Maamuzi ya NEC ya CCM na Hatima ya Spika Sitta

Maamuzi ya NEC ya CCM na Hatima ya Spika Sitta

kusema kweli umefika wakati watz tuamke usingizini kimatendo na pia chama tawala kiwe na ukweli na uwazi...jamani mnyonge mnyongeni lakini haki yake apewe.......
 
we are fed up with ss issues! kama yeye ni gentle man aendelee tu na mwisho wa siku atapatikana mshindi. mwanazuoni mmoja alipata kunisimulia kuwa mtoto wa haramu hata ukimtumbukiza katika chupa atatoa hata kidole kwenye mdomo wa chupa ili kila mtu aweze kumuona nakumtambua kuwa yeye ni mwana haram
 
The degree of ignorance in this board is shocking! full ushabiki, nobody is talking or at least pitching ideas how we are going to decrease the infant mortality in next ten years. Kama una uchungu na nchi kachukue form ugombee ubunge or something. If u guys are radicals and u want to change the country, get off your laptops huko ughaibuni na mliendeleze libeneke nyumbani. Every topic in is about wanasiasa na mafisadi, hata hao mafisadi wakiingia humu ndani wanawaona wengi wazushi tu because there are no ideas. Absolutely nothing. Now, tunashabikia Sitta kuwa kawashinda mafisadi---fine, but tell me how exactly that will help kupunguza mgao wa umeme, or what are the connections between Sitta na mafisadi that will increase victims wa ngoma kupata ARVs.

If we are truly "the home of great thinkers" then we ought outline our strategy out of poverty na ni jinsi gani mtanzania wa kawaida atanufaika. Hao mafisadi wakiingia humu ndani wanakuta nondo tu. You all want change, but none of you have spelled out C.H.A.N.G.E that you want. U hate CCM fine, then tell us what should Chadema do? and if you are kada then suggest what CCM as a serikali should do.. Think people and acheni kuendekeza malumbano ya kisiasa. I mean the whole freaking country is at awe, oooh excitement za drama za CCM..I mean none of these so called leaders have put forth a development agendas that will help regular Mtanzania like me..Sitta, Chiligati, Rostam, tunashabikia data, ES kaja na data flani, mara Zitto katoa hutuba somewhere. We want leaders who are policy oriented that can tell us tunakwenda paleeeee, and this is how we gonna get there. And u guys who are supposed to criticize serikali mnaongelea siasa allllll daaaaay--this place is so hopeless its unfuckingbelieavable. Its just incredible. How are we gonna provide umeme for everybody by 2015? or how can we improve kilimo and diversifying our crops to yield mavuno manono? or how can we fucking make more money out of our madini contracts and are there any legal possibilities to get us out of all these shady contracts that we are in, if yes How? weka suggestions mtumieni waziri. Shit like that..Can we set up a Dick Chaney style manipulative of law so as wala rushwa wote can be prosecuted with less ushahidi? lets do that, or how do we increase healthcare spending so as we are not loosing as many pregnant women as we do now? how are we going to make secondary school education free for everybody? I honestly expect to see that when I log into this site. I expect to learn some serious shit when I log in here, not chuki, fitina, and majungu. Now humu ndani full skendo, and gossip halafu eti tunajiita home of the greatest thinkers. Name ideas that were generated from this forum and have been implemented in our serikali? Jamii forum is so popular we can easily influence serikali intellectually and not majungucally. We are spending days and night blaming, and blaming, and blaming, with no matunda.

my two cents..
It is almost 45 minutes past the time that you posted your criticism (contrary to what you said above) and I do not see anything constructive from you. I thought you came to bring the change you preached about.
 
Kosa kubwa lililofanyika katika mkutano ule wa NEC ni kuruhusu baadhi ya wajumbe kumshambulia sitta. Huyu Spika anaweza kuwa na makosa lakini wale waliopanga kumsulubu katika NEC ni mambumbumbu wa nguvu za umma. Hapana shaka yoyote ile kuwa ikipigwa kura ya maoni leo hii, sitta anaonekana ni shujaa mbele ya umma.

