Maamuzi ya NEC ya CCM na Hatima ya Spika Sitta

Maamuzi ya NEC ya CCM na Hatima ya Spika Sitta

Jokakuu:

Nimesoma thread nyingi kuhusu Sitta na nimeona kuwa watanzania tuna vichwa vya panzi kwa kusahau haraka haraka.

Sitta kama sikosehi alikuwa waziri na baadaye akapigwa ukuu wa mkoa baada ya kuboronga. Hiki ni kipindi cha mzee Mwinyi.

Na kwenye nafasi yake ya mkoa alikuwa hakai kazi kuzurura. Na Mzee Mwinyi alipofanya ziara mkoani, Sitta alikuwa hayupo na ikabidi afukuzwe ukuu wa mkoa.

Lakini bado alibakiza ubunge wake. Na kwa matamko yake alikuwa anasema atafanya machachari bungeni mpaka arudishwe kwenye baraza la mawaziri. Hivyo machachari yake mengi yana self motivations ambazo hazina faida yoyote kwa taifa.

Baadaye ulitokea mtafaruku wa serikali tatu ukiongozwa na lile kundi 55 (G55), mara sita akawa waziri wa sheria na katiba. Na machafuko yote bungeni yakatulia. Na mtu yoyote mwenye listi ya G55 naomba aangalie kama huyu jamaa alikuwemo na alifanya nini baada ya kupata uwaziri.

Tukirudi kwenye suala la Richmond, huyu jamaa alikuwa tayari kulifanya bunge lisubiri mpaka atakaporudi kutoka Marekani. Na kuna posti nyingi hapa JF zinazoonyesha kuwa huyu jamaa hakutaka kuwasilisha ripoti.

Leo hii huyu ndio anakuwa shujaa. Ukweli wa mambo huyu sio Lyatonga Mrema.

Huyu jamaa ni like kundi la mawaziri wa toka enzi ya Nyerere ambao wakipoteza nafasi za uwaziri walikuwa wanarudi bungeni kupiga makelele hili warudi tena kwenye nafasi za uwaziri. Na wakipata nafasi hawachelewi kuboronga.

kwa mantiki ya mwadhama polycarp kadinali pengo...samwel sita yupo kundi gani ....wanaopinga ufisadi toka moyoni au wanaopinga ufisadi kwa vile nao wamekosa fursa ya kuwa mafisadi??
 
Zakumi,

..inabidi historia ya Samwel Sitta ifuatiliwe ili wananchi waelewe wana-deal na mtu wa aina gani.

..kwa ninavyomuelewa mimi Sitta siyo msafi, na zaidi he is not a presidential material.

mkuu

Zakuni,

Hapo ntakupinga kabisa ukisema Sitta siyo presidetial material.kwa huyo kikwete mliemuona ndio presidential material ametimiza ahadi gani ama zaidi ya kutimiza ahadi ya washikaji zake kwamba atawakumbatia mpaka kufa?mambo ya uraisi inategemea saana na msimamo wako kama unaonyesha angalau kidogo unamsimamo basi unaweza ukawa Raisi mzuri mwenye msimamo.Wewe unafikiri kama six akiwa rais nani atapona katika hao mafisadi watakamatwa tu baada ya kuapishwa yeye.katika historia bunge letu hakuna mambo makubwa yalitokea bungeni mpaka baada ya six kukalia kiti usifanye mchezo kupisha hoja nzito mpaka waziri mkuu kuachia ngazi haijawahi tokea kwa hiyo angalia saaana huyu bwana hatari,akiwa raisi watu wengi mafisadi watakimbilia nchi za nje maana moto utawawakia na haitakua kisasi ila kusafisha nchi kidogo

vijisenti vyangu

radikali
 
Dah, kazi ipo Tanzania, huwezi amini kabisa.Kuwa watu wanajadili ugomvi wa watu walio chama Kimoja, yet they call themselves great thinker!

