Maandamamano ya Kenya kuhamia Tanzania?

However, huyu Tutu hana credibility kabisaa zaidi ya hiyo Nobel thing ambayo hata Carter alipewa, huyu nasikia ndiye chanzo cha Mandela kuachana na mkewe Winnie, nasikia amegeuka kuwa agent wa makaburu ambao ndio hasa wasiomtak Zuma, hivi exactly ni nani aliyemtuma huko Kenya, au ni kihere here tu!

Haujui unachoongelea. The only credible person sasa hivi ni Tutu. Tutu ndiye pekee aliyeweza kumkemea Mandela ilpopendekezwa alipwe mshahara wa ajabu mara baada ya kushinda uchaguzi, Mandiba akamsikiliza na wakampunguza mshahara. Ni Tutu aliyemkemea tena Mandiba kwa kufanya kimada Gracia, naye akamsikiliza akafunga naye ndoa. Ni Tutu alikemea mashambulizi ya marekani Iraq. Ni Tutu aliyemwita Mugabe kikaragosi cha madikteta wa kiafrika ( au maneno kama hayo) kutokana na vitendo anavyovifanya. Ni Tutu aliyesema WOTE wawili, yaani Mbeki na Zuma hawafai kutokana na matendo yao. Ni Tutu ambaye amewaambia wazi viongozi wa kanisa lake la kianglikana kuwa wanapoteza wakati muhimu kushupalia masuala ya ushoga wakati hapa duniani kuna matatizo mengi makubwa zaidi. Tutu haogopi mtu. Tutu anasema ukweli anavyouona bila kujali ataeleweka vipi. Kumuita kibaraka wa makaburu ni kumtukana na kumwonea huyu shujaa wa Afrika. Unaiponda Nobel kwa sababu walipewa Tutu na Carter! Ulitaka apewe George W Bush ndiyo uiheshimu? Samahani kwa kutoka nje ya mada lakini hili sikuweza kuliachia lipite.
 
Wapinzani wazimwa Dar




na Happiness Katabazi



JESHI la Polisi jana lilifanikiwa kuzima maandamano yaliyokuwa yawashirikishe wafuasi wa vyama vinne vya upinzani vyenye ushirikiano wa kuunga mkono madai ya kambi ya upinzani nchini Kenya ya kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika Desemba 27.
Tangu saa 12 asubuhi, wakiwa na silaha nzito pamoja na mabomu, polisi walianza kutanda katika vitongoji vya Manzese, Urafiki na eneo la Mahakama ya Ndizi, maeneo ambayo wapinzani walipanga kupita katika maandamano yao.

Wakati polisi wakiwa wametanda katika maeneo hayo, wanachana na wafuasi wa vyama hivyo walianza kuwasili katika maeneo hayo majira ya saa mbili, lakini walipowaona askari walijificha katika nyumba za wakazi wa eneo hilo wakisubiri amri kutoka kwa viongozi wao.

Ilipofika majira saa nne, mmoja wa viongozi wa upinzani aliyesisitiza kuwapo kwa maandamano hayo, Chacha Wangwe alianza kuwasiliana na waandishi wa habari kupitia simu yake ya kiganjani akieleza kuwa yeye pamoja na wafuasi wa upinzani wapatao 100, wako mafichoni eneo hilo, wakipanga mikakati ya kukabiliana na polisi waliokuwa wametanda eneo hilo.

Wangwe alikataa kutaja eneo alilokuwa amejificha pamoja na wafuasi wake kwa kile alichodai kuwa sababu za kiusalama, lakini alisisitiza kuwa wanajiandaa kuvamia eneo hilo ghafla kama mvua.

Baadaye Wangwe aliwasiliana tena na waandishi na kuwaeleza kuwa kutokana na udhibiti wa polisi katika eneo hilo, wamebadilisha sehemu ya kuanzia maandamano hayo na kuwataka waandishi wakashuhudie wanavyoibuka wakitokea eneo la Tandale Uzuri Darajani.

Waandishi waliwahi katika eneo hilo lakini hadi saa saba mchana, waandamanaji hao hawakuwa wamejitokeza katika eneo hilo huku polisi wakiendelea na doria kali.

Wangwe aliwasiliana tena na waandishi wa habari na kuwataka waondoke eneo hilo kwa sababu nalo halikuwa salama, warudi Manzese. Muda mfupi baadaye alipiga tena simu na kueleza kuwa amepata wazo jipya na kuwataka waende eneo la Mkwajuni, Masai Pub ambako alisema angelipua bomu.

Baada ya waandishi wa habari kufika eneo hilo walipokewa na mtu ambaye hawakumfahamu mara moja, aliyewaelekeza waende karibu na msikiti uliokuwa eneo hilo ambako walizungushwa hadi nyumba ambayo haikufahamika pia mmiliki wake ni nani, wakakalishwa chini ya mti.

Wangwe aliungana na waandishi hao dakika chache baadaye na kukiri kuwa wapinzani wameshindwa kuandamana kutokana na nguvu kubwa iliyotumiwa na serikali kuzuia maandamano yao.

Alidai kuwa licha na maandamano hayo kutofanyika, serikali inapaswa itambue kuwa wapinzani wanajua kuwa Serikali ya Tanzania ilishiriki kuiba kura katika uchaguzi wa Kenya uliofanyika hivi karibuni.