Kama wangefanya kosa la kumnyang'anya uanachama wa CCM na hivyo nafasi yake ya Spika, naamini huo ndio ungekuwa mwisho wa CCM. Inavyoonekana ni kuwa wapo watu ndani ya CCM ambao hawajui kuwa jamii yetu imebadilika na kwamba ina uelewa mkubwa. Sasa hivi kinacbhozingatiwa siyo umaarufu na historia ya CCM bali ni hoja kuwa CCM itaifanyia nini nchi hii?

Propaganda inayopigwa sasa nchi nzima ni kuwa CCM ni chama cha mafisadi. Sasa hii ni propaganda mbaya sana. Ukweli ni kuwa CCM ni chama kizuri kuliko vyama vyote nchini na pengine Afrika nzima. Katiba yake ni nzuri, sera zake ninzuri pia. Lakini baadhi ya watu waliomo ndani ya CCM, na hasa baadhi ya viongozi, ni mafisadi wakubwa. Sasa hawa ndio wanaotuharibia chama chetu. Watu hawa wamejipanga kwelikweli. Wanahodhi uchumi na sasa wamejiingiza kwenye siasa ili wahodhi pia nguvu ya kuamua mambo mazito. Wewe tu jiulize kwanini wafanyabiashara wanajiingiza mno kwenye siasa? Jibu ni kuwa wanataka 'protection' kwa maovu yao wanayoyafanya. Yaani 'mafioso' ndio wanaotaka kuhodhi madaraka ya nchi. Sasa hii ni mbaya mno.

Sasa basi wale wajumbe 'walioropoka' kwenye NEC kwa kumshambulia Sitta ni kwamba walipangwa na wakasema yale waliyotakiwa waseme. Bahati nzuri kuwa hii ni dunia ya utandawazi. Umma ukafahamu haraka mno kilichotokea kwenye NEC tofauti na wakati wa miaka ya 1980 ambapo vyombo vya habari vilikuwa vichache gtena basi vya chama na serikali tu.

Tusubiri tuone hali ya kisiasa inavyoendelea lakini ipo siku, hakika nawaambieni, watu wazima na akili watapigwa mawe kama watatembea mitaani. Watu wanachoka.
 
Kikwete amtelekeza Sitta

jk_1.jpg

  • Aruhusu 'mafisadi' kumsulubu
  • Mpasuko mkubwa CCM waja
RAIS Jakaya Kikwete ameshindwa kulinda hadhi ya Spika wa Bunge la Jamhuri, Samwel Sitta katika vikao vya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mjini Dodoma.

Akiwa mwenyekiti wa chama hicho, Kikwete aliwaacha wajumbe wa Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM kumtuhumu Sitta kuwa aanatumia bunge kujeruhi chama na serikali yake.

Alikuwa mbunge wa kuteuliwa na rais, Kingunge Ngombale-Mwiru aliyemkana na kumsulubu kwa kauli kali akisema "…Sitta ametwaa madaraka vibaya kwa kuahidi wabunge kuboresha maslahi yao."

"…Huyu Sitta amepata madaraka kwa rungu la ulaghai. Alihadaa wabunge kwamba wakimchagua ataboresha maslahi yao.," Ngombale alinukuliwa na mtoa habari akisema ndani ya kikao cha NEC.

Aliongeza kuwa Sitta "Amechapisha hata kitabu, tena nje ya nchi kinachoitwa, 'Bunge lenye meno.' Haya ni meno dhidi ya serikali ya CCM," amenukuliwa na akisema.

Ngombale aliongea kwa kudhamiria. Alisema "Sitta anahutubia sana Bunge kuliko mbunge mwenyewe. Anapenda wabunge wa upinzani kuliko wa CCM. Tabia yake hii, ameipandikiza hata kwa naibu spika na wenyeviti wake wa Bunge," Ngombale alinukuliwa aking'aka.