Hakuna msafi CCM!
 
siku J Kikwete, mheshimiwa. anatangazwa kua mshindi ktk kinyang'anyiro cha uchaguzi nilikua kule mlimani ,Chuo kikuu cha Dar es salaam, kumtembelea rafiki yangu mmoja ambae ni mwalimu mahala pale, hakika kishindo cha vigelegele vilisikika na kuashiria mwanzo wa zama za matumaini mapya KWA Watanzania wa Tanganyika, kweli nilishangaa. lakini nikajipa moyo kua huenda wasomi wameona mbali,mbali sana.
UKAJA UCHAGUZI MKUU, nilirejea tena pale mlimani kwenda kusoma namna ambavyo aliungwa mkono na wanafunzi,kisha nikapita IFM, TIA, CBE . nilichokipata huko ni kua Jakaya M. Kikwete aliugwa mkono kwa zaidi ya 70% ktk taasisi za elimu ya juu za hapa Dar.
Nani wakulaumiwa katika haya tunayo yaona leo ?
Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliwekwa madarakani na kada zote za Watanzania , hasa upande wa Tanganyika, wasomi waliwadanganya watu wakaida kua kuna tumaini kwa huyu mtu, sasa itokeapo leo anasaliti majemedari wa Vita dhidi ya ufisadi ni ishara ya kushindwa kwake kama mtawala katika Jamuhuri ya Muungano wa TZ, kila nikiangalia mzee wa Kikwele anavyopwaya nawakumbuka wasomi hawa.
Simlaumu sana Jk, nawalaumu wasomi kwa kututia moyo Watanzania hadi kumchagua huyu mdau ...sawa Kikwete tumesikia tetesi hizi za Jemedari mkuu wa vita dhidi ya Ufisadi.
 
Dah, kazi ipo Tanzania, huwezi amini kabisa.Kuwa watu wanajadili ugomvi wa watu walio chama Kimoja, yet they call themselves great thinker!

Hakuna msafi CCM!

Hakuna msafi kabisaaa c.c.m,, lakini kuna wengine afadhali kidogo.ukitaka kuangalia nani msafi siajabu hata mimi na wewe sio wasafi kwa hiyo tusiseme kama vile chadema wakiingia wao ndio wasafi hapana kabisa ,kwanza ukiangalia historia ya hao wengi wa chadema ni c.c.m na sio kwamba ni wasafi wana madudu kibao wameyafanya huko nyuma

nawakilisha

Radikali
 
RADIKALI said:
Hapo ntakupinga kabisa ukisema Sitta siyo presidetial material.kwa huyo kikwete mliemuona ndio presidential material ametimiza ahadi gani ama zaidi ya kutimiza ahadi ya washikaji zake kwamba atawakumbatia mpaka kufa?mambo ya uraisi inategemea saana na msimamo wako kama unaonyesha angalau kidogo unamsimamo basi unaweza ukawa Raisi mzuri mwenye msimamo.Wewe unafikiri kama six akiwa rais nani atapona katika hao mafisadi watakamatwa tu baada ya kuapishwa yeye.katika historia bunge letu hakuna mambo makubwa yalitokea bungeni mpaka baada ya six kukalia kiti usifanye mchezo kupisha hoja nzito mpaka waziri mkuu kuachia ngazi haijawahi tokea kwa hiyo angalia saaana huyu bwana hatari,akiwa raisi watu wengi mafisadi watakimbilia nchi za nje maana moto utawawakia na haitakua kisasi ila kusafisha nchi kidogo

vijisenti vyangu

radikali

Radikali,

..binafsi sijasema Kikwete ni Presidential material. kile kitendo chake tu cha kushinda Uraisi kwa kuchafua wagombea wenzake, kukwepa mdahalo, kutokuwa na rekodi yoyote ile ya utendaji kazi kama waziri, na zaidi performance yake so far kama Raisi, inadhihirisha kwamba nafasi ya Uraisi hana uwezo nayo.

..Samuel Sitta naye tunasema hana uwezo kama alivyo Kikwete. zaidi tunasema ni mwanasiasa mwenye rekodi chafu ya ufisadi alipokuwa waziri wa ujenzi na baadaye waziri wa ustawishaji makao makuu Dodoma.

..tatizo wengi hamjisumbui kutafuta historia ya Samuel Sitta kabla ya kutupa karata zenu kwake.

..kusema hakuna mambo makubwa yaliyopata kutokea bungeni kabla ya Samuel Sitta kuwa Spika ni kutowatendea haki wabunge na ma-Spika waliopita.

