Mwiba
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 7,607
- 1,764
Kikwete hakuacha watu wamsulubu spika bali alihitajia ushahidi kamili ,kama ilivyoonekana kuwa madai ni kuwa sitta anaupendeleo na anatumia nafasi yake kuidhoofisha serikali na Chama chake,lakini ukiangalia kwa makini utaona kuna kundi ambalo ndilo linaloingilia madaraka ya spika ,kundi hili limeshahau kuwa Bunge si mali ya Chama wala serikali iliyopo madarakani ,kundi hili limeshindwa kufahamu kuwa yanayojadiliwa bungeni ni mambo yanayowahusu waTz wote ,hivyo mambo hayo yanaweza kuwa na muelekeo wa kuisema serikali au chama chochote kile bila ya kujali uzito wake.
Kwa ufupi Kikwete amepata uhakika wa yale aliyokuwa akipelekewa vikaratasi kuwa kuwa ndani ya CCM kuna makundi ambayo ndio yanayosababisha mtafaruku ndani ya CCM na kukizidishia maradhi ya kufa chama hicho.
Naona ni bora kusubiri tuone Mheshimiwa Raisi wa CCM na Raisi wa Jamhuri ya (Muungano)Tanzania kutoa tamko lake kitaifa kuhusiana na mkutano uliokwisha ambao ni wa Chama Tawala hapa Tanzania ,hamu ya WaTanzania ni kumsikia Raisi kama Raisi na sio mwenye kiti akiwahabarisha WaTanzania hatma ya nchi yao chini ya Uongozi wa CCM ,letus wait & c.