Lakini pamoja na tuhuma nyingi na nzito, wote walioongoza genge la "Kummaliza Sitta" kwa kumtoa uspika na hata kumfukuza kwenye chama, waliishia kunywea.

Naye Sitta, baada ya kusikiliza tuhuma, shutuma, kejeli, lakini na busara za rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi na Waziri Kiongozi wa Zanzibar Shamsi Vuai Nahodha, alipoza munkari wa wajumbe kwa njia ambayo mwanasiasa yeyote mzoefu angefanya.

Sitta alisema, "Kufanya kosa si kosa; kosa ni kurudia kosa." Hapo ndipo baadhi ya mahasimu wake walitazamana huku wakishindwa kucheka au kuendelea kununa.

Mtoa habari aliliambia MwanaHALISI kuwa hata wakati wa kutoka ukumbini, baadhi ya wajumbe walikuwa wakijiuliza, "Kwa kosa anasema nini? Kwamba angeasi na kuhama chama au kweli amekiri tuhuma alizotwishwa?"

Awali katika kikao cha Kamati Kuu cha Jumamosi na Jumapili, Sitta anaripotiwa kugeuka mbogo na kueleza kwa undani kile alichosema kinachosumbua serikali.

Mtoa taarifa alimnukuu Sitta akisema wakati "mtandao wa Kikwete" ulipokuwa unaomba ridhaa kwa wananchi, wao (akiiwemo yeye) hawakupanga kutumia nafasi hiyo kutafuta utajiri.

"Kama tunataka kuiba na kulea ufisadi, basi sawa. Lakini ni muhimu twende kwenye mkutano mkuu ili kubadilisha katiba ya chama chetu. Tukawaambie wanachama wetu, kwamba CCM imebadilika kutoka chama cha kutetea wanyonge na kuwa chama cha kulea mafisadi," alisema mtoa taarifa akimnukuu Sitta.

Kauli ya Sitta iliamsha munkari wa baadhi ya wajumbe waliokuwa wamebeba hoja kuu ya kumfukuza Sitta na wabunge wenzake waliotajwa kuwa 11ambao wanapiga vita ufisadi.

Katika kikao cha NEC ambacho kiliendelea hadi usiku wa Jumatatu, Asha Bakari Makame, makamu mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT), alisema Sitta anapasua chama na kwamba ndicho chanzo cha matatizo.

Asha alisema kwa sauti ya kufoka, kuwa Sitta aondoke na "kubakisha hapa kadi yetu."

Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe, akijibu hoja ya upatanishi, alinukuliwa na mtoa taarifa akisema kwamba hakuna upatanishi unaoweza kufanyika.

Alisema mgogoro uliomo ndani ya chama unatokana na makundi mawili; moja linalopinga ufisadi na lile linalounga mkono ufisadi.

"Ugomvi huu utaisha pale ufisadi utakapomalizika. Zaidi ya hapo, hakuna kinachoweza kuzungumzwa na kumaliza ugomvi wetu," alisema Mwakyembe.

Kwa mujibu wa taarifa, baadhi ya wajumbe watetezi wa Sitta walipokuwa wakiongea, zilikuwa zikisikika sauti za kuzomea, jambo ambalo lilimfanya mwenyekiti Kikwete kuingilia kati.

Kwa mfano, mbunge wa Igunga, Rostam Aziz alinukuliwa akisema, "Sikujua kama huyu ana akili ndogo kiasi hiki." Ilikuwa ni wakati mjumbe mwingine, Injinia Stella Manyanya alipokuwa akitetea Spika Sitta.

Manyanya alinukuliwa akisema, "Sitta ni mmoja wa viongozi wa kupigiwa mfano nchini."

Mtoa taarifa anasema baada ya Rostam kushambulia Manyanya, Nape Nnauye, aliyesikia kauli ya Rostam, alijibu kwa kusema, "Wewe usiyeelewa kinachosemwa, ndiyo mwenye akili ndogo."

Akizungumza katika siku ya kwanza ya kikao cha NEC, Nape alisema jina la Rais Kikwete linatumiwa vibaya na baadhi ya wasaidizi wake. Alisema baadhi yao wamo katika mkutano ule na kwamba rais angewakana hadharani.

Alitoa mfano wa sakata la Daniel ole Porokwa, Katibu Msaidizi wilaya ya Hanang, aliyefukuzwa kazi na Katibu Mkuu Yusuph Makamba kwa kisingizo cha "agizo kutoka kwa mwenyekiti Kikwete."

Hoja ya ufisadi iliyotajwa na Mwakyembe ilikuwa imeibuka mapema katika Kamati Kuu pale mjumbe Abdulrahman Kinana aliposimama upande wa Sitta na kusema, huku akitoa macho kuwa "Tuhuma za ufisadi zinazokabili baadhi ya viongozi ndizo zinaangamiza CCM."

Katika hali ambayo haikutegemewa, Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ngenda Kirumbi alimbeza Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP, Reginard Mengi, akisema kwanza si mwanachama wa CCM.

"Huyu Mengi si mwana-CCM. Namshangaa dada yangu Chilolo (Diana Chilolo mjumbe wa NEC), kusema kuwa Mengi ni mwanachama safi. Huyu Mengi ni mtu tu. Mimi nimekwenda hadi kwa balozi wa shina na katika tawi linalodaiwa kuwa Mengi ni mwanachama. Hajasajiliwa huko. Uanachama wake ni feki. Mimi siujui," alisema Kirumbi huku akimtolea macho Chilolo.

Miezi michache iliyopita Mengi alifanya ziara mkoani Singida na kwenye mkutano, Chilolo alimtaja kuwa mwanachama mzuri wa CCM. Kwenye mkutano, Mengi alichanga Sh. 100 milioni kwa ajili ya Saccos ya akinamama.

Sitta amebaki na nafasi yake ya spika na amebaki na kadi yake. Wachunguzi wa mambo wanasema inawezekana hazikuchukuliwa hatua dhidi yake kwa vile walihofia angechukua uamuzi mkali wa kuhama chama ambao ungekiumiza.

Mjadala wa kumsulubu Sitta ulitokana na mada iliyowasilishwa ndani ya vikao ambayo ilihusu hali ya kisiasa nchini, ndani ya CCM na nje ya chama hicho.

Naye mwenyekiti Kikwete,pamoja na kusema kuwa anampongeza Sitta kwa ujasiri wake, alionyesha wasiwasi wake jinsi spika anavyoendesha shughuli zake.

Alisema mambo ya ufisadi wanayojadili sharti iwe kwenye vikao vya chama na siyo bungeni; kwani yakipelekwa bungeni wanakuwa wameifanyia kazi kambi ya upinzani.

Kamati Kuu imeunda kamati ndogo ya watu watatu – Ali Hassan Mwinyi, Pius Msekwa na Abdulrahman Kinana kutafuta mahusiano kati ya bunge na kamati ya wabunge ya CCM.

Ukiacha mpambano huo kati ya Sitta na kundi zima la CCM, kitendo cha Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume kutohudhiria vikao hivyo kuanzia CC hadi NEC, nacho kilizua maswali mengi miongoni mwa wajumbe.
 
six abaki ndani ya chama ila akaze buti,aelewe ya kuwa wananchi wote tutakuwa naye kama akiwa na msimamo huo,wachafuzi ni wengi sana wametaka kumchafua kwa story kibao lakini mzee yupo fit,bravo mzee wetu
 
Kikwete hajamsaliti sitta,alichofanya ni kumuonyesha sitta the true picture ya cmm,ili ajue kuwa ccm imeoza kiasi gani,kikwete aliachia mambo yajioneshe yenyewe,sitta sasa ameshajua kwamba tatizo si kikwete bali ni ccm yote,kikwete ni sehemu tu ya tatizo,but tatizo kubwa ni ccm,ccm iko too corrupt hata kama kikwete ataondolewa,
 
Swala la kudhibiti watu ikiwamo wabunge lilianza na mikutano ya Kingunge. Bahati mbaya sana leo hii kingunge si yule aliyejulikana enzi za mMwalimu kuwa mjamaa na mwanamapinduzi. Sasa hivi ni mlevi wa 'politiburo politics, ambapo kila mtu lazima afyate mkia. Kumdhibiti Sita au mabadiliko ya jamii ya Tanzania leo, kama itawezekana, basi utakuwa ushindi mkubwa kwa CCM. Tunakoenda kwa mtindo huu ni udikteta wa chama kimoja ambao tumeulea wenyewe kwa kutochagua wabunge wengi wa upinzani. Taratibu za bunge zinaeleweka kama CCM wanahoja na wao wakiwa wengi bungeni. Wote wapigao vita ufisadi wataibuka washindi hata ikibidi kuhama chama. Tunaweza kuunda PanAfrican nyingie!!
 
Kikwete hajamsaliti sitta,alichofanya ni kumuonyesha sitta the true picture ya cmm,ili ajue kuwa ccm imeoza kiasi gani,kikwete aliachia mambo yajioneshe yenyewe,sitta sasa ameshajua kwamba tatizo si kikwete bali ni ccm yote,kikwete ni sehemu tu ya tatizo,but tatizo kubwa ni ccm,ccm iko too corrupt hata kama kikwete ataondolewa,

Mkuu heshima mbele sanaa na ninakubaliana na wewe kwa asilimia kubwa na naheshimu sana mtazamo wako katika hili ingawa kuna baadhi ya vitu sikubaliani navyo hasa hapo kwenye hizo bold

Kuhusu Kikwete kuwa sehemu ya tatizo nafikiri lazima utakubaliana na mimi ya kwamba bila ya Kikwete CCM ilikuwa inakwenda KUOZAAAAA KABISAAAA na ninachomsifu huyu bwana ni kuvipa sana uhuru vyombo vya habari maaana anaelewa kabisa wanahabari ndio wakombozi na wanamapinduzi hasa kwenye huu muda wa mkanganyiko na hawa mafisadi.

Pili kuhusu Kikwete kuondolewa nafikiri mpk sasa wameshashindwa ingawa katika kipindi cha nyuma kama miezi 3 nadhani (mawazo yangu) walikuwa na nguvu sana ingawa walichemka baadhi ya sehemu ndio maana JK akawa ahead of them.

Nyongeza kuhusu Spika Sitta, mimi naendelea kumpongeza sana kwa ujasiri wake aliouonyesha na naamini ameonyesha mfano ambao hata sisi vijana tunaafa kuuiga uwe mwanachama wa chama chochote cha siasa hapa nchini na nafikiri na naamini msimamo wake utaendeleza chachu cha mapinduzi ndani ya CCM na taifa kwa ujumla.
 
Pdiddy,
Mkuu sina hakika kama haya ni mawazo yako au ume copy na Ku paste hivyo hukuweka jina la mwandishi..Lakini kitu kimoja tu ukumbuke kwamba Kumlaumu JK kwa kutomlinda Sitta ndio excuses walizotumia Mafisadi kuhisana na Sitta, ya kwamba Sitta kama Spika na mbunge wa CCM hakuweza kuwalinda wabunge wa CCM bungeni against Wapinzani..

Sasa Unapoimtaka JK alinde Sitta kwa sababu yeye nirais na anazo nguvu kubwa sana sijui utakuwa na tofauti gani na Mafisadi ambao walitaka Spika Sitta atumie nguvu ya wadhifa wake kuwakwamisha Upinzani.

Sitta kama Spika alifanya jambo zuri kuachia hoja zote zijadiliwe kama zilivyoletwa au kuwakilishwa na wabunge na JK kama Mwenyekiti wa chama alifanya jambo zuri sana kuachia hoja hiyo ijadiliwe na haki kuaptikana kwani kilicho hatarini ktk utawala sio maisha na uhai wa Sitta isipokuwa ni vita against Ufisadi.

Unapojitoa Mhanga kutetea haki ya wananchi wako usitegemee siku zote kupata nafuu au njia za mkato. Sitta hakufanya alofanya ili kumsetiri JK ila haki ya utawala bora..na kujitolea mhanga huja na machungu yake! - Mandela alikaa jela miaka kibao na hakuwalaumu viongozi au wnachama wenzake kutomsaidia..Kama Sitta anategemea msaada toka kwa JK basi huyu sii Mpinganaji..ina maana JK akiondoka basi naye atatafuta mfalme mwnigne!
 
Nimefuatilia maoni ya wanaJF juu ya sakata la Sitta na NEC; wengi wanaonekana kumshauri aondoke CCM kwani hawezi kupambana na ufisadi akiwa ndani ya mafisadi.

Kwa juujuu inaoneka ni sawa ila kimkakati nina mawazo tofauti.


CCM imeweza kuvisambaratisha vyama vya upinzani kwa kutumia mbinu ya kupandikiza viongozi ndani ya vyama na hata kupandikiza vyama (yaani kuna vyama vya upinzani ambavyo ni matawi ya CCM). Mbinu hii ilitumika kuisambaratisha NCCR Mageuzi na ndiyo inazuia kuwepo kwa muungano/umoja wa vyama vya upinzani. Kwa mfano kuna mgombea urais mwaka 2000 wa chama cha upinzani,sasa amejiunga na CCM. Je mkimsimamisha mtu kama huyo katika muungano wa vyama na kabla ya uchaguzi kufanyika akajiengua na kujiunga na CCM si mtakuwa mmefanya zero?

Katika vita pia, ukiweza kuwa na askari wako ndani ya adui yako (makachero), basi kushinda ni rahisi maana siri zao utazijua mapema kabla hujashambuliwa.

Ni kwa mantiki hayo basi naona ni vyema watu kama Sitta wakawa ndani ya CCM; hii inasaidia kujua CCM wanapanga nini? Kwa mfano kama Sitta asingekuwa mjumbe wa NEC haya yote yasingejulikana wazi kwani wangekaa kisirisiri na kuamua kupiga kura ya kutokuwa na imani nae bungeni, lakini kwa kuwa alikuwemo ilibidi waseme waziwazi na hiyo imetusaidia kuwajua.

Pili ukiwa na akina Sitta, Mwakyembe, Selelii nk ndani ya CCM wanachochea mawazo mbadala ndani yake. Kuliko kuwa na wajumbe wote wanaosema 'ndiyo mzee' bora wawepo wale wanaoweza kuthubutu kusema 'siyo mzee'. Unajua wengine husema 'ndiyo mwenyekiti' kwa kuwa waoga kusema ila ukiwapa nafasi sirini wana mawazo tofauti. Hii ndiyo ilisaidia kutomuondoa Sitta maana kulijitokeza hoja mbili tofauti; moja arudishe kadi na nyingine ikisema hapana. Mwenyekiti alishindwa kuamua kwani angesema ipigwe kura hakuwa na uhakika ni upande gani utakaoshinda. Kama akina Sitta wasingekuwemo, hao wa kusema asirudishe kadi wasingekuwemo.

Ni juu yetu kuwatumia kikamilifu hao watu wa watu kama akina Sitta walio ndani ya CCM.

Nawasilisha.
 
Sitta mwenyewe fisadi, or at the very least hawezi kusimamisha ufisadi na/ au anaudekeza na kunufaika nao.

So the whole premise of your argument, which is based on the valor of Sitta's anti-ufisadi move, is flawed.
 
Ni kweli kabisa hawa wanaohamahama vyama unaweza kuwafananisha na askari mamluki kuna Tambwe,kuna Lwakatale kuna Akwilombe nina wasiwasi na watu hawa kuwa CUF imewasacrifice in advance in order to get things done well, huwezi kujua ila upande wa CUF mwanachama mpya nafikiri huwa anapewa miezi sita kabla ya kuruhusiwa kugombea nafasi yeyote ile, kama sikosei watu wa CUF wanaweza kuliweka sawa hilo.