..mwaka 1994 tukiwa bado na mfumo wa chama kimoja Spika wa bunge aliridhia mjadala wa kuanzishwa kwa serikali ya Tanganyika. sasa sidhani kama hilo lilikuwa jambo dogo kulinganisha na haya yanayotokea wakati wa Spika Sitta.

..pia nakuomba urejee ripoti za Tume kama ile ya Edward Ayila kuhusu ubadhirifu wa fedha BOT, pia hoja binafsi ya mbunge Patrick Quoro kuhusu uharibifu wa mazingira na hujuma za waziwazi ktk mbuga zetu za wanyama, pamoja na hoja binafsi ya Jenerali Ulimwengu iliyopelekea kuanzishwa kwa sheria ya maadili ya viongozi. hizo ni baadhi ya hoja nzuri tu zilizowahi kuwasilishwa bungeni na Samuel Sitta hakuwa Spika wakati huo.

..wanaostahili pongezi kwa kusababisha Waziri Mkuu Lowassa ajiuzulu ni Dr.Mwakyembe na wajumbe wenzake wa Tume ya Bunge. alichofanya Spika ni kuteua wajumbe wa Tume hiyo. labda kama unadai behind the scene alikuwa akiwafanyia au kuwaelekeza kazi.

..binafsi namshukuru sana Spika Samuel Sitta kwa kupinga ubinafsi sasa hivi. lakini lazima wananchi waelimishwe kwamba, Sitta alikuwa fisadi wakati akiwa waziri wa ujenzi, na baadaye waziri ustawishaji makao makuu Dodoma, hivyo wananchi wasithubutu kumpa nafasi nyingine itakamuezesha kurudia ufisadi.
 
Mkuu,

labda mzee six ametubu na kuokoka na sasa anataka kusaidia wanyonge ama unasema je?
 
Dah, kazi ipo Tanzania, huwezi amini kabisa.Kuwa watu wanajadili ugomvi wa watu walio chama Kimoja, yet they call themselves great thinker!

Hakuna msafi CCM!

- Mkuu acha matusi, siasa ni watu na hasa viongozi, unasema kuwajadili The Clintons Vs The Obamas ni kuwa less of Great Thinkers?

Respect.

FMEs!
 
Nimefuatilia maoni ya wanaJF juu ya sakata la Sitta na NEC; wengi wanaonekana kumshauri aondoke CCM kwani hawezi kupambana na ufisadi akiwa ndani ya mafisadi.

Kwa juujuu inaoneka ni sawa ila kimkakati nina mawazo tofauti.

CCM imeweza kuvisambaratisha vyama vya upinzani kwa kutumia mbinu ya kupandikiza viongozi ndani ya vyama na hata kupandikiza vyama (yaani kuna vyama vya upinzani ambavyo ni matawi ya CCM). Mbinu hii ilitumika kuisambaratisha NCCR Mageuzi na ndiyo inazuia kuwepo kwa muungano/umoja wa vyama vya upinzani. Kwa mfano kuna mgombea urais mwaka 2000 wa chama cha upinzani,sasa amejiunga na CCM. Je mkimsimamisha mtu kama huyo katika muungano wa vyama na kabla ya uchaguzi kufanyika akajiengua na kujiunga na CCM si mtakuwa mmefanya zero?

Katika vita pia, ukiweza kuwa na askari wako ndani ya adui yako (makachero), basi kushinda ni rahisi maana siri zao utazijua mapema kabla hujashambuliwa.

Ni kwa mantiki hayo basi naona ni vyema watu kama Sitta wakawa ndani ya CCM; hii inasaidia kujua CCM wanapanga nini? Kwa mfano kama Sitta asingekuwa mjumbe wa NEC haya yote yasingejulikana wazi kwani wangekaa kisirisiri na kuamua kupiga kura ya kutokuwa na imani nae bungeni, lakini kwa kuwa alikuwemo ilibidi waseme waziwazi na hiyo imetusaidia kuwajua.

