au Burma au Iraq.Kama serikali ya CCM imekuwa bubu kukemea ukiukwaji wa democracy Afrika au duniani isiwanyime watanzania haki hiyo ya msingi.

-Wembe
 
Ni woga wa bure tu. Ni tatizo la polisi kupokea maelekezo kutoka kwa wanasiasa badala ya kufuata sheria.
 
Haya maandamano si ya lazima ni sawa na kupulizia moto machafuko ya huko Kenya. Kama wanafikiri wanasaidia mimi sijui lakini binafsi siungi mkono maandamano hayo jinsi yalivyosasa, na badala yake viongozi wa upinzani wangeenda huko huko Kenya na kujaribu kuwashawishi rafiki zao kutafuta njia muafaka za kutatua matatizo ya watu wa Kenya.

Naungana na wewe mkuu, kwanza waandaaji wa maandamano washachukua side kwamba Raila kaibiwa! Kenya kuna mgogoro wajibu wetu kama jirani wema sio kutia petroli kwenye moto bali na kujaribu (diplomatically) ku mediate ili ipatikane suluhu na kuepusha mauaji.

Huko Kenya kwenyewe viongozi wa ODM wanaakhirisha maandamano kuepusha shari sie huku na wapinzani wetu wasio mtazamo chanya wanachochea maandamano eti ya amani yatakuwaje ya amani ikiwa mnaamini Raila kaibiwa?

Viongozi wetu wa upinzani ovyo kabisa tuna safari ndefu kufikia japo robo ya Kenya (of course ukiondoa ZNZ)
 
Kwani Masatu hadi leo bado huamini/hukubali kwamba Raila aliibiwa ushindi? Mwenyekiti wao wa tume ya uchaguzi "Kivutio" amesema kura za Odinga ziliibwa, Wananchi wa Kenya wamesema hivyo, watu wa kabila la Kibaki wamesema hivyo,Observers wamesema hivyo, Uingereza wamesema hivyo, Ufransa wamesema hivyo, Shivji wetu kasema hivyo, ulitaka nani tena asema ili umuamini?
 
Viongozi wetu wa upinzani ovyo kabisa tuna safari ndefu kufikia japo robo ya Kenya (of course ukiondoa ZNZ)

Sema sisi watz ovyo kabisa, nikiwemo mimi, wewe, JK na wale na yule; upinzani ni sehemu tu ya wananchi wa TZ wala hatukuwanunua kutoka maduka ya ng'ambo; they are our own making, yaani they are made in TZ, kwa hiyo unapowatukana ujue nawe umejitukana, upo humohumo!
 
sounds like mugongomugongo amesharudi, kama nimepatia karibu sana tena, hatuku-miss lakini!
 
acha waandamane. wengine hapa ni watetezi wa haki za binadamu, wengine wamepoteza ndugu zao, na wengine wanaguswa hili na lile.
 
Back
Top Bottom