Tatizo kuna baadhi ya vyama vinawavamia wanaohamia chama na kuwapa nafasi ya juu kabisa ,hili linafaa liangaliwe kwa makini isije kuwa unavamia mchongoma.
 
By the time mtakapojua kuwa Siita ni msanii tu mtakuwa mmechelewa sana.

The whole thing ni comedy kama kweli ana uchungu simple atoke huko ajiunge na wapiganaji wa kweli badala aya kutuchezea game. Huyu jamaa ni mjanja sana anauma na kupulizia, subiriini muda si mrefu rangi zake halisi zitaonekana.
 
Nani anayeshanga Mkuu kumsaliti Sitta now?😕
Kawaiada yake nyie si mnaona jinsi alivyowasaliti watanzania na hasa waliompigia kura
 
Mimi nafikiri kikwete ni more of a weak leader than kusema ameachia uhuru wa habari,
 
Wednesday August 26, 2009 Sitta, who dares wins!






Adam Lusekelo, 26th August 2009 @ 00:13,

THE Speaker to the Bunge, Sam Six, is now basking in unimaginable popularity and adoration in the United Republic of Tanzania.

He was recently crucified for siding with the good guys. When the Speaker asked for more security around him last month, I though the guy was simply being over the top. Who would want to harm Sam Six? It sounded so unreal. How could anyone want to be so crude?

Well, events over the past week have shown that indeed, Sam Six is being threatened. The man is being hunted. Some people have not been exactly tickled silly by the way he has been running the show in the Bunge.

While most of us observers have been thinking that the Speaker has been doing his job tolerably well, some forces have been baying calling for his blood. They wanted a lynching.

They want him out. The country has been looking on in horror as Sam Six was being savaged by his own ‘pals'. You wonder if this was a secret agenda or clever plot, but the whole affair has made him an instant national hero.

Buoyed by a collective approval of millions of Tanzanians, Sam has come back swinging back. He said on Sunday that he would continue to wage war on grand corruption and other forms of criminality both within the party and government. "I'll always make decisions which are good for the majority.

I firmly believe that God is with me, and will never relent," he said during a meeting organised by religious leaders. Which is music to most Tanzanians. The thing is the country has been held at ransom for a long time now.

Most of the people have been chafing under this spectacle of the rule of money by a few corrupt businessmen masquerading as politicians. The majority in the country are simply being bullied by a monied few. This just can't go on.

The late Mwalimu Nyerere said: "To bully someone is evil. But to agree to be bullied is an even worse crime." Are Tanzanians agreeing to be bullied? Yes, but not forever. It is just that the situation is getting to be obscene. This is just not right! You cannot have a situation whereby some sell-out politicians blatantly come out in support of grand corruption.

The situation had to give in, sooner or later. Well it is giving in now. Supporters of grand corruption are training their guns at the wrong targets. It is not only Sam Six and the hero MPs in the Bunge who are the problem.

It is millions of Tanzanians who are just fed up. They have been watching this steady rape of their country and are now getting angry and frustrated. They are not members of any party.
alusekelo@yahoo.com adamlusekelo.blogspot.com
 
Last edited:
Nani anayeshanga Mkuu kumsaliti Sitta now?😕
Kawaiada yake nyie si mnaona jinsi alivyowasaliti watanzania na hasa waliompigia kura


Ahsante sana Bob1 na hilo la Kikwete kutusaliti Watanzania wengi bado hawalioni. Alitoa ahadi chungu nzima lakini hata moja hajaweza kuitimiza na kwa maoni yangu huo ni usaliti kwa Watanzania kwa huyu muheshimiwa ambaye ni chaguo la Mafisadi. Maamuzi yake mengi yanalenga kuwalinda mafisadi badala ya kutetea maslahi ya Watanzania.
 
Well said, but ignorants tanzanians are far away the majority who help ccm retain power no matter what......
 
Back
Top Bottom