Pili ukiwa na akina Sitta, Mwakyembe, Selelii nk ndani ya CCM wanachochea mawazo mbadala ndani yake. Kuliko kuwa na wajumbe wote wanaosema 'ndiyo mzee' bora wawepo wale wanaoweza kuthubutu kusema 'siyo mzee'. Unajua wengine husema 'ndiyo mwenyekiti' kwa kuwa waoga kusema ila ukiwapa nafasi sirini wana mawazo tofauti. Hii ndiyo ilisaidia kutomuondoa Sitta maana kulijitokeza hoja mbili tofauti; moja arudishe kadi na nyingine ikisema hapana. Mwenyekiti alishindwa kuamua kwani angesema ipigwe kura hakuwa na uhakika ni upande gani utakaoshinda. Kama akina Sitta wasingekuwemo, hao wa kusema asirudishe kadi wasingekuwemo.

Ni juu yetu kuwatumia kikamilifu hao watu wa watu kama akina Sitta walio ndani ya CCM.

Nawasilisha.

ALIYEKUAMBIA SITA MSAFI NI NANI? usiwafuate hao walio upande wa njia nene, hakuna msafi CCM,

labda utupe time line kama SITA MSAFI UFISADI UTAISHA LINI YEYE AKIWEMO HUMO!
 
Fine, but you missunderstood the basic argument "CCM imeweza kuvisambaratisha vyama vya upinzani kwa kutumia mbinu ya kupandikiza viongozi ndani ya vyama na hata kupandikiza vyama" na
"Katika vita pia, ukiweza kuwa na askari wako ndani ya adui yako (makachero), basi kushinda ni rahisi maana siri zao utazijua mapema kabla hujashambuliwa. Kwa mantiki hayo......"

!

Hao vyama vya siasa wengi wao ni njaa tu! wala hakuna aliyewapandikiza wamejipandikiza na kujipendekeza.

Unataka kusema vyama vya siasa ni kama binti wa miaka 12, wakitongozwa wakakubali basi WAMENAJISIWA? kuwa havina akili, havina mashushushu wao, havina mikakati wala haviwezi kugundua kuwa kuna mapandikizi na wakawaondoa? unaweza kuthibitisha hili, au unabaki na kansa ile ile kuwa hakuna mabadiliko nje ya CCM?

Mkuu mbona mrema aliweza 1995, tena wakati Nyerere yuko hai?

hao akina Mwakyembe, kilango sita n.k wanapitishwa na vyama vyao wagombee UBUNGE, wanaowapitisha ni hao mafisadi then LEO KUNA BAADHI YA WATANZANIA WANAKUWA KAMA WANA UBONGO WENYE MTINDIO WANAOTAKA TUAMINI KUWA KUNA WASAFI NDANI YA CCM for 40 yrs, I repeat for 40 yrs.
 
- Mkuu acha matusi, siasa ni watu na hasa viongozi, unasema kuwajadili The Clintons Vs The Obamas ni kuwa less of Great Thinkers?

Respect.

FMEs!

Mkuu unaowasema hao wako chama kimoja na wanagombana na kupingana on policy issues sio issue za nani msafi na nani fisadi na nani mchafu.
 
Kwa vile Six anasoma biblia, mimi sio mjuzi wa kitabu hicho labda kidogo Koran, ila katika biblia kuna maneno yanasema ''ukiwa vugu vugu ntakutapika, yaani ni heri uwe moto au baridi. Sasa SIta anavuna alichopanda maana alikuwa anataka kucheza kati. NEC imemchokonoa ili sasa msimamo wake ueleweke. Sio wakiitwa ndege popo yupo, wakiitwa wanyama popo yupo. No lazima tujue msimamo wake. Asante NEC sasa ndio tutajua msimamo wake. Binafsi sitampongeza Six kuwa ni mpiganaji mpaka nitakapoona msimamo wake vikao vijavyo vya Bunge. Kama alivyosema Slaa kwamba hamsikitikii kwa yale yaliyomkuta maana kama angeruhusu wabunge wote 15 wachangie mjadala wa majibu ya serikali kuhusu utekelezaji wa maazimio ya bunge kuhusu Richmond yote haya yasingempata.

SIX amua moja kuwa baridi au moto................
 
Mkuu unaowasema hao wako chama kimoja na wanagombana na kupingana on policy issues sio issue za nani msafi na nani fisadi na nani mchafu.