Huku akiongea kwa wasiwasi, Wangwe alidai anao ushahidi kuwa Serikali ya Tanzania ilishiriki katika hujuma zilizofanyika kwenye uchaguzi mkuu wa Kenya, kutokana na ziara ya bingwa wa propaganda wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kingunge Ngombale- Mwiru, nchini Kenya wakati wa uchaguzi huo.

“Serikali yetu kupitia Kingunge imeshiriki kuiba kura za Wakenya na ndiyo maana hadi sasa haijatoa tamko la kulaani yanayotokea kwa jirani zetu, kwani nayo ni miongoni mwa walioshiriki kuharibu uchaguzi ule, na ndiyo maana leo (jana) wametumia nguvu kubwa ya dola kutuzuia sisi tusiandamane.” alisema Wakati akiendelea kueleza hayo, askari wawili wa upelelezi walipita eneo hilo na mara Wangwe alipowaona alinyamaza ghafla na kuwataka waandishi wakutane naye Masai Pub, hatua chache kutoka alipokuwa akizungumzia.

Baada ya kuyasema hayo aliondoka haraka eneo hilo akitumia gari aina ya Toyota Corolla lenye namba za usajili T 865 AMR, na haikueleweka alielekea wapi baada ya waandishi kumkosa Masai Pub.

Baadaye ilielezwa kuwa Wangwe alikuwa amekimbilia makao makuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) huko Kinondoni na waandishi walipofika eneo hilo walimkuta na alieleza kuwa alikuwa akiwasubiri waandamanaji waliokuwa na mabango ili maandamano yaanzie hapo.

Dakika chache baadaye aliwaita waandishi wa habari ndani ya ofisi za CHADEMA na kuwaambia kuwa maandamano hayo yamesitishwa lakini yatafanyika siku nyingine kwa nchi nzima, hata hivyo hakutaja siku ya kufanyika maandamano hayo.

Naye Mkuu wa Idara ya Habari wa CHADEMA, Erasto Tumbo, alitaka Kenya itolewe kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki iwapo Rais Kibaki hatajiuzulu, kwa vile ameingia madarakani kwa wizi wa kura.

Kwa ujumla mwenendo mzima wa pilika pilika hizo za jana ambazo zilikuwa kama sinema, zilivuta hisia za watu wengi huku baadhi ya wafanyabiashara wa eneo la Manzese wakiogopa kufanya shughuli zao.

Polisi waliokuwa wakiwafuata waandishi hatua kwa hatua, walisikika wakieleza kuwa iwapo kuna mpinzani atakayeonekana anaandamana barabarani, basi kila hatua yake moja itafuatia rungu la polisi moja.

Baadhi ya wafuasi wa upinzani nao walidai kuwa walichokuwa wakikifanya jana ni kulitikisa na kulihangaisha Jeshi la Polisi ili liendelee kufanya doria siku nzima ya jana chini ya Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Kinondoni, Damas Kasabi.

Nako katika ofisi za Ubalozi wa Kenya zilizo Mtaa wa Mafinga, Kinondoni na katika baadhi ya mitaa ya Jiji la Dar es Salaam, hali ya ulinzi iliimarishwa, huku magari ya polisi ya kurusha maji kwa ajili ya kuwatawanya waandamanaji yakiwa yameegeshwa Kituo cha Polisi Magomeni na Urafiki, yakiwa tayari kuwakabili waandamanaji.

Maandamano hayo yalipigwa marufuku juzi na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Alfred Tibaigana, kwa maelezo kuwa hali ya usalama hapa nchini kwa sasa si shwari.
 
Haujui unachoongelea. The only credible person sasa hivi ni Tutu. Tutu ndiye pekee aliyeweza kumkemea Mandela ilpopendekezwa alipwe mshahara wa ajabu mara baada ya kushinda uchaguzi, Mandiba akamsikiliza na wakampunguza mshahara. Ni Tutu aliyemkemea tena Mandiba kwa kmfanya kimada Gracia, naye akamsikiliza akafunga naye ndoa. Ni Tutu alikemea mashambulizi ya marekani Iraq. Ni Tutu aliyemwita Mugabe kikaragosi cha madikteta wa kiafrika ( au maneno kama hayo) kutokana na vitendo anavyovifanya. Ni Tutu aliyesema WOTE wawili, yaani Mbeki na Zuma hawafai kutokana na matendo yao. Ni Tutu ambaye amewaambia wazi kuwa wanapoteza wakati muhimu kushupalia masuala ya ushoga wakati hapa duniani kuna matatizo mengi makubwa zaidi. Tutu haogopi mtu. Tutu anasema ukweli anmavyouona bila kujali ataeleweka vipi. Kumuita kibaraka wa makaburu ni kumtukana na kumwonea huyu shujaa wa Afrika.Unaiponda Nobel kwa sababu walipewa Tutu na Carter! Ulitaka apewe George W Bush ndiyo uiheshimu? Samahani kwa kutoka nje ya mada lakini hili sikuweza kuliachia lipite.

Mimi naamini hii shule uliyotoa inatosha kumfanya yeyote aliyemkandia Tutu ajione ni mnyonge na akatubu palepale alipo tena kwa kupiga magoti. Ndio mimi nasema siku zote hapa kuwa mtu usijaribu kuongea jambo ambalo hulijui au huna uhakika nalo au kumkoromea mtu ambaye unamjua juu juu tu. Inaonekana huyu ndugu yetu alikuwa hamjui vizuri Tutu; namshauri asome kidogo biography yake ndipo atengeneze opinion yake. Vinginevyo ataonekana analeta "vioja" badala ya hoja. Ahsante sana Fundi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom