Mkuu Pakacha, sijazungumzia ukuu wala uhalali wa kikao hicho kuzungumzia issue hiyo. Ninachokizungumzia ni matumizi busara kwenye approach waliyoichukua ili kufikia lengo bila kutumia nguvu nyingi.Nafikiri labda ungejifunza uzuri katiba ya CCM. NEC ndio kikao kikuu, kilichopo kidemokrasia, na ni sahihi kwa kufanya hivyo ilivyofanya.
ila ukumbuke kura zao nyingi zinatoka kule kijijini kwenu ambako usafiri ni wa kutumia trecta na sukari mpaka ww ukienda likizo ndo uwapelekee.
Nasikia kuna uvumi kwamba, Sitta ndiye anaonekana msafi kidogo ndani ya chama. Ikitokea JK hakubaliki mwakani Sitta wanataka awe mbadala. Nawakilisha wakuu.
=Recta;555458]Mkuu Pakacha, sijazungumzia ukuu wala uhalali wa kikao hicho kuzungumzia issue hiyo. Ninachokizungumzia ni matumizi busara kwenye approach waliyoichukua ili kufikia lengo bila kutumia nguvu nyingi.
Ni kweli kuwa NEC ndicho kikao sahihi kabisa kufanya walichofanya. Lakini kwa ajili ya matokeo mazuri zaidi, wangeweza kuongea nae offline (if you know what I mean). Badala yake, ni kufuata taratibu kama walivyofanya na kupata political damage inayokuja.
Angalia upande wa pili wa shilingi. Kwa nini Bw. Sitta anatumia Bunge kutoa mambo mazito mazito yenye kukifadhaisha Chama chake, badala ya kutumia busara kwanza kuziibua hizo issue katika lujna yao CC- ambapo yeye ni mwanachama tena mwenye nguvu -kwa nini ameidharau CC halafu wewe unataka afanyiwe busara na CC hiyo hiyo.?Mkuu Pakacha, sijazungumzia ukuu wala uhalali wa kikao hicho kuzungumzia issue hiyo. Ninachokizungumzia ni matumizi busara kwenye approach waliyoichukua ili kufikia lengo bila kutumia nguvu nyingi.
Ni kweli kuwa NEC ndicho kikao sahihi kabisa kufanya walichofanya. Lakini kwa ajili ya matokeo mazuri zaidi, wangeweza kuongea nae offline (if you know what I mean). Badala yake, ni kufuata taratibu kama walivyofanya na kupata political damage inayokuja.
Asubuhi leo nimewasikia wale vijana wa Clouds FM wakimkejeli mtu (bila kumtaja jina) radioni, wanasema ''....kama unaona vipi rudisha kadi, sio kusemasema tu watu oooh mafisadi...., sasa unaomba huruma,...oooh nisameheni mzee mwenzenu....!'' Sijui huwa wanatumwa na nani wale vijana!
Na TBC radio kipindi cha asubuhi wakamtoa Chiligati akisema ''.....kama mtu hawezi kuwa na nidhamu ya chama, anataka kuzungumza bila utaratibu kama mlevi, arudishe kadi yetu akajiunge na chama kingine cha walevi wenzie...!"
Baada ya kupitia hii thread na kusoma magazeti ndio nimepata picha halisi kuhusu anayesemwa, lakini hakika nashangaa sana nchi hii inakopelekwa. Inahitajika sadaka ya ajabu kuepusha mustakabali huo wa hatari, na ninatamani hawa akina Sitta na wenzake wangekuwa na ujasiri huo.
Pakacha,
Mkuu hakuna serikali yoyote inayoweza kumhukumu Msika wake kwa sababu analitumia bunge kuwaadhibu viongozi wa chama chake ambao wanakiuka ilani za chama...Spika hayupo bungeni kuwakilisha chama isipokuwa kusimamia vikao vya Bunge kwa uwazi..ni kama hakimu ambaye pamoja na kuwa ni mwanasheria basi mnataka lazima awe upande wa district Attoney ktk mashtaka yote...
Nina hakika kabisa kuwa Demoktratic hawana uwezo wala nguvu ya kumnyang'anya kadi ya chama Nancy Pelosi kwa sababu tu anapingana na baadhi ya senata wa chama chake.
Binafsi sijaona kifungu wala sehemu ambayo inamweka Sitta hatiani kwa kushambulia viongozi wabaya ndani ya chama. Hajawahi kusema wala kuhoji katiba, ilani na mwongozo wa chama chake akiwa bungeni..
Mkuu wangu kumkataa Sheikh au Padre fulani haikuondoi ktk Uislaam au Ukristu...Ila nachoweza kusema JK anawachezea CCM sasa hivi. Kwa kuleta mada hii ktk kikao cha CC, JK anataka kuwajua wote waliosimama upande wa pili na walivyokuwa wajinga samaki wengi wameivaa ndoana yake. Leo hii JK anawafahamu wote waliosimama upande wake au wa Lowassa. Kazi imekwisha kilichobakia ni kuifanyia kazi report nzima na ndio maana Mzee wetu Mh. mwinyi anaifanyia kazi..
Nami naunga mkono Six angegoma kuomba msahama.....wamfukuze awe shujaa wa ufisadi,....kuliko kuomba msamaha....awe kibogoyooo maana yake nini??hakuna kitu aisee nchi hiii imekwisha na haifai tena