- Mkuu ugomvi wao ulianzia kwenye Race, kwamba nani ni racist na nani sio mkuu, halafu ufisadi nayo ni policy mkuu ndio maana tuna Takukuru au?

- Haiwezekani kumjadili Nixon, kama alikuwa msafi au mchafu katika Watergate ikawa ni less of a great thinking, au?

Respect.

FMEs!
 
Mkulu Pdidy, kwa maoni yangu you are damn right,

- Six anaaminika kukinyemelea sana na kwa muda mrefu kiti cha juu kwa hiyo hapa zilikuwa ni simple politics, kwamba Six ni a threat kwa wote, kuanzia Muungwana, mpaka Mtandao wa Lowassa, na hasa Asilia ambao hawamuamini Six a former Mtandao, ni bin-adam mwenye tabia za kubadilika badilika, kwa hiyo alikuwa kafara kwa makundi yote ya ndani ya CCM, labda sasa ndio ataamua kuchagua asimamie wapi ili aaminike,

- Nia na madhumuni ya Lowassa ilikuwa kumuondoa kabisa kwenye picha ya politics ili asiwe tatizo 2015, lakini nia ya Muungwana ilikuwa ni kumpunguza makali na speed, Asilia waliomuokoa walitaka kum-test waone kama ni trust-worthy, now the winner wa hii Cinema/Ze-comedy ni Membe, na the losers ni sisi wananchi wa Tanzania, kwa sababu in the process ya hii experiment a lot of damage has been done kwa political system yetu na hasa morale ya wapiganaji, na haiwezi kuwa repaired mpaka yafanyike mabadiliko ya katiba ya Jamhuri, ambayo yatazibana nguvu za chama tawala, chochote kile mbele ya safari.

- Walichofanya mafisadi kwenye hii Cinema ni kupanda mbegu za mbele ya safari ya 2015, ambako wana uhakika wa kuchukua power kwa 100%, kwa sababu dalili ziko wazi hapa, kwamba Muungwana anawahitaji kushinda tena 2010, na ninaamini kwamba ameshakata nao deal, akiamini kwamba anaweza kuwachezea akili mwishoni mwa 2015 halafu ampitishe Membe, by then wapiganaji wa kumsaidia hawatakuwepo tena na Muungwana for the first time atalipa the price kama ya Mkapa, atakabwa koo na kuwapa urais mafisadi, ambao watamchafua kila kona na kuua kabisa jina lake politically, kama umejifunza one thing kwenye hiii Cinema ya juzi, ni kwamba mafisadi they do not play, wakikupata wanakumaliza hawana huruma.

- Muungwana hawezi tena kutudanganya wabongo ni kwamba anawachukia mafisadi, na anajua ili abaki kwenye power ni lazima awe sawa nao kama alivyofanya hiki kikao cha NEC. Dodoma juzi mstari umechorwa rasmi asiyeweza kuusoma vizuri shauri yake!

Mungu Aibariki Tanzania.

Respect.

Field Marshall Es!
Mkuu, inawezekana ukawa sahihi kabisa. Ila nina wasiwasi sana na usahihi wa mawazo ya JK (kama kweli ndivyo anavyodhani), kuwa, kushiriki na mafisadi kutamsaidia kushinda uchaguzi ujao kwa urahisi. Nionavyo ni kuwa atapata shida sana akijiunga nao.

Kwa yaliyotokea Dodoma, nadhani JK hakuonyesha kwa kiasi kikubwa kuwa upande wa Mafisadi. Lakini pia hakuonyesha kuwa upande mwingine wowote. Ninavyohisi mimi ni kwamba, kadiri muda unavyosogea kuelekea kwenye uchaguzi ujao (2010), mafisadi watajitahidi sana kuhakikisha kuwa JK anaonyesha wazi yuko upande gani (wao au wa wapinzani wao). Hapo nadhani ndipo anapotakiwa kupaona sasa. Maana Mafisadi watamsumbua sana kuhakikisha wanajua mustakbali wao kisiasa. La sivyo wanajua kuwa watakuwa wamekwisha kisiasa.
 
Wameanza kuchapana bakora za makalioni bila huruma.
Subiri wakianza kuvuana nguo na kuonyesha aibu zao.
 
Mkuu, inawezekana ukawa sahihi kabisa. Ila nina wasiwasi sana na usahihi wa mawazo ya JK (kama kweli ndivyo anavyodhani), kuwa, kushiriki na mafisadi kutamsaidia kushinda uchaguzi ujao kwa urahisi. Nionavyo ni kuwa atapata shida sana akijiunga nao.

Kwa yaliyotokea Dodoma, nadhani JK hakuonyesha kwa kiasi kikubwa kuwa upande wa Mafisadi. Lakini pia hakuonyesha kuwa upande mwingine wowote. Ninavyohisi mimi ni kwamba, kadiri muda unavyosogea kuelekea kwenye uchaguzi ujao (2010), mafisadi watajitahidi sana kuhakikisha kuwa JK anaonyesha wazi yuko upande gani (wao au wa wapinzani wao). Hapo nadhani ndipo anapotakiwa kupaona sasa. Maana Mafisadi watamsumbua sana kuhakikisha wanajua mustakbali wao kisiasa. La sivyo wanajua kuwa watakuwa wamekwisha kisiasa.

- Mkuu Recta, heshima mbele sana ndugu yangu ninaheshimu sana hoja zako, lakini ushindi wa kikao cha siasa hutambuliwa na kupitishwa kwa agenda za ule mkutano wa siasa,

- Mafisadi walienda Dodoma wakiwa na agenda mbili, moja ni kumuondoa Six na pili kupitisha Azimio la kikao, la kwanza hawakufanikiwa lakini wamefanikiwa kumdhoofisha not olny Six, ila wapiganaji wote kwa sababu baada ya kile kikao kuisha ni makosa makubwa sana kuikosoa serikali na CCM unapokuwa kiongozi under CCM tiketi, ambalo ndio hasa Mafisadi wanted kwenye agenda yao ya pili ambalo lilipita likishuhudiwa na Mwenyekiti wa CCM,

- Toka hivi vita vianze kati ya wapiganaji na mafisadi, ukweli ni kwamba Mafisadi wamekuwa wakishinda hata wanaposhindwa hushinda anyways na siku zote wao humtumia Muungwana, kwa mfano:-

1. Lowassa alipokimbia kazi yake ya PM, alitakiwa kufikishwa kwenye sheria, lakini ni huyu huyu rais aliyemtetea kwamba hakukosea au umesahau mkutano wake na wazee wa Dar? Sasa who won hapa mkuu mafisadi au wapiganaji?

2. This time wapiganaji wakajaribu kupitisha agenda ya kuwathibiti mafisadi, look kwanza Makamba akaikwepesha na kujaribu kutoiweka hiyo Agenda, alipobanwa sana ikawekwa mezani tena dakika za mwisho, huyu huyu Muungwana akaizungusha zungusha, ikaishia makelele mengi ya kina Anna Abdallah na Kingunge, hakuna tamko rasmi la kikao on the ishu, nani aliyeshinda hapa mafisadi au wapiganaji?

3. Jambazi Nyari ambaye ni linked na mafisadi akaachiwa kati kati ya kikao cha NEC, baada ya ugomvi mkubwa ndani kikao kuhusu wabunge wa Arusha ambao walikamatwa kwa shinikizo la hao hao mafisadi, again hakuna tamko rasmi kuwapinga mafisadi na huku jambazi linked na mafisadi limeachiwa, nani aliyeshinda hapa Mafisadi au wapiganaji?

4. Uongozi wa UV-CCM, wapiganaji walimshauri Muungwana, asiruhusu mafisadi kugombea nafasi yoyote ile ya uongozi huo, tizama yaliyojiri, kwanza Nape akango'lewa na mafisadi asigombee, NEC kwa shinikioz la mafisadi ikaamua Mwenyekiti tu wa UV-CCM ndio atoke visiwani lakini nafasi zingine zigombewe na wote, kama mafisadi walivyotaka, sasa nani aliyeshinda hapa mafisadi au wapiganaji?

5. Oscar na kugombea ubunge wa Biharamulo, again baada ya vuta nikuvute huko NEC mafisadi wakampitisha kuwa mgombea wa ubunge, again nani aliyeshinda hapo mafisadi au wapiganaji?

6. Now juzi ndio haya, marufuku kwa kiongozi wa CCM kuishambulia CCM au serikali nje ya vikao vya chama, nani aliyeshinda mkuu sio hao hao mafisadi? Sasa mind you kwamba Mwenyekiti wa vikao vyote hivi ni Muungwana, sasa how could you say kwamba hajaonyesha yuko upande gani? Wakati hizi facts ziko wazi na clear kwamba anawaogopa? Mkuu baada ya hiki kikao cha juzi sasa ninaamini tena kwa 100% kwamba Muungwana anawaogopa zaidi hao mafisadi na yuko radhi kula nao ili ashinde uchaguzi na wapiganaji watakuwa ni wendawazimu kuamini tofauti!

Respect.

Field Marshall Es!
 
RAIS Jakaya Kikwete ameshindwa kulinda hadhi ya Spika wa Bunge la Jamhuri, Samwel Sitta katika vikao vya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mjini Dodoma.
Je hili ni sawa kweli, au kila kilicho andikwa kwenye magazeti lazima kiaminishwe kwa watanzania kuwa ni sahihi na cha kweli?
Kile kilikuwa ni kikao cha NEC ambacho ni cha CCM, pale Kikwete alienda kama mwenyekiti wa chama na wala siyo kama rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania au amiri jeshi mkuu, na pale Sita alienda kama mjumbe wa NEC na mwanachama wa chama cha mapinduzi, sasa suala la rais kumsaliti linatoka wapi spika linatoka wapi? CCM kina bunge au bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,mimi naona kusema rais Kikwete kashindwa kulinda hadhi ya spika siyo sahihi kabisa na ni upuzi mtupu.
 
- Mkuu tizama sheria za Jamhuri, Rais na Spika wanakuwa kazini masaa 24 kwa siku na ni 7 days, kwa hiyo wanapokuwa mahali popote pale nyadhifa zao kikatiba hazibadiliki zinakwua on kama kawaida, na infact Spika ni namba tatu kwa katiba ya Jamhuri yetu katika kukaimu urais iwapo Rais na makamu wake watashindwa ku-function kwenye hiyo nafasi ya urais,

- Ni wajibu wa Rais kama Chief Law-Enforcer wa Jamhuri kuilinda Jamhuri na wasiidizi wake kikatiba, ambapo Spika ni wa tatu kimadaraka toka kwake kama a sitting President, sasa bunge na Spika wanapokuwa assaulted na wajumbe wa chama cha siasa ambao sio hata wabunge tena kwa ishus ambazo sio Crimes against Jamhuri, Rais wa Jamhuri anatakiwa kuzima hayo mazungumzo mara moja kwa sababu hakuna sheria ya Jamhuri iliyovunjwa na utendaji kazi wa Spika, au wabunge wapiganaji,

- Ninasema hivi kama wajumbe wa CCM wangetaka Spika na wapiganaji kufunguliwa mashitaka huku wakitoa facts za hoja zao, Rais alitakiwa a-behave kama alivyofanya, lakini otherwise ana makosa makubwa sana kunyamaza na kuruhusu ule mjadala, infact ninaamini ilitakiwa sasa tuanze legal proceeedings za impeachment!, lakini kwa kuwa ni Tanzania ataongozewa five more years za uongozi!

Respect.

FMEs!
 
Kikwete ndiye mkombozi wa kweli, angekua dikteta angeegemea upande mmoja,demokrasia ya kweli ni kumuacha kila mtu aseme, whether unamuona right or wrong!! kumbuka truth and fact are ages apart, and truth is what you believe!!! hii ndio gharama ya demokrasi, ndio maana Democrats wanatetea mashoga na abortion, Republican wanapinga, ila huku Afrika karibu wote tunapinga pia, ila mbona tunampenda Obama!!! plz, remember that everything you share with others is common but relative...
 
Humu wanafiki wengi , hivi watu kama BLU RAY na wengine nyinyi mmeifanyia nini nchi hii...kazi kujificha tu kwenye JF. Hamna GUTS za kukemea chochote...MZEE SIX YUKO JUU
 
Back
Top Bottom